Baada ya kuvumilia kwa muda mrefu vitendo vya uongozi wa klabu ya Simba kutowapa huduma muhimu katika kuendesha timu ya B ya klabu hiyo, leo hii wachezaji na makocha wa timu Selemani Matola na Patrick Rweyemamu inasemekana wameamua kutoingiza timu hiyo uwanjani katika mchezo wa robo fainali ya kombe la Uhai linaloendelea katika viwanja vya Karume na Chamazi jijini Dar es Salaam.
Kwa mujibu wa chanzo cha habari kilicho karibu na timu hiyo ya Simba B kimesema uongozi wa klabu hiyo umekuwa ukiwatelekeza wachezaji wa timu hiyo kwa muda mrefu katika kuwapa mahitaji yao ya kimsingi - "Kiukweli uongozi hauna habari hata kidogo na hii timu B, wamewaachia Matola na Rweyemamu kila kitu. Wachezaji wanadai mishahara ya miezi mitatu sasa, fedha zao za ushindi wa Kombe la BancABC hawakuambulia kitu chochote. Na juzi zile fedha za maandalizi walizotoa wadhamini wa Uhai Cup, wamechukua na kwenda kulipia gym kwa ajili ya timu A huku wakishindwa kutoa hata senti tano kwa ajili ya timu husika yenye kushiriki kombe la Uhai Cup ambayo ni timu B.
"Hii ni makusudi wanayofanya uongozi sio kwamba timu haina fedha, mfano angalia jzui wametoa $40,000 na mshahara wa $2000 kwa kipa Dhaira, pia wamempa Okwi mapesa kibao lakini wanashindwa kuangalia msingi wa maendeleo ya Simba SC ambao ni timu ya pili. Rweyemamu amekuwa akijitoa sana katika kuisadia hii timu ya pili lakini sasa anashindwa kuendelea kwa sababu uongozi hauonyeshi kuwa na mapenzi ya dhati na Simba B. Timu jana ilipata aibu kubwa wakati ikitoka Chamazi - basi walilokuwa wakitembelea liliishiwa na mafuta na kupaki barabarani, hivi kweli jambo kama hilo la kuitokea timu kubwa kama ya Simba kweli? Sasa kutokana na mambo yote hayo leo hii wachezaji wanataka kugoma kwenda uwanjani kesho ili kuushinikiza uongozi kutimiza mahitaji yao." - kilimaliza chanzo cha habari.
**Kwa mtindo huu soka la Bongo litaendelea kudumaa mpaka tutakapopata viongozi wenye mapenzi na nia ya dhati ya kutaka maendeleo ya soka Tanzania****
Ni ubabaishaji tu wa uongozi wa juu, mi nadhani let people be serious, km huwezi kuwa kiongozi Simba SC endelea na business zako [ iwe siasa, uwakala wa mizigo, biashara nk] Simba SC ina watu wa kila kariba na weledi, wachumi, maafisa mipango, wahasibu, watawala nk si lazima uwe wewe bwana.
ReplyDeleteTz hatuna msingi bora wa hz timu B
ReplyDeleteInaboa sana. Hivi viongozi hawajui umuhimu wa timu ya vijana? Ni aibu sana!
ReplyDeletewanchama wa klabu ya simba ndo wa kulamiwa kwa kadhia hii. tunamjua Rage hatuwezi kumpa dhamana ya kuongoza klabu kama Simba. Rage amewageuza wanachama wa Simba Mazuzu, anapiga pesa ile mbaya. Ujenzi wa uwanja wamechanga mamailioni lkn hakuna kinachoendelea. Sisi watz ndo tulivyo namwona Rage akineemeka kwa migongo wa wachezaji na wanachama wa simba sio kimaisha hata kisiasa.
ReplyDeleteMakala kama hizi ni za kipuuzi!! Huwezi ukalinganisha usajiri wa Simba A na ushiriki wa bonaza la Uhai Cup! Simba inajiandaa na michuano ya kimataifa na unajua nini kinachostahili kwenye maandalizi leo unalaumu as if kumlipa Okwi na kumnunua huyo kipa ni kama kupoteza fedha.
ReplyDeleteHebu unavyoandika vitu kama hivi jaribu kuchimba kwa kina. Umejiuliza JKT Ruvu, Mgambo au hata Polisi Moro wanaishije kwa kulipwa nini na wanahudumiwaje katika mashindano? Au Simba inatoka kwenye nchi nyingine na kupewa udhamini tofauti na timu zingine?
Shaffih mimi sidhani kama viongozi wa vilabu na vyama vya soka Tanzania wanajitambua au wanatambua wajibu wao!kaka kama simba ilikuwa haina haja kusajili kipa mganda kwa mahela yote hayo,yule kipa wa simba b ni mzuri sana na angeisaidia simba a,viongoz wa tz hawana vision katika soka la vijana,kama rage analeta siasa katika soka,ushawah ona kiongoz wa timu za ulaya yuko ktk siasa au yeye ndo kawa mzungumzaj mkuu wa klabu??mi ni mshabiki wa simba lakini sipendezwi hata kidogo na vitendo vya viongozi wa klabu yetu.uhuni mwingi kuliko vitendo.Ivi kazi yote ile waliyofanya simba b ktk abc cup wasipewe kitu?ingekuw rage anaenda bungen anamaliza kikao afu hapewi posho angelidhia?au ndo mkuki kwa nguruwe kw binadamu mchungu?
ReplyDelete