Search This Blog

Tuesday, May 1, 2012

SIMBA WAFUATA UBANI WA KUIREHEMU YANGA ZANZIBAR - MILAOVAN AFURAHISHWA NA USHINDI DHIDI AL ALHLY

SIMBA jana ilienda Zanzibar kwa ajili ya kujiandaa na mechi ya mwisho ya Ligi Kuu Tanzania Bara dhidi ya mtani wake Yanga itakayofanyika Jumamosi wiki hii.

Vinara hao wa Ligi Kuu wamefunga safari hiyo ikiwa siku moja baada ya kuifunga Al Ahly Shandy ya Sudan mabao 3-0 katika mechi ya kwanza ya raundi ya tatu ya michuano ya Kombe la Shirikisho na hivyo kujiweka katika mazingira mazuri ya kufuzu hatua inayofuata katika mechi ya marudiano wiki mbili zijazo.


Habari za uhakika kutoka ndani ya Simba zilizopatikana jana zilisema uongozi wa timu hiyo umeamua kuipeleka Zanzibar kwa siku zilizosalia ili kujiandaa na mechi hiyo. Mechi dhidi ya Yanga ndio itaamua hatima ya ubingwa wa Simba, inahitaji ushindi au sare ili kutangaza ubingwa.


Simba ina pointi 59 na Azam inayoshika nafasi ya pili ina pointi 56, hivyo Simba ikifungwa na Yanga na Azam kushinda mechi yake ya mwisho zitalingana pointi na hivyo bingwa kuamuliwa kwa tofauti ya mabao.


“Tuko njiani tunakwenda Zanzibar kwa ajili ya kambi kujiandaa na mechi ya Yanga, nadhani tutarudi Ijumaa jioni,”alisema mchezaji mmoja alipozungumza na mwandishi wetu kwa simu jana.


Wakati huohuo Kocha Mkuu wa Simba Milovan Cirkovic ameelezea kufurahishwa na kiwango kilichooneshwa na wachezaji wa timu hiyo kwenye ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Al Ahly kwenye Uwanja wa Taifa juzi.


Akizungumza mara baada ya mchezo huo Milovan alisema kuwa ushindi huo unaiweka timu yake kwenye nafasi nzuri ya kusonga kwa hatua inayofuata.


Alisema kuwa timu yake ilicheza vizuri hasa kipindi cha pili na ndio maana waliweza kupata mabao hayo na kuongeza kuwa bado wanakabiliwa na kazi ngumu kuiondoa timu hiyo katika mashindano.


“Ni kama tumemaliza nusu ya kwanza ya mchezo, nusu ya pili itakuwa nyumbani kwao hivyo bado tuna kazi ya kuhakikisha tunaitoa na kusonga mbele,” alisema Milovan.


Maneno ya Milovan yaliungwa mkono na nahodha wa timu hiyo Juma Kaseja aliyesema bado wana kazi ngumu kuitoa timu hiyo mashindanoni watakaporudiana wiki mbili zinazokuja huko Kartoum Sudan.


“Kwanini tuone kama tumeitoa, hapana bado tunakabiliwa na mechi ngumu ya marudiano kama mlivyoiona ni timu nzuri, hivyo kazi haijaisha,”alisema Kaseja.

1 comment:

  1. ha ha ha ha ah ah aha ha ha aha haha ha ha, Kaka Shaffih wakija wale wazee wa "TFF HAWANA AKILI,Cannavaro kapewa red card, niyonzima tegemezi kapewa red card, Tegete reserve kapewa red card HUU NI UZALENDO,NI UZALENDOOO0^:wakiona hicho kichwa cha habari lazima wakuulize tena huu ni uzalendo.
    The way ulivyo kiweka hicho kichwa cha habari kimenifanya nicheke sana na naamini hakuna neno jingine la kuwasaidia Yanga zaidi ya hilo ngoja watu watumie madhaifu yao kwa sasa kuwa restisha in peace kiulaini.
    Mdau
    Mike

    ReplyDelete