Sir Alex Ferguson ametangaza kustaafu kuifundisha Manchester United baada ya miaka 27 ndani ya Old Trafford.
Taarifa za Fergie kutaka kustaafu zilianza kuzagaa tangu jana mchana na usiku zikazidi lakini hakuna habari yoyote rasmi iliyotoka United mpaka leo asubuhi.
Ferguson aliwasili kazini kama kawaida asubuhi akiendesha gari lake katika uwanja wa mazoezi wa United wa Carrington mnamo saa kumi na mbili.
Akitangaza uamuzi wake wa kustaafu alisema: "Uamuzi huu nimeufikiria sana na sikukurupuka. Ni muda sahihi.
'Ilikuwa ni muhimu kuiacha taasisi hii ikiwa katika hali nzuri na imara na ninaamini nimefanya kazi nzuri sana. Ubora wa kikosi hiki kilichoshinda ligi, na uwiano wa umri wa wachezaji unaonyesha kutaendelea kuwepo na mafanikio katika hatua ya juu - mfumo mzuri wa kukuza vipaji unatoa picha nzuri ya mafanikio ya siku zijazo ya klabu.
'Kutokea hapa, nina furaha kuchukua majukumu ya ukurugenzi na ubalozi wa klabu hii. Sasa naangalia mbele kuzitendea haki kazi zangu.
'Lazima niipe shukrani familia yangu, mapenzi yao na sapoti imekuwa muhimu sana kwangu. Mke wangu Cathy amekuwa mtu muhimu katika maisha yangu yote, kunipa moyo pale mambo yalipokuwa hayaendi sawa na kunisapoti. Maneno hayatoshi kuelezea namna gani wakati huu ulivyo kwangu.
'Kwa wachezaji wangu na wafanyakazi wengine wa klabu, wa sasa na zamani, ningependa kuwashukuru kwa kazi nzuri tuliyofanya pamoja iliyonisaidia kuleta kumbukumbu nyingi za ushindi zisizosahaulika. Bila mchango wao historia ya klabu hii kubwa isingekuwa tajiri kiasi hiki.
'Katika miaka yangu ya mwanzo hapa, utetezi wa bodi kwangu, na Sir Bobby Charlton zaidi, ulinipa hali ya kujiamini na muda wa kujenga timu ya soka.
'Katika kipindi cha muongo mmoja uliopita, familia ya Glazer imenipa kila kitu nilichohitaji katika kuiongoza Manchester United kwa ubora wote na nimekuwa nina bahati sana kuweza kufanya kazi na mtu mwenye kipaji na mwaminifu kama CEO David Gill, Nina washukuru sana.
'Kwa mashabiki, shukrani sana. Mapenzi na sapoti mliyonipa miaka yote siwezi kuielezea. Imekuwa ni heshima kubwa sana kuweza kuiongoza klabu yenu na nimekuwa na ufahari wa muda wangu kama kocha wa Manchester United." alimaliza Ferguson.
HAYA NDIO MAFANIKIO YA FERGUSON KAMA KOCHA
ST MIRREN
Scottish First Division (1): 1976-77.
ABERDEEN
Scottish Premier Division (3): 1979-80, 1983-84, 1984-85.
Scottish Cup (4): 1981-82, 1982-83, 1983-84, 1985-86.
Scottish League Cup (1): 1985-86.
European Cup Winners' Cup (1): 1982-83.
European Super Cup (1): 1983.
MANCHESTER UNITED
Premier League (13): 1992-93, 1993-94, 1995-96, 1996-97, 1998-99, 1999-2000, 2000-01, 2002-03, 2006-07, 2007-08, 2008-09, 2010-11, 2012-13.
FA Cup (5): 1989-90, 1993-94, 1995-96, 1998-99, 2003-04.
League Cup (4): 1991-92, 2005-06, 2008-09, 2009-10.
Charity/Community Shield (10): 1990 (shared), 1993, 1994, 1996, 1997, 2003, 2007, 2008, 2010, 2011.
Champions League (2): 1998-99, 2007-08.
European Cup Winners' Cup (1): 1990-91.
European Super Cup (1): 1991.
Intercontinental Cup (1): 1999.
FIFA Club World Cup (1): 2008.
Search This Blog
Wednesday, May 8, 2013
EXCLUSIVE: TAARIFA HALISI YA MAAGIZO YA FIFA KWA TFF KUHUSU UCHAGUZI MKUU
BARUA RASMI KUTOKA FIFA KUJA KWA TFF KUHUSU UCHAGUZI WA TFF
Tungependa
kuwafahamisha kuwa hali inayoendelea sasa kwenye shirikisho la soka la Tanzania
TFF ilijadiliwa na kamati ya dharura ya FIFA tarehe 28 aprili mwaka 2013.
Kamati hii ilizingatia yale ambayo yalionekana kama dosari na ujumbe wa FIFA, zaidi kitendo cha kamati za TFF kukataa kuwapitisha baadhi ya wagombea kwenye mchakato wa uchaguzi mkuu kwa kigezo cha ukiukwaji wa baadhi ya taratibu zinazosimamia uchaguzi huo vikiwemo kipengele cha tisa na cha saba pamoja na kipengele cha 29 kwenye katiba ya shirikisho. Kwa kufanya hivyo kamati ya uchaguzi ilifanya baadhi ya maamuzi ambayo ilijiridisha kuwa yameenda kinyume na taratibu ( mfano kupeleka kesi mahakamani, matumizi mabaya ya fedha za shirikisho na kutokuwepo kwa uwajibikaji ) wakati TFF haikuwahi kuchukua hatua zozote. Haya yote yalipelekea mgombea mmoja kuondolewa kwenye mchakato wa uchaguzi bila kujua adhabu yake. Iligunduliwa kuwa TFF ilikuwa haina vyombo ambavyo vinapaswa kushughulikia kesi za masuala ya maadili jambo ambalo lilipelekea kamati ya uchaguzi kujivika madaraka ya kuwahukumu wagombea wakati jukumu kubwa la kamati likiwa kuwathibitisha wagombea kama wanastahili kuingia kwenye mchakato au la.

Kwa mazingira hayo , kamati ya dharura ya FIFA iliamua yafuatayo.
*TFF iunde vyombo ambavyo vitasimamia masuala ya maadili ambayo yatasimamia kesi zote za maadili kwenye mchakato wa uchaguzi .
*Kuhakikisha mabadiliko ya katiba yanafanyika .
Kuanza upya mchakato wa uchaguzi kwa kufungua upya utaratibu wa usaili wa wagombea wote .
*Kuhakikisha mchakato wa uchaguzi unafanyika mpaka kufikia oktoba 30 .
*Maamuzi haya ya kamati ya a dharura ya FIFA yanamaanisha kuwa TFF lazima iite mkutano mkuu wa dharura ili kusimamia mabadiliko ya katiba na mchakato wa uchaguzi. FIFA na CAF ziko tayari kuisaidia TFF kwenye utekelezwaji wa maagizo haya
******* mwisho***********************************************
HII NDIO TAARIFA WALIYOTOA TFF KUTOKA FIFA WIKI ILIYOPITA
Shirikisho
la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA) limelitaka Shirikisho la Mpira wa
Miguu Tanzania (TFF) kuanza upya mchakato wa uchaguzi baada ya kubaini
kasoro iliyotokana na ukosefu wa kutokuwepo vyombo vya kushughulikia
ukiukwaji wa maadili.
FIFA
ambayo ilituma ujumbe wake katikati ya mwezi uliopita kufanya utafiti
kuhusu mchakato wa Uchaguzi Mkuu wa TFF ambao ulisimamishwa baada ya
baadhi ya wagombea kulalamika, imetaka uchaguzi ufanyike kabla ya tarehe
30 Oktoba 2013, lakini ukitanguliwa na mabadiliko ya katiba ambayo
yatahusisha uundwaji wa vyombo vya kushughulikia ukiukwaji wa maadili.
Raiswa
TFF, Leodegar Tenga aliwaambia waandishi wa habari kwenye ukumbi wa
mikutano wa shirikisho hilo kuwa suala la Tanzania lilijadiliwa kwenye
kikao cha Kamati ya Dharura ya FIFA kilichofanyika tarehe 28 Aprili 2013
na maamuzi yake kutumwa juzi kwa barua iliyosainiwa na KatibuMkuuwa
FIFA, Jerome Valcke.
Baada
ya kupokea barua hiyo, Rais wa TFF alifunga safari kwenda Dodoma jana
kukutana na Mheshimiwa Waziri na Naibu wake pamoja na Mwenyekiti wa
Baraza la Michezo la Taifa (BMT).
“Matarajio
yetu sote yalikuwa kupokea majina ya waliopitishwa ili tufanye
uchaguzi. Kinyume chake tumepokea maagizo hayo. Hata hivyo tumeona kuwa
hili ni jambo la kheri kwa vile siyo tu haki itatendeka bali pia
itaonekana imetendeka.” alisema Tenga, ambaye alishatangaza kuwa
hatagombea tena urais baada ya kuliongoza Shirikisho kwa vipindi viwili
vya miaka minne kila kimoja.
“Lengo
letu ni kuhakikisha maagizo hayo yanatekelezwa na uchaguzi kufanyika
mapema iwezekanvyo kabla ya tarehe iliyotolewa. Yale mambo nayoweza
kufanyika kwa pamoja yatafanyika ili tuharakishe utekelezaji wa maagizo
yaliyotolewa na FIFA.”
Uchaguzi
wa TFF ulipangwa kufanyik tarehe 23 na 24 Februari 2013 na ulikuwa
ukielekea ukingoni, lakini baadhi ya wagombea walienguliwa katika hatua
ya mwisho na Kamati ya Rufani ya Uchaguzi ya TFF na ndipo walipo andika
barua FIFA kuomba iingilie kati.
Rais
Tenga alisema kuwa ujumbe wa FIFA ulikutana na pande zote
zilizoathiriwa na mchakato wa uchaguzi na kwamba baada ya kukusanya
taarifa hizo, maagizohayo ya FIFA sasa yatakuwa ni suluhisho la matatizo
ya muda mrefu katika uendeshaji wa mpira wa miguu nchini.
Katika barua hiyo, FIFA imeiagizaTFF:
1. Kuunda
vyombo sahihi (Kamati ya Maadili itakayokuwa na vyombo viwili ambavyo
ni cha kutoa maamuzi ya awali na cha rufaa) ambavyo mamlaka yake
yatakuwa ni kushughulikia masuala ya ukiukwaji wa maadili;
2. Kufanya mabadiliko ya katiba kwa kuzingatia uundwaji wa vyombo hivyo;
3. Kuanza
upya kwa mchakato wa uchaguzi wa Kamati ya Utendaji kwa kufungua
milango kwa wagombea ambao walishachukua fomu na wagombea wapya:
4. Shughuli hiyo ikamilike ifikapo tarehe 30 Oktoba 2013.
Katika
kutekeleza hayo, TFF inatakiwa iitishe Mkutano Mkuu wa Dharura kwa
ajili ya kufanya mabadiliko ya Katiba kwa ajili ya kuunda kamati hizo za
maadili na Kanuni za Uchaguzi kabla ya kuendelea na Mkutano Mkuu wa
Uchaguzi wa Kamati Mpya ya Utendaji.
Katika
maoni yake FIFA imeeleza kuwa katika mchakato, Kamati ya Uchaguzi ya
TFF iliwaengua au kupitisha baadhi ya wagombea kwa kubaini kuwa
walikiuka Ibara ya 9 (7) ya Kanuni za Uchaguzi na pia Ibaray a 29 (7) ya
Katiba ya TFF ambavyo vinahusisha suala la kufungua kesi mahakamani,
kufuja fedha za shirikisho na ukosefu wa uwajibikaji wa pamoja.
Hata
hivyo, FIFA ilisema kuwa watu hao walitakiwa waadhibiwe kwanza na
kamati husika (kamati za maadili) kabla ya kuenguliwa na kamati za
uchaguzi za TFF.
“Kutokana
na ukosefu wa kamati za maadili matokeo yake, mmoja wa wagombea amekuwa
akienguliwa kwenye uchaguzi kila anapombea bila ya kujua adhabu yake ni
ya muda gani,” inasema barua hiyo ya FIFA.
Rais
Tenga ameagiza kuitishwa kwa kikao cha dharura cha Kamati ya Utendaji
ya TFF kupokea maagizo ya FIFA na kupanga ratiba ya utekelezaji wake kwa
lengo la kuhakikisha kuwa mchakato huu unatekelezwa mapema
iwezekanavyo.
ROBERT LEWANDOSKI: MSIMU WAKE NDANI YA LIGI YA MABINGWA WA ULAYA KWENYE NAMBA
Pamoja na mazungumzo mengi kuwahusu Lionel Messi na Cristiano Ronaldo, lakini ni Robert Lewandowski, mshambuliaji wa Borussia Dortmund, ambaye ameibuka kuwa mchezaji aliyeng'ara zaidi wakati wa hatua za mwisho za ligi ya mabingwa wa ulaya msimu huu.
Mpoland huyu ameiwezesha timu yake kutinga fainali, huku ushindi dhidi ya wapinzani wao wa Bundesliga ukimaanisha watakuwa mabingwa wa ulaya baada ya miaka takribani 16.
Mtazamo wa takwimu zake katika mechi michezo 12 (akianza mechi 11) zinaonyesha namna gani Lewandoski alivyokuwa na umuhimu.
Kwanza, takwimu muhimu zaidi kwenye soka: ni magoli. Lewandoski ana mabao 10 mpaka sasa, wa pili kwa mabao mengi kuliko mchezaji yoyote nyuma ya Cristiano Ronaldo mwenye magoli 12.
Ikiwa Lewandowski atacheza kwa kiwango kingine cha kutisha katika fainali, ana nafasi ya kuwa mchezaji bora kabisa kwa msimu huu.
Uwiano wa mabao ya Lewandowski ndio unaomtofautisha na wengine. Magoli yake 10 yametokana na mashuti 46 aliyoyapiga langoni mwa timu pinzani. Uwiano wa asilimia 21.
Burak Yilmaz na Thomas Muller pekee ndio ambao wana wastani mzuri Burak akiwa na 25% na Muller akiwa na 27%.
Lewandowski amekuwa mwiba mchungu kwa makipa wa timu pinzani. Ana wastani wa 3.8 wa kupiga mashuti katika mechi - anashika nafasi ya nne kwa wastani wa jumla.
Katika suala la pasi, namba zinaonyesha Lewandowski ni mshambuliaji wa kweli. Kazi yake sio kusambaza mipira, hivyo pasi zake zilizokamilika 206 kati ya 304 alizopiga zinaonyesha kiasi gani alivyo bora.
Pia ameonyesha anaweza kuwatengenezea wenzie, ingawa ametoa pasi 17 zilizopelekea jaribio kwenye goli la wapinzani - hivyo ana wastani wa 1.4 wa pasi za mwisho kwa mechi.
Uwezo wake wa ubunifu dimbani umeonekana wazi kwa jukumu analopewa ndani ya kikosi cha Dortmund; amekuwa akisababisha faulo kadhaa kwenye lango la adui - akiwa na wastani usiopungua kuchezewa rafu mara mbili kwa mechi.
Vitu vyote vilivyotajwa hapo juu vinaonyesha Lewandoski ni mchezaji wa daraja la dunia, lakini mtihani mgumu kwake utakuwa mchezo wa fainali ya ligi ya mabingwa wa ulaya. Takwimu zote nzuri zinazomhusu Mpoland huyu zinaweza zikasahaulika ikiwa hatoweza kucheza vizuri katika mchezo muhimu kuliko yote katika maisha yake ya soka.
Tuesday, May 7, 2013
MABAO 352 YATINGA NYAVUNI LIGI KUU MSIMU: TCHETCHE BAO ANAWAPELEKA PUTA WASHAMBULIAJI WENGINE
JUMLA ya mabao 352 yamefungwa katika mechi 173 zilizochezwa kwenye Ligi
soka Tanzania Bara iliyoanza kutimka rasmi Septemba 15, mwaka jana.
Kwa idadi hiyo ni sawa na wastani wa kila mechi ya ligi ambayo inachezwa, mabao mawili yanafungwa.
Yanga ambayo imeshatwaa taji hilo kabla ya ligi kumalizika imepachika mabao 45 kwenye ligi hiyo kwa mechi zake 25 iliyocheza, sawa na uwiano wa kupachika mabao mawili kila mchezo.
Pia, ni timu ambayo ina ngome imara ya ulinzi. Imeruhusu magoli 14 kutikisa nyavu zake ambayo ni machache zaidi.
Maafande wa JKT Ruvu ya Pwani ndiyo timu ambayo imekuwa na safu dhaifu zaidi ya ulinzi ikiwa imefungwa jumla ya magoli 39.
Polisi Moro iliyorejea Ligi Kuu na kushuka kwa mara nyingine imekuwa na fowadi butu zaidi ya timu zote 14 zilizoshiriki ligi hiyo.
Katika mechi zake 25 iliyocheza kwenye ligi hiyo imefanikiwa kufunga mabao 13 pekee.
Mshambuliaji wa Azam FC, Kipre Tchetche ndiye anayeongoza kwa kufunga mabao 16 akifuatwa na Mrundi Didier Kavumbagu wa Yanga mwenye magoli tisa.

"BAADA YA MECHI YETU NA YANGA MINZIRO ALINIFUATA KUNISHAWISHI NIJIUNGE NAO MSIMU UJAO"
WINGA wa Mgambo JKT, Chande Magoya ametoa siri kuwa alifuatwa na kocha
msaidizi wa Yanga, Fredy Minziro akimtaka ajiunge na timu hiyo kwa msimu
ujao wa ligi.
Akizungumza jijini Dar es Salaam winga huyo mwenye kasi na kipaji cha kipiga chenga za maudhi uwanjani alisema;
"Ni kweli. Mechi yetu na Yanga ilipomalizika Mkwakwani. Minziro alifuata na kunipongeza kuwa nilicheza vizuri na kuisumbua timu yake kwa dakika zote 90 za mchezo."
Magoya alisema baada ya kumpongeza kwa kiwango kizuri cha soka, kocha huyo alianza kumtania kuwa yupo tayari kutua Yanga iwapo itamwitaji.
"Baada ya kunipongeza aliniuliza iwapo timu hiyo itakuwa inataka kunisajili nipo tayari. Nikamjibu bila shaka isipokuwa sitaki kukaa benchi." alisema Magoya.
Minziro ilipotafuta kwa ajili ya kuthibitisha hilo, simu yake yake kiganjani ilikuwa akiita bila kupokelewa.
Katika pambano hilo lililopigwa kwenye Uwanja wa Mkwakwani, Tanga, timu hizo mbili zilitoka sare ya bao 1-1.

SIMBA SC KUUMANA NA MGAMBO KESHO - MECHI YAO NA RUVU SHOOTING YAINGIZA MILLIONI 17
Timu
za Simba na Mgambo Shooting ya Tanga zinaumana kesho (Mei 8 mwaka huu)
katika mchezo pekee wa Ligi Kuu ya Vodacom utakaofanyika Uwanja wa
Taifa, Dar es Salaam.
Viingilio
katika mechi hiyo itakayoanza saa 10.30 jioni vitakuwa sh. 5,000 kwa
viti vya bluu na kijani, sh. 8,000 viti vya rangi ya chungwa, sh. 15,000
kwa VIP C na B wakati VIP A ni sh. 20,000.
RUVU SHOOTING, SIMBA ZAINGIZA MIL 17
Mechi
namba 111 ya Ligi Kuu ya Vodacom kati ya Ruvu Shooting na Simba
iliyochezwa juzi (Mei 5 mwaka huu) kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam
na kumalizika kwa Simba kushinda mabao 3-1 imeingiza sh. 17,700,000.
Watazamaji
3,163 walikata tiketi kushuhudia mechi hiyo ambayo viingilio vilikuwa
sh. 5,000, sh. 8,000, sh. 15,000 na sh. 20,000 huku kila klabu ikipata
mgawo wa sh. 3,485,752.45 wakati Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT)
iliyolipwa ni sh. 2,700,000.
Kiingilio
cha sh. 5,000 ndicho kilichovutia watazamaji wengi ambapo waliokata
tiketi hizo walikuwa 2,901 na kuingiza sh. 14,505,000 wakati idadi ndogo
ya washabiki ilikuwa ya kiingilio cha sh. 20,000 kilichovutia washabiki
28 na kuingiza sh. 560,000.
Mgawo
mwingine wa mapato hayo ni asilimia 15 ya uwanja sh. 1,772,416.50,
tiketi sh. 3,183,890, gharama za mechi sh. 1,063,449.90, Kamati ya Ligi
sh. 1,063,449.90, Mfuko wa Maendeleo ya Mpira wa Miguu (FDF) sh.
531,724.95, Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Dar es Salaam (DRFA) sh.
206,781.93 na Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Pwani (COREFA) sh.
206,781.93.
GHANA NA HOFU YA WACHEZAJI WAKE KUCHEZA SOKA LA KULIPWA TP MAZEMBE
Sio mara nyingi unaweza ukasikia mashabiki wa nchi fulani wakiwa na wasiwasi juu ya wachezaji wa taifa lao kwenda kucheza soka la kulipwa nje ya nchi ili kuendeleza vipaji vyao.
Walinzi Daniel Nii Adjei, Yaw Frimpong, Richard Kissi Boateng kiungo Gladson Awako na mshambuliaji Solomon Asante wote waliondoka Ghana kwa muda mmoja mwanzoni mwa msimu.
"Watu wanaweza wakaona kama ni dalili ya kushuka kwa ligi ya Ghana kiasi kwamba wachezaji wakubwa wa Ghana wanaenda kucheza soka Congo," alisema mwandishi wa BBC Michael Oti Adjei.
Inaweza ikawa ni hofu isiyo sahihi ya mashabiki wa Ghana, lakini wanaweza wakawa na pointi nzuri kwenye hili kwamba klabu nyingine za Afrika zinawapita kwa umbali mrefu timu za Ghana kama Accra Hearts of Oak na Asante Kotoko.
"Watu wanapishana kwenye maoni. Wengine wanadhani wachezaji wale wapo Congo kwa sababu za michezo, wengine wanadhani sababu ya fedha," aliongeza Oti Adjei.
Kisoka, Ghana na Congo zipo mbalimbali - wanatenganishwa kwa pengo la nafasi 63 kwa viwango vya FIFA vya mwezi wa nne.
Wakati Black Stars wameshiriki mara mbili fainali za kombe la dunia tangu mwaka 2006, huku wachezaji wake wengi wakicheza katika ligi kubwa barani ulaya, Congo imeweza kushiriki fainali hizo mara moja tu, mwaka 1974 wakati ikiitwa Zaire.
Wakati huo wakaweka rekodi ya kipigo kikubwa zaidi kwenye fainali hizo kwa kufungwa 9-0 na Yugoslavia.
Lakini mabingwa wa mara nne wa kombe la mabingwa wa Afrika TP Mazembe, imekuwa ndio timu ya kwanza ya Afrika kucheza fainali ya klabu bingwa ya dunia mnamo mwaka 2010, na sasa wapo kwenye hali nzuri kisoka na kifedha kuliko vilabu vingi vya Ghana.
Ikiwa ipo kwenye eneo lilo na utajiri wa madini la Katanga, klabu inamiliki uwanja, ndege mbili, gym na kliniki.
Wapo chini ya uongozi wa tajiri mkubwa, Moise Katumbi, ambaye pia ni Gavana wa eneo hilo.
Wachezaji wa Ghana wanajua uhamisho wao kwenda Congo umegawanya maoni ya mashabiki lakini wanapenda maisha yao ya soka ndani ya Congo.
Beki Richard Kissi Boateng aliiambia BBC : "Kujiunga TP Mazembe ilikuwa ni hatua nzuri. Kama unavyoona wana ushawishi mkubwa katika soka la Afrika.
"Kwenye maisha inabidi uendele mbele. Tumejiunga nao ili tuweze kutengeneza majina katika soka la Afrika. Kila kitu ni kikubwa hapa, wachezaji, mashabiki na hata miundo mbinu ya klabu ni mizuri kufananisha na ya vilabu vingine na nafikiri soka la Congo limeendelea sasa kuliko la Ghana."
Mazembe wana wachezaji kutoka Zambia, Malawi, Tanzania, Ivory Coast, Uganda, Senegal na katika miaka miwili iliyopita klabu imeweza kuajiri wachezaji kutoka Zimbabwe, Brazil na Cameroon.
"Sipo hapa kwa sababu ya fedha. Katika maisha, ikiwa hautoweza kupambana na changamoto, huwezi kujipima mwenye dhidi ya kitu chochote," aliendelea Boateng.
Na akakiri kwamba rekodi ya Mazembe ya kuiwakilisha mara mbili Afrika katika kombe la dunia ngazi ya vilau iliupa ushawishi uamuzi wake wa kujiunga nao.
"Wachezaji wengine wakubwa tu barani ulaya hawajawahi kucheza kwenye michuano hiyo," alisisitiza.
Monday, May 6, 2013
HIZI NDIO TWEETS ZA MCHEZAJI WA CHELSEA ADAM NDITI AKIIPONDA SHOW YA DIAMOND PLATNUMZ JIJINI LONDON
SIKU KAMA YA LEO 2012 YANGA ILIPIGWA 5-0 NA SIMBA - MWALUSAKO ASEMA LAZIMA WARUDISHE HESHIMA ILIYOPOTEA
Wakati leo tarehe 6 Mei kipigo cha cha 5-0 cha Simba walichowapa watani wao wa jadi Yanga kikitimiza mwaka mmoja - uongozi wa Yanga umesema kuwa heshima waliyoipoteza msimu uliopita baada ya kutandikwa na Simba mabao 5-0, lazima irudi Jangwani katika mchezo wa mwisho wa Ligi Kuu utakaozikutanisha timu hizo mbili Mei 18 kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Katibu Mkuu wa Yanga, Lawrance Mwalusako amesema kuwa hivi sasa wapo katika maandalizi kabambe kwa ajili ya mechi hiyo ili kuhakikisha wanajibu kipigo hicho walichokipata msimu uliopita.
Alisema mechi hiyo ina umuhimu mkubwa sana kwao kuhakikisha wanashinda licha ya kuwa tayari wameishatwaa ubingwa wa Ligi Kuu msimu huu wakiwa bado na mechi mbili mkononi.
"Tayari timu yetu ipo kambini na inaendelea kujifua kwa mazoezi makali kabisa ya kujiandaa na mchezo wetu wa mwisho wa Ligi Kuu msimu huu dhidi ya Simba," alisema Mwalusako na kuongeza kuwa ushindi katika mechi hiyo utanogesha sherehe zao za kusherehekea ubingwa wao wa 24 wa Ligi Kuu tangu ilipoanzishwa.

MBWANA SAMATTA, YONDANI, KAPOMBE, BOCCO, NANI KUWA MCHEZAJI BORA WA TANZANIA - TCHETCHE, OKWI, NIYONZIMA NA KIIZA NANI KUWA MCHEZAJI BORA WA KIGENI?
KLABU ya Azam imeingiza wachezaji wawili katika kinyang’anyiro cha tuzo ya Mwanasoka Bora kwenye Tuzo za Wanamichezo Bora za Chama cha Waandishi wa
Habari za Michezo Tanzania (TASWA) 2012/2013.
Uongozi wa TASWA kupitia kwa katibu wake mkuu Amri Muhando aliwataja wanandinga hao wa Azam ambao wameingia katika tuzo hizo ambazo zitafanyika baadaye mwaka huu kuwa ni Khamis Mcha pamoja na John Bocco (Adebayo).
Hata hivyo, katika vita hiyo ya kumtafuta mwanasoka bora wa Tanzania wachezaji hao watachuana vikali na Kevin Yondani (Yanga), Shomary Kapombe (Simba) anayeshikilia tuzo hiyo, Mbwana Samatta pamoja Thomas Ulimwengu wote kutoka TP Mazembe ya DRC.
Azam pia imeingia mchezaji mmoja katika kipengele cha tuzo ya Mwanasoka Bora wa Kigeni anayecheza Tanzania, ambaye ni Kipre Tchetche kutoka Ivory Coast atakayechuana na Mganda Emmanuel Okwi aliyekuwa Simba na sasa anakipiga katika klabu Etoile du Sahel ya Tunisia.
Wachezaji wengine katika kipengele hicho ni, Haruna Niyonzima na Hamisi Kiiza (Yanga).
Upande wa wanasoka wa kike, Fatuma Mustafa atachuana na Asha Rashid, Mwanahamisi Omary, Sofia Mwasikili anayeshikilia tuzo huyo pamoja na Esther Chabruma.
Katika hatua nyingine Muhando alisema aliongeza kuwa kwa upande wa mchezo wa ngumi za kulipwa Francis Miyeyusho anachuana vikali na Ramadhan Shauri, Thomas Mashali, Said Mbelwa na Francis Cheka.

AMRI KIEMBA AZIDI KUDHIHIRISHA UMUHIMU WAKE NDANI YA KIKOSI CHA SIMBA
Kiungo Amri Kiemba alifunga bao moja na kutengeneza moja wakati Simba ilipoisambaratisha Ruvu Shooting kwa mabao 3-1 jana kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam katika harakati zake za kusaka nafasi ya tatu.
Kiemba alifunga bao lake kwa shuti la umbali wa mita 25 katika dakika ya 14, ambapo Shooting walisawazisha bao hilo katika dakika ya 52 kupitia Abdulrahman Musa kabla ya Kiemba kutengeneza bao la tatu lililofungwa na Rashid Mkoko dakika ya 89, wakati Christopher Edward alipachika bao la pili la Simba akimalizia mpira uliotemwa na kipa Benjamani Haule katika dakika ya 87.
Kwa matokeo hayo Simba imepanda hadi nafasi ya tatu ikiwa na pointi 42 na kuiacha Kagera Sugar katika nafasi ya nne katika msimamo wa ligi hiyo.
Kocha wa Simba, Patrick Liewig akizungumza baada ya mechi hiyo aliwasifu wachezaji wake kwa kucheza vizuri na kufanikiwa kupata matokeo hayo mazuri.
"Vijana wangu wanafuata maelekezo yangu vizuri, nadhani hiyo ndiyo siri ya mafanikio yetu kwa sasa,"alisema Liewig.
Ruvu Shooting waliianza mechi ya jana kwa kasi na kufika langoni kwa Simba katika dakika ya 7 baada ya shuti la Abraham Musa kutoka sentimita chake katika lango la Simba.
Simba walijibu mapigo katika dakika 14 na kufanikiwa kupata bao la kuongoza lililofungwa na Kiemba kwa shuti la umbali wa mita 25, akimalizia vizuri pasi ya Felix Sunzu aliyempokonya mpira beki wa Shooting, Shaaban Suzan.
Kama hiyo haitoshi, Sunzu nusura aipatie Simba bao baada ya kuunganisha kwa kichwa krosi ya Kiemba na kugongesha mwamba katika dakika ya 21.
Katika mechi hiyo kipa wa Shooting, Benjamin Haule alifanya kazi ya ziada kuokoa shuti la Haruna Chanongo katika dakika 34. Pia beki Said Madega wa Shooting alionyeshwa kadi ya njano kwa kumchezea vibaya Chanongo katika dakika ya 45.
Simba katika mechi hiyo walitumia zaidi winga zao mbili zinazoongozwa na Chanongo na Ramadhan Singano kupitisha krosi za juu kwa Sunzu, wakati Shooting wenyewe walicheza pasi fupifupi na kasi, lakini walikosa umakini kwenye umaliziaji.
Kurejea kwa Sunzu kunazidi kuimalisha safu ya ushambuliaji wa Simba kabla ya mchezo wao wa mwisho wa msimu huu dhidi ya mahasimu wao Yanga hapo Mei 18.
Shooting walisawazisha bao hilo katika dakika ya 52 baada ya Musa kuwahadaa mabeki wa Simba kabla ya kufunga bao hilo. Kocha Liewig alimpumzisha Sunzu na kumwingiza Mrisho Ngassa mwanzoni mwa kipindi cha pili mabadiliko yaliyokuwa na faida kubwa kwa vijana hao wa Msimbazi.
Katika dakika ya 87 Simba walifanikiwa kupata bao kupitia kwa Edward Christopher 'Edo' akimalizia mpira uliotemwa na kipa Haule, ambapo wakati Shooting wakijiuliza Mkoko aliipatia Simba bao la tatu katika dakika ya 89 akiunganisha kwa kichwa krosi ya Kiemba.
Simba sasa imebakiza mechi dhidi ya Mgambo JKT hapo Jumatano kabla ya kuivaa Yanga hapo Mei 18.

Sunday, May 5, 2013
PICHA ZA SIKU: DAVID LUIZ AKICHEKA BAADA YA RAFAEL KUPEWA KADI NYEKUNDU
PICHA NYINGINE ZA MATUKIO YANAYOFANANA NA HILI LA LUIZI
![David Luizs smile compared to Pepe, Busquets & Sideshow Bob [Memes] BJhJNOfCUAIyKNd David Luizs smile compared to Pepe, Busquets & Sideshow Bob [Memes]](https://pbs.twimg.com/media/BJhJNOfCUAIyKNd.jpg)
![David Luizs smile compared to Pepe, Busquets & Sideshow Bob [Memes] BJhFphBCAAEuo David Luizs smile compared to Pepe, Busquets & Sideshow Bob [Memes]](https://pbs.twimg.com/media/BJhFphBCAAEuo_-.jpg)
![David Luizs smile compared to Pepe, Busquets & Sideshow Bob [Memes] BJhJz2wCMAAHWfU David Luizs smile compared to Pepe, Busquets & Sideshow Bob [Memes]](https://pbs.twimg.com/media/BJhJz2wCMAAHWfU.jpg)
![David Luizs smile compared to Pepe, Busquets & Sideshow Bob [Memes] BJhKJCHCIAAiKIi David Luizs smile compared to Pepe, Busquets & Sideshow Bob [Memes]](https://pbs.twimg.com/media/BJhKJCHCIAAiKIi.jpg)
KALI YA LEO: RAISI WA REAL MADRID MWENYE MIAKA 87 MBIONI KUOA MWANAMKE ALIYEMZIDI MIAKA 50 - FAMILIA YAKE YAPINGA
Raisi wa heshima wa Real Madrid Alfredo Di Stefano, ambaye atatimiza miaka 87 mwezi Julai, anatarajiwa kumuona mwanamke mwenye miaka 36 ambaye alimsadia kutaarisha kitabu cha maisha kilichotolewa mwaka 2010. Di Stefano, ambaye amekuwa akipambana na matatizo kadhaa ya afya, amesema ucheshi wake ndio uliomvutia mwanamke huyo kuwa mpenzi wake.
Kutoka Reuters:
Akiwa kama mchezaji, Di Stefano alishinda makombe matano ya ulaya na Real Madrid kutoka mwaka 1956 na 1960. Akiwa kama kocha, aliiongoza Boca Juniors na Valencia kushinda makombe ya ligi.
Kutoka Reuters:
Akitajwa kama mmoja wa wachezaji bora wa muda wote, mzaliwa wa Argentina Di Stefano alisema alikuwa anajiandaa kumuoa Gina Gonzalez mwenye miaka 36 wiki chache zijazo "kwa dababu nahitaji kuwa na mwenza na pia nimekuwa mpweke kwa miaka 8 sasa", alinukuliwa na gazeti la El Mundo.
"Nimezama mapenzini na ninamuoa Gina," aliongeza. "Nina miaka 86 lakini nina moyo wa mwanaume kijana."Di Stefano alifiwa na mkewe miaka nane iliyopita. Alisema wanae hawataki aoe, lakini yeye hajali kuhusu hisia zao. "Ninachoangalia sasa ni maisha yangu na sio kitu kingine chochote.
Akiwa kama mchezaji, Di Stefano alishinda makombe matano ya ulaya na Real Madrid kutoka mwaka 1956 na 1960. Akiwa kama kocha, aliiongoza Boca Juniors na Valencia kushinda makombe ya ligi.
WAKATI WA KUUNDA KAMATI MLIZOELEKEZWA NA FIFA HAKIKISHE SUALA LA U-DSM, U SCHOOL MATE NA URAFIKI MNAVIEPUKA
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI;
YAH; MCHAKATO WA UCHAGUZI WA TFF 2012/2013.
Mimi Mbasha Matutu Mjumbe wa Mkutano Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga na niliyekuwa Mgombea wa Ujumbe wa Kamati ya Utendaji kupitia zone no 3.katika uchaguzi uliotakiwa kufanyika tangu 14/12/2012 nimepokea kwa furaha sana taarifa ya FIFA iliyotolewa na Rais wa TFF Bw Leodeger Tenga juu ya mchakato mzima wa uchaguzi wa TFF.
Pia napenda nichukue fulsa hii kuwapongeza wandishi wa habari kwa ujasiri wao mkubwa waliokuwa nao wa kulielezea jambo hili bila kumwonea mtu wala kupendelea mtu yeyote, kikubwa walichojali ni uzalendo wa Nchi yetu kwa ujumla.
Pia napenda nichukue fulsa hii kuishukru sana Serikari yetu ya tanzania chini ya uongozi wa jemedali mkuu Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Jakaya Mrisho Kikwete na Wizara husika ya Michezo inanyoongozwa na Mawaziri makikini wanaojali haki za Raia wake, kubwa zaidi namna walivyolishughulikia suala hili la Katiba ya TFF na mchakato mzima wa uchaguzi.
Nawapongeza pia FIFA kwa namna nzuri walivyoshughulika na suala hili na jinsi walivyoagiza litekelezwe, hii imenipa matumaini na faraja ya kwamba tutaenda kukomesha matabaka yaliyokuwa yameanza kujitokeza na kuhatarisha msitakabali mzima wa mpira miguu nchini mwetu na kunipa matumaini ya kunifanya nia yangu ya kugombea nafasi ya ujumbe ibaki pale pale muda utakapofika.
Pia nawapongeza watanzania wote kwa ujumla kwa namna walivyoonyesha uvumlilivu wao mkubwa kwa kipindi chote cha malumbano yaliyokuwepo ya nani anapaswa kugombea na nani hapaswi kugombea na kuchukua nafasi kubwa kwenywe vyombo vya habari hasa magazeti,Radio,Runinga na mitandao ya kijamii na hii inaweza kuwa ilipunguza baadhi ya taarifa muhimu zilizokuwa zinatakiwa kuwafika watanzania kwa ajili ya kukuza uchumi wao.
Vile vile napenda nichukue fulsa hii kuwapongeza wajumbe wa mkutano mkuu wa TFF wenzangu kwa uvumilivu wenu mliouonyesha maana mlikuwa na uwezo wa kuamua vyovyote vile, lakini kwa hekima mlizojaliwa na Mwenyezi Mungu mliendelea kuiamini Serikali yenu wakati wote wa mchakato na hii imedhihilisha kuwa Serikali yetu ni sikivu na inawapenda watu wake wote na ni kinara wa demokrasia pia tukumbuke tunalo jukumu kwa niaba ya watanzania wote kuhakikisha TFF inaendeshwa kwa kufuata Katiba,Kanuni na Miongozo hii itatusaidia kuinua mpira wa miguu nchini mwetu na haya ili yatimie tunahitaji mshikamano wetu kwa pamoja bila kujali rangi yetu, kabila letu, ukanda wetu au udini wetu.
Pia napenda kumshukru Mwenyekiti wangu wa SHIREFA Bw Bennester Rugora na Kamati nzima ya SHIREFA kwa namna walivyonishauri tangu pale nilipoonyesha nia ya kugombea ujumbe wa Kamati Tendaji sina cha kuwalipa naomba msikome kunishauri pale mchakato utakapoanza.
OMBI LANGU.
Naomba nichukue fulsa hii kutoa ombi langu kwa Rais wa TFF na kamati nzima ya Utendaji katika kutekeleza maagizo ya FIFA,nakuomba/nawaomba mtangulize utaifa na uzalendo kwanza mambo ya umimi msiyape nafasi tena.
Pia wakati wa kuunda kamati hizo mlizoelekezwa na FIFA hakikishe suala la u-Dar Es salaam, u School mate, na urafiki mnaviepuka badala yake zingatieni geografia ya Nchi yetu maana hata mikoani kuna watanzania wenye uwezo na uzalendo kwa nchi yao .
Pia mara tu baada ya kuwapendekeza wajumbe hao nawaomba majina yao na sifa zao zitangazwe hazarani na majina yao yaletwe kwenye mkutano mkuu wa TFF kwa ajili ya ukubali wa Wajumbe.
HITIMISHO.
Napenda nihitimishe kwa kuwaomba wadau wote wa mpira wa miguu kuwa wamoja wakati wote wa mchakato huu, na kuliombea zoezi zima kwa Mwenyezi Mungu liende salama mpaka hapo tutakapo pata viongozi wetu wapya,
‘Mungu ibariki Tanzania Mungu ibariki Africa ’’
……………………………..
Mbasha Matutu
Mjumbe wa Mkutano mkuu TFF
MKOA WA SHINYANGA
JUVE YATWAA TENA UBINGWA WA SERIE A.
Beki Giorgio Chiellini amebeba bango linalomaanisha ubingwa wa 31 wa Juve - ukiwemo mara mbili waliovuliwa kutokana na kashfa ya upangaji matokeo.
Juventus imefanikiwa kuchukua ubingwa wa Serie A kwa mara ya 29 kutokana na ushindi finyu leo hii kwenye uwanja wake wa nyumbani dhidi ya Palermo.
Bao la mkwaju wa penati lililofungwa kipindi cha pili na kiungo Arturo Vidal lilitosha kuwapatia Juve ushindi wa bao 1:0 na kujihakikishia ubingwa kwa msimu wa pili mfululizo huku ikiwa imebakia michezo mitatu,pia kwenye mchezo huo kiungo wa Juve Paul Pogba alilimwa kadi nyekundu kwa kosa la kumtemea mate mchezaji wa Palermo.

LIVE MATCH CENTRE: SIMBA SC VS RUVU SHOOTING
Dk 90+3 FULL TIME! RUVU 1-3 SIMBA
Dk 90 Ruvu wamepotea na Simba wanatawala tena kiungo. Dakika tatu zimeongezwa.
Dk 88 GOOOO....! Ismail Mkoko anaipatia Simba bao la tatu kwa kichwa akiunga krosi ya Kiemba. Ruvu 1-3 Simba.
Dk 86 GOOOOO....! Edward Christopher anaifungia Simba bao la pili akimalizia mpira uliotemwa na kipa Haule. Ruvu 1-2 Simba.
Dk 82 Simba wanafanya mabadiliko ametoka Haruna Chanongo ameingia Ismail Mkoko.
Dk 81 Ruvu wanafanya mabadiliko ametoka Said Madega ameingia Hamis Kisuke.
Dk 80 Kipa wa Ruvu, Haule anaumia na kutibiwa kwa muda.
Dk 74 Ngassa anachezewa faulo nje kidogo ya lango la Ruvu.
Dk 70 Simba imefanya mabadiliko ametoka Messi ameingia Edward Christopher.
Dk 64 Kulwa Mfaume anapiga shuti kali linalotoka nje kidogo ya lango la Simba.
Dk 59 YELLOW CARD...! Ngassa anaonyeshwa kadi ya njano baada ya kuutumbukiza mpira wavuni baada ya filimbi ya kuotea kupulizwa.
Dk 55 Ruvu wamefanya mabadiliko wametoka Said Dilunga na Raphael Keyala na wameingia Kulwa Mfaume na Ayoub Kitala. Ruvu 1-1 Simba
Dk 52 GOOOOO.....! Abdulhaman Mussa anaifungia Ruvu bao la kwanza baada ya kuichambua ngome ya Simba. Ruvu 1-1 Simba.
Dk 51 YELLOW CARD....! Ernest Ernest wa Ruvu anaonyeshwa kadi ya njano baada ya kumchezea vibaya Messi wa Simba.

Dk 45 KIPINDI CHA PILI KIMEANZA!
Dk 45 Simba imefanya mabadiliko ametoka Sunzu ameingia Mrisho Ngassa.
Dk 45 HALF TIME! Ruvu 0-1 SimbaDk 44 YELLOW CARD....! Said Madega wa Ruvu anaonyeshwa kadi ya njano baada ya kumchezea vibaya Abdallah Seseme. Ruvu 0-1 Simba
Dk 42 Simba inaendelea kutawala kiungoDk 40 Simba inapata karibu na lango la Ruvu wanapiga lakini kipa Haule anaudaka mpira. Ruvu 0-1 Simba
Dk 36 Ruvu wamepunguza kasi yao waliyoanza nayo na kutoa nafasi kwa Simba kutawala mchezo.
DK 35: Simba SC 1 - 0 Ruvu Shooting
Dk 34 Haruna Chanongo anakosa bao baada ya mpira aliopiga kuokolewa na kipa Haule na kuwa kona.
Dk 29 Sunzu anakosa bao la wazi akishindwa kuunga krosi ya Nassor Masoud 'Chollo'.
Dk 21 Felix Sunzu anakosa bao la wazi baada ya kichwa alichopiga kuunga krosi ya Kiemba kugonga mwamba wa juu na kutoka nje ya uwanja.
Dk 18 Ruvu wanapata kona. Said Dilunga anashindwa kuunganisha mpira wa kona na kipa wa Simba, Abel Dhaira anaudaka.
Dk 14 GOOOOO......! Amri Kiemba anaipatia Simba bao la kwanza kwa shuti kali kutoka nje ya eneo la hatari. Kiemba aliuwahi mpira uliopokonywa na Felix Sunzu kutoka kwa beki wa Ruvu, Nyambiso Athuman. Ruvu 0-1 Simba.
Dk 12 Idadi ya mashabiki waliojitokeza katika uwanja huu wa taifa ni ndogo mno.
Dk 10 Bado mpira unachezwa taratibu mno huku kila timu ikimsoma mwenzake.
DK 5:Simba SC 0 - 0 Ruvu Shooting
Mpira umeanza uwanja wa Taifa - Simba SC vs Ruvu Shooting
Simba line up: Abel Dhaira, Nassor Masoud 'Chollo', Haruna Shamte, Shomari Kapombe, Mussa Mudde, William Lucian, Haruna Chanongo, Abdallah Seseme, Felix Sunzu, Amri Kiemba na Ramadhan Singano 'Messi'.
Line up: Ruvu Shooting; Benjamini Haule, Michael Pius, Baraka Nyakamande, Nyambiso Athuman, Shaban Suzan, Ernest Ernest, Said Madega, Hassan Dilunga, Abdulhaman Mussa, Said Dilunga na Raphael Keyala.
Saturday, May 4, 2013
LIVE SCORE: AS FAR RABAT 2 - 1 AZAM FC FULL TIME
Mpira unamalizika kwa Azam kutolewa kwa kufungwa mabao mawili kwa moja.
DK 90: Mwamuzi anaongeza dakika 3 za nyongeza.
DK 88: AS FAR Rabat 2 - 1 Azam FC
DK 82: John Bocco anapiga penati na kukosa
DK 81; Azam wanapata penati baada ya beki wa AS FAR Rabat kuunawa mpira.
DK 80: Azam pamoja na kuwa pungufu wanajitahidi kwenda mbele kujaribu kutafuta bao la kusawazisha - Ameingia Gaudence Mwaikimba.
DK 75: AS FAR Rabat 2 - 1 Azam FC
DK 74: Waziri Omary anapata kadi nyekundu baada ya kumshika mchezaji wa AS FAR Rabataliyekuwa anaelekea langoni mwa Azam.
DK 68: Waziri Omary wa Azam anapewa kadi ya njano kwa mchezo mbaya.
DK 65: Anatoka Brian Umony anaingia Khamis Mcha kwa upande wa Azam
DK 60: Timu zote zinapoteza nafasi kadhaa za kufunga katika kipindi cha dakika 3 zilizopita.
DK 55: Mwamuzi anatoa kadi nyepesi kabisa nyekundu kwa David Mwantika wa Azam
DK 48: Azam bado wanaendelea kucheza kwa kushambulia lango la AS FAR Rabat lakini wanakosa umakini wa kuweza kuingiza mpira kwenye 18 ya wapinzani.
DK 46: Azam wanaanza kipindi cha pili kwa kasi na kufanikiwa kupata ambayo haizai matunda.
Kipindi cha pili kimeanza AS FAR Rabat 2 - 1 Azam FC
Mpira ni mapumziko
DK 45: Mwamuzi anaongeza dakika 3
DK 43: Azam wanafungwa bao la pili hapa -AS FAR Rabat 2-1 Azam
DK 38: Kipre Balou anapewa kadi ya njano - AS FAR Rabat pamoja na kuwa pungufu wanacheza mchezo wa kasi na nguvu.
DK 35: Mchezaji wa AS FAR Rabat anapewa kadi nyekundu kwa kumpiga teke la uso Brian Umony
DK 33: Kipre Tchetche anakosa bao la wazi akiwa amebaki na kipa tu wa AS FAR Rabat
DK 30: AS FAR Rabat wanamiliki mpira kwa muda mrefu huku Azam wakicheza kwa mashambulizi ya kushtukiza
DK 25: Mchezaji yupo akitubiwa baada ya kupata maumivu wakati akizuia shuti liloelekezwa golini kwake
DK 20: A.F.R 1 - 1 Azam FC
DK 12: AS FAR Rabat 1-1 Azam FC. Dakika ya 12 wanasawazisha.
DK 6: Goaaal John Bocco anaipa Azam bao la kuongoza hapa
KICK OFF
1. Mwadini
2. Himidi
3. Waziri
4. Mwantika
5. Atudo
6. Bolou
7. Umony
8. Salum 'sure boy'
9. Bocco (C)
10. Mieno
11. Kipre
Akiba
Aishi
Mwaipopo
Mwaikimba
Abdi Kassim
Mcha Viali
Jabir
Luckson
LAWAMA JUU YA UTEUZI WA KIKOSI CHA TAIF STARS KWA KIM POULSEN - KIBADENI ASEMA WA KULAUMIWA NI MARSH
Baadhi ya wadau wa soka nchini wamekuwa wakimlalamikia kocha Mkuu wa Taifa Stars Kim Poulsen kwa uteuzi wa timu hiyo, ingawa kocha wa Kagera Sugar, Abdallah Kibadeni 'Mputa' ametamka kuwa wakulaumiwa ni msaidizi wake.
Katika hatua nyingine nyota wa timu hiyo Themi Felix alisema; "Nafikiri atueleze kuwa kucheza timu ya Taifa Stars ni mpaka uwe Simba, Yanga au Azam FC ndiyo unaweza kuonekana." alisema
kocha wa Mkuu wa Ruvu Shooting, Boniface Mkwasa hivi karibuni alisema uteuzi wa kocha huyo umeegemea zaidi kwenye klabu za Simba, Yanga, Azam FC na Mtibwa Sugar.
Mkwasa alimtaka kocha huyo kujaribu kuwafuatilia wachezaji wa timu nyingine kwani wapo wenye sifa zote za kuichezea timu hiyo na hata kuwazidi baadhi ya waliopo kwa sasa.
Kibadeni alisema jijini Dar es Salaam kuwa kocha Kim hapaswi kulaumiwa kwa hilo isipokuwa msaidizi wake ambaye ni Silvester Marsh kushindwa kumshauri.
"Kwa upande wangu lawama hizi nafikiri zinapaswa kubebwa na msaidizi wake (Marsh) kwa kushindwa kumshauri mkubwa wake.
"Siamini kama Marsh amewahi kumshauri kitu halafu akakipinga. Kim ni kocha muelewa isipokuwa amekosa mtu sahihi wa kumshauri." alisema Kibadeni.
Katika hatua nyingine nyota wa timu hiyo Themi Felix alisema; "Nafikiri atueleze kuwa kucheza timu ya Taifa Stars ni mpaka uwe Simba, Yanga au Azam FC ndiyo unaweza kuonekana." alisema
Felix ambaye yupo kwenye kiwango kizuri cha soka.
SIMBA MPIRA PESA KUIWEKEA KIKAO MECHI DHIDI YA YANGA JUMAPILI
Wanachama wa Tawi la Simba la Mpira Pesa la Magomeni jijini Dar es Salaam wanatarajia kukutana (Jumapili) kwa ajili ya kuweka mikakati ya kuhakikisha timu hiyo inaibuka ushindi katika mchezo wa mwisho na mtani wake Yanga.
Mwenyekiti wa tawi hilo, Ustaadh Masoud alisema jijini Dar es Salaam kuwa wamepanga kukutana wanachama wote wa tawi hilo hiyo kesho kwa lengo la kuweka mikakati yakuifunga Yanga.
"Tunafikiri klabu yetu ya Simba imepoteza ubingwa wa ligi. Pia kumaliza nafasi ya pili kwenye ligi
ambayo ingetupa fursa ya kushiriki Kombe la CAF mwakani. Kwa hiyo, furaha yetu ambayo imebaki
kwa sasa ni kumfunga mtani wetu Yanga katika mchezo wa mwisho wa ligi na kutibua sherehe hizo za ubingwa." alisema Masoud.
Pambano hilo la kufunga pazia la msimu wa Ligi soka Tanzania Bara 2012/13 litachezwa kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam Mei 18, mwaka huu.
Katika mchezo wa kwanza timu hizo mbili kongwe kwa soka zilitoka sare ya kufungana bao 1-1.
Simba ilikuwa ya kwanza kujipatia bao lake lililozamishwa na Amri Kiemba wakati Said Bahanuzi akiisawazishia Yanga bao hilo kwa mkwaju wa penalti.
Simba ilikuwa ya kwanza kujipatia bao lake lililozamishwa na Amri Kiemba wakati Said Bahanuzi akiisawazishia Yanga bao hilo kwa mkwaju wa penalti.
Friday, May 3, 2013
KALI YA LEO: MKURUGENZI WA DORTMUND AJIFUNGIA CHOONI KUOGOPA COMEBACK YA REAL MADRID
Mkurugenzi mtendaji wa Borussia Dortmund Hans-Joachim Watzke alikuwa kwenye hali ngumu mno katika dakika z mwish za mchezo wa pili wa nusu fainali ya Ligi ya mabingwa wa ulaya dhidi ya Real Madrid kiasi cha kuacha kuangalia mpira na kukimbilia chooni.
Borussia Dortmund walikuwa wakishambuliwa kama nyuki huku Madrid wakipata mabao mawili ya haraka haraka hivyo kukaribia kuwatoa Wajerumani hao ikiwa wangepata bao lingine.
Mwishoni Dortmund wakakaza na kufanikiwa kuitoa Real kwa jumla ya mabao 4-3, lakini Watzke anakiri dakika za mwisho za mchezo huo zilikuwa ni ngumu kuliko zote katika maisha yake ya uongozi wa soka.
Alisema: “Inaonekana tunapenda sana kujipa presha wenyewe
“Kwa mara kwenye maisha yangu ya soka niliacha kuangalia mpira kwa kuhofia matatizo ya moyo wangu.
“Ilinibidi niende chooni kwenye dakika za mwisho, nikajifungia, nikayafunga masikio yangu na nikawa naangalia tu muda kwenye saa yangu.
“Nilikuwa kwenye hali mbaya sana - mawazo kibao yalikuwa ndani ya kichwa changu kwa muda ule.”
Watzke hakuwa kiongozi pekee wa Dortmund aliyekuwa kwenye hali mbaya kiasi cha kutishia afya yake. Mkurugenzi wa michezo wa Borussia Michael Zorc alikiri nae nusra apate mshtuko wa moyo.
KOCHA WA SIMBA: MPIRA WA KASI NDIO TUTAOTUMIA KUIMALIZA YANGA
Kocha Mkuu wa Simba, Patrick Liewig ametamka kuwa silaha yake kubwa kwenye mchezo wa Yanga ni kasi ya wachezaji
wake, ingawa amekiri wanatakiwa kuwa makini kwa dakika zote 90 za mchezo.
Mfaransa huyo alisema jijini Dar es Salaam kuwa tayari wamepoteza ubingwa wa ligi pamoja na nafasi ya pili ambayo
ingeweza kuifanya timu hiyo ishiriki Kombe la CAF mwakani.
"Hatuna nafasi tena ya kushinda taji la ligi kwa msimu huu wala kumaliza katika nafasi ya pili ambayo ingetupa fursa ya kushiriki Kombe la CAF mwakani.
"Kilichobaki ni kulinda heshima yetu kwa kuwafunga mabingwa (Yanga) katika mchezo wetu wa mwisho hiyo Mei 18. Timu yangu ya Simba ina wachezaji wengi vijana ambao wana kasi kubwa kuwazidi Yanga." alisema kocha huyo aliyerithi mikoba ya Mserbia Milovan Cirkovic aliyetupiwa virago na klabu hiyo mwaka jana.
Kocha huyo aliongeza; "Yanga ni timu nzuri hakuna mtu anayepinga hilo, lakini haiwezi kumudu kasi ya wachezaji
wangu vijana.
"Nimewaona katika mechi kadhaa za ligi, wanacheza vizuri ingawa sitaki kuamini kwamba watashinda mbele ya vijana wangu imara."
Liewig alisema katika kambi ya kujiwinda na mchezo huo ataongeza muda wa programu yake ya mazoezi kuhakikisha kikosi chake kinakuwa katika hali nzuri ya ufiti kabla ya kukutana na watani hao wa jadi katika soka la Tanzania Bara na kuharibu sherehe za ubingwa huo.

HAYA NDIO MAPATO YA MECHI YA YANGA DHIDI YA COASTAL UNION - LIGI KUU KUENDELEA WIKIENDI SIMBA VS RUVU
YANGA, COASTAL UNION ZAINGIZA MIL 66
Mechi
namba 172 ya Ligi Kuu ya Vodacom kati ya Yanga na Coastal Union
iliyochezwa juzi (Mei 1 mwaka huu) kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam
na kumalizika kwa timu hizo kutoka sare ya bao 1-1 imeingiza sh.
66,022,000.
Watazamaji
11,478 walikata tiketi kushuhudia mechi hiyo ambayo viingilio vilikuwa
sh. 5,000, sh. 8,000, sh. 15,000 na sh. 20,000 huku kila klabu ikipata
mgawo wa sh. 15,378,927.45 wakati Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT)
iliyolipwa ni sh. 10,071,152.54.
Kiingilio
cha sh. 5,000 ndicho kilichovutia watazamaji wengi ambapo waliokata
tiketi hizo walikuwa 10,230 na kuingiza sh. 51,150,000 wakati idadi
ndogo ya washabiki ilikuwa ya kiingilio cha sh. 20,000 kilichovutia
washabiki 69 na kuingiza sh. 1,380,000.
Mgawo
mwingine wa mapato hayo ni asilimia 15 ya uwanja sh. 7,819,793.62,
tiketi sh. 3,818,890, gharama za mechi sh. 4,691,876.17, Kamati ya Ligi
sh. 4,691,876.17, Mfuko wa Maendeleo ya Mpira wa Miguu (FDF) sh.
2,345,938.09 na Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Dar es Salaam (DRFA)
sh. 1,824,618.51.
LALA SALAMA VPL KUENDELEA JUMAPILI
Ligi
Kuu ya Vodacom (VPL) inaendelea Jumapili (Mei 5 mwaka huu) kwa mechi
moja kati ya Ruvu Shooting na Simba itakayochezwa Uwanja wa Taifa, Dar
es Salaam kuanzia saa 10.15 jioni.
Hiyo
itakuwa mechi ya raundi ya 24 kwa timu hizo ambapo Simba iko nafasi ya
nne ikiwa na pointi 39 nyuma ya mabingwa Yanga wenye pointi 57, Azam
yenye pointi 48 na Kagera Sugar ambayo ina pointi 40. Ruvu Shooting iko
katika nafasi ya saba ikiwa na pointi 31.
Hadi
sasa mabao 348 yameshafungwa katika ligi hiyo huku Yanga ikiongoza kwa
kufunga 45. Polisi Morogoro yenye pointi 22 katika nafasi ya 12 ndiyo
iliyofunga mabao machache ikiwa nayo 13 tu.
African
Lyon yenye pointi 19 katika nafasi ya mwisho ndiyo inayoongoza kwa kuwa
na kadi nyingi. Timu hiyo inayofundishwa na Charles Otieno ina kadi 44
ambapo kati ya hizo nne ni nyekundu. Mtibwa Sugar ya Manungu, Turiani
mkoani Morogoro yenyewe inaongoza kwa kuwa na kadi nyingi nyekundu
ambapo hadi sasa inazo saba.
Subscribe to:
Posts (Atom)