Wanachama wa Tawi la Simba la Mpira Pesa la Magomeni jijini Dar es Salaam wanatarajia kukutana (Jumapili) kwa ajili ya kuweka mikakati ya kuhakikisha timu hiyo inaibuka ushindi katika mchezo wa mwisho na mtani wake Yanga.
Mwenyekiti wa tawi hilo, Ustaadh Masoud alisema jijini Dar es Salaam kuwa wamepanga kukutana wanachama wote wa tawi hilo hiyo kesho kwa lengo la kuweka mikakati yakuifunga Yanga.
"Tunafikiri klabu yetu ya Simba imepoteza ubingwa wa ligi. Pia kumaliza nafasi ya pili kwenye ligi
ambayo ingetupa fursa ya kushiriki Kombe la CAF mwakani. Kwa hiyo, furaha yetu ambayo imebaki
kwa sasa ni kumfunga mtani wetu Yanga katika mchezo wa mwisho wa ligi na kutibua sherehe hizo za ubingwa." alisema Masoud.
Pambano hilo la kufunga pazia la msimu wa Ligi soka Tanzania Bara 2012/13 litachezwa kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam Mei 18, mwaka huu.
Katika mchezo wa kwanza timu hizo mbili kongwe kwa soka zilitoka sare ya kufungana bao 1-1.
Simba ilikuwa ya kwanza kujipatia bao lake lililozamishwa na Amri Kiemba wakati Said Bahanuzi akiisawazishia Yanga bao hilo kwa mkwaju wa penalti.
Simba ilikuwa ya kwanza kujipatia bao lake lililozamishwa na Amri Kiemba wakati Said Bahanuzi akiisawazishia Yanga bao hilo kwa mkwaju wa penalti.
No comments:
Post a Comment