Kupambanisha boxers zaidi ya mara tatu ni makosa kisheria, hapa kwetu tunafanya kwa kutojua sheria au kwa mapromoter kutengeneza pesa.
Wadau tumeliona ilo na tukiendelea kukaa kimya tutalitia aibu Taifa.International fight zote zinaruhusu re-match na grand final after re-match, mfano Manny Pacquiao vs Erick Morales game ya kwanza alipigwa Many paquiao kwa points, akaomba re-match akashinda Manny Pac kwa KO round ya kumi.
Elick Morales akaomba grand final re-match akapigwa KO round ya 3, akataka tena re-match sheria zikambana mpaka leo anataka kurudiana na Manny Pac ila walishamaliza three times fighting.Mfano mwingine Manny Pacquiao vs Juan Manuel Marquez game ya kwanza draw, ikaja re-match akashinda Manny pac kwa points, Marquez akaomba grand final re-match ikapigwa akashinda Manny pac kwa pints ilikua very close fight, mpaka leo wanataka re-match ila sheria za boxing zinawabana haiwezekani tena.Riddic Bowe vs Evender Holifield zimepigwa three times, moja draw mbili alipigwa Evander, na Evander alitaka re-match ikashindikana kwa kuwa walishamaliza zile three times fighting na awawezi kupigana tena.
Na mifano mingi tu ila hiyo michache inatosha.Hapa kwetu tumeshuudia boxers wakipigana zaidi ya mara saba na watu kwa kutojua sheria wanaona ni jambo la kawaida ila ni makosa kisheria, vyama vyetu vya ngumi PST, TPBO, TPBC ect, baadhi vinajua hilo na baadhi havijui hilo kabisa. Ni makosa kupiganisha watu zaidi ya mara tatu.Rashid Matumla vs Maneno Osward wamepigana zaidi ya mara 5 au 6 na bado wanataka kupigana tena je hapo sheria zinafutwa au wanatubuluza???????Francis Cheka vs Rashid Matumla wameshapigana zaidi ya mara 4 na bado kuna plan ktk mwaka huu kuwapiganisha tena.Mada Maugo vs Francis cheka, walipigana PTA akapigwa Maugo, akaomba re-match zikapigwa Morogoro Jamuhuri akapigwa tena Maugo, sasa wameingia ktk grand final zitapigwa tena April tunaomba game hii iwe ya mwisho kwao la sivyo tutawashtaki mapromoter na chama chochote kitakachotoa kibali kwa ajiri ya fight nyingine baada ya hii ya April.
Mbwana Matumla vs Francis Miyeyusho wameshapigana mara tatu wameshamaliza ila wanataka kuandaliwa pambano la nne, je ni sheria zipi zinazofuatwa hapo.Vyama vya ngumi za kulipwa walitazame hili kwa makini mkubwa sana tena sana, kama sheria awazijui basi waulize au waingie ktk mitandao waangalie na kufuatilia International fight na sheria zake, sio kubuluza watu na huku wanafanya madudu.
Naomba kuwakilisha!
Mdau wa boxing
Changamoto nayoiona kwenye mchezo huu ni utitiri wa vyombo vinavyosimamia mchezo wenyewe. Kiukweli sijawahi kuona mchezo wenye taasisi nyingi zenye majukumu yanashabihiana kama mchezo huu. Na hili linaanzia kutoka levo ya kidunia moja kwa moja hadi huku chini. Mathalani, kuna WBC, WBA, IBF, IBO, WBO, WBU na kadhalika. Kila moja ya hizi taasisi inajitegemea na ina sheria, kanuni na taratibu zinazoongoza upataji wa wanachama wake na mambo ya jumla ya kiuendeshaji. Aidha kila moja ina toa mikanda ya madaraja tofauti tofauti mf. Heavyweight, nk…
ReplyDeleteKwa hapa nchini, hali imekuwa ni vivyo hivyo, kuna taasisi kadhaa (za kiserikali na binafsi) zinazohusika kwa namna moja ama nyingine na mchezo huu. Mfano Kuna Baraza la Michezo ambalo ni mwakilishi wa serikali katika michezo, kuna taasisi binafsi kama zilizotajwa na mdau hapo kama PST, TPBO, TPBC na n.k. Katika hali kama hiyo si tu inakuwa ni vigumu kujua mipaka ya majukumu ya vyombo hivi, bali inakuwa ngumu kutambua hata uhalali wa baadhi ya vyombo hivi. Kwa upande mwingine pia ni vigumu kuona na kujiridhisha jitihada za serikali kuhakikisha mambo yanaenda sawa katika mchezo huu. Na hii ni kuanzia ngumi za ridhaa hadi hizo zinazodaiwa kuwa za kulipwa. Kuna mambo ya msingi ambayo yanapaswa kufanyiwa kazi kama kweli kuna nia ya dhati ya kuendeleza mchezo huu. Hii itasaidia kurudisha imani ya wananchi na wadau wengine hususani wadhamini, ambao kwa kiasi kikubwa ni wazi wamepoteza imani na uendeshaji wa mchezo huu.
Nina imani kama serikali ingekuwa siriaz na mchezo huu ni wazi ungeweza kuvutia uwekezaji wa uhakika na kutoa nafasi ya kuajiri vijana wengi zaidi na kuongeza pato kwa serikali. Kwa mtazamo wangu, kwa hali ya sasa wadau mbalimbali wanakatishwa tamaa na yale yanayoendelea kwenye mchezo huu. Na hali ikiachwa iendelee hivi mchezo utabaki kuwa hapohapo kama sio kurudi nyuma zaidi. Kwa waandaaji wa mapambano haya napenda kuwapongeza kwa kuendelea kusapoti mchezo huu katika mazingira hayo niliyoyaeleza, lakini naomba waandaaji hawa wasitangulize mbele maslahi na kusahau kuwa kuna sheria zinapaswa kufuatwa katika kuendesha mchezo huu. Sio mambo yanapelekwa kwa stahili ya bora liende. Mjirekebishe kwa kufuata sheria za mchezo kama ilivyoshauriwa na mdau sadiki.
Mdau.