Katika
kukiimarisha kikosi chake kwa ajili ya mzunguko wa pili na mashindano
ya Afrika Azam FC imefanya usajili wa wachezaji nane wapya katika
kipindi hiki cha dirisha dogo
Azam FC ambayo ilikuwa na
wachezaji wanne wa kimataifa kufuatia George Odhiambo kuondolewa mapema
kutokana na utovu wa nidhamu pia iliwapunguza wachezaji Ibrahim Shikanda
na Joseph Owino na hivyo kuwa na nafasi tatu za kimataifa
Azam
FC imejaza nafasi hizo kwa kuwasajili Jockins Atudo, beki wa kati wa
Harambee Stars na klabu ya Tusker FC, Kiungo mshambuliaji wa Harambee
Stars na Sofapaka Humphrey Mieno pamoja na mshambualiaji na mchezaji
bora wa mashindano ya CECAFA Challenge Cup Brian Umony.
Pia Azam FC imemsajili kinda anayeshika nafasi ya pili kwa kufunga
magoli ligi kuu akiwa na magoli sita nyuma ya Kipre Tchetche na Didier
Kavumbangu wenye magoli nane kila mmoja Seif Rashid Abdallah toka Ruvu
Shooting Stars
Kama hiyo haitoshi Azam FC ambayo ilikuwa na
uwakilishi mkubwa zaidi kwenye mashindano ya CECAFA Challenge Cup mwaka
huu kwa kuwa na wachezaji 11, imemewarudisha walinzi Malika Ndeule na
Omary Mtaki waliocheza katika vilabu vya African Lyon na Mtibwa Sugar
katika mzunguko wa kwanza.
Katika kuimarisha safu yake ya
ulinzi pia imemsajili mlinzi wa kati wa Tanzania Prisons David Mwantika.
Na kumsajili kwa mkopo winga wa Simba Uhuru Selemani.
Usajili
huu umesimamiwa na mwalimu Stewart Hall mwenyewe ambaye anaamini
maboresho haya yatakiongezea nguvu kikosi cha Azam FC katika mzunguko wa
pili wa ligi kuu ya Vodacom inayotarajiwa kuanza januari 20.
Azam FC ipo jijini Kinshasa DRC ikijiandaa na mzunguko wa pili na
mashindani ya kimataifa kwa kusaka uzoefu wa kucheza nje ya nchi na
imeshacheza michezo miwili na timu za Dragons and FK Sharks ambapo
ilitoka sare 1-1 mchezo wa kwanza na kufungwa mchezo wa pili 0-2.
Azam FC inatarajia kurejea nchini December 26 ambapo itaelekea visiwani
Zanzibar moja kwa moja kushiriki mashindano ya Mapinduzi Cup ambayo
inayashikilia.
Pia Azam FC imemsajili kinda anayeshika nafasi ya pili kwa kufunga magoli ligi kuu akiwa na magoli sita nyuma ya Kipre Tchetche na Didier Kavumbangu wenye magoli nane kila mmoja Seif Rashid Abdallah toka Ruvu Shooting Stars
Kama hiyo haitoshi Azam FC ambayo ilikuwa na uwakilishi mkubwa zaidi kwenye mashindano ya CECAFA Challenge Cup mwaka huu kwa kuwa na wachezaji 11, imemewarudisha walinzi Malika Ndeule na Omary Mtaki waliocheza katika vilabu vya African Lyon na Mtibwa Sugar katika mzunguko wa kwanza.
Katika kuimarisha safu yake ya ulinzi pia imemsajili mlinzi wa kati wa Tanzania Prisons David Mwantika. Na kumsajili kwa mkopo winga wa Simba Uhuru Selemani.
Usajili huu umesimamiwa na mwalimu Stewart Hall mwenyewe ambaye anaamini maboresho haya yatakiongezea nguvu kikosi cha Azam FC katika mzunguko wa pili wa ligi kuu ya Vodacom inayotarajiwa kuanza januari 20.
Azam FC ipo jijini Kinshasa DRC ikijiandaa na mzunguko wa pili na mashindani ya kimataifa kwa kusaka uzoefu wa kucheza nje ya nchi na imeshacheza michezo miwili na timu za Dragons and FK Sharks ambapo ilitoka sare 1-1 mchezo wa kwanza na kufungwa mchezo wa pili 0-2.
Azam FC inatarajia kurejea nchini December 26 ambapo itaelekea visiwani Zanzibar moja kwa moja kushiriki mashindano ya Mapinduzi Cup ambayo inayashikilia.
yap mwalimu aachwe afanye maamuzi ya kusajili kutokana na mapungufu yaliyoonekana ktk timu,sio timu inasajili kupitia viongozi mwisho wa siku ktk kikosi unakuta kuna viungo 16 kisa na mkasa usajili usio na mpango.
ReplyDelete