Search This Blog

Wednesday, December 19, 2012

CRISTIANO RONALDO ANAISHI KWENYE KIVULI CHA LIONEL 'MABAO' MESSI

Mabao 90 ndani ya mwaka mmoja. Chukua muda kufikiria uzito wa jambo hili. Lionel Messi ameweka kambani mabao hayo ndani ya mwaka 2012; anastahili kutukuzwa na kupewa sifa zote kama mchezaji bora kabisa katika kipindi hiki. Ingawa kama ambavyo Messi anavyostahili sifa kutoka kwa mashabiki, wachambuzi wa soka na wachezaji wenzake, Cristiano Ronaldo nae anafanya kazi kubwa katika kuipa mwanga wa mafanikio klabu kubwa duniani yenye maskani yake pale Santiago Bernabeu.
 
Mchezaji ghali zaidi katika historia ya soka amefunga mabao zaidi ya 169 katika miaka mitatu aliyokaa na Real Madrid; hiyo pekee ni mafanikio tosha. Messi amefunga zaidi ya hayo katika kipindi husika, na katika kipindi hicho amefanikiwa kushinda tuzo ya Ballon d'Or mara tatu huku Ronaldo akiwa ameshinda mara moja tu akiwa na klabu ya Manchester United mwaka 2008. Kuna uwezekano mkubwa Messi atashinda tena tuzo hiyo mwaka huu tena kwa haki, mabao 86 yanayoongea kila kitu. Kwa upande mwingine Ronaldo amefunga mabao machache mwakak - 63, japokuwa kwa namna nyingine mafanikio ya Ronaldo yanavutia zaidi ya Messi.

Pale Barcelona, Messi ndio star, ndio mhimili wa timu. Guardiola aliijenga Barcelona yake kumzunguka kijana huyu mfupi wa kiargentina na Vilanova amefuata mfumo huu (nani anaweza kuwalaumu?). Kila mpira unapokuwepo nje ya nusu ya uwanja wao anaangalia Messi, katika mechi  zote za kutoka kipindi kati ya November 2011 mpaka November 2012, Messi amepokea mipira mingi mara mbili zaidi ya Ronaldo alivyopokea, lakini hii inatokana zaidi na staili ya uchezaji wa Barcelona, Messi ameweza kucheza pasi zaidi ya 700 katika tatu ya mwisho ya uwanja na kujaribu kufanya dribbling zaidi ya mara 130 kuliko Ronaldo.

 Mwaka 2012 pekee, Messi alipata kupiga penati 14, ambazo ni idadi kubwa kuliko idadi kubwa zaidi ya ambazo timu yoyte ya Premier League imefanikiwa kupata katika msimu wa 2011/2012. 

Kila ambapo siku zilivyokuwa zikisogea kwa Messi kuifikia rekodi ya mabao 86, wachezaji wengi wa Barca walizungumzia matamanio yao kuona Messi akiweka rekodi hiyo. Huu ni ushahidi tosha namna magoli ya Messi yalivyoaptikana katika miezi kadhaa iliyopita, wachezaji wenzie waliweka mbele ushindi lakini pia kumpa mwenzao nafasi ya kuweka rekodi. Messi amefunga zaidi ya nusu ya mabao ya Barca katika kipindi cha miezi 12 iliyopita.

Njoo upande ya kesi ya Ronaldo ndani ya Real Madrid, anahangaika kugombea spotlight ndani ya moja ya klabu kubwa kabisa duniani. Galaticos wa Mourinho wanaundwa na watu kama Higuian na Karim Benzema katika safu ya ushambuliaji, washambuliaji wenye uchu barani ulaya. Ronaldo alifunga mabao yasiyopungua 60 katika kipindi cha 2011/2012, hii ni idadi kubwa. Benzema na Higuian wanafuatia wa pili na watatu, walifunga mabao 58. Linganisha hizi takwimu na sapoti ambayo Messi anapokea kutoka kwa wachezaji wenzake wa Barcelona kama , Fabregas na Sanchez ambao wamefunga mabao 30 kwa ujumla. Katika mwaka uliopita, Ronaldo amefunga asilimia 42 ya mabao ya Real Madrid wakati Messi amefunga asilimia 56 ya mabao ya Barcelona. 

Umuhimu na namna mabao ya wachezaji jinsi yalivyofungwa yanavutia kusoma: Messi amefunga 91% ya mabao yake katika mwaka uliopita kwa mguu wake wa dhahabu wa kushoto, wakati Ronaldo amefunga 73% ya mabao yake na mguu wake wenye nguvu zaidi wa kulia. Pia Ronaldo amefunga mabao mengi ya ushindi kuliko Messi. Asilimia 21 kwa Ronaldo dhidi ya asilimia 18 za mabao ya ushindi kwa Messi, kwa maana hiyo mabao mengi ya Muargentina huyu aliyafunga wakati mechi tayari timu yake imeshashinda. 

Ukweli ni kwamba ingekuwa Ronaldo anacheza katika kizazi kingine cha soka, angekuwa akitajwa kuwa mchezaji bora wa dunia kwa kipindi hicho. Imekuwa bahati mbaya kwa upande wa Mreno huyu ambaye amekuwa akipambana kumzidi mchezaji wa soka kwa sasa ambaye anacheza kwenye timu bora kabisa kuwahi kutokea katika ulimwengu wa soka.

Baadhi ya watu wanajaribu kusema kwamba Ronaldo ni Andy Murray wa soka, anastahili sifa zaidi lakini ana bahati mbaya ya kucheza katika kipindi kimoja na Messi na Barcelona hii ya miaka ya hivi karibuni.

Wachezaji hawa wawili siku zote wataendelea kupambanishwa; kila mshabiki wa soka ana maoni yake juu ya wachezaji hawa wawili.

Akizungumzia Messi, Pep Guardiola alisema: "Usijaribu kuandika chochte kumhusu, usijaribu kumuelezea, we mtazame tu."
Wakati Mourinho alipomzungumzia Ronaldo alisema: "Kama Messi ndio mchezaji bora wa dunia basi Ronaldo hastahili kuwepo katika hii dunia kwa ubora wake."  

Mwisho wa siku kuwafananisha wachezaji hawa kunaleta mjadala usioisha. Hivyo ni bora kukaa na kutulia kuangalia wachezaji bora kabisa katika historia ya soka wakishindana kila wiki kucheza kwa ubora mchezo ambao mabilioni ya watu tunaupenda. 

3 comments:

  1. Bado najishawishi kuamini kwamba Ronaldo ni bora,kwa takwimu ulizotoa ni dhahiri kabisa Ronaldo ni bora licha ya Messi kumzidi idadi kubwa ya mabao,kwa ubora wa timu ya barca,kwa mfumo wanaotumia kumzunguka Messi na aina ya wachezaji wanaomzunguka,huduma hiyo angekuwa anaipata Ronaldo,naamini angefunga mara mbili ya hayo,.Ukiangalia mfumo wa madrid,c wa kumzunguka Ronaldo,mara nyingi huwa anahangaika kujitafutia mwenyewe,laiti km Messi angekuwapo huko,asingefikisha idadi hiyo ya magoli,mfano anapokuwa timu ya taifa.Kifupi Messi ni spoon feeding..

    ReplyDelete
  2. sasa katika mabao 90 kajitahidi Ila Argentina ilifika wapi kwa hayo mabao na mabao 90 Barca iliambulia Copa Del Rey Tu-These are still trophless goals

    ReplyDelete