Wakati leo tarehe 6 Mei kipigo cha cha 5-0 cha Simba walichowapa watani wao wa jadi Yanga kikitimiza mwaka mmoja - uongozi wa Yanga umesema kuwa heshima waliyoipoteza msimu uliopita baada ya kutandikwa na Simba mabao 5-0, lazima irudi Jangwani katika mchezo wa mwisho wa Ligi Kuu utakaozikutanisha timu hizo mbili Mei 18 kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Katibu Mkuu wa Yanga, Lawrance Mwalusako amesema kuwa hivi sasa
wapo katika maandalizi kabambe kwa ajili ya mechi hiyo ili kuhakikisha wanajibu kipigo hicho walichokipata msimu uliopita.
Alisema mechi hiyo ina umuhimu mkubwa sana kwao kuhakikisha wanashinda licha ya kuwa tayari wameishatwaa ubingwa wa Ligi Kuu msimu huu wakiwa bado na mechi mbili mkononi.
"Tayari timu yetu ipo kambini na inaendelea kujifua kwa mazoezi makali kabisa ya kujiandaa na mchezo wetu wa mwisho wa Ligi Kuu msimu huu dhidi ya Simba," alisema Mwalusako na kuongeza kuwa ushindi katika mechi hiyo utanogesha sherehe zao za kusherehekea ubingwa wao wa 24 wa Ligi Kuu tangu ilipoanzishwa.
HAPPY BIRTHDAY 5-0
ReplyDeleteMwalusako ndg yangu kwa yeboyebo kuchomoa!! ili heshima irudi, hilo sahau.Mnyama anatisha!dhahiri kitete na mchecheto vimeanza!
ReplyDeleteLipa Kwanzaa zile sita za 77 ndo baadaye ulipe 5. Kulipa tano ndoto ya mchana kweupeeeee pole mwalusako
ReplyDelete