Search This Blog

Monday, May 6, 2013

MBWANA SAMATTA, YONDANI, KAPOMBE, BOCCO, NANI KUWA MCHEZAJI BORA WA TANZANIA - TCHETCHE, OKWI, NIYONZIMA NA KIIZA NANI KUWA MCHEZAJI BORA WA KIGENI?

KLABU ya Azam imeingiza wachezaji wawili katika kinyang’anyiro cha tuzo ya Mwanasoka Bora kwenye Tuzo za Wanamichezo Bora za Chama cha Waandishi wa Habari za Michezo Tanzania (TASWA) 2012/2013.

Uongozi wa TASWA kupitia kwa katibu wake mkuu Amri Muhando aliwataja wanandinga hao wa Azam ambao wameingia katika tuzo hizo ambazo zitafanyika baadaye mwaka huu kuwa ni Khamis Mcha pamoja na John Bocco (Adebayo).

Hata hivyo, katika vita hiyo ya kumtafuta mwanasoka bora wa Tanzania wachezaji hao watachuana vikali na Kevin Yondani (Yanga), Shomary Kapombe (Simba) anayeshikilia tuzo hiyo, Mbwana Samatta pamoja Thomas Ulimwengu wote kutoka TP Mazembe ya DRC.

Azam pia imeingia mchezaji mmoja katika kipengele cha tuzo ya Mwanasoka Bora wa Kigeni anayecheza Tanzania, ambaye ni Kipre Tchetche kutoka Ivory Coast atakayechuana na Mganda Emmanuel Okwi aliyekuwa Simba na sasa anakipiga katika klabu Etoile du Sahel ya Tunisia.

Wachezaji wengine katika kipengele hicho ni, Haruna Niyonzima na Hamisi Kiiza (Yanga).


Upande wa wanasoka wa kike, Fatuma Mustafa atachuana na Asha Rashid, Mwanahamisi Omary, Sofia Mwasikili anayeshikilia tuzo huyo pamoja na Esther Chabruma.

Katika hatua nyingine Muhando alisema aliongeza kuwa kwa upande wa mchezo wa ngumi za kulipwa Francis Miyeyusho anachuana vikali na Ramadhan Shauri, Thomas Mashali, Said Mbelwa na Francis Cheka.

2 comments:

  1. Kuna mapungufu makubwa katika zoezi hili,sijui ni vigezo gani wanavyotumia kama ni mwaka wa kalenda au mwaka wa fedha.Kama ni msimu wa 2012/2013 Okwi amecheza mechi zisizozidi tano tu hivyo huwezi kumweka okwi ukamuacha Mbuyu Twite aliyeng'ara msimu mzima.Halafu kwa wachezaji wa ndani bado kuna watu kama Mrisho Ngassa, Amri Kiemba na Salum Abubakar wameng'ara msimu mzima lakini wameachwa

    ReplyDelete
  2. Nje mada kidogo Shaffih.Nani anategeneza jezi za timu ya Taifa stars?Jezi utadhani sijui nini.Naongelea quality ya materials.Zinatepeta mno.Jasho kidogo vimeshatepeta,angalia hizo Bukta..Halafu nenda Chini Angalia jezi ya Simba aliyovaa Amri Kiemba na wachezaji wa Azam hapo juu,jezi ni nzito na nzuri.TFF iliangalie hili suala.Timu za Ulaya zile ziko mbali kidogo,quality ya jezi zao iko juu mno.Wachezaji wakizivaa "zinawatoa' kweli.

    Asante

    ReplyDelete