Search This Blog

Wednesday, March 14, 2012

VILLA SQUAD YAPINGA KIWANJA CHAKE KUVAMIWA na kampuni ya SMEC International ya nchini Australia !

...Kuna ule usemi wa Waswahili wa Pwani ya Afrika ya Mashariki usemao Fedha ni sabuni ya roho na mwenye nazo hashindwi na lolote anaweza kuhamisha Hata mito na milima popote atakapo….
Pengine usemi huu ndio ambao umetumiwa na Uongozi wa kampuni ya SMEC International yenye makao yake makuu nchini Australia kwa kuamua kupinga agizo la Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dr.Jakaya Kikwete la kuwataka wawekezaji wote kuacha mara moja kujenga kwenye viwanja vya Jangwani kwaajili ya kuwapa nafasi timu ya Villa Squad kuutumia uwanja huo.
Kauli hiyo ya JK ambayo aliitoa katikati ya Mwezi wa nne mwaka jana,ilikuja baada ya mashabiki wa klabu hiyo kutaka kuandamana hadi Ikulu kumueleza Rais kero yao hiyo…
Lakini Hali hiyo imejitokeza tena hii leo ikiwa ni mwaka mmoja baada ya kauli ambapo kundi la Mashabiki wa klabu hiyo yenye maskani yake Magomeni Jijini DSM kuwalalamikia wawekezaji hao na kuwataka kuondoka kwenye eneo hilo la Uwanja….Lakini wadosi hawa wao wanadai wana vibali maalumu vya kufanya kazi hiyo ya ujenzi wa kituo cha mabasi yaendayo mwendo wa kasi kutoka Serikalini…


 Mashabiki wa Villa Squad ya Magomeni wakiwa hawaamini kama uwanja wao wa mazoezi umepitiwa na Greda.



  Kifusi kikiwa kimemwagwa kwenye Uwanja wa Villa Squad.

      Mwenyekiti wa kamati ya Mashindano ya Villa Squad Bw Idd Godigodi Akizungumzia namna walivyofadhaishwa na kitendo wakala wa barabara nchini Tanroads kugomea agizo la Serikali kutoruhusu viwanja hivyo vilivypo maeneo ya Jangwani jijini Dar E s Salaam na kuipa tender kampuni ya SMEC International.

No comments:

Post a Comment