BARUA RASMI KUTOKA FIFA KUJA KWA TFF KUHUSU UCHAGUZI WA TFF
Tungependa
kuwafahamisha kuwa hali inayoendelea sasa kwenye shirikisho la soka la Tanzania
TFF ilijadiliwa na kamati ya dharura ya FIFA tarehe 28 aprili mwaka 2013.
Kamati hii ilizingatia yale ambayo yalionekana kama dosari na ujumbe wa FIFA, zaidi kitendo cha kamati za TFF kukataa kuwapitisha baadhi ya wagombea kwenye mchakato wa uchaguzi mkuu kwa kigezo cha ukiukwaji wa baadhi ya taratibu zinazosimamia uchaguzi huo vikiwemo kipengele cha tisa na cha saba pamoja na kipengele cha 29 kwenye katiba ya shirikisho. Kwa kufanya hivyo kamati ya uchaguzi ilifanya baadhi ya maamuzi ambayo ilijiridisha kuwa yameenda kinyume na taratibu ( mfano kupeleka kesi mahakamani, matumizi mabaya ya fedha za shirikisho na kutokuwepo kwa uwajibikaji ) wakati TFF haikuwahi kuchukua hatua zozote. Haya yote yalipelekea mgombea mmoja kuondolewa kwenye mchakato wa uchaguzi bila kujua adhabu yake. Iligunduliwa kuwa TFF ilikuwa haina vyombo ambavyo vinapaswa kushughulikia kesi za masuala ya maadili jambo ambalo lilipelekea kamati ya uchaguzi kujivika madaraka ya kuwahukumu wagombea wakati jukumu kubwa la kamati likiwa kuwathibitisha wagombea kama wanastahili kuingia kwenye mchakato au la.
Kamati hii ilizingatia yale ambayo yalionekana kama dosari na ujumbe wa FIFA, zaidi kitendo cha kamati za TFF kukataa kuwapitisha baadhi ya wagombea kwenye mchakato wa uchaguzi mkuu kwa kigezo cha ukiukwaji wa baadhi ya taratibu zinazosimamia uchaguzi huo vikiwemo kipengele cha tisa na cha saba pamoja na kipengele cha 29 kwenye katiba ya shirikisho. Kwa kufanya hivyo kamati ya uchaguzi ilifanya baadhi ya maamuzi ambayo ilijiridisha kuwa yameenda kinyume na taratibu ( mfano kupeleka kesi mahakamani, matumizi mabaya ya fedha za shirikisho na kutokuwepo kwa uwajibikaji ) wakati TFF haikuwahi kuchukua hatua zozote. Haya yote yalipelekea mgombea mmoja kuondolewa kwenye mchakato wa uchaguzi bila kujua adhabu yake. Iligunduliwa kuwa TFF ilikuwa haina vyombo ambavyo vinapaswa kushughulikia kesi za masuala ya maadili jambo ambalo lilipelekea kamati ya uchaguzi kujivika madaraka ya kuwahukumu wagombea wakati jukumu kubwa la kamati likiwa kuwathibitisha wagombea kama wanastahili kuingia kwenye mchakato au la.
Kwa mazingira hayo , kamati ya dharura ya FIFA iliamua yafuatayo.
*TFF iunde vyombo ambavyo vitasimamia masuala ya maadili ambayo yatasimamia kesi zote za maadili kwenye mchakato wa uchaguzi .
*Kuhakikisha mabadiliko ya katiba yanafanyika .
Kuanza upya mchakato wa uchaguzi kwa kufungua upya utaratibu wa usaili wa wagombea wote .
*Kuhakikisha mchakato wa uchaguzi unafanyika mpaka kufikia oktoba 30 .
*Maamuzi haya ya kamati ya a dharura ya FIFA yanamaanisha kuwa TFF lazima iite mkutano mkuu wa dharura ili kusimamia mabadiliko ya katiba na mchakato wa uchaguzi. FIFA na CAF ziko tayari kuisaidia TFF kwenye utekelezwaji wa maagizo haya
******* mwisho***********************************************
HII NDIO TAARIFA WALIYOTOA TFF KUTOKA FIFA WIKI ILIYOPITA
Shirikisho
la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA) limelitaka Shirikisho la Mpira wa
Miguu Tanzania (TFF) kuanza upya mchakato wa uchaguzi baada ya kubaini
kasoro iliyotokana na ukosefu wa kutokuwepo vyombo vya kushughulikia
ukiukwaji wa maadili.
FIFA
ambayo ilituma ujumbe wake katikati ya mwezi uliopita kufanya utafiti
kuhusu mchakato wa Uchaguzi Mkuu wa TFF ambao ulisimamishwa baada ya
baadhi ya wagombea kulalamika, imetaka uchaguzi ufanyike kabla ya tarehe
30 Oktoba 2013, lakini ukitanguliwa na mabadiliko ya katiba ambayo
yatahusisha uundwaji wa vyombo vya kushughulikia ukiukwaji wa maadili.
Raiswa
TFF, Leodegar Tenga aliwaambia waandishi wa habari kwenye ukumbi wa
mikutano wa shirikisho hilo kuwa suala la Tanzania lilijadiliwa kwenye
kikao cha Kamati ya Dharura ya FIFA kilichofanyika tarehe 28 Aprili 2013
na maamuzi yake kutumwa juzi kwa barua iliyosainiwa na KatibuMkuuwa
FIFA, Jerome Valcke.
Baada
ya kupokea barua hiyo, Rais wa TFF alifunga safari kwenda Dodoma jana
kukutana na Mheshimiwa Waziri na Naibu wake pamoja na Mwenyekiti wa
Baraza la Michezo la Taifa (BMT).
“Matarajio
yetu sote yalikuwa kupokea majina ya waliopitishwa ili tufanye
uchaguzi. Kinyume chake tumepokea maagizo hayo. Hata hivyo tumeona kuwa
hili ni jambo la kheri kwa vile siyo tu haki itatendeka bali pia
itaonekana imetendeka.” alisema Tenga, ambaye alishatangaza kuwa
hatagombea tena urais baada ya kuliongoza Shirikisho kwa vipindi viwili
vya miaka minne kila kimoja.
“Lengo
letu ni kuhakikisha maagizo hayo yanatekelezwa na uchaguzi kufanyika
mapema iwezekanvyo kabla ya tarehe iliyotolewa. Yale mambo nayoweza
kufanyika kwa pamoja yatafanyika ili tuharakishe utekelezaji wa maagizo
yaliyotolewa na FIFA.”
Uchaguzi
wa TFF ulipangwa kufanyik tarehe 23 na 24 Februari 2013 na ulikuwa
ukielekea ukingoni, lakini baadhi ya wagombea walienguliwa katika hatua
ya mwisho na Kamati ya Rufani ya Uchaguzi ya TFF na ndipo walipo andika
barua FIFA kuomba iingilie kati.
Rais
Tenga alisema kuwa ujumbe wa FIFA ulikutana na pande zote
zilizoathiriwa na mchakato wa uchaguzi na kwamba baada ya kukusanya
taarifa hizo, maagizohayo ya FIFA sasa yatakuwa ni suluhisho la matatizo
ya muda mrefu katika uendeshaji wa mpira wa miguu nchini.
Katika barua hiyo, FIFA imeiagizaTFF:
1. Kuunda
vyombo sahihi (Kamati ya Maadili itakayokuwa na vyombo viwili ambavyo
ni cha kutoa maamuzi ya awali na cha rufaa) ambavyo mamlaka yake
yatakuwa ni kushughulikia masuala ya ukiukwaji wa maadili;
2. Kufanya mabadiliko ya katiba kwa kuzingatia uundwaji wa vyombo hivyo;
3. Kuanza
upya kwa mchakato wa uchaguzi wa Kamati ya Utendaji kwa kufungua
milango kwa wagombea ambao walishachukua fomu na wagombea wapya:
4. Shughuli hiyo ikamilike ifikapo tarehe 30 Oktoba 2013.
Katika
kutekeleza hayo, TFF inatakiwa iitishe Mkutano Mkuu wa Dharura kwa
ajili ya kufanya mabadiliko ya Katiba kwa ajili ya kuunda kamati hizo za
maadili na Kanuni za Uchaguzi kabla ya kuendelea na Mkutano Mkuu wa
Uchaguzi wa Kamati Mpya ya Utendaji.
Katika
maoni yake FIFA imeeleza kuwa katika mchakato, Kamati ya Uchaguzi ya
TFF iliwaengua au kupitisha baadhi ya wagombea kwa kubaini kuwa
walikiuka Ibara ya 9 (7) ya Kanuni za Uchaguzi na pia Ibaray a 29 (7) ya
Katiba ya TFF ambavyo vinahusisha suala la kufungua kesi mahakamani,
kufuja fedha za shirikisho na ukosefu wa uwajibikaji wa pamoja.
Hata
hivyo, FIFA ilisema kuwa watu hao walitakiwa waadhibiwe kwanza na
kamati husika (kamati za maadili) kabla ya kuenguliwa na kamati za
uchaguzi za TFF.
“Kutokana
na ukosefu wa kamati za maadili matokeo yake, mmoja wa wagombea amekuwa
akienguliwa kwenye uchaguzi kila anapombea bila ya kujua adhabu yake ni
ya muda gani,” inasema barua hiyo ya FIFA.
Rais
Tenga ameagiza kuitishwa kwa kikao cha dharura cha Kamati ya Utendaji
ya TFF kupokea maagizo ya FIFA na kupanga ratiba ya utekelezaji wake kwa
lengo la kuhakikisha kuwa mchakato huu unatekelezwa mapema
iwezekanavyo.
Asante kwa kutufungua macho. Agizo la 1 na 2 linasema
ReplyDelete-establish appropriate organs(ethics Committee-first and second instance)whose competences would cover the above mentioned causes
-amend the TFF statutes accordingly
Halafu "the decision of the FIFA Emergence Committee means that the TT has to convene an extra-ordinary general assembly to amend the statutes and the electoral code before proceeding with an elective general assembly...
Sasa kwa maoni yangu ni kwamba mabadiliko ya katiba na Kanuni za uchaguzi yanayotakiwa kufanyika yanahusu kuingiza kamati za maadili tu na haimaainishi kwamba mabadiliko yaliyofanywa kwa waraka ni batili na yafanyike upya kwenye mkutano huo,neno "accordingly"limebeba maana kubwa.Halafu maneno ya mwisho kabisa yanasisitiza kwamba uamuzi huo wa kamati ya dharura ya FIFA unamaanisha kwamba TFF itatakiwa kuitisha mkutano mkuu wa dharura kufanya mabadiliko hayo mabadiliko hayo ya katiba na kanuni za uchaguzi za TFF(Kuingiza kamati za maadili ambazo zitashughulikia kesi za maadili za watu walioenguliwa)kabla ya kuitisha mkutano mkuu wa uchaguzi
Kuna wagombea walithubutu kuitisha mkutano wa waandishi wa habari na kutamka HADHARANI kuwa katiba ya TFF ya 2012 ni batili kabla hata ya mamlaka husika kuibatilisha,na wakawa wanawashambulia viongozi wa TFF kwa maamuzi yaliyofanywa na vyombo halali vya maamuzi vya TFF kana kwamba wamefanya viongozi hao binafsi,wakawadhalilisha wajumbe wa kamati hizo kama vibaraka wa viongozi wa TFF ilhali hawa ni watu wenye hadhi zao katika jamii,na wakadiriki kuandika barua Serikalini kupinga kusajiliwa kwa katiba ya TFF huku wao wakiwa siyo wajumbe wa mkutano mkuu wa TFF na huku wakiwa wameshakata rufaa FIFA.Watu hawa wanataka kujenga culture ya kutokuaminiana katika familia ya soka na kuwafanya watu wenye heshima zao waogope kuteuliwa kwenye vyombo vya maamuzi vya TFF.JE HUU SIO UTOVU WA MAADILI?Aidha kuna watu walimpotosha Waziri kwamba FIFA haina mamlaka ya kuingilia mambo ya ndani ya nchi yetu na kutaka atumie mabavu kumaliza mgogoro huu ingawa watu hao hao wamejkuwa wa kwanza kuipongeza FIFA
ReplyDelete