TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI;
YAH; MCHAKATO WA UCHAGUZI WA TFF 2012/2013.
Mimi Mbasha Matutu Mjumbe wa Mkutano Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga na niliyekuwa Mgombea wa Ujumbe wa Kamati ya Utendaji kupitia zone no 3.katika uchaguzi uliotakiwa kufanyika tangu 14/12/2012 nimepokea kwa furaha sana taarifa ya FIFA iliyotolewa na Rais wa TFF Bw Leodeger Tenga juu ya mchakato mzima wa uchaguzi wa TFF.
Pia napenda nichukue fulsa hii kuwapongeza wandishi wa habari kwa ujasiri wao mkubwa waliokuwa nao wa kulielezea jambo hili bila kumwonea mtu wala kupendelea mtu yeyote, kikubwa walichojali ni uzalendo wa Nchi yetu kwa ujumla.
Pia napenda nichukue fulsa hii kuishukru sana Serikari yetu ya tanzania chini ya uongozi wa jemedali mkuu Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Jakaya Mrisho Kikwete na Wizara husika ya Michezo inanyoongozwa na Mawaziri makikini wanaojali haki za Raia wake, kubwa zaidi namna walivyolishughulikia suala hili la Katiba ya TFF na mchakato mzima wa uchaguzi.
Nawapongeza pia FIFA kwa namna nzuri walivyoshughulika na suala hili na jinsi walivyoagiza litekelezwe, hii imenipa matumaini na faraja ya kwamba tutaenda kukomesha matabaka yaliyokuwa yameanza kujitokeza na kuhatarisha msitakabali mzima wa mpira miguu nchini mwetu na kunipa matumaini ya kunifanya nia yangu ya kugombea nafasi ya ujumbe ibaki pale pale muda utakapofika.
Pia nawapongeza watanzania wote kwa ujumla kwa namna walivyoonyesha uvumlilivu wao mkubwa kwa kipindi chote cha malumbano yaliyokuwepo ya nani anapaswa kugombea na nani hapaswi kugombea na kuchukua nafasi kubwa kwenywe vyombo vya habari hasa magazeti,Radio,Runinga na mitandao ya kijamii na hii inaweza kuwa ilipunguza baadhi ya taarifa muhimu zilizokuwa zinatakiwa kuwafika watanzania kwa ajili ya kukuza uchumi wao.
Vile vile napenda nichukue fulsa hii kuwapongeza wajumbe wa mkutano mkuu wa TFF wenzangu kwa uvumilivu wenu mliouonyesha maana mlikuwa na uwezo wa kuamua vyovyote vile, lakini kwa hekima mlizojaliwa na Mwenyezi Mungu mliendelea kuiamini Serikali yenu wakati wote wa mchakato na hii imedhihilisha kuwa Serikali yetu ni sikivu na inawapenda watu wake wote na ni kinara wa demokrasia pia tukumbuke tunalo jukumu kwa niaba ya watanzania wote kuhakikisha TFF inaendeshwa kwa kufuata Katiba,Kanuni na Miongozo hii itatusaidia kuinua mpira wa miguu nchini mwetu na haya ili yatimie tunahitaji mshikamano wetu kwa pamoja bila kujali rangi yetu, kabila letu, ukanda wetu au udini wetu.
Pia napenda kumshukru Mwenyekiti wangu wa SHIREFA Bw Bennester Rugora na Kamati nzima ya SHIREFA kwa namna walivyonishauri tangu pale nilipoonyesha nia ya kugombea ujumbe wa Kamati Tendaji sina cha kuwalipa naomba msikome kunishauri pale mchakato utakapoanza.
OMBI LANGU.
Naomba nichukue fulsa hii kutoa ombi langu kwa Rais wa TFF na kamati nzima ya Utendaji katika kutekeleza maagizo ya FIFA,nakuomba/nawaomba mtangulize utaifa na uzalendo kwanza mambo ya umimi msiyape nafasi tena.
Pia wakati wa kuunda kamati hizo mlizoelekezwa na FIFA hakikishe suala la u-Dar Es salaam, u School mate, na urafiki mnaviepuka badala yake zingatieni geografia ya Nchi yetu maana hata mikoani kuna watanzania wenye uwezo na uzalendo kwa nchi yao .
Pia mara tu baada ya kuwapendekeza wajumbe hao nawaomba majina yao na sifa zao zitangazwe hazarani na majina yao yaletwe kwenye mkutano mkuu wa TFF kwa ajili ya ukubali wa Wajumbe.
HITIMISHO.
Napenda nihitimishe kwa kuwaomba wadau wote wa mpira wa miguu kuwa wamoja wakati wote wa mchakato huu, na kuliombea zoezi zima kwa Mwenyezi Mungu liende salama mpaka hapo tutakapo pata viongozi wetu wapya,
‘Mungu ibariki Tanzania Mungu ibariki Africa ’’
……………………………..
Mbasha Matutu
Mjumbe wa Mkutano mkuu TFF
MKOA WA SHINYANGA
Umeongea la maana mwanawane! Lakini siku nyingine uwe unapiga summary! Ama sivyo watu watachoka kusoma kitabu na ujumbe usiwafikie walengwa! Ushauri tu.
ReplyDeletesure shukrani zimekuwa na maneno mengi sana inachosha. ni kweki urafiki na ushemeji sio fleshi chagueni watu makini na huyu mwenyekiti kamati ya uchaguzi aondolewe kabisa hafai na haogopwe kama ukoma!
ReplyDeleteWanashinyanga kwani mmeshakamilisha zoezi la kukusanya saini za wajumbe ili kuitisha mkutano wa dharura wa kumng'oa Tenga?halafu hilo hitimisho la Mungu ibarki Tanzania nbio kitambulisho cha kambi fulani
ReplyDelete