WINGA wa Mgambo JKT, Chande Magoya ametoa siri kuwa alifuatwa na kocha
msaidizi wa Yanga, Fredy Minziro akimtaka ajiunge na timu hiyo kwa msimu
ujao wa ligi.
Akizungumza jijini Dar es Salaam winga huyo mwenye kasi na kipaji cha kipiga chenga za maudhi uwanjani alisema;
"Ni kweli. Mechi yetu na Yanga ilipomalizika Mkwakwani. Minziro alifuata
na kunipongeza kuwa nilicheza vizuri na kuisumbua timu yake kwa dakika
zote 90 za mchezo."
Magoya alisema baada ya kumpongeza kwa kiwango
kizuri cha soka, kocha huyo alianza kumtania kuwa yupo tayari kutua
Yanga iwapo itamwitaji.
"Baada ya kunipongeza aliniuliza iwapo timu hiyo itakuwa inataka
kunisajili nipo tayari. Nikamjibu bila shaka isipokuwa sitaki kukaa
benchi." alisema Magoya.
Minziro ilipotafuta kwa ajili ya kuthibitisha hilo, simu yake yake kiganjani ilikuwa akiita bila kupokelewa.
Katika pambano hilo lililopigwa kwenye Uwanja wa Mkwakwani, Tanga, timu hizo mbili zilitoka sare ya bao 1-1.
No comments:
Post a Comment