Ligi ya mabingwa barani ulaya inaendelea tena usiku huu kwa michezo miwili mikali.Nchini ujerumani Bayern Munich watakuwa wenyeji wa Fc Basel toka uswisi.
Timu hizi zinaingia uwanjani hii leo kwenye mchezo ambao ni wa marudiano huku matokeo ya mchezo wa kwanza yakiwa ushindi wa 1-0 kwa Basel.Moja ya timu ambazo zimewashngaza wengi kwenye michuano ya msimu huu ni Fc Basel.
Wakiongozwa na kinda Xherdan Shaqiri kwenye safu ya kiungo huku mbele kwenye ushambuliaji wakiwepo kina Marco Streller na Alex Frei. Basel wameingia kwenye hatua hii baada ya kuwang’oa mashindanoni Manchester United walipowafunga kwenye mchezo wa mwisho wa kundi lao. Basel hawakuishia hapo kwani wakati wengi walipokuwa wanaamini kuwa shughuli yao itaishia mikononi mwa Bayern, Basle walipata ushindi japo finyu ynumbani kwao.
Bayern Munich wamekuwa kwenye wakati mgumu kwa siku za hivi karibuni hasa kwenye ligi ya nyumbani Bundesliga ambako waliongfoza kwa muda mrefu lakini matokeo mabaya dhidi ya timu kama Borusia Dortmund na Monchengladbach yamewafanya wapoteze mwelekeo ambapo wamejikuta kwenye nafasi ya pili.
Moja ya sababu kuu za BAYERN kufanya vibaya kwenye Bundesliga ilikuwa kukosekana kwa kiungo ambaye ni mhimili kwenye timu ya Bayern Munich Bastian Schweinsteiger. Katika kipindi ambcho Bastian amekaa nje ya uwanja ndio kipindi ambacho Bayern imejikuta ikishuka hadi nafasi ya pili huku wastani wa ushindi kwenye michezo ukishuka .
Pamoja na kumkosa Bastian kufanya vibaya kwa Bayern kuliendana na kushuka kwa form ya wachezaji kama Mario Gomez , Franck Ribery na Arjen Robben.Taarifa njema kwa mashabiki wa Bayern ni kwamba wachezaji wote hawa walikuwepo jumamosi wakati Bayern wakiifunga Tsg Hoffeiheim 7-1 ambapo Gomez alifunga mabao matatu , Robben mawili na Riberry Moja.
Wachezaji wote hawa wakiwa kwenye kiwango chao cha kawaida ni dhahiri Fc Basel watapata tabu kulinda bao lao moja walilofunga kwneye mchezo wa kwanza huko uswisi.Kocha wa Bayern Jupp Heyckness anatarajiwa kupanga kikosi cha kushambulia mwanzo mwisho kutokana na ‘nature’ ya mchezo wenyewe ambapo idadi ndogo ya bao moja bila waliyofungwa ambayo wachezaji wa Bayern watakuwa wanaamini wanao uwezo wa kugeuza matokeo na kusonga mbele.
Hatari pekee ambayo Bayern wanayo ni ukweli kwamba Bastian Schweisteiger wana kadi za njano kila mmoja na wako hatarini kufungiwa endapo watapata kadi tena.Fc Basel wanayo nafasi ya kuidhuru Bayern kutokana na uwezo wao ambao wameonyesha . Hii ni timu ambayo inashambulia kwa kasi na ubunifu wa hali ya juu.
Basel imeshinda michezo yake mitatu ya mwisho kwenye michuano hii japo imefanya hivyo kwa kufunga bao moja ushindi ambao kwa hatua hii unaweza kuonekana kuwa finyu.Pamoja na hayo timu hii ya uswisi pia imeweza kupata ushindi katika michezo yake minne ya mwisho kwenye michuano yote nah ii inamaanisha kuwa bado wako kwenye form nzuri inayoweza kuwachagiza kupata ushindi.
Ushindi kwa Bayern unaweza kuwa ndio utabiri wa kila mtu bhasa ukizingatia ukweli kuwa timu hii imeshinda michezo yake 7 ya mwisho waliyocheza nyumbani.Bado Bayern wanatarajiwa kuwakosa mabeki Daniel Van Buyten na Breno pamoja na na Rafinha ambao wana majeraha.Kwa upande wa Fc Basel mchezaji pekee atakayekosekana ni mkorea Park Joo Hoo ambaye aliukosa mchezo dhidi ya Grasshoppers na Scott Chipperfield anakosekana pia.Mchezo utakuwa mgumu sana kwa Bayern Munich kwa kuwa presha yote itakuwa kwao kushinda kwani ndio wanategemewa kama Favorites na kutokana na ukweli huo Fc Basel watakuwa hatari na wanaweza kuwashangaza Bayern.
No comments:
Post a Comment