Rais
wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Leodegar Tenga
amewashukuru wajumbe wa Mkutano Mkuu kwa kupigia kura waraka wa
marekebisho ya Katiba, kwani wametimiza wajibu wao.
Akizungumza
na Waandishi wa Habari, Dar es Salaam leo, Rais Tenga amesema
marekebisho ya Katiba ni jambo muhimu, lakini lazima yapate ridhaa ya
wanaohusika ambao ni wajumbe.
“Nawasukuru
wajumbe kwa kupitisha jambo hili. Nawashukuru wote, waliokubali na
waliokataa. Ndivyo demokrasia ilivyo. Tulitaka waseme ndiyo au hapana,
hivyo tulitarajia kupata majibu yoyote kati ya hayo mawili.
Marekebisho
mengine yalikuwa ni maelekezo (directives) kutoka FIFA na CAF. Katiba
yetu inasema tutatekeleza maagizo ya CAF na FIFA, lakini kwa misingi ya
utawala bora tuliona ni lazima tupate ridhaa kutoka kwa wajumbe,”
amesema.
Jumla
ya wajumbe waliopiga kura kwa njia hiyo ya waraka ni 103 ambapo 70
waliunga mkono wakati waliokataa ni 33. Idadi hiyo ni asilimia 68 ya
kura zote zilizopigwa, hivyo kupatikana theluthi mbili ya kura
zilizopigwa ili kufanya marekebisho kikatiba.
Vipengele
vilivyoingizwa katika marekebisho hayo ni ‘club licencing’ kama
ilivyoagizwa na Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF), Kamati ya
Rufani ya Uchaguzi wa TFF kama ilivyoshauriwa na Shirikisho la Kimataifa
la Mpira wa Miguu (FIFA) na kuondoa nafasi ya Makamu wa Pili wa Rais.
Vilevile
Kamati ya Utendaji itakutana Desemba 23 mwaka huu kufanya marekebisho
ya Kanuni za Uchaguzi, kutokana na kupitishwa kwa marekebisho hayo
ambayo yanaunda Kamati ya Rufani ya Uchaguzi wa TFF. Pia itachagua
wajumbe wa Kamati ya Rufani ya TFF.
Mkutano
Mkuu wa TFF ambapo pia utakuwa na ajenda ya uchaguzi utafanyika
Februari 23 na 24 mwakani. Kwa mujibu wa Katiba ya TFF, wajumbe
wanatakiwa kupewa taarifa ya Mkutano Mkuu siku 60 kabla.
No comments:
Post a Comment