Search This Blog

Tuesday, May 1, 2012

BREAKING NEWS: AFRICAN LYON WAKATA RUFAA DHIDI YA MAAMUZI YA KAMATI YA NIDHAMU NA USULUHISHI KUHUSU MTIBWA SUGAR

5th Floor

Barclays House

P.O. Box 11133

Dar es Salaam

Tanzania

­­
REF No: ALFC/VOL.11/21/021
MWENYEKITI WA KAMATI YA NIDHAMU NA USULUHISHI ­TFF
S.L.P 1574
DAR ES SALAAM
TANZANIA

YAH: KUKATA RUFAA KWA TIMU YETU YA AFRICAN LYON FC DHIDI YA
KUCHEZA NA TIMU BATILI YA MTIBWA SUGAR LIGI KUU YA VODACOM
MCHEZO NO 174

Husika na somo la hapo juu kwa mujibu wa kanuni za ligi .KANUNI YA 15(1)
tunakata rufaa katika kamati yako kupinga kuendelea kwa uwepo wa timu ya
MTIBWA SUGAR katika ligi kuu Tanzania.

Sababu kubwa ya kukata rufaa hii ni kutokana na kamati ya ligi ya mashindano kutoa
maamuzi ya kutatanisha na yasiyozingatia kanuni dhidi ya mchezo AZAM FC VS
MTIBWA uwanja wa Chamanzi tarehe 22/4/2012.

Kamati ya ligi na mashindano katika maamuzi ya mchezo huo imepindisha KANUNI
MAKUSUDI kwa lengo la kutoa MAAMUZI KWA KUTUMIA KANUNI NA
TARATIBU KWA NJIA CHAFU ZISIZOKUBALIKA (KANUNI ZA LIGI
UTANGULIZI PARA YA MWISHO)

Sababu za kukata rufaa hii ni kama ifuatavyo:-
1. Kamati ya ligi na mashindano haikuzingatia kanuni no. 22. ( kifungu kidogo cha
kwanza), Ambayo ndio inayobeba dhana nzima ya KUVURUGA MCHEZO.

2. KANUNI NO.22 kifungu kidogo cha 1­6 ZINAELEZEA MCHAKATO MZIMA
WA KUVURUGA MCHEZO na adhabu zake, hivyo kamati kutumia kipengele
no 3 kuhusu muda wa mwamuzi kusubiria ni kitendo cha kutaka kuyumbisha
kanuni kwa makusudi.
Tafsiri halisi ya 22.(3) ni kuwa kuna tamko linalompa mwamuzi muda (nukuu)
‘’MWAMUZI ATASUBIRI KWA DAKIKA ZISIZOPUNGUA 15’’ Hivyo
mwamuzi anayo mamlaka ya kuona muda unaofaa kati ya dakika 1 hadi 15.
Kamati imelipotosha hili kwani mwamuzi alizingatia muda wa KIKANUNI.

3. Tunapinga pia kamati kutumia kipengele cha kanuni no. 5 na 6 kwani Tafsiri yake
halisi hata kama timu iliyo kwisha kuabidhiwa kwa kanuni no 22.(1)bado

4. itashushwa daraja na kutekeleza kanuni 22. Kifungu kidogo cha 4,5na 6. Kamati
hili nalo ilipotosha na kuyumbisha kanuni kwa maslahi binafsi.

Kamati ya ligi
5. Kunukuu kanuni za FIFA katika kutoa adhabu bado kanuni inaelekeza jukumu la
Tafsiri ya kanuni na chombo kinachopaswa kuelekeza kanuni za FIFA na CAF
(KANUNI ZA LIGI IBARA YA 69).

29/4/2012

6. Hoja yetu nyingine ni kuwa kamati ya ligi na mashindano maamuzi yake
yanaonekana wazi ni ya kimaslahi zaidi kuzingatia uhalisia wa kanuni
Mfano hai:
a. Mwenyekiti wa kamati : WALLACE KARIA ni mjumbe kutoka klabu ya
Mtibwa hivyo ana maslahi na timu ya Mtibwa fc.

b. Makamu mwenyekiti

c. Mjumbe wa kamat

: Kamati ya ligi SAID MOHAMED ni mwenyekiti wa
Klabu ya Azam Fc ambayo ina maslahi na mchezo huo.

:

GODFREY NYANGE KABURU ni makamu

mwenyeki Simba maamuzi halali ya KANUNI
yanaiathiri klabuyake ya Simba kuelekea mbio za
ubingwa

d. Mjumbe wa kamati

:

YAHAYA AHMED ni mfanyakazi wa kiwanda
cha mtibwa sugar­ hatatenda haki kwa kuwa ana
maslahi na mtibwa.

e. Mjumbe wa kamati

:

Damas Ndumbaro
Ni mwenyekiti kamati ya uchaguzi Simba ana
maslahi na Simba. Pia kisheria haruhusiwi
kuwepo kwenye kamati ya ligi kwa kuwa ni
WAKALA WA FIFA. Na FIFA imelikataza hilo
la mwakala wake kua kwenye kamati zozote za
shirikisho la mpira wa miguu.

Hivyo basi kwa kuwa wajumbe hawa niliowataja hapo juu walikuwa na maslahi
binafsi na uamuzi wowote ndani ya kikao hicho ni dhahiri maamuzi hayakuwa ya
haki na iwapo kama kamati ya ligi ilizingatia hoja hizi. Basi KORAM isingeweza
kutimia na kikao kilikuwa ni BATILI.

7. Sisi African Lyon tunashaka hata utekelezaji wa adhabu kabla ya mchezo wetu
no 174 dhidi ya mtibwa haikutekelezwa. Kanuni ya 22 kifungu no.6 (Adhabu ya
faini tunaomba kamati yako ijiridhishe na uhakiki wa hilo)

8. Kanuni bado hazizingatiwi hasa ukiangalia swala la mchezaji Salum Swed
aliyecheza mchezo no. 174 huku akiwa na adhabu kwa kumpiga mwamuzi
mchezo Azam vs Mtibwa.

MAJUMUISHO
Iwapo kama kweli kamati ya ligi na mashindano ingetaka kutoa maamuzi ya haki kwa
sababu ilizotoa basi maamuzi ya kamati yasingeegemea upande mmoja wa maamuzi
yenye utata. Kwakua wajumbe wengi wana maslahi na maamuzi ya kikanuni hivyo
basi ilipelekea wao kuangalia maslahi yao binafsi.

Kamati yako tukufu tuna imani itazingatia taarifa za mchezo husika na pia itazingatia
kanuni no.24 kifungu cha (i) na kuitolea tafsiri halisi ya kanuni no.22. (1 –6) ili haki
itendeke.

Tunatanguliza shukrani zetu za awali tukiwa na IMANI KUBWA NA KAMATI
YAKO KUWA ITATENDA HAKI KATIKA KUSIMAMIA KANUNI ZA LIGI NA
KUTOA MAAMUZI YA HAKI KWA MUJIBU WA KANUNI ZA LIGI KUU ZA
2011/12 AMBAZO ZILIZOPITISHWA NA KAMATI YA UTENDAJI 20 JULAI
2009.

AHSANTE

……………………………………
Rahim Kangezi
CEO/OWNER AFRICAN LYON FC
Mob: +255 784 255614
Email: Kangezi@gmail.com

Na ambatanisha na ada ya rufaa shilingi laki tatu (300,000/=)

www.africalyon.com

3 comments:

  1. Hili sakata la Mtibwa sasa linatia kichefuchefu na naamini busara isipotumika basi litaleta mkanganziko mkubwa sana kwenze ligi hii,binafsi siungi mkono hata kidogo jambo walilofanya Mtibwa la kugomea mcheyo hayo ni mambo ya kizamani na kwenye soka la kiwango cha ligi kuu wanapaswa kupewa adhabu lakini chanzo lazima kiwekwe wazi kwani kwa mujibu wa maelezo inaonekana palikuwa na njama za kutaka kuwabeba Azam katika mchezo huo na pamoja na kwamba hakuna ushahidi wa moja kwa moja ila ushindi wa Azam sasa umeanza kunipa mashaka makubwa na nashawishika kukubaliana na maneno ya Mohamed Simba Banka akisema kwanini utumie mamilioni kununua wachezaji na bado unanunua mechi inakuwa haina maana.
    Hilo jina jipya la mtibwa limenifurahisha Timu BATILI ya Mtibwa ikiwa na maana hawana uhalali wa kucheza ligi kuu tena.

    Ila busara za hali ya juu kabisa zitumike kuamua suala hilo na si ushabiki.
    Mdau
    Mike

    ReplyDelete
    Replies
    1. Jamani,Mtibwa ikishushwa dalaja itakuwa balaa! Maanayake matokeo ya mechi zote za Mtibwa yatafutwa. Msimamo wa ligi unaweza ukabadilika vibaya sana na kuathiri timu za juu na chini. Kwa kweli busara za hali ya juu zitumike.

      Delete
  2. Mr rahim nimependa barua yako umeelezea kila kitu kwa ufasaha isipokua kuna marekebisho kidogo sio dakika zisizopungua 15 Bali ni DAKIKA ZISIZOZIDI 15

    ReplyDelete