Search This Blog

Tuesday, May 7, 2013

MABAO 352 YATINGA NYAVUNI LIGI KUU MSIMU: TCHETCHE BAO ANAWAPELEKA PUTA WASHAMBULIAJI WENGINE

JUMLA ya mabao 352 yamefungwa katika mechi 173 zilizochezwa kwenye Ligi soka Tanzania Bara iliyoanza kutimka rasmi Septemba 15, mwaka jana.
Kwa idadi hiyo ni sawa na wastani wa kila mechi ya ligi ambayo inachezwa, mabao mawili yanafungwa.
Yanga ambayo imeshatwaa taji hilo kabla ya ligi kumalizika imepachika mabao 45 kwenye ligi hiyo kwa mechi zake 25 iliyocheza, sawa na uwiano wa kupachika mabao mawili kila mchezo.
Pia, ni timu ambayo ina ngome imara ya ulinzi. Imeruhusu magoli 14 kutikisa nyavu zake ambayo ni machache zaidi.
Maafande wa JKT Ruvu ya Pwani ndiyo timu ambayo imekuwa na safu dhaifu zaidi ya ulinzi ikiwa imefungwa jumla ya magoli 39.
Polisi Moro iliyorejea Ligi Kuu na kushuka kwa mara nyingine imekuwa na fowadi butu zaidi ya timu zote 14 zilizoshiriki ligi hiyo.
Katika mechi zake 25 iliyocheza kwenye ligi hiyo imefanikiwa kufunga mabao 13 pekee.
Mshambuliaji wa Azam FC, Kipre Tchetche ndiye anayeongoza kwa kufunga mabao 16 akifuatwa na Mrundi Didier Kavumbagu wa Yanga mwenye magoli tisa.

1 comment:

  1. Umesahau kitu kimoja kwamba hadi hivi sasa Simba imefungwa mabao 23 katika mechi 24walizocheza,rekodi mbovu zaidi ya magoli ya kufungwa kwa Simba kwa karibu misimu mitano iliyopita.Kila timu katika timu zote 12 imeweza kujipatia angalau bao moja katika moja wapo ya mechi ilizocheza na Simba.Kaseja amefungwa magoli 18 kwa mechi 19 alizocheza,Dhaira amefungwa goli 4 kwa mechi 3 na Mweta goli 1 kwa mechi 1.Hii ndiyo defence itakayoizuia Yanga kufunga magoli Mei 18

    ReplyDelete