Search This Blog

Friday, March 16, 2012

MANCHESTER UNITED YATOLEWA EUROPA NA BILBAO - WAFUNGWA 2-1.

MAMBO YAMEZIDI KUWA MAGUMU KWA MANCHESTER UNITED MSIMU HUU BAADA YA KUFUNGWA 2-1 KATIKA MCHEZO WA PILI WA MARUDIANO YA LIGI YA EUROPA NA ATLETICO BILBAO.





SISIMIZI WALIOMUANGUSHA TEMBO - ATLETICO MADRID WAKISHANGILIA USHINDI WAO DHIDI YA UNITED.

UNITED WALIFUNGWA 3-2 KATIKA MECHI YA KWANZA ILIYOFANYIKA OLD TRAFFORD WIKI ILIYOPITA,HIVYO KWA MATOKEO YA LEO INA MAANA KIKOSI CHA FERGUSON KIMETOLEWA KWA JUMLA YA MABAO 5-3.

Thursday, March 15, 2012

TBL yaidhamini Taifa Stars miaka mitano kwa Sh. 15bil


LAMPS COLLIN
KAMPUNI ya Bia Tanzania (TBL) imemwaga zaidi ya Shilingi 15 bilioni kuidhamini timu ya taifa ya Tanzania 'Taifa Stars' kwa muda wa miaka mitano.

Habari za uhakika kutoka vyanzo vyetu vya habari, zinasema kuwa siku chache zijazo TBL na Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) watasaini mkataba huo mkubwa na aina yake kuwahi kutokea nchini.

Taifa Stars ipo katika mechi za kufuzu fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika zitakazofanyika Afrika Kusini mwakani huku pia ikijiandaa kwa michuano ya kufuzu fainali za Kombe la Dunia nchini Brazil mwaka 2014.

Habari za uhakika zinasema kuwa TBL imekubali kuidhamini Taifa Stars kwa Shilingi tatu bilioni kila mwaka hivyo kwa miaka mitano itakuwa Sh.15 bilioni.

Huu utakuwa ni udhamini mkubwa zaidi kuwahi kutokea katika historia ya soka nchini.

Hakuna upande uliokuwa tayari kuzungumzia suala hilo kwani pande zote zinataka kufanya hafla ya nguvu wakati wa kusaini mkataba huo mbele ya vyombo vya habari.

Siku chache zilizopita TFF ilitangaza kuwa haitaongeza mkataba na wadhamini wao wa zamani Kampuni ya Bia Serengeti (SBL) ambao kwa miaka mitano walioidhamini Taifa Stars kulikuwa na msisimko mkubwa wa soka.
Source: mwanaspoti.co.tz

JACQUES ROGGE akerwa na Tabia ya wanamichezo kubadili uraia

Na kuelekea michezo ya olimpiki ambayo kwa mwaka huu itafanyika huko London , Uingereza , Rais wa Kamati ya kimataifa inayosimamia michezo hiyo yaani THE NTERNATIONAL OLYMPIC COMMITEE au I.O.C mcanada JACQUES ROGGE ameelezea kukerwa kwake na Tabia ya wanamichezo kubadili uraia wao ili wapate nafasi ya kushiriki michezo hiyo.

ROGGE ametoa dukuduku lake juu ya kubadili uraia kwenye Mkutano wa siku mbili wa bodi ya Kamati Yake ambapo Moja ya agenda kuu ilikuwa uraia kwa wanamichezo , katika mkutano huo MWanariadha Yamile Aldama ambaye ni mzaliwa wa Cuba na mwendesha baiskeli ambaye ni mzaliwa wa Ujerumani Philip Hindes wa Waliidhinishwa Kuiwakilisha Uingereza kwenye michezo a mwaka huu ya olimpiki inayotarajiwa kuanza mwezi agosti .

CHISORA ANYANG'ANYWA LESENI.

Kwenye masumbwi Bondia mzaliwa wa Zimbabwe Mwenye uraia wa Uingereza Derek Chisora amenyang'anywa leseni Yake kwenye Mchezo wa masumbwi ikiwa ni adhabu ya bodi ya Mchezo huo kwa chisora kufuatia vitendo vya utovu wa nidhamu Alivyoonyesha chisora kabla na Baada ya pambano Kati Yake na Bondia toka Ukraine Vitaly Klitschko.

Taarifa iliyonukuliwa kwenye barua aliyoandikiwa Chisora juu ya adhabu hiyo imesema kuwa Derekc Chisora hayuko kwenye Hali sahihi a kiakili anayotakiwa kuwa nayo mtu aliyeaminiwa kuwa na leseni a Mchezo wa masumbwi.

Bodi hiyo imeweka wazi milango ya rufaa kwa Chisora na amepewa siku 14 za Kufanya hivyo endapo atahisi Kutoridhishwa na adhabu aliyopewa. Derek Chisora Alimpiga kofi mpinzani wake wakati wa hafla ya kupimwa uzito na alienda mbali zaidi pale alipomtemea mate Usoni mdogo wa Vitali  vladmir na Kali kuliko zote ilikuwa Ugomvi Kati Yake na aliyekuwa Bondia wa uzito wa juu ambaye kwa sasa amestaafu Mchezo huo David Haye kwenye mkutano wa waandishi wa habari Baada ya pambano lake dhidi ya Vitaly Klitschko huko Munich.

Europa League kuendelea leo !


Michuano ya pili kwa hadhi huko barani ulaya uefa Europa inaendelea tena usiku huu ambapo michezo ya marudiano itapigwa kwenye viwanja mbalimbali.

Macho na masikio ya wengi yataelekezwa kwenye viwanja via Hispania na huko England ambako vigogo vya jiji la Manchester vitakuwa na kazi a kubadili matokeo mabaya waliyopata kwenye michezo ya kwanza endapo watataka kuendelea kuipeperusha vyema bender ya England kwenye michuano hiyo .

Huko Etihad stadium man city watawakaribisha sporting club Lisbon toka ureno katika Mchezo ambao city wanahitaji ushindi wa angalau mabao mawili ya wazi huku wakipaswa kuwazuia sporting wasipate bao la ugenini . Nao wapinzani wa jadi wa City mashetani Wekundu Manchester united watakuwa na kibarua kigumu zaidi watakapokuwa wanacheza na athletic club Bilbao Kwenye uwanja wa the cathedral . United waliopoteza Mchezo wa kwanza uliopigwa huko old trafford wanahitaji ushindi wa mabao mawili bila au zaidi ili kusonga mbele.

Taarifa za matumaini kwa mashabiki wa united ni kurejea kwa kiungo wa pembeni Antonio Valencia aliyekuwa nje a uwanja kwa wiki nne Baada ya kuumia kwenye Mchezo wa hatua ya 16 bora dhidi ya Ajax .

Chelsea na Real Madrid Zaingia Robo Fainali ya UEFA CHAMPIONS LEAGUE kwa kishindo !

.Michuano ya ligi ya mabingwa barani playa hapo Jana ilikamilisha hatua ya kwanza ya mtoano ambayo ni hatua ya 16 bora. Huko Stamford Bridge wawakilishi pekee wa visiwa via malkia Chelsea the blues walifanya maajabu yasiyotarajiwa na wengi Baada ya kugeuza matokeo ya kipigo cha mabao Matatu kwa Moja na kuwafunga wapinzani wao Napoli ya Italia kwa mabao manne kwa Moja katika Mchezo ulioamuliwa kwa dakika 30 za nyongeza . Mabao ya Chelsea hiyo Jana yaliwekwa wavuni na Didier Drogba , John Terry , Frank lampard na Branislav Ivanovic Aliyefunga kwenye dakika za nyongeza na kuipa Chelsea ushindi wa jumla wa mabao matano kwa manne.

Mchezo Mwingine uliopigwa Jana uliwashuhudia mabingwa wa kihistoria kwenye michuano hii Real Madrid ya uhispania wakiwafunga CSKA Moscow toka Urusi kwa mabao manne kwa Moja . Real walipata mabao Yao kupitia kwa Cristiano Ronaldo Aliyefunga mabao mawili , Gonzalo Higuain na Karim Benzema ,Real wamesonga mbele kwa matokeo ya jumla ya mabao matano kwa mawili .Michuano hiyo sasa inaingia kwenye hatua ya robo ambapo ratiba ya hatua hiyo itapangwa siku ya ijumaa huko Munich itakakofanyika fainali ya michuano hiyo.



Wednesday, March 14, 2012

KADI NYEKUNDU YA BEKI BEKI WA SIMBA KELVIN YONDANI Vs TOTO AFRICANS

Huyu ndo John Bocco ' Adebayor '

Kibarua kigumu cha Chelsea dhidi ya Napoli.


Wiki iliyopita dunia ilishuhudia msisimko wa dakika 90 toka kwa Arsenal iliyokuwa inatafuta kufanya maajabu ya kugeuza matokeo ya kipigo cha mabao manne bila walichopewa kwenye mchezo wa kwanza dhidi ya AC Milan .Almanusra wafanye hivyo baada ya kupata mabao matatu ya haraka kwenye kipindi cha kwanza .Ugumu uliokuwa unaizunguka mechi ya Arsenal ulionekana kwenye kipindi cha pili ambapo Arsenal ilikosa mpango mbadala huku wachezaji wakiwa wamechoka .
 Upande wa pili Milan ni kama walitengeneza wenyewe tatizo lililowasababishia kufungwa mabao matatu kwenye kipindi cha kwanza .Leo timu nyingine ya London itajaribu kutekeleza kibarua ambacho kwa macho ya haraka kinaonekana rahisi kuliko cha Arsenal dhidi ya Milan.Chelsea wanaingia uwanjani kuwakaribisha Napoli huku wakijaribu kugeuza ubao wa matokeo utakaokuwa unasoma 1-3 dhidi yao .Mara ya mwisho wakati Chelsea waliposafiri hadi Italia kucheza na Napoli makosa ya kiufundi ya aliyekuwa kocha Andre Villas Boas yaliigharimu Chelsea vibaya.
AVB aliona busara kuwapanga Ramires na Raul Meireles kwenye midfield na kumuacha Michael Essien na aliona ni vyema kumpanga beki wa kulia Jose Bosingwa kushoto na kumuacha Ashley Cole ambaye siku hiyo aliapia miungu yake yote kuwa yuko fit benchi.Upangaji mbovu wa kikosi hiki uliiua Chelsea na matokeo yake ni mabadiliko ambayo yanapelekea leo hii Roberto Di Matteo kuongoza mechi yake ya kwanza ya Champions League.3-1 si matokeo ya kutisha kama ilivyokuwa 4-0 ya Arseanl , lakini ukitazama kasi waliyo nayo Napoli kwa sasa tofauti na kasi waliyokuwa nayo Milan siku wlaiyocheza na Arsenal na kufungwa 3-0 ndio utakapoona ugumu wa mchezo wa leo .
Walter Mazzari kwa vyovyote hatafanya makosa aliyoyafanya Allegri na zaidi ya hayo Napoli hawana tatizo la kukosa mfumo mmoja husika wa kuutumia ambao unawaruhusu kuwa-accommodate wachezaji wao bora kwenye nafasi zao bora . Edinson Cavani anajulikana kuwa ndiyo anayeongoza mashambulizi huku akipewa support na Ezequiel Lavezzi , nyuma ya wachezaji hawa kuna viungo Gokan Inler na Marek Hamsik. Kilichotokea kwenye mchezo wa kwanza ndio ambacho kimekuwa kikitokea karibu msimu mzima . Kokote ambako Napoli imeshinda , mchango mkubwa wa ushindi umetokana na either bao au mabao ya mmojawapo kati ya Lavezzi na Cavanni huku mwingine akitoa Assist.
Wiki tatu zilizopita Lavezzi alipiga mbili huku mojawapo likitengenezwa na Cavanni na bao alilofunga Cavanni mwenyewe lilitengenezwa na Lavezzi .Tatizo ambalo wanalo Napoli wanalo ni kwenye Defense ambayo mara nyingi huwa ina tatizo la kupoteza focus au concentration ambayo kwa lugha ya kiswazi tunaweza kusema wana tatizo la kuzubaa nah ii mara nyingi huwa inatokana na ukweli kuwa timu nyingi ambazo zinajulikana kwa kuwa na wachezaji hatari kwenye upande wa pili wa uwanja lina matatizo ya focus kwenye defense kwani mara nyingi falsafa ya tufunge moja tukufunge matatu huwa inaathiri na pia mara nyingi timu inakuwa inashambulia kiasi cha mabeki kutokuwa mchezoni .
Ndio maana Chelsea walianza kufunga kwenye mchezo wa kwanza uliozikutanisha timu hizi kina Paolo Canavarro na kipa wao Morgan De Sanctis waliruhusu bao la mapema ambalo liliwakuta wamezubaa.Kwa upande wa Chelsea kuanzia kwenye safu ya ushambuliaji kuna tatizo kubwa . Hadi sasa kwa msimu huu ukiachilia mbali dogo Daniel Sturidge hakuna mshambuliaji yoyote wa Chelsea ambaye unaweza kusema yuko kwenye form msimu huu na ndio maana kati ya Didier Drogba na Fernando Torres hakuna magoli , si kwa kuwachanganya wote wawili au hata mmoja wao.Nguvu kwa upande wa Chelsea hasa kwenye mechi dhidi ya timu za daraja la kawaida imekuwa mabao yanayofungwa na mabeki ambako watu kama David Luiz na Gary Cahil wote wana uwezo mkubwa wa kufunga mabao na kwa beki nahodha ambaye amerejea John Terry naye ana uwezo mkubwa wa kufunga .
Safu ya kiungo hasa kwa mhispania Juan Matta ndio hasa mahali ambako Chelsea wanaweza kujivunia mchezaji anayeweza kubadilisha matokeo. Kama kuna matumaini ya Chelsea kubadili ubao wa matokeo leo ni kupitia kwa Juan Matta , uwezo wake wa kutoa pasi za mwisho na hata wakati mwingine kufunga iwe kupitia mipira iliyokufa au hata mabao ya mashuti ya mbali Matta anao uwezo huo. Viungo wengne kama Frank Lampard na Michael Essien wanaweza kuchezeshwa leo lakini kwa Frank Lampard huu si mchezo wake , Chelsea inaweza kufaidika zaidi kama ikiwapanga John Obi Mikel , Michael Essien , Ramires na Juan Matta .
Umri alio nao Lampard kwa sasa unafanya kasi ya mchezo kama wa leo kumzidi na kuna hatari ya kuwa pedestrian kwa Chelsea kama akicheza leo.Kuna kila uwezekano kuwa Di Matteo atampanga Daniel Sturidge peke yake au na Didier Drogba ambapo Sturidge anaweza kushambulia kwa kutokea pembeni.Branislav Ivanovc , Ashley Cole , Gary Cahil na nahodha John Terry kwa vyovyote ndio watakaopangwa kwenye safu ya ulinzi baada ya kuonekana kuwa thabiti kwenye mchezo wa wikiendi dhidi ya Stoke City .Kama Chelsea watataka kushinda wanapaswa kuwakamata Napoli kwa kutumia ‘element of surprise’ .
Kuingia na kushambulia mwanzo mwisho kama walivyofanya Arsenal . Chelsea wanaweza kubadili ubao wa matokeo lakini ugumu unatokana na ukweli kuwa Napoli huenda hawatawaruhusu Chelsea kufanya hili .Bado mchezo unabakia kuwa mgumu lakini ugumu zaidi uko kwa Chelsea kwa sababu wao ndio wako kwenye ‘dis advantage position’ na uzoefu mdogo wa kocha wao Roberto Di Matteo unaweza kui-expose Chelsea kwani approach atakayoingia nayo kwenye mchezo itaamua kama Chelsea watasuka au watanyoa.

IN NUMBERS | MADRID'S IMPRESSIVE


7 - Real's biggest home win this term was a 7-1 win over Osasuna

13 - Mourinho's men have hit 13 goals in their three home fixtures in the current Champions League; they thrashed Ajax 3-0, trounced Lyon 4-0 and hammered Dinamo Zagreb 6-2

17 - Madrid have won 17 out of 20 games at the Santiago Bernabeu this season, failing to beat Barcelona in the other three

78 - The goals scored by Madrid at home in 2011-12. They have scored in every single home game, with three or more against everyone except Barcelona

129 - Should they maintain their current scoring rate, Madrid are on target to reach 129 goals and smash the record of 107 set by John Toschack's side in La Liga in 1989-90

0 - CSKA have never lost in Spain, having knocked out Barcelona in the 1992-93 Champions League with a 3-2 win at Camp Nou in the second round, and eliminated Sevilla with a 2-1 success at the Sanchez Pizjuan in the last 16 in 2009-10

chemsha bongo ! hawa ni kina nani ?

Somali yafurahishwa na urejeo wa Jeenyo United FC

chama cha soka nchini Somalia kimefurahishwa na uzinduzi wa klabu maarufu nchini humo ya Jeenyo Fc, klabu hiyo maarufu nchini Somalia ilifutwa miaka 22 iliyopita.

YANGA NA SIMBA ZASHINDA HII LEO.


Ligi kuu ya Vodacom Tanzania Bara imeendelea hii leo kwenye viwanja viwiwli,
jijini Dar es Salaam mabingwa watetezi wa ligi hiyo Yanga imeifunga African Lyon bao 1:0 kwa bao la Kigi Makassy.
huko mkoani Dodoma Simba imefanikiwa kuifunga Polisi ya mjini humo bao 1:0
bao la ushindi la Simba limefungwa na kiungo Patrick Mutesa Mafisango.

VILLA SQUAD YAPINGA KIWANJA CHAKE KUVAMIWA na kampuni ya SMEC International ya nchini Australia !

...Kuna ule usemi wa Waswahili wa Pwani ya Afrika ya Mashariki usemao Fedha ni sabuni ya roho na mwenye nazo hashindwi na lolote anaweza kuhamisha Hata mito na milima popote atakapo….
Pengine usemi huu ndio ambao umetumiwa na Uongozi wa kampuni ya SMEC International yenye makao yake makuu nchini Australia kwa kuamua kupinga agizo la Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dr.Jakaya Kikwete la kuwataka wawekezaji wote kuacha mara moja kujenga kwenye viwanja vya Jangwani kwaajili ya kuwapa nafasi timu ya Villa Squad kuutumia uwanja huo.
Kauli hiyo ya JK ambayo aliitoa katikati ya Mwezi wa nne mwaka jana,ilikuja baada ya mashabiki wa klabu hiyo kutaka kuandamana hadi Ikulu kumueleza Rais kero yao hiyo…
Lakini Hali hiyo imejitokeza tena hii leo ikiwa ni mwaka mmoja baada ya kauli ambapo kundi la Mashabiki wa klabu hiyo yenye maskani yake Magomeni Jijini DSM kuwalalamikia wawekezaji hao na kuwataka kuondoka kwenye eneo hilo la Uwanja….Lakini wadosi hawa wao wanadai wana vibali maalumu vya kufanya kazi hiyo ya ujenzi wa kituo cha mabasi yaendayo mwendo wa kasi kutoka Serikalini…


 Mashabiki wa Villa Squad ya Magomeni wakiwa hawaamini kama uwanja wao wa mazoezi umepitiwa na Greda.



  Kifusi kikiwa kimemwagwa kwenye Uwanja wa Villa Squad.

      Mwenyekiti wa kamati ya Mashindano ya Villa Squad Bw Idd Godigodi Akizungumzia namna walivyofadhaishwa na kitendo wakala wa barabara nchini Tanroads kugomea agizo la Serikali kutoruhusu viwanja hivyo vilivypo maeneo ya Jangwani jijini Dar E s Salaam na kuipa tender kampuni ya SMEC International.

TAARIFA KUTOKA TFF!

UHARIBIFU WA VITI UWANJA WA TAIFA
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) leo (Machi 14 mwaka huu) limepokea barua kutoka Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo juu uharibifu uliofanyika kutokana na vurugu za washabiki wa Yanga kwenye mechi dhidi ya Azam.

Kwa mujibu wa tathmini ya Serikali, katika vurugu hizo kwenye mechi hiyo ya Ligi Kuu ya Vodacom iliyochezwa Machi 10 mwaka huu Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam jumla ya viti 119 viliharibiwa. Gharama za uharibifu huo ni sh. milioni 5 ambazo Serikali imeagiza zilipwe mara moja.

Kwa vile washabiki wa Yanga ndiyo waliohusika na vurugu na uharibifu huo, gharama hizo zitabebwa na klabu hiyo ili Serikali iweze kufanya ukarabati haraka.

TFF inarudia tena kulaani na kukemea vurugu zinazofanywa na washabiki viwanjani na kusababisha usumbufu, uvunjifu wa amani na uharibifu wa vifaa  hasa kutokana na ukweli kuwa mpira wa miguu ni mchezo wa burudani.

Tunapenda kuwakumbusha washabiki na klabu kuwa vitendo hivyo si vya kistaarabu, hivyo havikubaliki katika mpira wa miguu, na TFF haitasita kuchukua hatua kali kwa wahusika iwapo vitaendelea kutokea viwanjani.

TENGA KUZUNGUMZA NA WAANDISHI LEO
Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Leodegar Tenga kesho (Machi 15 mwaka huu) atakuwa na mkutano na waandishi wa habari. Mkutano huo utafanyika saa 6 kamili mchana kwenye ofisi za TFF.
Powered by Sorecson : Creation de site internet
Boniface Wambura
Ofisa Habari
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)

Kupambanisha boxers zaidi ya mara tatu ni makosa kisheria

Kupambanisha boxers zaidi ya mara tatu ni makosa kisheria, hapa kwetu tunafanya kwa kutojua sheria au kwa mapromoter kutengeneza pesa.

Wadau tumeliona ilo na tukiendelea kukaa kimya tutalitia aibu Taifa.International fight zote zinaruhusu re-match na grand final after re-match, mfano Manny Pacquiao vs Erick Morales game ya kwanza alipigwa Many paquiao kwa points, akaomba re-match akashinda Manny Pac kwa KO round ya kumi.

 Elick Morales akaomba grand final re-match akapigwa KO round ya 3, akataka tena re-match sheria zikambana mpaka leo anataka kurudiana na Manny Pac ila walishamaliza three times fighting.Mfano mwingine Manny Pacquiao vs Juan Manuel Marquez game ya kwanza draw, ikaja re-match akashinda Manny pac kwa points, Marquez akaomba grand final re-match ikapigwa akashinda Manny pac kwa pints ilikua very close fight, mpaka leo wanataka re-match ila sheria za boxing zinawabana haiwezekani tena.Riddic Bowe vs Evender Holifield zimepigwa three times, moja draw mbili alipigwa Evander, na Evander alitaka re-match ikashindikana kwa kuwa walishamaliza zile three times fighting na awawezi kupigana tena.

Na mifano mingi tu ila hiyo michache inatosha.Hapa kwetu tumeshuudia boxers wakipigana zaidi ya mara saba na watu kwa kutojua sheria wanaona ni jambo la kawaida ila ni makosa kisheria, vyama vyetu vya ngumi PST, TPBO, TPBC ect, baadhi vinajua hilo na baadhi havijui  hilo kabisa. Ni makosa kupiganisha watu zaidi ya mara tatu.Rashid Matumla vs Maneno Osward wamepigana zaidi ya mara 5 au 6 na bado wanataka kupigana tena je hapo sheria zinafutwa au wanatubuluza???????Francis Cheka vs Rashid Matumla wameshapigana zaidi ya mara 4 na bado kuna plan ktk mwaka huu kuwapiganisha tena.Mada Maugo vs Francis cheka, walipigana PTA akapigwa Maugo, akaomba re-match zikapigwa Morogoro Jamuhuri akapigwa tena Maugo, sasa wameingia ktk grand final zitapigwa tena April tunaomba game hii iwe ya mwisho kwao la sivyo tutawashtaki mapromoter na chama chochote kitakachotoa kibali kwa ajiri ya fight nyingine baada ya hii ya April.

Mbwana Matumla vs Francis Miyeyusho wameshapigana mara tatu wameshamaliza ila wanataka kuandaliwa pambano la nne, je ni sheria zipi zinazofuatwa hapo.Vyama vya ngumi za kulipwa walitazame hili kwa makini mkubwa sana tena sana, kama sheria awazijui basi waulize au waingie ktk mitandao waangalie na kufuatilia International fight na sheria zake, sio kubuluza watu na huku wanafanya madudu.

Naomba kuwakilisha!

Mdau wa boxing

Sadick Rashid Kinyogoli

Mkimbizi toka Burundi anayefanya mambo makubwa huko Coventry City.

Maajabu hutokea sana duniani na huwa yanatokea pale ambapo mtu hategemei.
Moja ya vitu ambavyo vimeiwasha Ligi daraja la kwanza nchini England maarufu kama The Coca Cola Championship ni kijana toka nchini Burundi Gael Bigirimana ambaye anachezea klabu ya Coventry City.
Hadithi ya Gael Bigirimana ilianzia kwenye Supermarket moja kwenye jiji la Coventry ambako alikwenda na kaka yake kununua vitu vya kutumia nyumbani. Wakati wakiwa Supermarket Gael alikiona kituo cha kuendelezea vipaji vya wachezaji wachanga cha Coventry na pasipo kusita alikwenda moja kwa moja hadi kwenye kituo hicho.
Siku iliyofuata Gael alikwenda kwenye kituo hicho kuomba kuandikishwa . Makocha wa kituo hicho walimuambia kuwa wana mfumo maalum wa kuandikisha watoto ambapo ni lazima mchakato wa scouting ufuatwe . Gael hakukata tamaa , alichofanya ni kuwapa makocha hao maelekezo ya shule anayosomea huku akiwa na matumaini kuwa watakuja kumtazama , wakati anaondoka mmoja wa makocha alimuuliza kama amekuja na vifaa akawaambia ndio japo alikuwa akiwadanganya.

Siku iliyofuata walimpa Gael nafasi ya majaribio na majaribio ya siku moja yalitosha kuwaridhisha juu ya uwezo aliokuwa nao na tangu wakati huo mpaka hii leo Gael amekuwa mchezaji wa Coventry City.  Baada ya miaka 7 , Gael Bigirimana akiwa na umri wa miaka 18 alipata nafasi ya kuichezea Coventry kwenye mchezo wake wa kwanza na hadi sasa ameshacheza michezo 21 akiwa kwenye kikosi cha kwanza.

 Msimu huu Gael amepewa tuzo ya mchezaji kijana bora wa mwaka baada ya kuisaidia Coventry kwa uwezo wake mkubwa akicheza nafasi ya kiungo .Gael Bigirimana ni raia wa Burundi na alienda England na familia yake kama wakimbizi . Mwenyewe anasema alianza kucheza soka nyumbani kwao huko Bujumbura na jijini Kampala ambako aliwahi kuishi kwa muda .Tangu alipocheza mechi yake ya mwisho mwezi Januari mambo yalianza kumwendea vibaya baada ya kurudishwa kwenye kikosi cha vijana walio na umri chini ya miaka 19.

Kwa mtu mwingine angeweza kuchukulia hili kama pigo lakini Gael ambaye ni muumini wa dini ya kristo anaamini kuwa wote huu ni mpango wa Mungu uliolenga kumjenga zaidi kwenye maisha .Tangu akiwa mdogo ilikuwa inajulikana kuwa angeishia kuwa mcheza soka kutokana na kipaji alichokuwa nacho na wakati anaifuata familia yake nchini England mwaka 2004 alijua kuwa hiyo ndio nafasi pekee ya kutimiza ndoto zake na hakuangalia nyuma pale alipopata nafasi yake.

Steven Gerrard Afunga Hat Trick kwenye mchezo wake 400 !

Bayern Munich yaingia Robo Fainali Uefa champions league kwa kishindo. Inter Out !!!



Azam Fc yaanza mchakato wa kutengeneza kadi za wananachama !

Chagua moja yenye BLUE au yenye NYEKENDU kisha toa maoni yako.... tupo kwenye mchakato wa kuleta kadi za uanachama.... Jisikie furaha kuwa mwana Azam FC, Timu bora bidhaa bora

Tuesday, March 13, 2012

INTER MILAN LEO KUSUKA AU KUNYOA !


Msimu wa Inter Milan kwa sasa umeegemeza matumaini yake yote kwenye Ligi ya mabingwa barani ulaya ambako hata huko hali si nzuri. Inter inaingia uwanjani usiku huu ikitafuta kugeuza matokeo ya kipigo cha 1-0 ilichokipata dhidi ya Marseile wiki tatu zilizopita.
 Matokeo ya mchezo huo hayakuakisi mchezo wenyewe ulivyokuwa kwani inter Milan iltengeneza nafasi za kutosha lakini haikuwa na bahati unaweza kusema na ni kipindi hicho hicho ambapo Inter ilikuwa kwenye wakati mgumu wakati ambao ilipoteza zaidi ya michezo mitano.
Wengi wamekuwa wakijiuliza ni wapi yalipo matatizo ya Inter huku sababu nyingi zikitolewa wengine wakisema mzimu wa Jose Mourinho , wengine wakisema kuwa makocha waliokuja na waoga na wenye hadhi ya chini kiasi cha kudharauliwa na wachezaji lakini suala la msingi ni moja Inter inahitaji mabadiliko ya kizazi chake cha sasa kwani asilimia kubwa ya wachezaji  walioko kwenye kikosi cha kwanza wanakaribia kumaliza nyakati zao kama wachezaji kwenye kiwango cha juu.
Ushindi ilioupata Ijumaa dhidi ya Chievo kwa vyovyote umerudisha hali ya ari ya ushindi kwenye kambi ya Inter hasa baada ya mfululizo wa michezo mingi bila ya kupata ushindi , lakini bado Inter inabakia kuwa klabu yenye matatizo makubwa yanahotaji kutatuliwa.Katika mchezo wa leo inter itamkosa Christian Chivu ambaye alionyeshwa kadi ya njano kwenye mchezo wa mwisho ambayo ilikuwa kadi yake ya tatu hivyo ataukosa mchezo wa leo.
 Hii inaanisha kuwa Inter watamchezesha Yuchi Nagatomo kwenye upande wa kushoto wa Defence huku Douglas Maicon akicheza upande wa kulia .Olympique Marseile wanategemea kuwarudisha Loic Remy na Mathieu Valbuena ambao walikosa mchezo wa kwanza jambo ambalo linaweza kuwatatiza Inter kwa kiasi kikubwa kutokana na ukweli kuwa hawa ndio wachezaji ambao Marseile inawategemea na wanapokuwa kwenye kikosi cha kwanza hali huwa tofauti na pale wanapokosekana. Pamoja na hao Andre Pierre Gignac na Andre Ayew na watakuwepo baada ya kupimwa na kuonekana kuwa wataweza kuhimili mchezo.
 Alou Diarra naye ataingia kwenye nafasi ya Charles Kabore huku Souleymane Diawara na Jeremy Morel nao wakirejea kwenye kikosi cha kwanza baada ya kupumzishwa .Tatizo kwa Marseile limekuwa form yao baada ya mchezo wao wa mwisho dhidi ya Inter . Marseile wamepoteza michezo minne mfululizo na ukioanisha rekodi hiyo na morali waliyo nayo Inter baada ya mchezo wa Ijumaa unaweza kuona ugumu wa mchezo ulipo.

SAKATA YA YANGA HILI HAPA !

CHEMSHA BONGO! KITAJE HIKI KIKOSI CHA YANGA ....

HAPPY BIRTHDAY : GEOFREY LEA NA EDGAR DAVIDS.

     RAZACK FORD ACHA UROHO........
  goff akimsalimia Bibi yake
  hapa yupo na mama mdogo wake,huyu mama mdogo ndiye aliyemlea ...
   NILIKUEPO PIA KULIPA SUPPORT JEMBE LANGU.
    HII NDO KEKI ........ KUNA SWALI ?
GEOFLEY LEA AKIMLISHA KEKI MAMA YAKE.

Mechi za leo , Ligi ya mabingwa .Bayern Munich na Fc Basel

Ligi ya mabingwa barani ulaya inaendelea tena usiku huu kwa michezo miwili mikali.Nchini ujerumani Bayern Munich watakuwa wenyeji wa Fc Basel toka uswisi.
Timu hizi zinaingia uwanjani hii leo kwenye mchezo ambao ni wa marudiano huku matokeo ya mchezo wa kwanza yakiwa ushindi wa 1-0 kwa Basel.Moja ya timu ambazo zimewashngaza wengi kwenye michuano ya msimu huu ni Fc Basel.
 Wakiongozwa na kinda Xherdan Shaqiri kwenye safu ya kiungo huku mbele kwenye ushambuliaji wakiwepo kina Marco Streller na Alex Frei. Basel wameingia kwenye hatua hii baada ya kuwang’oa mashindanoni Manchester United walipowafunga kwenye mchezo wa mwisho wa kundi lao. Basel hawakuishia hapo kwani wakati wengi walipokuwa wanaamini kuwa shughuli yao itaishia mikononi mwa Bayern, Basle walipata ushindi japo finyu ynumbani kwao.
Bayern Munich wamekuwa kwenye wakati mgumu kwa siku za hivi karibuni hasa kwenye ligi ya nyumbani Bundesliga ambako waliongfoza kwa muda mrefu lakini matokeo mabaya dhidi ya timu kama Borusia Dortmund na Monchengladbach yamewafanya wapoteze mwelekeo ambapo wamejikuta kwenye nafasi ya pili.
Moja ya sababu kuu za BAYERN kufanya vibaya kwenye Bundesliga ilikuwa kukosekana kwa kiungo ambaye ni mhimili kwenye timu ya Bayern Munich Bastian Schweinsteiger. Katika kipindi ambcho Bastian amekaa nje ya uwanja ndio kipindi ambacho Bayern imejikuta ikishuka hadi nafasi ya pili huku wastani wa ushindi kwenye michezo ukishuka .
Pamoja na kumkosa Bastian kufanya vibaya kwa Bayern kuliendana na kushuka kwa form ya wachezaji kama Mario Gomez , Franck Ribery na Arjen Robben.Taarifa njema kwa mashabiki wa Bayern ni kwamba wachezaji wote hawa walikuwepo jumamosi wakati Bayern wakiifunga Tsg Hoffeiheim 7-1 ambapo Gomez alifunga mabao matatu , Robben mawili na Riberry Moja.
Wachezaji wote hawa wakiwa kwenye kiwango chao cha kawaida ni dhahiri Fc Basel watapata tabu kulinda bao lao moja walilofunga kwneye mchezo wa kwanza huko uswisi.Kocha wa Bayern Jupp Heyckness anatarajiwa kupanga kikosi cha kushambulia mwanzo mwisho kutokana na ‘nature’ ya mchezo wenyewe ambapo idadi ndogo ya bao moja bila waliyofungwa ambayo wachezaji wa Bayern watakuwa wanaamini wanao uwezo wa kugeuza matokeo na kusonga mbele.
Hatari pekee ambayo Bayern wanayo ni ukweli kwamba Bastian Schweisteiger wana kadi za njano kila mmoja na wako hatarini kufungiwa endapo watapata kadi tena.Fc Basel wanayo nafasi ya kuidhuru Bayern kutokana na uwezo wao ambao wameonyesha . Hii ni timu ambayo inashambulia kwa kasi na ubunifu wa hali ya juu.
Basel imeshinda michezo yake mitatu ya mwisho kwenye michuano hii japo imefanya hivyo kwa kufunga bao moja ushindi ambao kwa hatua hii unaweza kuonekana kuwa finyu.Pamoja na hayo timu hii ya uswisi pia imeweza kupata ushindi katika michezo yake minne ya mwisho kwenye michuano yote nah ii inamaanisha kuwa bado wako kwenye form nzuri inayoweza kuwachagiza kupata ushindi.
Ushindi kwa Bayern unaweza kuwa ndio utabiri wa kila mtu bhasa ukizingatia ukweli kuwa timu hii imeshinda michezo yake 7 ya mwisho waliyocheza nyumbani.Bado Bayern wanatarajiwa kuwakosa mabeki Daniel Van Buyten na Breno pamoja na na Rafinha ambao wana majeraha.Kwa upande wa Fc Basel mchezaji pekee atakayekosekana ni mkorea Park Joo Hoo ambaye aliukosa mchezo dhidi ya Grasshoppers na Scott Chipperfield anakosekana pia.Mchezo utakuwa mgumu sana kwa Bayern Munich kwa kuwa presha yote itakuwa kwao kushinda kwani ndio wanategemewa kama Favorites na kutokana na ukweli huo Fc Basel watakuwa hatari na wanaweza kuwashangaza Bayern.

TAARIFA KUTOKA TFF!

TEMEKE UTD, SMALL KIDS KUSHUSHANA MACHI 31
Kamati ya Ligi ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) iliyokutana Dar es Salaam jana (Machi 12 mwaka huu) imeamua timu za daraja la kwanza za Temeke United na Small Kids zicheze mechi Machi 31 mwaka huu mjini Dodoma ili kupata moja itakayoshuka daraja.

Kwa mujibu wa Kanuni ya 4 ya Ligi Daraja la Kwanza timu tatu zitashuka daraja, moja kutoka katika kila kundi. Kwa vile AFC ya Arusha na Manyoni ya Singida kutoka kundi C tayari zimeshashuka, Kamati ya Ligi imeamua Temeke United na Small Kids zilizoshika nafasi ya mwisho katika makundi yao ya A na B zicheze mechi hiyo ili kupata moja itakayokamilisha idadi ya timu tatu za kushuka daraja.

Baada ya kumalizika hatua ya kwanza ya Ligi Daraja la Kwanza, timu tisa zimefanikiwa kucheza hatua ya fainali ya Tisa Bora na nyingine tano za Burkina Faso ya Morogoro, Morani ya Manyara, Polisi ya Iringa, Majimaji ya Songea na Green Warriors (94KJ) zimefanikiwa kubaki Ligi Daraja la Kwanza.

KITUO FAINALI LIGI DARAJA LA KWANZA
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) linaendelea kupokea maombi ya uenyeji wa kituo cha Fainali za Ligi Daraja la Kwanza iliyopangwa kuanza Machi 31 mwaka huu ikishirikisha timu tisa.

Mikoa kadhaa imeshawasilisha maombi ya uenyeji lakini hakuna ambao umekamilisha masharti ya kulipa sh. milioni 25 TFF ikiwa ni gharama za uendeshaji wa fainali hizo.

Baadhi ya mikoa ambayo imeshatuma maombi ya kuwa mwenyeji wa fainali hizo ni Mbeya, Morogoro, Mwanza, Ruvuma na Tabora. Kamati ya Ligi itatangaza kituo cha fainali hizo baada ya Machi 15 mwaka huu ambayo ni siku ya mwisho kupokea maombi na kutimiza masharti yaliyowekwa.

Timu zilizofuzu kucheza hatua ya fainali kutoka kundi A ni Polisi ya Dar es Salaam, Mgambo Shooting ya Tanga na Transit Camp ya Dar es Salaam. Kundi B ni Mbeya City Council, Mlale JKT ya Ruvuma na Tanzania Prisons ya Mbeya wakati kundi C ni Polisi ya Tabora, Polisi ya Morogoro na Rhino Rangers ya Tabora.

KAMATI YA LIGI YAADHIBU WACHEZAJI 5 YANGA
Kamati ya Ligi ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) iliyokutana Dar es Salaam jana (Machi 12 mwaka huu) imetoa adhabu kwa klabu mbalimbali na wachezaji sita wakiwemo watano wa Yanga.

Villa Squad imepigwa faini ya sh. 500,000 baada ya washabiki wake kufanya vurugu kwenye mechi namba 122 dhidi ya Azam iliyochezwa Februari 15 mwaka huu Uwanja wa Chamazi. 

Pia klabu hiyo imepigwa faini ya sh. 300,000 kwa kuchelewa uwanjani kwenye mechi namba 129 dhidi ya Mtibwa Sugar iliyochezwa Februari 19 mwaka huu Uwanja wa Manungu. Adhabu hiyo ni kwa mujibu wa Kanuni ya 8(13) ya ligi hiyo.

Nayo Yanga imepigwa faini ya sh. 500,000 kutokana na washabiki wake kufanya vurugu kwenye mechi namba 132 dhidi ya Azam iliyochezwa Machi 10 mwaka huu. Pia klabu hiyo imepigwa faini ya sh. 500,000 kwa mujibu wa Kanuni ya 25(d) baada ya kuoneshwa kadi kuanzia tano kwenye mechi hiyo.

Mchezaji Juma Mohamed wa Polisi Dodoma amefungiwa mechi tatu na kupigwa faini ya sh. 500,000 baada ya kuwashambulia watazamaji kwa chupa ya maji katika mchezo namba 114 kati ya timu yake na Villa Squad uliochezwa Februari 11 mwaka huu.

Nadir Haroub ‘Cannavaro’ wa Yanga amefungiwa mechi sita za Ligi Kuu na kupigwa faini ya sh. 500,000 baada ya kuoneshwa kadi nyekundu kwa kosa la kumshambulia mwamuzi Israel Nkongo kwenye mechi hiyo namba 132.

Wachezaji wengine wa Yanga walioadhibiwa kutokana na mechi hiyo ni Nurdin Bakari amefungiwa mechi tatu na faini ya sh. 500,000, Omega Seme amefungiwa mechi tatu na faini ya sh. 500,000, Jerryson Tegete amefungiwa miezi sita na faini ya sh. 500,000.

Stephano Mwasika amefungiwa mwaka mmoja na faini ya sh. milioni moja kwa kumpiga mwamuzi Nkongo. Adhabu zote zimetolewa kwa mujibu wa Kanuni za Ligi Kuu.

Kamati ya Ligi imempongeza nahodha wa Yanga, Shadrack Nsajigwa na mshambuliaji wa timu hiyo Hamis Kiiza kwa kuwa mstari wa mbele kuzuia wenzao kumshambulia mwamuzi. Pia imempongeza kocha Kostadin Papic wa Yanga kwa kukemea vurugu zilizofanywa na wachezaji wake.

Pia Kamati ya Ligi imeiagiza Sekretarieti kutoa waraka kwa makamishna wote wa ligi juu ya utaratibu wa wageni rasmi wakati wa mechi za ligi.

Powered by Sorecson : Creation de site internet
Boniface Wambura
Ofisa Habari
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)


LIGI KUU VODACOM YAINGIA RAUNDI YA 21

Ligi Kuu ya Vodacom inaingia raundi ya 21 kesho (Machi 14 mwaka huu) kwa mechi mbili ambapo mabingwa watetezi Yanga watakuwa nyumbani kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam kuikabili African Lyon. Viingilio katika mechi hiyo itakayoanza saa 10.30 jioni ni sh. 3,000 viti vya bluu na kijani, sh. 5,000 viti vya rangi ya chungwa, sh. 10,000 kwa VIP C na B wakati VIP A itakuwa sh. 15,000. Mechi nyingine ya kesho itachezwa kwenye Uwanja wa Jamhuri mjini Dodoma ambapo Simba watakuwa wageni wa timu ya Polisi Dodoma. Yanga itarejea tena uwanjani Machi 17 mwaka huu kwa pambano dhidi ya wenyeji Villa Squad litakalofanyika Uwanja wa Chamazi, Dar es Salaam wakati siku hiyo hiyo Coastal Union itacheza na Oljoro JKT kwenye Uwanja wa Mkwakwani, jijini Tanga. Machi 18 mwaka huu kutakuwa na mechi tatu ambapo Simba itakuwa ugenini Uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro dhidi ya Mtibwa Sugar, Toto African itaikaribisha Polisi Dodoma jijini Mwanza wakati Azam na Ruvu Shooting Stars zitaoneshana kazi kwenye Uwanja wa Chamazi.

UMEGUNDUA NINI KATIKA HIZI PICHA!


Haya Wadau mwangalieni TRESOR MPUTU wa TP MAZEMBE!

Jerry Tegete Afungiwa miezi sita!

Mshambuliaji wa Yanga Jerry Tegete amefungiwa kutocheza soka kwa kipindi cha miezi sita, Tegete amefungiwa kutokana na kuhusika kwenye vurugu zilizotokea kwenye mchezo wa ligi kuu ya Vodacom kati ya Yanga na Azam, Tegete amehukumiwa kwa kosa la kutoka benchi na kuingia uwanjani.
hapo jana usiku Blog hii ililipoti taarifa za Tegete na Naadir kufungiwa michezo sita,lakini leo asubuhi blog imeongea na mmoja wa wajumbe wa kamati ya mashindano ya mashindano akasema Tegete amefungiwa miezi sita na si mechi sita.

TANZANIA YAZIDI KUPOROMOKA VIWANGO VYA FIFA!

 

RnkTeamPts+/- Pos
1Spain15610Equal
2Netherlands13791Up
3Germany1332-1Down
4Uruguay12890Equal
5Brazil11572Up
6England1121-1Down
7Portugal1106-1Down
8Argentina11023Up
9Italy1062-1Down
10Croatia1049-1Down
11Denmark1025-1Down
12Russia10031Up
13Greece9531Up
14Chile950-2Down
15Côte d'Ivoire9440Equal
16France9381Up
17Sweden9261Up
18Switzerland891-2Down
19Republic of Ireland8721Up
20Australia8682Up
21Bosnia-Herzegovina850-2Down
22Mexico849-1Down
23Ghana8200Equal
24Norway7970Equal
25Paraguay7912Up
26Serbia779-1Down
27USA7724Up
28Slovenia765-1Down
29Czech Republic7620Equal
30Korea Republic7514Up

 
31Colombia7481Up
32Turkey747-7Down
33Japan740-3Down
34Peru720-1Down
35Algeria7101Up
35Slovakia7103Up
37Hungary6580Equal
38Israel651-3Down
39Ecuador6481Up
40Belgium642-1Down
41Zambia6302Up
42Mali6292Up
43Gabon6172Up
44Armenia601-3Down
44Montenegro6017Up
46Venezuela5930Equal
47Estonia5857Up
48Wales580-6Down
49Ukraine57810Up
50Panama576-1Down
51Iran574-4Down
51Scotland574-3Down
53Romania573-1Down
54Jamaica571-4Down
55Libya566-2Down
56Tunisia5640Equal
57Nigeria557-1Down
58El Salvador554-4Down
59Costa Rica5504Up
60South Africa549-2Down
61Morocco5451
1Up
62Cape Verde Islands5427Up
63Honduras533-4Down
64Egypt530-3Down
65Guinea5090Equal
66Cameroon5050Equal
67Uzbekistan50210Up
68China PR4958Up
69Belarus490-2Down
70Senegal482-2Down
71Austria4720Equal
72Haiti469-1Down
73Sierra Leone465-9Down
74Georgia4627Up
75Poland461-5Down
76Iraq4603Up
77Burkina Faso451-2Down
78Latvia444-4Down
79Canada443-8Down
80Albania432-2Down
81Angola4242Up
82Trinidad and Tobago4233Up
83Jordan420-1Down
84Finland412-5Down
85Bulgaria4063Up
86Guatemala404-2Down
87Northern Ireland400-1Down
88Qatar3888Up
88Saudi Arabia3881Up
88Uganda388-1Down
91Lithuania3832Up
2Up
92Oman3813Up
93Bahrain3734Up
94Kuwait368-3Down
95Antigua and Barbuda360-5Down
96Malawi3542Up
97Togo349-3Down
98Vietnam3472Up
99Guyana341-7Down
100Botswana3384Up
101Congo33129Up
102FYR Macedonia328-1Down
103Bermuda3212Up
104Mozambique319-2Down
105Rwanda3163Up
106Bolivia3071Up
106Zimbabwe307-7Down
108Equatorial Guinea3052Up
109St. Kitts and Nevis3018Up
110Sudan3001Up
111Korea DPR299-5Down
112Chad29329Up
113Kenya29210Up
114Niger289-3Down
115São Tomé e Príncipe28853Up
116Azerbaijan285-7Down
116Cuba2850Equal
116Faroe Islands2852Up
119New Zealand2841Up
120Congo DR281-1Down
121Iceland277-18Down
121Iceland277-18Down
122United Arab Emirates27510Up
123Gambia271-8Down
124Lebanon270-10Down
125Liberia2680Equal
126Syria267-4Down
127Benin2649Up
127Luxembourg2646Up
129Cyprus262-2Down
130Suriname254-4Down
131Central African Republic251-3Down
132Burundi25011Up
132Namibia250-12Down
134Puerto Rico249-21Down
135Dominican Republic247-6Down
136Belize238-1Down
137Grenada236-4Down
137Liechtenstein236-13Down
139Thailand235-9Down
140Ethiopia231-3Down
141Tanzania228-2Down
142Kazakhstan224-4Down
143Moldova216-1Down
144Nicaragua2110Equal
145Tajikistan210-5Down
146St. Vincent and the Grenadines188-1Down
147Indonesia160-1Down
148Malta15211Up
148Yemen152-1Down
150Samoa1491Up
150Singapore149-2Down
   152Malaysia148-2Down
153Nepal144-1Down
154Curaçao142-1Down
155Bahamas141-1Down
156Philippines1360Equal
157Fiji1332Up
158Hong Kong1325Up
158India132-4Down
160Lesotho1311Up
160Palestine1312Up
162New Caledonia1261Up
163Madagascar123-5Down
164Aruba1201Up
164Bangladesh120-7Down
166Cambodia1146Up
166Turkmenistan114-17Down
168Chinese Taipei110-2Down
168Guinea-Bissau110-2Down
170Barbados107-1Down
171Mongolia106-1Down
172Vanuatu1031Up
173Laos96-2Down
174Dominica952Up
174Maldives951Up
176Tonga881Up
177Myanmar86-3Down
178Afghanistan850Equal
179Swaziland830Equal
180US Virgin Islands820Equal
181Pakistan760Equal
0Equal
182Solomon Islands750Equal
183Tahiti731Up
184Cayman Islands721Up
185St. Lucia651Up
186Sri Lanka62-4Down
187American Samoa610Equal
188Comoros550Equal
189Seychelles470Equal
190Eritrea450Equal
191Somalia430Equal
192Kyrgyzstan390Equal
193Guam360Equal
194Papua New Guinea340Equal
195Mauritius320Equal
196Cook Islands281Up
197British Virgin Islands231Up
197Djibouti231Up
199Macau20-3Down
200Anguilla90Equal
201Bhutan60Equal
201Brunei Darussalam60Equal
203Mauritania40Equal
204Timor-Leste20Equal
205Andorra00Equal
205Montserrat00Equal
205San Marino00Equal
205Turks and Caicos Islands00Equal