Search This Blog

Wednesday, December 19, 2012

MANCHESTER UNITED NA SAKATA LA KUBEBWA



MIMI  AMBAYE NI MDAU WA  SPORTS EXTRA  NAPENDA  KUONGELEA  KAWAIDA  ILIYOPO  KWA  MASHABIKI  WENGI  WASIOIPENDA  UNITED  AMBAO MARA NYNGI WAMEKUWA WAKISEMA  INABEBWA,  KWA  UJUMLA  SUALA  HILI  MARA  NYINGI  HUA  NALICHUKULIA  KISHABIKI  JAPO  KUWA  HUWA  NAONA  WAO WAPO  SERIOUS.
LAKINI  KUBWA ZAIDI  WATANGAZAJI  NAO  WAMEKUA  WAKIWAUNGA  MKONO  MASHABIKI  HAO NA  HASA  WATANGAZAJI  WA  SPORTS  EXTRA  HUWA  NAWASIKIA  MARA  KWA  MARA PAMOJA NA KATIKA  SPORTS  BAR (Labda pia ni kwasababu ndio kipindi cha michezo cha redio na TV ambacho huwa nasikiliza hivyo sijui redio na TV zingine kama nao hua wanaiponda man united).
SASA HILI  LA  WATANGAZAJI  NDIO  LIMENIFANYA  NIANDIKE  WARAKA  HUU  SABABU  NYIE  NDIO  TUNAWATEGEMEA  ZAIDI  KUTUPA  ELIMU/TAARIFA  ZA  KIMICHEZO  NA  BURUDANI  KWA USAHIHI.
NILITEGEMEA  MNGEENDELEA  KUWA  TETRACICLINE  HATA  KATIKA  ANGA  ZA  KIMATAIFA  KAMA  ILIVYO  HAPA BONGO,  JAPO  KUNA  BAADHI  YA  MASHABIKI  WA  HAPA  BONGO  UPANDE  WA  MSIMBAZI  WANAWASAKAMA NYIE  HASA  SHAFII  KWAMBA  ANAFAGILIA  JANGWANI,  HAPO NAWEZA  KUWASHANGAA HAWA  MASHABIKI  KWA   KUSAHAU  KUWA  KUNA  WAKATI  HUKOHUKO  JANGWANI  SHAFII  ALISHAZUSHIWA  KUWA  ANATUMA E-MAIL  KWA  MAXIMO  ILI  MAXIMO  ASIJE  YANGA. KWAKWELI KWA HAPA BONGO NAWASIFU KWA KUWABANA WABABAISHAJI WA MPIRA  WA  BONGO  MKO  JUU NA  HAMUONYESHI  MAHABA  KWA  UPANDE  WOWOTE.
TUKIRUDI KWENYE  MADA  KUU   UNITED  KUBEBWA  NDANI  YA  EPL    
HIVI  SASA  IMEKUWA  NI  KAWAIDA  KILA  MAN UNITED  ANAPOPATA  FAIDA  KWA  MAKOSA  YA  REFA  INAONEKENA  MAN  U  KABEBWA  NA  SIO  KOSA  LA  MWAMUZI  LAKINI  MWAMUZI  HUYOHUYO  ANAPOIUMIZA  MAN  U  INAKUA  NI  KOSA  LA  MWAMUZI  NA  SIO  KWAMBA  MPINZANI  AMEBEBWA  SASA  NASHINDWA  KUELEWA  HII  TERMINOLOGY  YA  KUBEBWA  TAFSIRI  YAKE  NI  NINI?.
KUNA  MIFANO  MINGI  AMBAYO  INAONYESHA  NAMNA  AMBAVYO  UNITED  IMEKANDAMIZWA  NA  WAAMUZI  NA  MIFANO  MINGI  AMBAYO  TIMU  ZINGINE  ZIMEFAIDI  DHIDI  YA  UNITED  NA  PIA  DHIDI  YA  TIMU  ZINGINE;
1.     KOLO TOURE  ALISHAWAHI  KUDAKA  SHUTI  LA  ROONEY  NDANI  YA  MITA  6 WAKATI  KIPA  ALISHAPOTEA  NA  REFA  HAKUONA  TUKIO  HILO  UNITED  WAKAPEWA  KONA  BADALA  YA PENALT- hakuna  aliyeshika  bango
2.     FLETCHER AKIWA KTK KIWANGO BORA  ALIIKOSA  FAINALI  YA  BARCELONA  MWAKA 2009  BAADA  YA  KUPEWA  KADI  NYEKUNDU  ISIYO  SAHIHI NA PENALTI  IKAPIGWA  KTK  NUSU  FAINALI- hakuna  aliyeshika  bango
3.     DROGBA  ALISHAFUNGA  MAGOLI  YA OFF SIDE  MFANO DHIDI  YA  MAN CITY  NA  PIA DHIDI YA  MAN  UNITED  MWAKA 2009 NA  CHELSEA  WAKACHUKUA  UBINGWA  KWA POINT  MOJA  JUU YA UNITED.  hakuna  aliyeshika  bango
4.     DEMBA BA WA NEWCASTTLE  ALIZAWADIWA PENALT 28/11/2011 WAKATI  RIO  RERDINAND  HAKUCHEZA  FAULO.  hakuna  aliyeshika  bango
5.     JUZI 9/12/2012 GOLI  LA  ASHLEY YOUNG  LIMEKATALIWA  DHIDI  YA MAN CITY.  kuna  mashabiki  mpaka  leo  wanasema  Young  alikua  offside.   ILA HILI  CLOUDS  WALIZUNGUMZIA  NA  HATA  SHAFII  AME-POST  KTK  BLOG  YAKE  KUONYESHA  KUWA  YOUNG  HAKUWA  OFFSIDE  ILA  ALICHOMOZA  WAKATI  WA  KUICHEZA  RE-BOUND AMBAPO  HAPO  HAKUNA  OFFSIDE
6.     JUZI  9/12/2012  PIA  EVRA  ALINYIMWA  PENALT  KWA  FAULO  YA  KOLO  TOURE  NDANI  YA MITA  18.  hakuna  aliyeshika  bango
7.     SANT CARZOLA ALIPATA PENALT ISIYO SAHIHI DHIDI YA WEST BROM  MPAKA  KOCHA  WAKE  KAOMBA  MSAMAHA.  Angalau Wenger kaonyesha uanamichezo
8.     MATERSAKA  ALISHIKA  MPIRA  NDANI  YA  MITA 18  LAKINI  WEST BROM  HAWAKUPEWA  PENALT  WAKATI  ARSENAL  WALIPATA  PENALT  MBILI  KATIKA  MECHI  HIYO.  hakuna  aliyeshika  bango

KUTOKANA  NA  MIFANO  HIYO  MICHACHE  SIJAWAHI  KUSIKIA  MASHABIKI  AU  WATANGAZAJI  WAKISEMA  ARSENAL  AU  CHELSEA  AU  MAN CITY  KABEBWA  AU KUSIKIA  KUWA  DROGBA NI  MUOTEAJI, ILA  UTASIKIA  ‘’MAKOSA  YA  REFA’’  ‘’REFA NAE  BINADAMU’’  AU  PRESHA  ILIKUA  KUBWA  HIVYO  REFA HAKUONA.  LAKINI  KWA UNITED SABABU HUWA  SIO  PRESHA, NA  HAPO  INASAHAULIKA KABISA  KUWA  KARIBU  MECHI  ZOTE  ZA  UNITED  HUWA  PRESHA  YA  MCHEZO  IKO  JUU.

KWA  MTAZAMO WANGU;
 UNITED  INACHUKIWA  NA  WENGI  SABABU  YA  MAFANIKIO  YAKE.  NDIO  MAANA  HATA IKIFANYA  VIZURI  WATU WANATAFUTA WAPI PA KUSHIKA KAMA WAFA MAJI, KUNA KIPINDI KIKOSI  KILIKUA KINATISHA SANA  KILIKUA  KINAPIGA GOLI NYINGI KILA MPINZANI  PALE ENGLAND  BASI  WAPINZANI  UTETEZI  WAO  IKAWA  ‘’UNAMKUMBUKA  REDONDO?’’  ‘’UNAMKUMBUKA  KAKA?’’,  ‘’KIBOKO  YENU  MADRID’’  BADALA YA KUONGELEA  TIMU ZAO.  KWASASA  TIMU  INASHINDA  JAPO  HAITISHI  SANA,  SASA WANASEMA ‘’INABEBWA’’. KIFUPI  HAWAKUBALI  UKWELI  SUALA  AMBALO  SIO  UANAMICHEZO.  MCHEZAJI  AKIWA  UNITED  SIO MZURI  AKITOKA  ANAKUA  MZURI  KWA  KIWANGO KILEKILE  MFANO  MZURI NI  RONALDO  NA SASA  VAN  PERSE  ONA HATA  KWASASA  YALE  MAJINA HATUYASIKII  TENA  ‘’VAN MAGOLI’’  ‘’VAN   HAKUNAGA’’  YAMEISHIA WAPI NA KIDUME BADO ANATUPIA!  KAZIPIGA TIMU  KUBWA ZOTE MPAKA SASA.
KAKA  SHAFII  ALIKUWA NI MTU AMBAYE  ANAMFAGILIA  SANA  RVP  NA  KUMPAMBA KWA MAJINA  HAYO LAKINI  KWA SASA  KAHAMIA  KWA  FALCAO.
SIJUI  ITAKUAJE  PALE  RVP  ATAKAPOKUJA  KUWA  KAMA  TORRES  ALIVYO  SASA 
AU  SIJUI  ITAKUA  VIPI  IKITOKEA  GHAFLA  JANUARY  FALCAO  AKATUA  MAN UNITED.

UNITED INA MASHABIKI WENGI LAKINI PIA INA WAPINZANI WENGI;
SABABU WALE  WOTE  AMBAO  HUWA INAPAMBANA  NAO NA BAADAE  WAKAKATA  PUMZI WENGI WAO HUANGUKIA  KWA WAPINZANI WENGINE, MFANO MZURI  TANGU 1992 NDANI YA PREMIER LEAGUE UNITED IMEBADILI WAPINZANI WENGI. BINAFSI  NIMEANZA  KUFUATILIA KIDOGO LIGI HII MWAKA 1996 NA NIKAWA ZAIDI MWAKA 1998 MPAKA SASA.
HIVYO  KUMBUKA  KUWA  TANGU 1992 WALIKUWEPO  LIVERPOOL,  LEEDS UNITED (Kina Tonny Yeboah), BLACKBURN ROVERSE (Kina Allan Wright na Allan Shearer kabla hajaingia Newcastle mwaka 1996 kwa £15 million) , NEWCASTLE UNITED (Kina Les Ferdinand na Faustin Asprilla)  WAKAJA ARSENAL   WAKAJA CHELSEA (miaka ya 2000 baada ya kuja Abramovich) WAKAJA MAN CITY (baada ya sheikh Mansoor)
HAWA NINAOSEMA  WALIKUJA  SINA MAANA KUWA  HAWAKUWEPO  AU KWAMBA  NAWADHARAU  ILA  NI KWAMBA  WALIKUA KAMA  ASTON VILLA WASASA (yaani walikua wa kawaida tu). HII  NI DHAHIRI KUWA WALE WALIOKUA  LEEDS, NEWCASTLE NA BLACK BURN+ WALE WASIOZIJUA HIZO TIMU KAMA LEEDS  NDIO  SASA  WAKO  KWA  MAN  CITY  NA CHELSEA. NA  PIA  WAKIKIMBIA  LIVERPOOL  NA  ARSENAL  WENGI  WANAENDA HUKO(CITY NA CHELSEA).  HIVYO CHUKULIA  HAO  TU WALIOKUA TIMU  HIZO SABA WAWE DHIDI YA  UNITED  INAKUAJE  HAPO  HALI  YA  HEWA  LAZIMA  ICHAFUKE,  ACHILIA  MBALI  TIMU  ZINGINE  ZOTE  ZINAZOSHIRIKI  LIGI  KUU.

SABABU  YA  KUSEMA  TIMU HIZI  ZINAIKIMBIZA  UNITED  NI  KUWA  TANGU  1992  UNITED  INABADILISHA  WAPINZANI  WA  MBIO  ZA  UBINGWA  SABABU  IMEKUA  AKIKOSA  UBINGWA ANAKUA  WAPILI  ISIPOKUWA  MISIMU  MITATU TU (2001/2002, 2003/2004 NA 2004/2005 TU) INAMAANA HII MISIMU MITATU NDIO  ALIFANYA  VIBAYA  ZAIDI  NA  HAPA  TATIZO  KUBWA  ILIKUA  PENGO  LA  PETER  SCHMEICHEL KABLA YA KUPATA KIPA MWINGINE  MZURI,  JE  HII INAWEZEKANA  KWA  KUBEBWA  TU!?.  HAO  WABEBAJI  HAWACHOKI  KATIKA  MIAKA  YOTE  HIYO?.
 WAKATI HAWA WENYE UWEZO KAMA  LIVERPOOL  AMESHAWAHI  KUWA  WA  8 MWAKA 1993/94 NA  ARSENAL  AMESHAWAHI KUWA WA 12 MWAKA 1992  SIKUAMBII KUHUSU  CHELSEA  NA  MAN CITY.

MSAADA

IKIWEZEKANA  TUSAIDIANE  ILI  KAMA NI KWELI  TUWEZE  KUJUA   UNITED   ANATOA  NINI  ILI  KUBEBWA  AMBACHO  KINAWASHINDA   MAN  CITY, CHELSEA  AU QUEENS PARK RANGERS KUTOA  ILI  NAO WABEBWE!?

UNITED  NDANI  YA  CHAMPIONS  LEAGUE

UNITED HUYU  ANAYEBEBWA  KWENYE EPL  VIPI  KWENYE  CHAMPIONS  LEAGUE MBONA  NI BINGWA  MARA  3  NA KACHEZA  FAINALI  NYINGI TU NA ALISHAKUA BINGWA WA VILABU DUNIANI.  VIPI  HAWA  WENYE  UWEZO  WA MPIRA KAMA  ARSENAL, MAN CITY  MBONA  HATA  KOMBE HAWAJAWAHI  KUBEBA,  NA  CHAMPIONS  LEAGUE  INACHEZESHWA  NA  MAREFA  WENGI  WA  KIWANGO  CHA  JUU  WASIOTOKA  UINGEREZA KWENYE MAREFA WACHOVU KAMA WAO WASEMAVYO?.


NAOMBA  MUELEWE  KUWA  MPINZANI WA  UNITED  HAWEZI  KUISIFU  UNITED
·       HATA  MOURINHO  ALIPOKUA  CHELSEA ALIKUWA  ANAMPONDA  RONALDO  NA KUMUITA  MSHENZI  HANA  ELIMU, LAKINI  KWASASA  NDIE  ANAYEMPA  UHAKIKA  WA  KULA  FEDHA  ZA PALE SANTIAGO BERNABEU  (sio siri ndio jembe lake) NA UTAMWAMBIA  NINI KUHUSU  RONALDO.


MTANGAZAJI  ANAYEONGOZA  KWA  KULIPEPERUSHA  NENO  MBELEKO  KWA  UNITED 
NI  ALEX  LUAMBANO  SABABU  HATA  IKISHINDA  BILA  REFA  KUIPA  FAIDA  YEYE  ATAULIZA  MBELEKO  VIPI.  MFANO  KUNA  SIKU  ALIKUA  YEYE  NA  JEFF REDIONI  UNITED  ILIKUA  IMEPATA  MATOKEO  MAZURI  KTK  MECHI  KUBWA  AMBAYO SIKUMBUKI VIZURI  ILIKUA  KAMA  SIO  DHIDI  YA  ARSENAL  BASI  NI  LIVERPOOL  AU  CHELSEA  NDANI  YA  MSIMU  HUU.  JEFF  AKAWA  ANASEMA  UNITED  WANGETULIA  WANGEPATA  MAGOLI  MENGI  LAKINI  LUAMBANO   AKAWA  ANACHOMEKEA  MANENO  YANAYOMAANISHA  MBELEKO  ILIISHIA  HAPO  NDIO  MAANA  HAWAKUFUNGA  ZAIDI.
VITU  KAMA  HIVI  SIDHANI  KAMA  NI  SAHIHI  KWA NYIE  WATANGAZAJI  KUVIONGEA  HEWANI  SABABU  NI  DALILI  YA  KUONYESHA  MAHABA  YENU  KWA  HIZI  TIMU  HALI  YA  KUWA  MNATAKIWA  KUWA  NEUTRAL  PINDI  MUWAPO  HEWANI.

HAIWEZI  KUWA  RAHISI  KUWABADILI  MASHABIKI WOTE  HUKU  MTAANI  SABABU  WAKO  HURU  KUONGEA  CHOCHOTE  JAPO  WENGINE  HATA  HIZO  MECHI  HUA  HAWAANGALII  ILA  WANAONGEA  TU.

USHAURI  WANGU
·      NI  KAMA  NI  LAZIMA NENO KUBEBWA  LITUMIKE HEWANI  BASI  LITUMIKE  KWA  USAWA  PALE  MWAMUZI  ATAKAPOIPA  FAIDA  TIMU  YOYOTE BASI IWE  HIVYO  KUWA  TIMU  ILE  IMEBEBWA  NA  SIO  NENO  HILO  KUAMBATANISHWA  NA  UNITED  TU HIYO  ITAKUA SIO  FAIR.
·      WATANGAZAJI  MUWAPO  HEWANI  HAMTAKIWI  KUONYESHA  MAPENZI  YENU  KTK  TIMU YOYOTE. NA HATA UKIONYESHA KUIPONDA SANA  TIMU  FULANI WAKATI  INAFANYA VIBAYA  KUWA  TAYARI  KUISIFIA SANA  INAPOFANYA  VIZURI  KINYUME NA  HAPO  ITAKUA  NI KAMA  WEWE  UNAOMBEA IWE INAFANYA  VIBAYA  TU  ILI  UPATE CHA  KUONGEA (Yaani usiwe na uchambuzi wa kina ktk mabaya tu wakati yanapokuja mazuri ya timu hiyo unaona ni kitu cha kawaida tu, na ku-act kuwa hauko deep kwenye mambo mazuri ya timu hiyo ‘’that is not fair’’) FAIR PLAY SIO KTK PITCH PEKEE NI HATA HUKU KWENYE HABARI.    
·      NA  KUWA TUJARIBU  KUUPA  SUPPORT  MSEMO  WA  JEFF  KUWA  TUNATAKIWA  KUWAPA  HESHIMA  ZAO  WAPINZANI  PALE  WANAPOPATA  USHINDI  KWA  JUHUDI  ZAO. NA NDIO  MAANA VYAMA VYA MICHEZO  HUMWAJIBISHA MWAMUZI PALE  ANAPOCHEMSHA NA SIO TIMU ILIYOPATA FAIDA KUTOKANA NA MAKOSA YA MUAMUZI.

NINA UHAKIKA KUWA HAYA YOTE NYIE WATANGAZAJI MNAYAFAHAMU ILA HII NI KUKUMBUSHANA TU NA KUCHANGIA MAWAZO ILI HATA WASIKILIZAJI WENGINE WAWEZE KUPATA KILE WASICHOFAHAMU.  
PIA MIMI KWA UJUMLA NAOMBA MUENDELEE KUTUPATIA HABARI SAHIHI KAMA MFANYAVYO SASA. SABABU MAMBO MENGI HUWA TUNAANZA KUYASIKIA KWENU NA BAADA YA MUDA TUNAYASHUHUDIA DHAHIRI.
HUO NI UTHIBITISHO KUWA CLOUDS NI CHOMBO AMBACHO KINA WAANDISHI MAKINI NA WATANGAZAJI BORA HAPA TANZANIA KUTOKANA NA KUA NA HABARI ZA UHAKIKA KILA WAKATI.

KWA LEO NI HAYO TU.
NATANGULIZA SHUKURANI ZANGU KWENU.
MDAU-SPORTS EXTRA






SUALA LA ZANZIBAR HEROES KUFUNGIWA KUJADILIWA NA KAMATI YA NIDHAMU - MTIBWA YATINGA NUSU FAINALI YA UHAI CUP

SUALA LA AKINA MORRIS, CANNAVARO KWENDA KAMATI YA NIDHAMU
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limepokea barua ya Chama cha Mpira wa Miguu Zanzibar (ZFA) ikieleza kuwafungia wachezaji kadhaa Wazanzibari wanaochezea klabu mbalimbali za timu za Tanzania Bara na timu ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars).

Suala hilo limepelekwa kwa Kamati ya Nidhamu na Usuluhishi ya TFF kwa hatua zaidi, hivyo kwa sasa Shirikisho litasubiri uamuzi wa kamati hiyo. Baadhi ya wachezaji hao ni nahodha msaidizi wa Taifa Stars, Aggrey Morris, Nadir Haroub ‘Cannavaro’, Nassoro Masoud Cholo, Mcha Khamis, Seif Abdallah na Selemani Kassim Selembe.

MTIBWA YAINGIA NUSU FAINALI KOMBE LA UHAI
Mtibwa Sugar imekata tiketi ya kucheza nusu fainali ya michuano ya Kombe la Uhai inayoshirikisha timu za vijana wenye umri chini ya miaka 20 za klabu za Ligi Kuu ya Vodacom baada ya leo asubuhi (Desemba 19 mwaka huu) kuzamisha African Lyon mabao 3-1.

Katika mchezo huo uliofanyika Uwanja wa Kumbukumbu ya Karume, Dar es Salaam,  hadi mapumziko Mtibwa Sugar ilikuwa mbele kwa bao 1-0 lililofungwa dakika ya 22 na Hillary Kasela. Hassan Kabunda aliisawazishia African Lyon katika dakika ya 53.

Mabao mengine ya washindi yalifungwa na Godfrey Mohamed dakika ya 64 na Juma Lazio akapachika la mwisho dakika ya 87. Kwa ushindi huo, Mtibwa Sugar sasa itacheza mechi ya kwanza ya nusu fainali dhidi ya Azam ambayo nayo leo asubuhi (Desemba 19 mwaka huu) iliilaza JKT Ruvu bao 1-0 katika mchezo uliofanyika Uwanja wa Chamazi. Bao la Azam lilifungwa dakika ya 46 na Mudathiri Yahya.

Mechi hiyo ya kwanza ya nusu fainali itachezwa Ijumaa (Desemba 21 mwaka huu) saa 8 kamili mchana kwenye Uwanja wa Kumbukumbu ya Karume, Dar es Salaam. Nusu fainali ya pili nayo itachezwa kwenye uwanja huo huo kuanzia saa 10 kamili jioni.

Robo fainali ya tatu kati ya Oljoro JKT na Simba, na robo fainali ya nne zinachezwa leo saa 10 kamili jioni (Desemba 19 mwaka huu) kwenye viwanja vya Karume na Chamazi, Dar es Salaam.

Mechi ya fainali na ile ya kutafuta mshindi wa tatu zitachezwa Jumapili (Desemba 23 mwaka huu) kwenye Uwanja wa Kumbukumbu ya Karume, Dar es Salaam.

BREAKING NEWS: KOCHA WA BARCELONA TITO VILANOVA AUGUA GHAFLA NA KUACHA KAZI - BARCA WATAFUTA MBADALA


Stepping down: Barcelona coach Tito Vilanova has suffered a relapse of a tumor he had removed last November Kocha wa Barcelona Tito Vilanova anajiandaa kuachia ngazi kutoka kwenye nafasi yake ya ukocha wa Barca baada ya kurudia kuugua ugonjwa uliokuwa unamsumbua wa tezi kwenye mdomo ambalo alifanyiwa upasuaji mwaka uliopita.

Kocha huyo mwenye miaka 44 alifanyiwa upasuaji wa kuondoa uvimbe/tezi hilo mwezi November 2011 wakati alipokuwa kocha msaidizi wa klabu hiyo.

Alichukua majukumu ya kuwa kocha mkuu wa Barcelona baada ya Pep Guardiola kuachia ngazi na Vilanova akasaini mkataba wa miaka miwili.

Barcelona wametangaza kusitisha shamra shamra za sikukuu ya Krismas huku wakiwa kwenye mchakato wa kumtafuta mbadala wa Tito

RECORD ZA VILANOVA AKIWA NA BARCELONA MPAKA SASA

Pld 27 W 23 D 2 L 2 (85.18% win ratio)
Successor: Vilanova replaced Pep Guardiola (right) as Barcelona manager in the summer

KOCHA WA STARS: NIPO TAYARI KUPOTEZA KAZI KWA KUTOWACHEZESHA WATOVU WA NIDHAMU SAMATTA NA ULIMWENGU

KOCHA wa Timu ya Taifa (Taifa Stars), Kim Poulsen amesema yuko tayari kutimuliwa kazi iwapo tu msimamo wake wa kutetea nidhamu kwa wachezaji kwenye kikosi chake utakuwa kikwazo kwa wengine.
Poulsen alisema hayo wakati akizungumzia kitendo cha Mbwana Samata na Thomas Ulimwengu kuchelewa kujiunga Stars kujiandaa mchezo wa kirafiki wa kimataifa dhidi ya Zambia mwishoni mwa wiki hii.

Ulimwengu na Samata wanaocheza soka la kulipwa na timu ya TP Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, wameitwa kuja kuivaa Chipolopolo.
Poulsen alisema hana muda wa kuwabembeleza wachezaji hao, na kama ni lazima afanye hivyo ili wacheze, basi yuko tayari kuachia ngazi.
“Nasisitiza nidhamu. Timu ya Taifa siyo kitu cha mchezo.

Mchezaji hapaswi kubembelezwa kucheza timu ya taifa, yeye mwenyewe ndiye wa kufanya juhudi kwa taifa lake,” alisema Poulsen.
“Kama wanadhani ipo sababu ya mimi kuwabembeleza ndipo wacheze, ni heri nikatishe mkataba wangu kuliko kufundisha wachezaji waliokosa nidhamu,” alisema wakati akiongea na Mwananchi.


“Sina tena sababu ya kuwachezesha, siko tayari kuona wachache wanavunja nidhamu ya timu, mchezo wa soka ni pamoja na nidhamu, siyo kipaji tu.”
Kauli ya Poulsen imekuja baada ya kuulizwa kama haoni atakuwa anahatarisha kibarua chake kwa kuwaacha nyota hao, hasa ukizingatia makocha watangulizi wake walitimuliwa kwa sababu ya nidhamu mbaya ya wachezaji.


Alisema: “Moja ya falsafa yangu kama kocha mwenye taaluma ni kusimamia nidhamu ya timu. Siwezi kulea watovu wa nidhamu kwa sababu tu ya kulinda kibarua changu.
“Wachezaji wanajifunza kila siku, kuna mema na mabaya.
Kuwaruhusu Samata na Ulimwengu kuwafundisha wengine utovu wa nidhamu kwa sababu wao wanajua soka, wanacheza nje ya nchi na kupendwa na mashabiki, maana yake ni kuivuruga timu. Siko tayari.”


Aliongeza: “Uamuzi wao wa kukaa nyumbani bila kutoa taarifa, ni dharau kwa taifa lao, wachezaji wenzao, mashabiki na pia wamenidharau mimi na benchi langu lote.”
Kocha Marcio Maximo, alitanguliwa na wakati mgumu kutoka kwa mashabiki kabla ya kuondoka, kufuatia uamuzi wake wa kutowachezesha kwenye kikosi, Haruna Moshi, Athumani Idd na Juma Kaseja, huku Jan Poulsen naye akiingia matatani baada ya kumtema Samata kwa madai ya kutojituma.


Source: Mwananchi

MADA MAUGO NA MATUMLA WAJIANDAA KUFANYA MAANGAMIZI KWA WAPINZANI WAO



Kocha wa ngumi Pascal Mhagama kushoto anaemfua bondia Mbwana Matumla kwa ajili ya mpambano wake na David Chalanga wa kenya mpambano utakaochezwa Desemba 25 katika ukumbi wa Dar Live picha nawww.superdboxingcoach.blogspot.com
Bondia Mbwana Matumla kushoto akionesha ufundi wa kutupa masumbwi mbele ya kocha wake Pascal Mhagama kwa ajili ya mpambano wake na David Chalanga wa kenya mpambano utakaochezwa Desemba 25 katika ukumbi wa Dar Live picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com
Bondia Mada MAUGO AKILUKA KAMBA KWA AJILI YA MAANDALIZI YA MPAMBANO WAKE NAbondia Yiga Juma wa Uganda mpambano utakaofanyika Desemba 25 katika ukumbi wa Dar Live jijini Dar es salaam picha nawww.superdboxingcoach.blogspot.com
Kocha wa Mchezo wa Masumbwi Said Chaku kushoto akimwelekeza bondia Mada Maugo jinsi ya kutupa Ngumi wakati wa mazoezi yake ya mwisho kwa ajili ya kumkabili bondia Yiga Juma wa Uganda mpambano utakaofanyika Desemba 25 katika ukumbi wa Dar Live jijini Dar es salaam picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com
Bondia Mada Maugo kushoto akionesha umaili wa kutupa makonde na kocha wake Said Chaku wakati wa mazoezi yake ya mwisho kabla ya kupambana na bondia Yiga Juma wa Uganda Desemba 25 katika ukumbi wa Dar Live jijini Dar es salaam Picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com

PRIMETIME PROMOTIONS YATOA MILLION 105 KUFANIKISHA SHAMRA SHAMRA ZA MKUTANO MKUU WA YANGA

Pichani kulia ni Mkurugenzi wa Prime Time Promotions Ltd,Joseph Kusaga akikabidhi mfano wa hundi yenye thamani ya shilingi millioni 105 kwa uongozi wa timu ya Yanga kwa ajili ya maandalizi ya mkutano wao mkuu pamoja na mechi ya kirafiki ya kimataifa katika kukamilisha shamrashamra za kusindikiza mkutano huo wa kwanza wa uwazi wa kihistoria kwa Club ya Yanga. 
Mkurugenzi wa Prime Time Promotions Ltd,Joseph Kusaga na Makamu Mwenyekiti wa Club ya Yanga,Clement Sanga wakikabidhiana mikataba yao ya makubaliano ya kikazi.
 Mkurugenzi wa Prime Time Promotions Ltd,Joseph Kusaga akitiliana saini ya makubaliano na club ya Yanga kuhusiana na makubaliano ya timu ya Yanga  kusaini mkataba wa maelewano na kampuni ya Primetime Promotions Ltd,ambapo Prime Time Promotions imekubali majukumu ya matayarisho yote ya mkutano wa wanachama wote wa Yanga uliopangwa kufanyika Januari 19 2013.
Mkurugenzi wa Prime Time Promotions Ltd,Joseph Kusaga akifurahia jambo na baadhi ya Wanahabari mara baada ya kutiliana saini mikataba yao ya kikazi na Club ya Yanga,uliofanyika mapema leo kwenye makao makuu ya ofisi za club hiyo,Jangwani jijiini Dar
Mkurugenzi wa Prime Time Promotions Ltd,Joseph Kusaga akizungumza machache kuhusiana na makubaliano yao ya kikazi na Club ya Yanga ikiwemo sambamba na makabidhiano ya mfano wa hundi yenye thamani ya shilingi milioni 105 yaliyotolewa na kampuni ya Prime Time Promotions Ltd.
Pichani kati ni Makamu Mwenyekiti wa Club ya Yanga,Clement Sanga akizungumza mapema leo kwenye makao makuu ya timu hiyo na Waandishi wa habari kuhusiana na timu ya Yanga  kusaini mkataba wa maelewano na kampuni ya Primetime Promotions Lt,ambapo Prime Time Promotions imekubali majukumu ya matayarisho yote ya mkutano wa wanachama wote wa Yanga uliopangwa kufanyika Januari 19 2013.Kushoto ni katibu mkuu wa Yanga Lawrence Mwalusako na kulia ni Mkurugenzi wa Prime Time Promotions Ltd,Joseph Kusaga.

Aidha katika mkutano huo imeelezwa kuwa matayarisho hayo yatahusisha ukumbi na viambatanisho vyote muhimu,ikiwemo Live TV coverage na matangazo mbalimbali ya kuhamasisha mafanikio ya mkutano.


Aidha katika kuongeza mapato kwa maendeleo ya club na matayarisho ya kumalizia ligi, Prime Time Promotions Ltd,imetoa milioni 105 mapato ya uhakika kwa timu ya Yanga na Prime Time Promotions  itaandaa mechi ya kirafiki ya kimataifa katika kukamilisha shamrashamra za kusindikiza mkutano huo wa kwanza wa uwazi wa kihistoria kwa Club ya Yanga. Habari Picha na Michuzijr Blog.

PICHA YA KWANZA YA MTOTO WA MARIO BALOTELLI

Mchumba wa Mario Balotelli akiwa mtoto wao ambaye amezaliwa siku kadhaa zilizopita

CRISTIANO RONALDO ANAISHI KWENYE KIVULI CHA LIONEL 'MABAO' MESSI

Mabao 90 ndani ya mwaka mmoja. Chukua muda kufikiria uzito wa jambo hili. Lionel Messi ameweka kambani mabao hayo ndani ya mwaka 2012; anastahili kutukuzwa na kupewa sifa zote kama mchezaji bora kabisa katika kipindi hiki. Ingawa kama ambavyo Messi anavyostahili sifa kutoka kwa mashabiki, wachambuzi wa soka na wachezaji wenzake, Cristiano Ronaldo nae anafanya kazi kubwa katika kuipa mwanga wa mafanikio klabu kubwa duniani yenye maskani yake pale Santiago Bernabeu.
 
Mchezaji ghali zaidi katika historia ya soka amefunga mabao zaidi ya 169 katika miaka mitatu aliyokaa na Real Madrid; hiyo pekee ni mafanikio tosha. Messi amefunga zaidi ya hayo katika kipindi husika, na katika kipindi hicho amefanikiwa kushinda tuzo ya Ballon d'Or mara tatu huku Ronaldo akiwa ameshinda mara moja tu akiwa na klabu ya Manchester United mwaka 2008. Kuna uwezekano mkubwa Messi atashinda tena tuzo hiyo mwaka huu tena kwa haki, mabao 86 yanayoongea kila kitu. Kwa upande mwingine Ronaldo amefunga mabao machache mwakak - 63, japokuwa kwa namna nyingine mafanikio ya Ronaldo yanavutia zaidi ya Messi.

Pale Barcelona, Messi ndio star, ndio mhimili wa timu. Guardiola aliijenga Barcelona yake kumzunguka kijana huyu mfupi wa kiargentina na Vilanova amefuata mfumo huu (nani anaweza kuwalaumu?). Kila mpira unapokuwepo nje ya nusu ya uwanja wao anaangalia Messi, katika mechi  zote za kutoka kipindi kati ya November 2011 mpaka November 2012, Messi amepokea mipira mingi mara mbili zaidi ya Ronaldo alivyopokea, lakini hii inatokana zaidi na staili ya uchezaji wa Barcelona, Messi ameweza kucheza pasi zaidi ya 700 katika tatu ya mwisho ya uwanja na kujaribu kufanya dribbling zaidi ya mara 130 kuliko Ronaldo.

 Mwaka 2012 pekee, Messi alipata kupiga penati 14, ambazo ni idadi kubwa kuliko idadi kubwa zaidi ya ambazo timu yoyte ya Premier League imefanikiwa kupata katika msimu wa 2011/2012. 

Kila ambapo siku zilivyokuwa zikisogea kwa Messi kuifikia rekodi ya mabao 86, wachezaji wengi wa Barca walizungumzia matamanio yao kuona Messi akiweka rekodi hiyo. Huu ni ushahidi tosha namna magoli ya Messi yalivyoaptikana katika miezi kadhaa iliyopita, wachezaji wenzie waliweka mbele ushindi lakini pia kumpa mwenzao nafasi ya kuweka rekodi. Messi amefunga zaidi ya nusu ya mabao ya Barca katika kipindi cha miezi 12 iliyopita.

Njoo upande ya kesi ya Ronaldo ndani ya Real Madrid, anahangaika kugombea spotlight ndani ya moja ya klabu kubwa kabisa duniani. Galaticos wa Mourinho wanaundwa na watu kama Higuian na Karim Benzema katika safu ya ushambuliaji, washambuliaji wenye uchu barani ulaya. Ronaldo alifunga mabao yasiyopungua 60 katika kipindi cha 2011/2012, hii ni idadi kubwa. Benzema na Higuian wanafuatia wa pili na watatu, walifunga mabao 58. Linganisha hizi takwimu na sapoti ambayo Messi anapokea kutoka kwa wachezaji wenzake wa Barcelona kama , Fabregas na Sanchez ambao wamefunga mabao 30 kwa ujumla. Katika mwaka uliopita, Ronaldo amefunga asilimia 42 ya mabao ya Real Madrid wakati Messi amefunga asilimia 56 ya mabao ya Barcelona. 

Umuhimu na namna mabao ya wachezaji jinsi yalivyofungwa yanavutia kusoma: Messi amefunga 91% ya mabao yake katika mwaka uliopita kwa mguu wake wa dhahabu wa kushoto, wakati Ronaldo amefunga 73% ya mabao yake na mguu wake wenye nguvu zaidi wa kulia. Pia Ronaldo amefunga mabao mengi ya ushindi kuliko Messi. Asilimia 21 kwa Ronaldo dhidi ya asilimia 18 za mabao ya ushindi kwa Messi, kwa maana hiyo mabao mengi ya Muargentina huyu aliyafunga wakati mechi tayari timu yake imeshashinda. 

Ukweli ni kwamba ingekuwa Ronaldo anacheza katika kizazi kingine cha soka, angekuwa akitajwa kuwa mchezaji bora wa dunia kwa kipindi hicho. Imekuwa bahati mbaya kwa upande wa Mreno huyu ambaye amekuwa akipambana kumzidi mchezaji wa soka kwa sasa ambaye anacheza kwenye timu bora kabisa kuwahi kutokea katika ulimwengu wa soka.

Baadhi ya watu wanajaribu kusema kwamba Ronaldo ni Andy Murray wa soka, anastahili sifa zaidi lakini ana bahati mbaya ya kucheza katika kipindi kimoja na Messi na Barcelona hii ya miaka ya hivi karibuni.

Wachezaji hawa wawili siku zote wataendelea kupambanishwa; kila mshabiki wa soka ana maoni yake juu ya wachezaji hawa wawili.

Akizungumzia Messi, Pep Guardiola alisema: "Usijaribu kuandika chochte kumhusu, usijaribu kumuelezea, we mtazame tu."
Wakati Mourinho alipomzungumzia Ronaldo alisema: "Kama Messi ndio mchezaji bora wa dunia basi Ronaldo hastahili kuwepo katika hii dunia kwa ubora wake."  

Mwisho wa siku kuwafananisha wachezaji hawa kunaleta mjadala usioisha. Hivyo ni bora kukaa na kutulia kuangalia wachezaji bora kabisa katika historia ya soka wakishindana kila wiki kucheza kwa ubora mchezo ambao mabilioni ya watu tunaupenda. 

Tuesday, December 18, 2012

EXCLUSIVE: UONGOZI WA SIMBA WAITELEKEZA TIMU B, WATUMIA FEDHA ZAO ZA MAANDALIZI KULIPA GYM YA SIMBA A - WACHEZAJI KUGOMA KUINGIA UWANJANI KESHO

Baada ya kuvumilia kwa muda mrefu vitendo vya uongozi wa klabu ya Simba kutowapa huduma muhimu katika kuendesha timu ya B ya klabu hiyo, leo hii wachezaji na makocha wa timu Selemani Matola na Patrick Rweyemamu inasemekana wameamua kutoingiza timu hiyo uwanjani katika mchezo wa robo fainali ya kombe la Uhai linaloendelea katika viwanja vya Karume na Chamazi jijini Dar es Salaam.

Kwa mujibu wa chanzo cha habari kilicho karibu na timu hiyo ya Simba B kimesema uongozi wa klabu hiyo umekuwa ukiwatelekeza wachezaji wa timu hiyo kwa muda mrefu katika kuwapa mahitaji yao ya kimsingi - "Kiukweli uongozi hauna habari hata kidogo na hii timu B, wamewaachia Matola na Rweyemamu kila kitu. Wachezaji wanadai mishahara ya miezi mitatu sasa, fedha zao za ushindi wa Kombe la BancABC hawakuambulia kitu chochote. Na juzi zile fedha za maandalizi walizotoa wadhamini wa Uhai Cup, wamechukua na kwenda kulipia gym kwa ajili ya timu A huku wakishindwa kutoa hata senti tano kwa ajili ya timu husika yenye kushiriki kombe la Uhai Cup ambayo ni timu B.

"Hii ni makusudi wanayofanya uongozi sio kwamba timu haina fedha, mfano angalia jzui wametoa $40,000 na mshahara wa $2000 kwa kipa Dhaira, pia wamempa Okwi mapesa kibao lakini wanashindwa kuangalia msingi wa maendeleo ya Simba SC ambao ni timu ya pili. Rweyemamu amekuwa akijitoa sana katika kuisadia hii timu ya pili lakini sasa anashindwa kuendelea kwa sababu uongozi hauonyeshi kuwa na mapenzi ya dhati na Simba B. Timu jana ilipata aibu kubwa wakati ikitoka Chamazi - basi walilokuwa wakitembelea liliishiwa na mafuta na kupaki barabarani, hivi kweli jambo kama hilo la kuitokea timu kubwa kama ya Simba kweli? Sasa kutokana na mambo yote hayo leo hii wachezaji wanataka kugoma kwenda uwanjani kesho ili kuushinikiza uongozi kutimiza mahitaji yao." - kilimaliza chanzo cha habari.

**Kwa mtindo huu soka la Bongo litaendelea kudumaa mpaka tutakapopata viongozi wenye mapenzi na nia ya dhati ya kutaka maendeleo ya soka Tanzania****   

MADUDU YA UCHAGUZI WA DRFA! WADAU MNA MAONI GANI ?

SANTI CAZORLA APIGA HAT-TRICK ARSENAL IKIITANDIKA READING 5-2

CAZORLA NA WILSHARE

Reading vs Arsenal 2:5 MATCH HIGHLIGHTS by UCL2410

TETESI: SUNZU AIPIGA CHANGA LA MACHO SIMBA - YUPO NJIANI KUJIUNGA NA TP MAZEMBE - MDOGO AKARIBIA KUJIUNGA NA ARSENAL

Mshambuliaji mzambia, Felix Sunzu, ameizidi ujanja Simba baada ya kufanikiwa kuishawishi kwamba anaumwa na ikamwachia aende zake, lakini habari mpya ni kuwa ameibukia TP Mazembe ya DR Congo ingawa baba yake anajaribu kukataa.

Sunzu ambaye aliondoka nchini hivi karibuni kwa kisingizio kwamba Simba imwache anaumwa moyo, mdogo wake Stopila Sunzu ambaye alikuwa akiichezea Mazembe nafasi ya ulinzi wiki hii atatua Arsenal ya England kwa majaribio.

Mchezaji huyo alifanya mazungumzo ya kina na Simba akiwa sambamba na baba yake mzazi na Wekundu wa Msimbazi hao wakamruhusu akaondoka.
Lakini gazeti maarufu la michezo la Kickoff, toleo la Zambia limeripoti kwamba alikuwa na dili mbili moja ya Zanaco na nyingine TP Mazembe.

Dili ya Zanaco imeshindikana wiki iliyopita kutokana na dau lao kuwa dogo na kwamba Jumamosi aliondoka kwenda Lubumbashi, DR Congo kwa ajili ya mazungumzo ya mwisho ya mkataba na uwezekano wa kusaini ni mkubwa.

Baba yake Sunzu alipoulizwa jana Jumatatu kwa njia ya simu alisema kwa kusitasita: Hatufanya makubaliano na Mazembe kuna uwezekano wa kurudi Simba.

Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili ya Simba, Zacharia Hanspope, aliiambia Mwanaspoti kwa simu jana Jumatatu kutoka Uingereza akisema: Sisi tulimuangalia tukaona kwamba ni mgonjwa na hawezi kutufanyia kazi yoyote katika kipindi cha ligi kilichobaki ndio maana tukamuachia aende zake.
 

Hizo habari za kusajiliwa Mazembe hatujazipata rasmi lakini kama akisaini itabidi atulipe mshahara wa miezi sita aliyokuwa amebakiza kwenye mkataba wetu, kwa kuwa yeye ndiye aliomba kusitisha mkataba.
Katika hatua nyingine, beki Stopila Sunzu atatua Arsenal wiki hii baada ya kukamilisha taratibu za kupata hati yake ya kusafiria.

Mmoja wa viongozi wa Shirikisho la Soka la Zambia (FAZ) alisema: Ni kweli Sunzu (Stopila) anakwenda Arsenal, lakini hajaondoka, amekwenda Lubumbashi kukamilisha mambo yake. 

Kama Stopila akikamilisha dili hiyo atakuwa Mzambia wa pili kucheza Ligi Kuu England baada ya Emmanuel Mayuka anayecheza Southampton.


Source

KESI YA KANUMBA: LULU AEPUKA ADHABU YA KIFO - ABADILISHIWA MASHTAKA KUWA YA KUUA BILA KUKUSUDIA

MSANII Elizabeth Michael, maarufu kama Lulu, ameepuka adhabu ya kunyongwa hadi kufa kwa tuhuma za kumuua msanii mwenzake, Steven Kanumba baada ya Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP), kumbadilishia mashtaka, ambapo sasa anatuhumiwa kuua bila kukusudia.
Kutokana na mabadiliko hayo, Lulu ameepuka adhabu hiyo kwani hata kama atapatikana na hatia, adhabu yake ni kifungo cha maisha au kuachiwa huru.
Hii inatokana na kifungu cha 196 cha kanuni za adhabu ya kosa la kuua bila kukusudia, ambapo anayepatikana na hatia anaweza kuhukumiwa kifungo cha maisha, miaka kadhaa au kuachiwa huru.
Hata hivyo, baadhi ya wanasheria waliliambia gazeti hili kwamba uzoefu wa adhabu nyingi za kuua pasipo kukusudia zilizowahi kutolewa nchini, ni kati ya miaka 15 na wengine waliachiwa huru.
Lulu alifikishwa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Aprili 11, mwaka huu akikabiliwa na tuhuma za kumuua Kanumba Aprili 7, 2012.
Alikuwa akidaiwa kutenda kosa hilo kinyume na kifungu cha 196 cha Sheria ya Mwenendo wa Makosa ya Jinai (CPA), shtaka ambalo mshtakiwa anayepatikana na hatia adhabu yake ni kunyongwa hadi kufa.
Hata hivyo, jana upande wa mashtaka ulieleza mahakamani kuwa kwa sasa imebadilisha mashtaka kutoka kuua kwa kukusudia na kuwa kuua bila kukusudia, kinyume cha kifungu cha 195 cha CP.
Mshtakiwa huyo alitarajiwa kusomewa mashtaka hayo mapya jana pamoja na maelezo yote ya kesi, ambapo angesomewa ushahidi wa mashahidi wote pamoja na vielelezo muhimu katika kesi hiyo.
Hata hivyo, hatua hiyo ilikwama kutokana na Wakili wa Serikali Mwandamizi, Tumaini Kweka anayeiendesha kesi hiyo kutokuwapo mahakamani na badala yake aliwakilishwa na Wakili wa Serikali, Ofmedy Mtenga.
“Upelelezi wa shauri lako umeshakamilika na tungeweza kukusomea comital (maelezo ya kesi) leo, lakini kwa kuwa waendesha mashtaka hawapo basi tunaliahirisha mpaka tarehe nyingine.”, alisema Hakimu Mkazi Agustina Mmbando, anayesikiliza kesi hiyo katika hatua hiyo ya awali.
Taarifa hizo za kukamilika kwa ushahidi wa kesi hiyo zilipokewa kwa furaha na shangwe na msanii huyo, kiasi kwamba alishindwa kujizuia kuonyesha furaha yake.
Wakili wake Peter Kibatala aliiomba mahakama itoe ahirisho fupi hadi Ijumaa kwa ajili ya mshtakiwa kusomewa mashtaka haya mapya pamoja na maelezo ya awali.
Hakimu Mmbando alikubaliana na ombi hilo la Wakili Kibatala na akaahirisha kesi hiyo hadi Ijumaa.


Baada ya Mahakama ya Kisutu kukamilisha taratibu hizo kesi hiyo itahamishiwa Mahakama Kuu ambako ndiko itakaposikilizwa.
Lulu alipandishwa kizimbani mahakamani hapo kwa mara ya kwanza Aprili 11, 2012 na kusomewa shtaka moja la mauaji ya msanii mwenzake, Kanumba.
 Source:Mwananchi

AZAM FC YATANGAZA USAJILI WA WACHEZAJI NANE WAPYA DIRISHA DOGO - WAKENYA WAWILI, MGANDA MMOJA NA WABONGO 5

Katika kukiimarisha kikosi chake kwa ajili ya mzunguko wa pili na mashindano ya Afrika Azam FC imefanya usajili wa wachezaji nane wapya katika kipindi hiki cha dirisha dogo

Azam FC ambayo ilikuwa na wachezaji wanne wa kimataifa kufuatia George Odhiambo kuondolewa mapema kutokana na utovu wa nidhamu pia iliwapunguza wachezaji Ibrahim Shikanda na Joseph Owino na hivyo kuwa na nafasi tatu za kimataifa

Azam FC imejaza nafasi hizo kwa kuwasajili Jockins Atudo, beki wa kati wa Harambee Stars na klabu ya Tusker FC, Kiungo mshambuliaji wa Harambee Stars na Sofapaka Humphrey Mieno pamoja na mshambualiaji na mchezaji bora wa mashindano ya CECAFA Challenge Cup Brian Umony.

Pia Azam FC imemsajili kinda anayeshika nafasi ya pili kwa kufunga magoli ligi kuu akiwa na magoli sita nyuma ya Kipre Tchetche na Didier Kavumbangu wenye magoli nane kila mmoja Seif Rashid Abdallah toka Ruvu Shooting Stars
Kama hiyo haitoshi Azam FC ambayo ilikuwa na uwakilishi mkubwa zaidi kwenye mashindano ya CECAFA Challenge Cup mwaka huu kwa kuwa na wachezaji 11, imemewarudisha walinzi Malika Ndeule na Omary Mtaki waliocheza katika vilabu vya African Lyon na Mtibwa Sugar katika mzunguko wa kwanza.

Katika kuimarisha safu yake ya ulinzi pia imemsajili mlinzi wa kati wa Tanzania Prisons David Mwantika. Na kumsajili kwa mkopo winga wa Simba Uhuru Selemani.

Usajili huu umesimamiwa na mwalimu Stewart Hall mwenyewe ambaye anaamini maboresho haya yatakiongezea nguvu kikosi cha Azam FC katika mzunguko wa pili wa ligi kuu ya Vodacom inayotarajiwa kuanza januari 20.

Azam FC ipo jijini Kinshasa DRC ikijiandaa na mzunguko wa pili na mashindani ya kimataifa kwa kusaka uzoefu wa kucheza nje ya nchi na imeshacheza michezo miwili na timu za Dragons and FK Sharks ambapo ilitoka sare 1-1 mchezo wa kwanza na kufungwa mchezo wa pili 0-2.

Azam FC inatarajia kurejea nchini December 26 ambapo itaelekea visiwani Zanzibar moja kwa moja kushiriki mashindano ya Mapinduzi Cup ambayo inayashikilia.

Monday, December 17, 2012

HUYU NDIO MCHEZAJI BORA WA AFRIKA - AWAFUNIKA DROGBA, YAYA NA DEMBA BA

Christopher Katongo amechaguliwa mchezaji bora wa soka barani Afrika kwenye tuzo za BBC.

Nahodha wa timu ya taifa ya Zambia amewashinda wachezaji wakubwa barani ulaya kama Demba Ba, Didier Drogba, Younes Belhanda na Yaya Toure na kuwa mchezaji wa kwanza kushinda tuzo kutokea katika upande wa kusini mwa Afrika katika historia ya tuzo hizo.

Katongo aliambia BBC Sport: "Ni wakati mzuri zaidi kwangu. Nawashukuru watu walionipigia kura. Ni kitu ambacho sitosahau katika maisha yangu. Nilijitahidi kucheza kwa bidii na watu wameongea kupitia kura zao - huu ndio uzuri wa tuzo hii.

"Hii ina maana kubwa kwa wachezaji chipukizi ambao wananitazama mimi. Nisingeweza kufanikiwa hivi bila sapoti ya wachezaji wenzangu."

Katongo alifunga mabao matatu muhimu na kuisadia timu yake ya Zambia kutawazwa kuwa mabingwa wa AFCON 2012 katika fainali zilizofanyika katika nchi za Equatorial Guinea na Gabon, pia alifunga penati ya ushindi katika zoezi la upigaji penati dhidi ya Ivory Coast waliyocheza nayo fainali.

Miezi saba baada ya kuiongoza Zambia kushinda AFCON Katongo kwa mara nyingine alikuwa shujaa wa taifa lake baada ya kufunga goli pekee lilosaidia nchi hiyo  katika harakati za kufuzu fainali za AFCON 2013 katika mechi dhidi ya Uganda.

MARIO BALOTELLI AGOMA KUKATWA MSHAHARA WA WIKI MBILI NA CITY KAMA FAINI - AWAPELEKA MAHAKAMANI

MARIO BALOTELLI atakutana na Manchester City kwenye jopo la kisheria la majaji wa ligi kuu ya England wiki hii.

Mshambuliaji huyo wa kitaliano amezidi kujiweka kwenye wakati mgumu ndani ya klabu yake na kuweka sehemu mbaya mahusiano yake na kocha Roberto Mancini baada ya kuamua kupambana na uamuzi wa klabu yake kumpiga faini ya £340,000. 

Balotelli ameadhibiwa na City kwa rekodi yake mbaya ya utovu wa nidhamu msimu uliopita, tabia ambayo ilimfanya akose mechi 11 kwenye mechi za ligi ya nyumbani na ulaya kutokana na kusimamishwa.  

Alikata rufaa juu ya uamuzi huo ndani ya klabu lakini akashindwa na sasa ameamua kupeleka suala hilo kwenye jopo la majaji wa ligi kuu ya England.

Mshambuliaji huyo anategemewa kwenda mbele ya jopo la watu watatu siku ya jumatano. 
Balotelli ataungana na wakili wake wa kiitaliano na mwakilishi wa chama cha wanasoka wa England, wakati City wataleta timu yao ya kisheria.

City walianza hatua za kumuadhibu Balotelli kufuatiwa red card aliyoipata katika mechi dhidi ya Arsenal  mnamo mwezi wa nne mwaka huu.

NIGERIA KUANZISHA LIGI YA SOKA LA UFUKWENI

Nigeria inajipanga kuanzisha ligi ya mchezo wa soka wa ufukweni mwakani.

Mkurugenzi wa  ufundi wa shirikisho la soka la Nigeria (NFF) , Dr Emmanuel Ikpeme, amethibitisha hilo baada Supersand Eagles kuwafunga Ureno kwa 8-7 katika Copa Lagos Beach Soccer Worldwide na kufanikiwa kutetea ubingwa wa mchezo huo.

Ikpeme amesema kwamba shirikisho la soka la nchi hiyo lipo katika hatua za mwisho za maandalizi ya ligi ya soka la mchangani ndani ya mwaka 2013.

"Maandalizi ya kuanzisha ligi yameanza, lakini siwezi kukupa uhakika kwamba itaanza mapema 2013, namaanisha katika robo ya kwanza ya mwaka, inagwa itaanza mapema katikati ya mwaka," alisema Ikpeme.  

Timu ya soka ya Nigeria ya soka la ufukweni Supersand Eagles imeshashinda CAF Beach Soccer Championship mara mbili mwaka 2007 na 2009, na wameshafikia robo fainali ya FIFA Beach soccer mara mbili mwaka 2007 na 2011.


SIMBA B NJIA PANDA - AZAM, MTIBWA, COASTAL, OLJORO, RUVU NA JKT ZAFUZU ROBO FAINALI UHAI CUP

Timu sita zimeshakata tiketi ya kucheza hatua ya robo fainali ya michuano ya Kombe la Uhai inayoshirikisha wachezaji wenye umri chini ya miaka 20 (U20) wa klabu za Ligi Kuu ya Tanzania.

Hatua ya robo fainali ya michuano hiyo inayofanyika viwanja vya Karume na Chamazi, Dar es Salaam na kudhaminiwa na kampuni ya Said Salim Bakhresa kupitai maji Uhai itafanyika Desemba 19 mwaka huu kwenye viwanja hivyo hivyo.

Timu zilizofuzu kutoka kundi  A ni Coastal Union ya Tanga, Mtibwa Sugar ya Morogoro na JKT Ruvu ya Dar es Salaam. Kundi C ni Oljoro JKT ya Arusha na Ruvu Shooting ya Pwani wakati iliyofuzu kutoka kundi A hadi sasa ni Azam pekee.

Katika mechi zilizochezwa leo asubuhi (Desemba 17 mwaka huu) Coastal Union na Mtibwa Sugar zimetoka suluhu kwenye Uwanja wa Kumbukumbu ya Karume, wakati Uwanja wa Azam ulishuhudia African Lyon ikiifunga Mgambo Shooting mabao 2-1.

Nafasi mbili za robo fainali zilizobaki kutoka kundi B zinawaniwa na timu za Simba, African Lyon na Polisi Morogoro. Mechi itakayochezwa leo saa 10 jioni katika Uwanja wa Chamazi kati ya Polisi Morogoro na Simba ndiyo itakayoamua timu zitakazoungana na Azam kutoka kundi hilo.

TENGA AWASHUKURU WALIOUPITISHA WARAKA WA MAREKEBISHO YA KATIBA

Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Leodegar Tenga amewashukuru wajumbe wa Mkutano Mkuu kwa kupigia kura waraka wa marekebisho ya Katiba, kwani wametimiza wajibu wao.

Akizungumza na Waandishi wa Habari, Dar es Salaam leo, Rais Tenga amesema marekebisho ya Katiba ni jambo muhimu, lakini lazima yapate ridhaa ya wanaohusika ambao ni wajumbe.

“Nawasukuru wajumbe kwa kupitisha jambo hili. Nawashukuru wote, waliokubali na waliokataa. Ndivyo demokrasia ilivyo. Tulitaka waseme ndiyo au hapana, hivyo tulitarajia kupata majibu yoyote kati ya hayo mawili.

Marekebisho mengine yalikuwa ni maelekezo (directives) kutoka FIFA na CAF. Katiba yetu inasema tutatekeleza maagizo ya CAF na FIFA, lakini kwa misingi ya utawala bora tuliona ni lazima tupate ridhaa kutoka kwa wajumbe,” amesema.

Jumla ya wajumbe waliopiga kura kwa njia hiyo ya waraka ni 103 ambapo 70 waliunga mkono wakati waliokataa ni 33. Idadi hiyo ni asilimia 68 ya kura zote zilizopigwa, hivyo kupatikana theluthi mbili ya kura zilizopigwa ili kufanya marekebisho kikatiba.

Vipengele vilivyoingizwa katika marekebisho hayo ni ‘club licencing’ kama ilivyoagizwa na Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF), Kamati ya Rufani ya Uchaguzi wa TFF kama ilivyoshauriwa na Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA) na kuondoa nafasi ya Makamu wa Pili wa Rais.

Vilevile Kamati ya Utendaji itakutana Desemba 23 mwaka huu kufanya marekebisho ya Kanuni za Uchaguzi, kutokana na kupitishwa kwa marekebisho hayo ambayo yanaunda Kamati ya Rufani ya Uchaguzi wa TFF. Pia itachagua wajumbe wa Kamati ya Rufani ya TFF.

Mkutano Mkuu wa TFF ambapo pia utakuwa na ajenda ya uchaguzi utafanyika Februari 23 na 24 mwakani. Kwa mujibu wa Katiba ya TFF, wajumbe wanatakiwa kupewa taarifa ya Mkutano Mkuu siku 60 kabla.

MESSI ATIMIZA MABAO 90 - BARCA WAKIWATANDIKA AKINA FALCAO 4-1



Barcelona 4-1 Atletico Madrid footyroom.com by Futbol2101

HALI YAZIDI KUWA TETE KWA MOURINHO NA MADRID: YATOKA SARE BARCA IKIPAA



Real Madrid vs Espanyol 2-2 16.12.12 (All Goals) by ourmatch

Sunday, December 16, 2012

PICHA YA WIKI: WACHEZAJI WA LIVERPOOL VS SHABIKI WA EVERTON


CHELSEA YASHINDWA KUIFIKIA REKODI YA MAN U - KOMBE LA KLABU BINGWA YA DUNIA

Klabu ya Chelsea imeshindwa kuifikia rekodi ya mahasimu wao wa EPL Manchester United ya kuwa timu pekee ya England kuwahi kuchukua kombe la klabu bingwa ya dunia baada ya kufungwa kwa 1-0 na Corinthians ya Brazil.

Corinthians - Chelsea footyroom.com by footyroom

Mh Membe aitakia kila lakheri na fanaka Clouds media group kwenye shamra shamra zake za kutimiza miaka 13

div class="separator" style="clear: both; text-align: center;">
Waziri wa Mambo ya Nje na Uhusiano ya Kimataifa,Mh Bernard Membe pichani kulia akiagana na Ofisa Habari wa Clouds Media Group,Simalenga Saimon mapema leo mchana,kwenye viunga vya ofisi hizo zilizopo Mikocheni jijini Dar,Mh Membe alifika kwenye ofisi hizo kwa ajili ya kufanya mahojiano mafupi kuhusiana na mambo mbalimbali yanayoihusu wizara yake sambamba na kuitakia kheri na fanaka kampuni ya Clouds Media Group wakati ikiwa kwenye msimu wa sherehe na shamra shamra zake za kutimiza miaka 13 tangu kuanzishwa kwake.