Na kuelekea michezo ya olimpiki ambayo kwa mwaka huu itafanyika huko London , Uingereza , Rais wa Kamati ya kimataifa inayosimamia michezo hiyo yaani THE NTERNATIONAL OLYMPIC COMMITEE au I.O.C mcanada JACQUES ROGGE ameelezea kukerwa kwake na Tabia ya wanamichezo kubadili uraia wao ili wapate nafasi ya kushiriki michezo hiyo.
ROGGE ametoa dukuduku lake juu ya kubadili uraia kwenye Mkutano wa siku mbili wa bodi ya Kamati Yake ambapo Moja ya agenda kuu ilikuwa uraia kwa wanamichezo , katika mkutano huo MWanariadha Yamile Aldama ambaye ni mzaliwa wa Cuba na mwendesha baiskeli ambaye ni mzaliwa wa Ujerumani Philip Hindes wa Waliidhinishwa Kuiwakilisha Uingereza kwenye michezo a mwaka huu ya olimpiki inayotarajiwa kuanza mwezi agosti .
No comments:
Post a Comment