MARIO BALOTELLI atakutana na Manchester City kwenye jopo la kisheria la majaji wa ligi kuu ya England wiki hii.
Mshambuliaji huyo wa kitaliano amezidi kujiweka kwenye wakati mgumu ndani ya klabu yake na kuweka sehemu mbaya mahusiano yake na kocha Roberto Mancini baada ya kuamua kupambana na uamuzi wa klabu yake kumpiga faini ya £340,000.Balotelli ameadhibiwa na City kwa rekodi yake mbaya ya utovu wa nidhamu msimu uliopita, tabia ambayo ilimfanya akose mechi 11 kwenye mechi za ligi ya nyumbani na ulaya kutokana na kusimamishwa.
Alikata rufaa juu ya uamuzi huo ndani ya klabu lakini akashindwa na sasa ameamua kupeleka suala hilo kwenye jopo la majaji wa ligi kuu ya England.
Mshambuliaji huyo anategemewa kwenda mbele ya jopo la watu watatu siku ya jumatano.
Balotelli ataungana na wakili wake wa kiitaliano na mwakilishi wa chama cha wanasoka wa England, wakati City wataleta timu yao ya kisheria.
City walianza hatua za kumuadhibu Balotelli kufuatiwa red card aliyoipata katika mechi dhidi ya Arsenal mnamo mwezi wa nne mwaka huu.
No comments:
Post a Comment