Timu
sita zimeshakata tiketi ya kucheza hatua ya robo fainali ya michuano ya
Kombe la Uhai inayoshirikisha wachezaji wenye umri chini ya miaka 20
(U20) wa klabu za Ligi Kuu ya Tanzania.
Hatua
ya robo fainali ya michuano hiyo inayofanyika viwanja vya Karume na
Chamazi, Dar es Salaam na kudhaminiwa na kampuni ya Said Salim Bakhresa
kupitai maji Uhai itafanyika Desemba 19 mwaka huu kwenye viwanja hivyo
hivyo.
Timu zilizofuzu kutoka kundi A
ni Coastal Union ya Tanga, Mtibwa Sugar ya Morogoro na JKT Ruvu ya Dar
es Salaam. Kundi C ni Oljoro JKT ya Arusha na Ruvu Shooting ya Pwani
wakati iliyofuzu kutoka kundi A hadi sasa ni Azam pekee.
Katika
mechi zilizochezwa leo asubuhi (Desemba 17 mwaka huu) Coastal Union na
Mtibwa Sugar zimetoka suluhu kwenye Uwanja wa Kumbukumbu ya Karume,
wakati Uwanja wa Azam ulishuhudia African Lyon ikiifunga Mgambo Shooting
mabao 2-1.
Nafasi
mbili za robo fainali zilizobaki kutoka kundi B zinawaniwa na timu za
Simba, African Lyon na Polisi Morogoro. Mechi itakayochezwa leo saa 10
jioni katika Uwanja wa Chamazi kati ya Polisi Morogoro na Simba ndiyo
itakayoamua timu zitakazoungana na Azam kutoka kundi hilo.
kila la herisimba
ReplyDeleteInshalal tutashinda [hayo yalikuwa maneno ya mara kwa mara ya Marehem Mansour Magrahm, ikiiombea timu yake ya Simba SC pindi ikiwa na mechi..]
ReplyDelete