Search This Blog

Wednesday, May 2, 2012

JUVENTUS WAGOMA KUTOA MKATABA MPYA: DEL PIERO ATANGAZA KUONDOKA KWA KIBIBI KIZEE CHA TURIN

Kwaherini.

Baada ya kukaa kwa misimu 19 akiwa na Kibibi Kizee cha Turin hatimaye mfalme wa Turin Alessandro del Piero ametangaza ataondoka katika klabu hiyo mwishoni wa msimu huu., huku Juventus wakikaribia kutwaa kombe la Scudetto tangu waliporudi kwa ligi ya Serie A.

Juve wanaweza kuchukua kombe la Coppa Italia  mwishoni mwa msimu ambapo watacheza dhidi ya Napoli: mchezo ambao utakuwa wa mwisho kwa Del Piero katika jezi maarufu za rangi nyeusi  na nyeupe.

Del Piero anamaliza mkataba wake mwishoni mwa msimu, na mpaka sasa hajapewa mkataba mpya wa kuongeza muda wake wa kukaa Turin kwa msimu wa 20.

"Kwa sasa kama mambo yalivyo, mechi ya fainali ya Coppa Italia dhidi ya Napoli mwezi huu tarehe 20 ndio utakuwa mchezo wa mwisho kuitumikia Juventus kwa sababu mkataba wangu unamalizika mwezi June," Del Piero aliliambia La Gazzetta dello Sport.

"Lakini kwa sasa napenda kufikiria kuhusu wakati huu. Mapenzi waliyonionyesha mashabiki kila siku niliyokuwepo hapa ni makubwa. Hivyo kama la kutokea litatokea.






Huku siku zake za kukaa na Juventus zikiwa zinakaribia kuisha - ebu tukumbuke career ya Del Piero kwa namba.

702
Del Piero amecheza mechi 702 akiwa na Juventus - hii ni idadi kubwa kuliko mchezaji yoyote katika historia ya klabu hiyo.
 Del Piero alifunga bao lake la kwanza katika mechi dhidi ya Biaconeri  ikiwa ndio mechi yake ya pili na Juventus.

4
Del Piero amecheza mara nne fainali ya Champions League akiwa na Juventus - ingawa walifanikiwa kushinda mara moja na kupoteza mara 3.

7

Del Piero ameshinda kikombe cha Scudetto mara 7 akiwa na Juventus - kombe la kwanza akishinda katika msimu wake wa pili tu tangu aanze kucheza kikosi cha wakubwa cha Juventus.

289
Akiwa na magoli 289 katika mechi 702 na Juventus - Del Piero ndio mfungaji bora wa muda wote katika historia ya klabu hiyo.

32
Msimu ambao Del Piero alitisha zaidi ni msimu wa 1997-98 ambapo alifunga magoli 32 katika mashindano yote na kuiwezesha Juventus kuchukua kombe la Scudetto na kufika fainali ya Champions league.

No comments:

Post a Comment