Christopher Katongo amechaguliwa mchezaji bora wa soka barani Afrika kwenye tuzo za BBC.
Katongo aliambia BBC Sport: "Ni wakati mzuri zaidi kwangu. Nawashukuru watu walionipigia kura. Ni kitu ambacho sitosahau katika maisha yangu. Nilijitahidi kucheza kwa bidii na watu wameongea kupitia kura zao - huu ndio uzuri wa tuzo hii.
"Hii ina maana kubwa kwa wachezaji chipukizi ambao wananitazama mimi. Nisingeweza kufanikiwa hivi bila sapoti ya wachezaji wenzangu."
Katongo alifunga mabao matatu muhimu na kuisadia timu yake ya Zambia kutawazwa kuwa mabingwa wa AFCON 2012 katika fainali zilizofanyika katika nchi za Equatorial Guinea na Gabon, pia alifunga penati ya ushindi katika zoezi la upigaji penati dhidi ya Ivory Coast waliyocheza nayo fainali.
Miezi saba baada ya kuiongoza Zambia kushinda AFCON Katongo kwa mara nyingine alikuwa shujaa wa taifa lake baada ya kufunga goli pekee lilosaidia nchi hiyo katika harakati za kufuzu fainali za AFCON 2013 katika mechi dhidi ya Uganda.
Katongo hatakuwa mchezaji wa kwanza kutoka Kusini mwa Afrika kupata tuzo hiyo. Mwaka 1988 mzambia Kalusha Bwalya alikuwa mchezaji bora wa Afrika. Pia mwaka 1973 mzaire(mkongo) Tshimeni Bwanga alikuwa mchezaji bora wa Afrika.
ReplyDeleteNaamini CAF hawajatoa hii ya kusema Katongo ni mchezaji wa kwanza kutoka Kusini mwa Afrika, bila shaka itakuwa imetoka kwenye blogu za hapa hapa Bongo!