Search This Blog

Monday, December 17, 2012

NIGERIA KUANZISHA LIGI YA SOKA LA UFUKWENI

Nigeria inajipanga kuanzisha ligi ya mchezo wa soka wa ufukweni mwakani.

Mkurugenzi wa  ufundi wa shirikisho la soka la Nigeria (NFF) , Dr Emmanuel Ikpeme, amethibitisha hilo baada Supersand Eagles kuwafunga Ureno kwa 8-7 katika Copa Lagos Beach Soccer Worldwide na kufanikiwa kutetea ubingwa wa mchezo huo.

Ikpeme amesema kwamba shirikisho la soka la nchi hiyo lipo katika hatua za mwisho za maandalizi ya ligi ya soka la mchangani ndani ya mwaka 2013.

"Maandalizi ya kuanzisha ligi yameanza, lakini siwezi kukupa uhakika kwamba itaanza mapema 2013, namaanisha katika robo ya kwanza ya mwaka, inagwa itaanza mapema katikati ya mwaka," alisema Ikpeme.  

Timu ya soka ya Nigeria ya soka la ufukweni Supersand Eagles imeshashinda CAF Beach Soccer Championship mara mbili mwaka 2007 na 2009, na wameshafikia robo fainali ya FIFA Beach soccer mara mbili mwaka 2007 na 2011.


No comments:

Post a Comment