Search This Blog

Tuesday, March 13, 2012

Jerry Tegete Afungiwa miezi sita!

Mshambuliaji wa Yanga Jerry Tegete amefungiwa kutocheza soka kwa kipindi cha miezi sita, Tegete amefungiwa kutokana na kuhusika kwenye vurugu zilizotokea kwenye mchezo wa ligi kuu ya Vodacom kati ya Yanga na Azam, Tegete amehukumiwa kwa kosa la kutoka benchi na kuingia uwanjani.
hapo jana usiku Blog hii ililipoti taarifa za Tegete na Naadir kufungiwa michezo sita,lakini leo asubuhi blog imeongea na mmoja wa wajumbe wa kamati ya mashindano ya mashindano akasema Tegete amefungiwa miezi sita na si mechi sita.

13 comments:

  1. Elimu kwa wachezaji,namna mabvyo wanatakiwa kuwa kioo cha jamiii ni muhimu mno.Pia klabu ziwe na wataalamu wa Saikolojia itasaidia sana kupunguza baadhi ya matukio yasiyo ya lazima

    ReplyDelete
  2. anastahili ili kurudisha nidhamu katika soka la bongo.

    ReplyDelete
  3. Sorry for my Brother Jerry! Jamani.. alikuwa bench muda.. TFF tunaomba mpunguze adhabu hii. Miezi 6!!! hii ni kuua kipaji cha mchezaji

    ReplyDelete
  4. Aaaargh kwenye ligi isiyo kuwa ya kulipwa,hv vitu nilitegemea vitokee I wish cku moja kungekuwa na kanuni znazoruhusu viongoz wa TFF kufungiwa na kulipa faini coz they are INDISCIPLINE and very DISORGANISED,Tenga na watu wako ni bure kabisa shame on you MAFISADI wa soka la Tanzania kiama chenu kinakuja....

    ReplyDelete
  5. Shaffii kafurahii balaa, nakuona tu unavyoshadadia hili sakata. Kuanzia radioni hadi kwenye TV utadhania unalipwa. Ukiendelea hivyo hutafika mbali ki-uandishi. U-simba umekuzidi. Unadiriki hadi kumpamba mwizi Wambura.......absurd!!

    ReplyDelete
  6. \wacha kipaji kife manake ameshindwa kucheza soka anaendeleza majungu

    ReplyDelete
  7. Naona sasa ni full ndondo kaka..

    ReplyDelete
  8. Kazoea huyo,mwaka jana kapiga waandishi wa habari,tatizo TFF wanaibeba sana yanga,sasa imewavua nguo.tena adhabu ndogo hiyo.

    ReplyDelete
  9. tff ndio wanaoua mpira wa nchi hii uwezi klumfungia mchezaji miezi sita au mwaka 1 kama sio kumkomoa ni nn,na hizi habari za azam fc kumuhonga mwamuzi zlikuwepo siku mbila kabla ya mechi so tff wangeanza kuchunguza hilo kwanaza je lina ukweli sio majungu na fitna tu

    ReplyDelete
  10. me na soka la bongo sasa basii bora kushabikia timu za wenzetu, tff imejaa majungu,fitina, refa aliongwa taarifa zilikuwepo, na kuna tetesi hata hapo ndani ya tff kuna watu wamehongwa kuhakikisha azam inachuki=ua nafasi mbili ktk ligi ndo mana soka linakufa..... tff ovyoooooooooo

    ReplyDelete
    Replies
    1. Acha fikra mgando wewe...
      Sasa unataka kusema refa alihongwa ili JOHN BOKO awe mwepesi kuwapita mabeki wa yanga na kufunga mabao mawili?Kuna ushahidi hapo wa refa kuhongwa?Ingekua mmefunga akakataa bao tungesema sawa.

      Kuwa muwazi tu.Siku ile gemu halikua la yanga ndo maana walijaribu kufanya Triki ya furugu ili gemu livunjike wajipange upya ila nashukuru refa aliigundua janja yao.Angeweza kutoa kadi nyekundu hata sita lakini aliamua kuwavumilia na rafu zao ili mechi ikamilike.

      Labda tubadilishe mada na tuseme uvumilivu ule wa refa kutotoa kadi nyingi ili mechi isiharibike ndo kuhongwa kwenyewe...

      Azam oyeeee??

      Nawapenda sana AZAM kwani wana lengo zuri sana na soka la tanzania.Sio kama SIMBA na YANGA miaka kibao bado wana viwanja vya mabondeni(jangwani)na vi hiace vya ASANTE WALEVI.

      Angalia AZAM.Kiwanja kama EMIRATES na basi UTONG kama madrid vile.

      Delete
  11. Kamati ya ligi imepewa mamlaka ya kushughulikia makosa ya kikanuni,yaani kuthibitisha kadi na adhabu anazotoa mwamuzi.Jerry,Mwasyika,Nurdin na Omega adhabu zao haziwezi kutolewa na kamati kwani makosa yao si ya kikanuni hivyo kamati ilitakiwa kuwapeleka kwenye kamati ya nidhamu.Angalia kamati yenyewe,wajumbe wako hivi 1.Mwenyekiti-Coastal Union,2.Makamu-Azam,Wajumbe,3.Makamu Mwenyekiti wa Simba,4.Mjumbe wa moja ya kamati za simba 5.Kiongozi wa Kagera 6.Kiongozi wa Coastal Union 7.Mjumbe-Kamati ya mashindano ya Yanga.
    JE UNATEGEMEA KAMATI HII IWE NEUTRAL WAKATI NA YENYEWE INAWANIA NAFASI ZA JUU KWENYE LIGI? COMPOSITION YA WAJUMBE HAWA ITASEMA CHOCHOTE KUHUSU MWAMUZI WAKATI KAMATI AU SEHEMU YA KAMATI ILITUHUMIWA KUHONGE/A NA MWAMUZI SIKU MOJA KABLA YA MECHI?JE SI KAMATI HII YENYE WAJUMBE AMBAO WAMETUHUMIWA AU KUTAJWA KWENYE KESI ZA KUTOA RUSHWA.SI HAWA AMBAO SAUTI ZAO ZILINASWA WAKISHAWISHI WACHEZAJI WA TIMU PINZANI KUCHEZA CHINI YAKIWANGO?

    KAMATI HII ILITOA TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI HATA KABLA KIKAO CHAKE HAKIJAISHA NA KISHA IKATOA PRESS RELEASE NA KURUHUSU PRESS CONFERENCE KABLA WAHUSIKA YANGA HAWAJAPATA BARUA.SIJUI KAMA WATAKUWA WAMEPATA MPAKA PRE-MATCH LEO SAA NNE.IKIWA WATAKUWA HAWAJAPATA,BASI YANGA WANAWEZA KUWACHEZESHA WANAODAIWA KUFUNGIWA MAANA TAARIFA RASMI HAZITOKI KWA MAGAZETI.

    KAMATI IMEANZA VIBAYA KAZI YAKE,HAINA WEREDI NA UADILIFU NA SIDHANI KAMA INA UWEZO WA KUTUVUSHA KWENDA LIGI HURU.

    SITETEI VITENDO VYA KUMPIGA MWAMUZI,HAVIKUBALIKI LAKINI SITETEI UOZO WA RUSHWA KATIKA LIGI YETU.IMAGINE MCHEZAJI ANAFANYA MAZOEZI MWEZI MZIMA HALAFU ANASHUHUDIA JUHUDI YAKE IKIPORWA NA MTU ALIYESIMAMA KATI...UCHUNGUZI WA KINA UNATAKIWA ILI BADALA YA KUSHUGHULIKIA MATOKEO TUSHUGHULIKIE CHANZO.JIULIZE,TIMU AMBAYO MSIMU ULIOPITA ILIMALIZA LIGI BILA KUPATA KADI NYEKUNDU INAPATA KADI LUKUKI KTK MECHI MOJA.JIULIZE TIMU INAPOAJIRI MTU NA KUMPA NAFASI YA AFISA WA FITINA!TIMU HIYOHIYO MATOKEO YAKE/UAMUZI WA MECHI ZINAZOIHUSU UNATILIWA SHAKA NA TIMU INAZOCHEZA NAZO.

    ReplyDelete
  12. such a talent going wasted as a result of that it underpins our national team development.

    ReplyDelete