Search This Blog

Tuesday, March 13, 2012

INTER MILAN LEO KUSUKA AU KUNYOA !


Msimu wa Inter Milan kwa sasa umeegemeza matumaini yake yote kwenye Ligi ya mabingwa barani ulaya ambako hata huko hali si nzuri. Inter inaingia uwanjani usiku huu ikitafuta kugeuza matokeo ya kipigo cha 1-0 ilichokipata dhidi ya Marseile wiki tatu zilizopita.
 Matokeo ya mchezo huo hayakuakisi mchezo wenyewe ulivyokuwa kwani inter Milan iltengeneza nafasi za kutosha lakini haikuwa na bahati unaweza kusema na ni kipindi hicho hicho ambapo Inter ilikuwa kwenye wakati mgumu wakati ambao ilipoteza zaidi ya michezo mitano.
Wengi wamekuwa wakijiuliza ni wapi yalipo matatizo ya Inter huku sababu nyingi zikitolewa wengine wakisema mzimu wa Jose Mourinho , wengine wakisema kuwa makocha waliokuja na waoga na wenye hadhi ya chini kiasi cha kudharauliwa na wachezaji lakini suala la msingi ni moja Inter inahitaji mabadiliko ya kizazi chake cha sasa kwani asilimia kubwa ya wachezaji  walioko kwenye kikosi cha kwanza wanakaribia kumaliza nyakati zao kama wachezaji kwenye kiwango cha juu.
Ushindi ilioupata Ijumaa dhidi ya Chievo kwa vyovyote umerudisha hali ya ari ya ushindi kwenye kambi ya Inter hasa baada ya mfululizo wa michezo mingi bila ya kupata ushindi , lakini bado Inter inabakia kuwa klabu yenye matatizo makubwa yanahotaji kutatuliwa.Katika mchezo wa leo inter itamkosa Christian Chivu ambaye alionyeshwa kadi ya njano kwenye mchezo wa mwisho ambayo ilikuwa kadi yake ya tatu hivyo ataukosa mchezo wa leo.
 Hii inaanisha kuwa Inter watamchezesha Yuchi Nagatomo kwenye upande wa kushoto wa Defence huku Douglas Maicon akicheza upande wa kulia .Olympique Marseile wanategemea kuwarudisha Loic Remy na Mathieu Valbuena ambao walikosa mchezo wa kwanza jambo ambalo linaweza kuwatatiza Inter kwa kiasi kikubwa kutokana na ukweli kuwa hawa ndio wachezaji ambao Marseile inawategemea na wanapokuwa kwenye kikosi cha kwanza hali huwa tofauti na pale wanapokosekana. Pamoja na hao Andre Pierre Gignac na Andre Ayew na watakuwepo baada ya kupimwa na kuonekana kuwa wataweza kuhimili mchezo.
 Alou Diarra naye ataingia kwenye nafasi ya Charles Kabore huku Souleymane Diawara na Jeremy Morel nao wakirejea kwenye kikosi cha kwanza baada ya kupumzishwa .Tatizo kwa Marseile limekuwa form yao baada ya mchezo wao wa mwisho dhidi ya Inter . Marseile wamepoteza michezo minne mfululizo na ukioanisha rekodi hiyo na morali waliyo nayo Inter baada ya mchezo wa Ijumaa unaweza kuona ugumu wa mchezo ulipo.

No comments:

Post a Comment