Odhiambo mwenye jezi nyeupe. |
Mchezaji wa zamani wa Randers FC George Blackberry Odhiambo ameondoka leo jijini Nairobi kuja Tanzania ambapo anategemewa kufanya mazungumzo na klabu ya Azam ambayo imeonyesha nia ya kumsajili.
George Odhiambo alirudi Kenya wiki iliyopita kutoka Denmark baada ya mkataba wake wa miaka minne na klabu ya kidenish kuvunjwa kwa makubaliano baina ya timu hiyo na mchezaji mwenyewe.
Odhiambo pia amekuwa akihusishwa na kusajiliwa na klabu yake ya zamani ya Gor Mahia lakini hii ilikuwa inategemea na uamuzi wa kocha Logarusic ambaye ndio anahusika na kusajili na kuruhus wachezaji kuondoka au kuuzwa. Jana jumanne kocha huyo alitangaza kuwaacha wachezaji tisa katika kile kilichoitwa kuipa uhai mpya klabu hiyo.

No comments:
Post a Comment