KOCHA wa Timu ya Taifa (Taifa Stars), Kim Poulsen amesema yuko
tayari kutimuliwa kazi iwapo tu msimamo wake wa kutetea nidhamu kwa
wachezaji kwenye kikosi chake utakuwa kikwazo kwa wengine.
Poulsen alisema hayo wakati akizungumzia
kitendo cha Mbwana Samata na Thomas Ulimwengu kuchelewa kujiunga Stars
kujiandaa mchezo wa kirafiki wa kimataifa dhidi ya Zambia mwishoni mwa
wiki hii.
Ulimwengu na Samata wanaocheza soka la kulipwa na timu ya TP Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, wameitwa kuja kuivaa Chipolopolo. Poulsen alisema hana muda wa kuwabembeleza wachezaji hao, na kama ni lazima afanye hivyo ili wacheze, basi yuko tayari kuachia ngazi. “Nasisitiza nidhamu. Timu ya Taifa siyo kitu cha mchezo.
Ulimwengu na Samata wanaocheza soka la kulipwa na timu ya TP Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, wameitwa kuja kuivaa Chipolopolo. Poulsen alisema hana muda wa kuwabembeleza wachezaji hao, na kama ni lazima afanye hivyo ili wacheze, basi yuko tayari kuachia ngazi. “Nasisitiza nidhamu. Timu ya Taifa siyo kitu cha mchezo.
Mchezaji hapaswi kubembelezwa kucheza timu ya taifa, yeye mwenyewe ndiye wa kufanya juhudi kwa taifa lake,” alisema Poulsen. “Kama wanadhani ipo sababu ya mimi kuwabembeleza ndipo wacheze, ni heri nikatishe mkataba wangu kuliko kufundisha wachezaji waliokosa nidhamu,” alisema wakati akiongea na Mwananchi.
“Sina tena sababu ya kuwachezesha, siko tayari kuona wachache wanavunja nidhamu ya timu, mchezo wa soka ni pamoja na nidhamu, siyo kipaji tu.” Kauli ya Poulsen imekuja baada ya kuulizwa kama haoni atakuwa anahatarisha kibarua chake kwa kuwaacha nyota hao, hasa ukizingatia makocha watangulizi wake walitimuliwa kwa sababu ya nidhamu mbaya ya wachezaji.
Alisema: “Moja ya falsafa yangu kama kocha mwenye taaluma ni kusimamia nidhamu ya timu. Siwezi kulea watovu wa nidhamu kwa sababu tu ya kulinda kibarua changu. “Wachezaji wanajifunza kila siku, kuna mema na mabaya. Kuwaruhusu Samata na Ulimwengu kuwafundisha wengine utovu wa nidhamu kwa sababu wao wanajua soka, wanacheza nje ya nchi na kupendwa na mashabiki, maana yake ni kuivuruga timu. Siko tayari.”
Aliongeza: “Uamuzi wao wa kukaa nyumbani bila kutoa taarifa, ni dharau kwa taifa lao, wachezaji wenzao, mashabiki na pia wamenidharau mimi na benchi langu lote.” Kocha Marcio Maximo, alitanguliwa na wakati mgumu kutoka kwa mashabiki kabla ya kuondoka, kufuatia uamuzi wake wa kutowachezesha kwenye kikosi, Haruna Moshi, Athumani Idd na Juma Kaseja, huku Jan Poulsen naye akiingia matatani baada ya kumtema Samata kwa madai ya kutojituma.
Source: Mwananchi
No comments:
Post a Comment