Search This Blog

Wednesday, March 14, 2012

Kibarua kigumu cha Chelsea dhidi ya Napoli.


Wiki iliyopita dunia ilishuhudia msisimko wa dakika 90 toka kwa Arsenal iliyokuwa inatafuta kufanya maajabu ya kugeuza matokeo ya kipigo cha mabao manne bila walichopewa kwenye mchezo wa kwanza dhidi ya AC Milan .Almanusra wafanye hivyo baada ya kupata mabao matatu ya haraka kwenye kipindi cha kwanza .Ugumu uliokuwa unaizunguka mechi ya Arsenal ulionekana kwenye kipindi cha pili ambapo Arsenal ilikosa mpango mbadala huku wachezaji wakiwa wamechoka .
 Upande wa pili Milan ni kama walitengeneza wenyewe tatizo lililowasababishia kufungwa mabao matatu kwenye kipindi cha kwanza .Leo timu nyingine ya London itajaribu kutekeleza kibarua ambacho kwa macho ya haraka kinaonekana rahisi kuliko cha Arsenal dhidi ya Milan.Chelsea wanaingia uwanjani kuwakaribisha Napoli huku wakijaribu kugeuza ubao wa matokeo utakaokuwa unasoma 1-3 dhidi yao .Mara ya mwisho wakati Chelsea waliposafiri hadi Italia kucheza na Napoli makosa ya kiufundi ya aliyekuwa kocha Andre Villas Boas yaliigharimu Chelsea vibaya.
AVB aliona busara kuwapanga Ramires na Raul Meireles kwenye midfield na kumuacha Michael Essien na aliona ni vyema kumpanga beki wa kulia Jose Bosingwa kushoto na kumuacha Ashley Cole ambaye siku hiyo aliapia miungu yake yote kuwa yuko fit benchi.Upangaji mbovu wa kikosi hiki uliiua Chelsea na matokeo yake ni mabadiliko ambayo yanapelekea leo hii Roberto Di Matteo kuongoza mechi yake ya kwanza ya Champions League.3-1 si matokeo ya kutisha kama ilivyokuwa 4-0 ya Arseanl , lakini ukitazama kasi waliyo nayo Napoli kwa sasa tofauti na kasi waliyokuwa nayo Milan siku wlaiyocheza na Arsenal na kufungwa 3-0 ndio utakapoona ugumu wa mchezo wa leo .
Walter Mazzari kwa vyovyote hatafanya makosa aliyoyafanya Allegri na zaidi ya hayo Napoli hawana tatizo la kukosa mfumo mmoja husika wa kuutumia ambao unawaruhusu kuwa-accommodate wachezaji wao bora kwenye nafasi zao bora . Edinson Cavani anajulikana kuwa ndiyo anayeongoza mashambulizi huku akipewa support na Ezequiel Lavezzi , nyuma ya wachezaji hawa kuna viungo Gokan Inler na Marek Hamsik. Kilichotokea kwenye mchezo wa kwanza ndio ambacho kimekuwa kikitokea karibu msimu mzima . Kokote ambako Napoli imeshinda , mchango mkubwa wa ushindi umetokana na either bao au mabao ya mmojawapo kati ya Lavezzi na Cavanni huku mwingine akitoa Assist.
Wiki tatu zilizopita Lavezzi alipiga mbili huku mojawapo likitengenezwa na Cavanni na bao alilofunga Cavanni mwenyewe lilitengenezwa na Lavezzi .Tatizo ambalo wanalo Napoli wanalo ni kwenye Defense ambayo mara nyingi huwa ina tatizo la kupoteza focus au concentration ambayo kwa lugha ya kiswazi tunaweza kusema wana tatizo la kuzubaa nah ii mara nyingi huwa inatokana na ukweli kuwa timu nyingi ambazo zinajulikana kwa kuwa na wachezaji hatari kwenye upande wa pili wa uwanja lina matatizo ya focus kwenye defense kwani mara nyingi falsafa ya tufunge moja tukufunge matatu huwa inaathiri na pia mara nyingi timu inakuwa inashambulia kiasi cha mabeki kutokuwa mchezoni .
Ndio maana Chelsea walianza kufunga kwenye mchezo wa kwanza uliozikutanisha timu hizi kina Paolo Canavarro na kipa wao Morgan De Sanctis waliruhusu bao la mapema ambalo liliwakuta wamezubaa.Kwa upande wa Chelsea kuanzia kwenye safu ya ushambuliaji kuna tatizo kubwa . Hadi sasa kwa msimu huu ukiachilia mbali dogo Daniel Sturidge hakuna mshambuliaji yoyote wa Chelsea ambaye unaweza kusema yuko kwenye form msimu huu na ndio maana kati ya Didier Drogba na Fernando Torres hakuna magoli , si kwa kuwachanganya wote wawili au hata mmoja wao.Nguvu kwa upande wa Chelsea hasa kwenye mechi dhidi ya timu za daraja la kawaida imekuwa mabao yanayofungwa na mabeki ambako watu kama David Luiz na Gary Cahil wote wana uwezo mkubwa wa kufunga mabao na kwa beki nahodha ambaye amerejea John Terry naye ana uwezo mkubwa wa kufunga .
Safu ya kiungo hasa kwa mhispania Juan Matta ndio hasa mahali ambako Chelsea wanaweza kujivunia mchezaji anayeweza kubadilisha matokeo. Kama kuna matumaini ya Chelsea kubadili ubao wa matokeo leo ni kupitia kwa Juan Matta , uwezo wake wa kutoa pasi za mwisho na hata wakati mwingine kufunga iwe kupitia mipira iliyokufa au hata mabao ya mashuti ya mbali Matta anao uwezo huo. Viungo wengne kama Frank Lampard na Michael Essien wanaweza kuchezeshwa leo lakini kwa Frank Lampard huu si mchezo wake , Chelsea inaweza kufaidika zaidi kama ikiwapanga John Obi Mikel , Michael Essien , Ramires na Juan Matta .
Umri alio nao Lampard kwa sasa unafanya kasi ya mchezo kama wa leo kumzidi na kuna hatari ya kuwa pedestrian kwa Chelsea kama akicheza leo.Kuna kila uwezekano kuwa Di Matteo atampanga Daniel Sturidge peke yake au na Didier Drogba ambapo Sturidge anaweza kushambulia kwa kutokea pembeni.Branislav Ivanovc , Ashley Cole , Gary Cahil na nahodha John Terry kwa vyovyote ndio watakaopangwa kwenye safu ya ulinzi baada ya kuonekana kuwa thabiti kwenye mchezo wa wikiendi dhidi ya Stoke City .Kama Chelsea watataka kushinda wanapaswa kuwakamata Napoli kwa kutumia ‘element of surprise’ .
Kuingia na kushambulia mwanzo mwisho kama walivyofanya Arsenal . Chelsea wanaweza kubadili ubao wa matokeo lakini ugumu unatokana na ukweli kuwa Napoli huenda hawatawaruhusu Chelsea kufanya hili .Bado mchezo unabakia kuwa mgumu lakini ugumu zaidi uko kwa Chelsea kwa sababu wao ndio wako kwenye ‘dis advantage position’ na uzoefu mdogo wa kocha wao Roberto Di Matteo unaweza kui-expose Chelsea kwani approach atakayoingia nayo kwenye mchezo itaamua kama Chelsea watasuka au watanyoa.

1 comment:

  1. Sikubaliani na wewe hata kidogo juu ya Lampard, na leo hii ameonyesha uwezo wake...Grogba as well..haya mambo ya analyze hivi na vile hayana ukweli wowote, Lampard bado yupo kwenye form ile ile.

    Mdau
    Washington

    ReplyDelete