Search This Blog

Thursday, August 23, 2012

Airtel Rising Stars Tanzania yatoka sare na Burkina Fasso


Michuano ya Afrika Airtel Rising Stars Tanzania yatoka sare na Burkina Fasso
Wawakilishi wa Tanzania katika michuano ya Airtel Rising Stars kwa
nchi za Afrika, (leo hii)  imetoka sare ya bao 1-1 na Burkina Fasso,
katika mchezo uliofanyika katika uwanja wa Nyayo, jijini Nairobi.
Matokeo hayo yanaiweka Tanzania shakani kusonga mbele katika michuano
hiyo baada ya jana kuianza vibaya kwa kukubali kufungwa bao 1-0 na
Gabon katika mchezo wake wa kwanza.

Kufuatia matokeo hayo Tanzania inasubiri bahati tu ili kusonga mbele
kwani sasa itabidi kushinda mchezo wake wa mwisho utakaofanyika kesho
23/08/2012 dhidi ya Zambia na wakati huo huo kuiombea Gabon iifungwe
na Zambia katika mchezo wao wa mwisho. Kila kundi itatoa timu moja
kusonga mbele hatua ya robo fainali zinazotarajiwa kuanza kesho kutwa.
Katika mchezo wa jana, Burkina Fasso ndiyo ilikuwa ya kwanza kupata
bao la kushtukiza katika dakika ya kwanza ya kipindi cha pili na hivyo
kuwafanya vijana hao wa Tanzania kutulia na kuanza kucheza pasi za
kuonana hali iliyozaa matunda dakika kumi baadaye.
Goli la kusawazisha la Tanzania lilipachikwa kimiani na mshambuliaji
wake hatari Paulo Balama aliyepokea pasi akiwa kati ya uwanja na
kuchanja mbuga kuelekea langoni mwa wapinzani wao, ambapo kabla ya
kufunga aliwapunguza mabeki watatu na kisha kumlamba chenga kipa wa
Burkina Fasso na kuachia kiki kali iliyokwenda moja kwa moja wavuni.
Akizungumza mara baada ya mchezo huo, Kocha na mkuu wa msafara wa timu
ya Tanzania, Salum Madadi alisema vijana wake walicheza vizuri
isipokuwa tatizo ni kutopata muda wa kutosha wa wachezaji wake
kuzoeana hasa ikizingatiwa kuwa timu hiyo inaundwa na kombaini ya
wachezaji kutoka mikoa sita tofauti.
"Kwa mfano mchezo wetu wa juzi dhidi ya Gabon vijana walicheza vizuri
sana pamoja na tatizo la kutozoeana hata hivyo waliweza kuwabana
wapinzani kwa muda mwingi na hata kufika langoni mwa wapinzani wetu
kwa kupiga mashuti kadhaa ila bahati haikua yetu tu," alisema Madadi.
Matokeo mengine ya mechi zilizochezwa jana kwa wanaume ni Kenya kutoka
sare ya 1-1 na Ghana, Malawi pia kutoka sare ya 1-1 na Madagascar,
Nigeria kutoka sare ya 1-1 na Niger, Congo DRC kuichakaza Chad bao 5-0
na Zambia kuichapa Burkina Fasso 5-0. Kwa upande wa wanawake Congo DRC
iliichakaza Burkina Fasso magoli 8-0, Ghana nayo ikaichapa Kenya bao
7-2, Chad ikaifunga Nigeria bao 1-0 na Uganda kuifunga Sierre Leone
3-0.
Michuano hiyo ya Airtel Rising Stars kwa ngazi ya Afrika iliyoanzishwa
kwa lengo la kuibua vipaji kwa vijana wenye umri chini ya miaka 17,
Inafikia kilele keshokutwa kwa bingwa kupatikana ambapo mshindi huyo
atapata nafasi kwa wachezaji wa timu nzima kuhudhuria kliniki ya soka
ya kimataifa itakayoendeshwa na jopo la makocha kutoka klabu ya
Manchester United na Arsenal za Uingereza itakayofanyika kuanzia
Agosti 26 hadi 30 mwaka huu jijini Nairobi.

LIONEL MESSI AMFANYA KAI ROONEY AMSALITI BABA YAKE WAYNE ROONEY

Mtoto wa mchezaji wa Manchester United Wayne Rooney - Kai akiwa na mama yake Coleen na Mjomba wake huku akiwa ametinga jezi za klabu yenye upinzani mkubwa wa kisoka na kibiashara na timu anayochezea Baba yake- Wayne Rooney, Manchester United.

Kai akiwa ametinga jezi namba 10 ya Barcelona ambayo huvaliwa na Lionel Messi - taarifa zinasema mtoto huyo ana mapenzi makubwa na Messi kiasi cha wazazi wake kuamua kumridhisha na kumnunulia jezi za Barca.

LUOL DENG NA HASHEEM THABEET KUJA KUTOA MAFUNZO YA BASKETBALL DAR

Mcheza mpira wa kikapu wa timu ya Chicago Bulls raia wa Sudan ya Kusini Luol Deng kwa kushirikiana na mwanamichezo tajiri kabisa wa kitanzania, mwana kikapu Hasheem Thabeet watafanya clinic -draft program ya siku mbili kwa ajili ya wanafunzi wa shule za sekondari jijini Dar es Salaam tarehe 24 na 25 mwezi huu katika viwanja vya Don Bosco .

Clinic hii itakuwa maalum kwa kutoa mafunzo kwa vijana wa kitanzania ambao wana vipaji vya kucheza Basketball ili kuweza kukuza vipaji vyao zaidi.

Kabla ya kuja Bongo Luol na Hasheem walikuwa nchini Kenya, na leo mchana kwenye mtandao wa Twitter kuwa anakuja Dar es Salaam.


 
Kwa wale ambao hawamfahamu Luol Deng huu ndio wasifu wake.




Twitter: @LuolDeng9
Team: Chicago Bulls
Number: 9
Position: Forward
Country: South Sudan 
Born: April 16, 1985
Height: 6-9 / 2.06
Weight: 220 lbs. / 99.8 kg
Years Pro: 8
CAREER HIGHLIGHTS
·       Has started 439 of his 485 career appearances
·       Holds career averages of 16.0 points per game, 6.4 rebounds per game, while shooting 47% from the floor
·       Has posted 65 double-doubles
·       Drafted number seven overall by the Phoenix Suns in the 2004 NBA Draft / Traded to the Chicago Bulls on June 24 2004
AWARDS
·       United States Basketball Writers Association National Freshman of the Year – 2004
·       NBA All-Rookie First Team – 2005
·       NBA Sportsmanship Award – 2007
·       NBA All-Star – 2012
·       NBA All-Defensive Second Team – 2012
CAREER HIGHS
·       Points – 40 (Chicago Bulls – Portland Trail Blazers, Nov. 1 2010)
·       Rebounds – 20 (Chicago Bulls – Milwaukee Bucks, Nov. 3 2009)
·       Assists – 11 (Chicago Bulls – Sacramento Kings, Feb. 14 2012)

YANGA YAZURU MAKABURI YA WAHANGA WA MAUAJI YA KIMBARI RWANDA


Mwenyekiti wa bodi ya wadhamini wa klabu ya Young Africans, Mama Fatma Karume akiwaongoza viongozi na wachezaji wa yanga kwenda kuweka mashada ya maua katika makaburi ya mauaji ya Kimbari katika eneo la gisozi jijini kigali






Timu ya Young Africans iliyoko Kigali nchini Rwanda imetembelea eneo la makumbusho ya mauaji ya kimbari yaliyotokea mwaka 1994 na kusababisha wanyarwanda wengi kupoteza maisha katika vita iliyohusisha makabila mawili tofauti.
Young Africans iliyoko nchini Rwanda kwa ziara ya mafunzo ya wiki moja, jana jioni ilifanya mazoezi katika uwanja wa Nyamahoro kujiandaa na mchezo wake wa kwanza wa kirafiki dhidi ya Rayon Sports, mchezo utakaochezwa hapo kesho majira ya jioni. 

viongozi wa yanga wakisubiri kuzuru na kuweka mashada ya maua katika makaburi ya mauaji ya kimbari mwaka 1994.




Young Africans wakiwasili katika makaburi ya mauaji ya kimbari mjini kigali














Wachezaji na Viongozi wa yanga wakipata maelezo kabla ya kuingia kutembelea nyumba ya makumbusho ya mauaji ya kimbari














Jeryson Tegete akimtoka Godfrey Taita, wakati wa mazoezi katika uwanja wa Nyamirambo











Saimon Msuva (kulia) akichuana na Jeryson Tegete (kushoto) wakati wa mazoezi














Wachezaji wa Young Africans wakiwa wamejipumzisha katika hoteli ya kisasa ya La pallais mjini kigali (picha zote na PICHA NA SALEH ALLY WA CHAMPIONI

TAFAKARI! KUNA UTOFAUTI GANI KATIKA PICHA HIZI.





MJADALA: GOLI LA TORRES - JE HII ILIKUWA OFFSIDE???


EDEN HAZARD AENDELEA KUNG'ARA - CHELSEA IKIUA 4-2


C-R footyroom.com by footyroom

EXCLUSIVE: TENGA - BANGI SASA BASI KWENYE SOKA LA TANZANIA

Baada soka la Tanzania kuandamwa na kashfa ya wachezaji kutumia madawa ya kulevya aina ya bangi, sasa suala hilo linakaribia kupatikana njia ya kulizuia.

Akiongea exclusive na mtandao huu, Raisi wa shirikisho la soka la nchini Leogdar Tenga amesema suala la matumizi ya bangi kwa wacheza soka lipo sana kwenye soka na akasisitiza kwamba ni moja vitu vikubwa vinavyochangia maendeleo ya soka Tanzania kudumaa.

Leodgar Tenga ambaye mwishoni mwa mwaka huu anamaliza muda wake wa utawala kwenye uongozi wa TFF, amesema moja ya vitu vikubwa atakavyopigania wakati akiwa bado madarakani ni kulimaliza tatizo hilo la matumizi ya marijuana na madawa mengine yasiyoruhusiwa michezoni.

"Ni kweli tatizo la wachezaji kutumia Bangi lipo sana kwenye soka letu la Tanzania. Sasa nataka kuweka wazi kwamba kuanzia msimu ujao wale watumiaji wote watakumbana na hatari kubwa ya kupata adhabu kali. Kwa sababu tunajipanga kuwa tunawafanyia vipimo kila mara wanapocheza kwa kuwashtukiza tena ili kuweza kufanikisha kulimaliza tatizo hili." - Tenga.

Katika hatua nyingine Raisi huyo wa TFF ameshangazwa na baadhi ya viongozi wa soka kuendekeza siasa za kampeni kuhusu uchaguzi ujao wa TFF na kusahau kufanya shughuli za maendeleo na kukabiliana na changamoto zinazoikabili tasnia ya mchezo wa soka nchini.

EMMANUEL ADEBAYOR ATAMBULISHWA RASMI TOTTENHAM

Mshambulia wa kimataifa wa Togo Emmanuel Adebayor akiwa anatambulishwa kwa waandishi wa habari baada ya kujiunga moja kwa moja na klabu ya Tottenham Hotspur akitokea Manchester City.

Wednesday, August 22, 2012

MJADALA: NANI ZAIDI - MESSI MTOTO NA MESSI MKUBWA

KALI YA LEO: RAFU YA KALI YA WIKI - HIVI ALIKUSUDIA AU BAHATI MBAYA?

TOA MAONI YAKO: NANI AMELAMBA DUME KWENYE MABADILISHANO YA WACHEZAJI HAWA KATI AC MILAN NA INTER MILAN

Klabu mbili za Italia mahasimu AC Milan na Inter Milan zimekubalina juu ya mabadilishano ya wachezaji wao Giampaolo Pazzini na Antonio Cassano. Taarifa zinasema kwamba Rossoneri wameilipa Inter €7million ili kufanikisha dili hilo. Je kwa maoni yako unadhani kati ya vilabu hivi viwili nani amelamba dume kwa kubadilshana wachezaji hawa. Angalia video hizi then utoe maoni yako. 

 ANTONIO CASSANO GIAMPOLO PAZZINI

MANCHESTER CITY NA MFUMO MPYA WA KUCHEZA NA MABEKI WATATU. JE WATAFANIKIWA?




Manchester City walianza msimu wake kwa ushindi wa mabao 3-2 dhidi ya Chelsea wiki iliyopita. Kitu cha kukumbukwa kwenye mchezo huu ukiachilia mbali kadi nyekundu ya Ivanovic yalikuwa majaribio ya Roberto Mancini kuchezesha watu watatu nyuma badala ya mfumo uliozoeleka wa kuchezesha mabeki wanne.
Kuchezesha watu watatu si jambo geni sana kwa City . Mara kadhaa Mancini alijaribu kuchezesha watu watatu mara kadhaa kuelekea mwishoni mwa msimu uliopita kwenye baadhi ya michezo. Kipya katika mfumo huu hata hivyo ni ukweli kwamba anaanza mechi akitumia mfumo huu kinyume na msimu uliopita ambapo alikuwa akitumia mfumo huu kumaliza mechi.

Kwanini mabadiliko haya.


Moja ya shida ambazo Man City ilizipata msimu uliopita ilikuwa kukosa mashambulizi toka pembezoni mwa uwanja. David Silva na Samir Nasri si wachezaji ambao wanacheza vyema wakiwa pembeni ,wote ni viungo ambao hucheza vizuri zaidi wakiwa wanapitia katikati ya uwanja badala ya pembeni , kucheza kwa wachezaji hawa katikati mwa uwanja kuliwanyima wachezaji wanaotumia nafasi kubwa uwanjani kama Tevez na Yaya Toure kwa kuwa kama ilivyo kwa Silva na Nasri nao hupenda kucheza katikati.
Tatizo hili lilipatiwa ufumbuzi kwa muda msimu uliopita wakati alipocheza mtu kama Adam Johnson ambaye angetanua uwanja na kuipa timu balance iliyohitajika . Ila shida moja ni kwamba Mancini hana imani na Adam kiasi cha kumchezesha kila mara hivyo bado hali hii iliendelea kuwa tatizo.
Mancini alikuwa na ufumbuzi wa aina yake kwenye suala hili hasa kwenye mchezo muhimu wa ugenini kuelekea mwishoni mwa ligi dhidi ya Newcastle United. Huku mechi ikiwa inaelekea kuwa 0-0 kuelekea kipindi cha pili , Mancini alimuingiza Nigel De Jong kwenye nafasi ya Samir Nasri na kumsogeza mbele Yaya Toure . Katika akili ya mtu wa kawaida haya yalikuwa mabadiliko ya kujihami zaidi lakini mabadiliko haya yalimpa Toure nafasi ya kupanda na kusaidia mashambulizi. Baada ya hapa Toure alifunga mabao mawili yaliyoipa City ushindi wa mabao 2-0.
Kuchezesha mabeki watatu moja kwa moja kutaipa City nafasi zaidi ya kushambulia hata kama itamaanisha baadhi watalazimika kushuka kusaidia ulinzi. Na zaidi ya hapa Mancini anajaribu kuipa City mtazamo mbadala .

Inavyofanya kazi.


Mfumo wa City wa 3-4-1-2 unashuhudia walinzi watatu wakiwa wanalindwa na viungo wawili wakabaji mbele yao, wachezaji wawili wa pembeni na washambuliaji watatu.
Wakati timu ikimiliki mpira wachezaji wa Pembeni wanakuwa kama mabeki wa kushoto na wa kulia , wakijaza nafasi inayoachwa wazi na washambuliaji wa pembeni wakiwa wamepanda . Kwenye kipindi cha pili, City walichezesha mabeki wa pembeni ambao ni Clichy na Zabaleta kama mabeki wa kati wanaocheza pembeni . Beki anayecheza kati anacheza chni zaidi kati ya mabeki watatu.


Wakati timu ikiwa na mpira mfumo wa ulinzi wachezaji wanaocheza nyuma wanasaidia kumiliki mpira na kupoza presha lakini inafanya hali ya ukabaji kuwa ngumu na madhara yake ni kuifanya timu kuwa wazi sana na inaweza kufungika rahisi kwenye mashambulizi ya ghafla.
Kitu muhimu kwenye mfumo wa 3-5-2 ni wachezaji wanaocheza pembeni. Wanapaswa kutimiza majukumu ya mawinga na mabeki huku wakitanua uwanja wakati wa mashambulizi na kulazimika kukimbia kukaba wakati mpira ukipotea.


Wakati jukumu la beki wa pembeni ambaye anashambulia linapokuwa lazima kuliko lile la winga anayecheza mbele yake mara nyingi mabeki wa pembeni katika mifumo ya kisasa wanacheza kwa kutumia nafasi kubwa iliyoko mbele yao na mara nyingi hulazimika kukata na kuingia ndani.
Sababu kubwa ya beki anayecheza pembeni ya kuwafanya washambulie zaidi ni kwamba kwa mfumo wa sasa hakuna mchezaji maalum wa kukabana na beki wa pembeni .

Mwisho.

Majaribio ya Mancini ya kutumia mfumo wa 3-4-1-2 unaonyesha ishara ya kuleta vita ya kusisimua ya kimbinu wakati City ikiwa inacheza na timu nyingine hasa kwenye ligi ya mabingwa. Kama itakuwa inatumika kama mpango mbadala wa kiulinzi au mfumo wa kushambulia kwa kushtukiza tutapata majibu wakati michuano hii ikianza na mfumo huu utakapotumika, itakuwa tofauti na kile tulichozoea kukiona na kingine cha msingi ni jinsi mfumo huu utakavyofanya kazi dhidi ya timu kubwa kwenye ligi ya England.

KUTOKA 'A' MPAKA 'Z' KUHUSIANA NA MAISHA YA MARIO BALOTELLI



 A TO Z KUHUSU MARIO BALOTELLI


A - Ni kwa ajili ya AC Milan. Ikiwa wewe ni mchezaji wa Inter Milan, kitu gani cha kijinga ambacho unaweza kufanya na ukawakera kabisa kabisa mashabiki wa klabu yako? Kutembelea kwenye television ya taifa huku ukiwa umevaa jezi ya mahasimu wakubwa wa Inter, AC Milan!



B - Bib. Ni kipande cha nguo anachovaa Balotelli juu ya fulana yake ya kufanyia mazoezi.

C - Ni kwa ajili ya Camorra. Balotelli anatuhumiwa na wengi kwamba ana mahusiano na kundi la The Camorra - kundi ambalo linafanan kabisa na Mafia - na hii ilitokana na yeye kuonekana akipewa muongozo wa jiji la Napoli hasa kwenye viunga vya maeneo yenye sifa ya uhalifu sana na wahuni wa eneo hilo ambao ni wafanyakazi wa Camorra. Balotelli mwenyewe anadai hakuwa akiwafahamu watu hao kama wahalifu.

D  - Ni kwa ajili ya Derby.
Manchester United 1-6 Manchester City. Mario Balotelli alifunga mabao mawili na kuisadia City kuipa UTD  kipigo kizito katika historia yao katika premier league - kitu ambacho sio rahisi kwa washabiki wa United kusahau.

E - Ni kwa jili ya Ego - Kujiona au Majivuno: "Kuna mchezaji mmoja ambaye ana uwezo mkubwa kuliko mie lakini sio sana Lionel Messi. Wngine wote wananifuatia mimi."

F - Kwa ajili ya Fireworks
- Aina ya vifaa vya ulipuaji moto: Msimu uliopita aliripotiwa kurusha fireworks bafuni kwake na kusababisha moto mkubwa kwenye nyumba anayoishi.

G - Kwa ajili ya Generosity
- Ukarimu: Mario Balotelli amekuwa na kawaida ya kutoa noti za £20 kwa wapita njia barabarani.

H - Homeless - Kutokuwa na makazi - Baada ya kushinda £25,000 kwenye Casino, Balotelli akampa mwanaume mmoja ambaye hakuwa na makazi £1,000 cash. Alipoulizwa kwanini amefanya vile, alijibu ni kwa sababu alipenda nywele za yule aliyempa msaada.

I - Impound - kuwa chini miliki ya kisheria: Balotelli ameripotiwa kuwa gari lake aina Maserati sports limekuwa likikimatwa na kuwekwa kwenye kizuizi cha kisheria kwa mara 27 na kumfanya Balotelli alipe kiais cha £10,000 kama faini za kupaki ovyo gari lake hilo.

J - Jenny Thompson.
Changudoa ambaye alishawahi kuhusishwa kutembea na Wayne Rooney, alikuwepo kwenye mgahawa mmoja jijini Manchester na ndani ya mgahawa huo alikuwepo Balotelli, muitaliano huyo alipomuona msichana yule akaanza kuimba "Rooney Rooney Rooney" tena kwa sauti kubwa.

K - Karma - Jaribio la Balotelli kufunga bao kwa kisigino dhidi ya LA Galaxy lilimpa wakati mgumu mbele ya kocha wake Roberto Mancini. Alitolewa haraka baada ya kufanya jaribio hilo. Balotelli akadai alijaribu kufunga kwa kisigino kwa sababu alidhani alikuwa ameotea tayari.

L - Lothario. Balotelli aliripotiwa kumuita kwa nguvu mwanadada Lothario katika Mgahawa mmoja huko Manchester. Huku chakula kikimtoka mdomoni alimwambia Lothario amfuate. Kwa bahati nzuri msichana yule akaja. Akampa simu yake na kumwambia Lothario aandike namba yake ya simu na aifadhi. Binti yule akafuata maelekezo ya Balo na akaondoka bila kuongea kingine chochote na Mchizi Balotelli, na baadae ikaripotiwa kuwa wamekuwa wapenzi.

M - Kwa ajili ya Mario

N - Ni kwa ajili ya Nicklas Bendtner Syndrome.
Balotelli anagua kwa kile kitu ambacho wanasaikolojia wanakiita "Nicklas Bendtner Syndrome" - Mario Balotelli anaamini yeye ndio mchezaji bora kabisa ambaye duniani imewahi kumshuhudia.

O - Open top bus. Wakati City waliposhinda kombe la FA, Balotelli alitoa sharti kwamba angeenda kupanda basi la kulitembeza kombe barabarani ikiwa tu kama angepanda na mbwa wake. Kwa bahati mbaya sharti lake hilo lilikataliwa.

P - Passenger seat - Siti ya abiria. - Mario Balotelli alisimamishwa na polisi muda mfupi baada ya kuhamia Manchester kwa sababu alikuwa akiendesha gari hilo huku akiwa ameweka £25,000 cash kwenye siti ya abiria. Alipoulizwa kwanini anafanya vile akajibu kwa sababu anazo fedha za kufanya vile.

Q - Question. Ni nani anayefaa zaidi kusimama mbele kwa ajili ya kampeni ya usalama wa fireworks? - Jibu ni Mario Balotelli, kiumbe kilichochoma jumba lake la £3million kwa fireworks, siku mbili kabla ya kampeni ya usalama dhidi ya fireworks.

R - Role Model - Mario Balotelli amekuwa ni kioo kwa watoto wadogo kwa michezo yake ya kijinga na ya maana. Aidha anachezea fireworks au anacheza mchezo wa darts.

S - Show off - Kujionyesha. - Wakati Balotelli aliposhinda tuzo ya mchezaji bora chipukizi wa Ulaya alijitamba sana na kusema hakuwahi kumuona wala kumsikia mpinzani wake wa karibu, Jack Wilshare, lakini angejaribu kujua ni nani huyo mtuthen amkumbushe kwamba amekuwa namba 2 nyuma yake.





T- Tyle track - Ni staili ya unyoaji kwa Balotelli yenye kufanana na mistari ya tairi ambayo anaipenda sana.

U - Undoubted Talent - Kipaji kisichotia shaka. - Akiwa na miaka 22 Balotelli tayari ameshafunga mabao 50 kwenye level ya juu soka, kashinda makombe 7 makubwa likiwemo ya Champions league.

V - Visitor
- Mtembeleaji - Balotelli siku moja alimchukua mdogo wake wa kiume na kwenda nae kuwatembelea akina mama walio jela. Alipoulizwa na walinzi wa jela Mario alisema yeye na mdogo wake walikuwa wanataka tu kujua ukweli tu kama ilikuwa jela ya wanawake.





W - Why always me?

X- Xray. Balotelli amekuwa akisumbuliwa sana matatizo ya goti jambo ambalo limemfanya awe karibu sana na mashine za Xray.

Y - Youth team. Uchizi wa Balotelli siku ulimtuma awafanyie uchizi wachezaji wa timu ya vijana ya Man City. Akawarushia vimishale vinavyotumika kuchezea mchezo wa Darts. Alipoulizwa kisingizio chake akajibu kwamba alikuwa bored ikabidi acheze mchezo ule kupitisha muda.

Z - Zoom, kufuatiwa ushindi wa 6-1 dhidi ya mahasimu wao Man United. Mario Balotelli aliripotiwa kuendesha gari lake mji mzima na kutoa tano kwa washabiki wote wa City akiwa ndani ya gari lake.

Tuesday, August 21, 2012

SIMBA B: VIONGOZI TUPENI NAFASI NA MASLAHI MAZURI TUIFANYE SIMBA ITISHE AFRIKA

ABUU HASHIM: MRITHI WA KASEJA ALIYEWASHANGAZA WAJERUMANI - ASHINDA TUZO TATU NDANI YA MWEZI 1

Abuu Hashim akiwa na hundi yake ya millioni 2 ya mchezaji bora wa mashindano ya BancABC Super8


Takribani wiki mbili baada ya kufanya vizuri na kufanikiwa kuchukua tuzo mbili za ugolikipa bora kwenye michuano mbalimbali aliyoshiriki akiwa na kikosi cha TSC Mwanza kilichofanya ziara nchini Ujerumani - golikipa Abuu Hashim ambaye ni mchezaji wa timu ya Simba B, ameendelea kucheza kwa kiwango cha juu kwenye michuano ya BancABC Super8 na kuiongoza timu yake ya Msimbazi kuibuka mabingwa wa kombe hilo.
Abuu Hashim akiwa anakabidhiwa hundi ya EURO 400 aliyopata kama zawadi baada ya kuwa golikipa wa mashindano ya Insel Cup.
Abuu Hashim akiwa na tuzo yake ya Golikipa bora wa mashindano ya Intensel
Abuu Hashim ambaye alikuwa mmoja wa wachezaji wa Simba B waliochukuliwa na kituo cha TSC Mwanza kwa ajili ya kwenda kuwapa exposure nchini Ujeruman na kufanikiwa kucheza kwa kiwango cha juu, sasa hivi anaangaliwa kama mrithi sahihi wa golikipa Juma Kaseja katika klabu yake ya Simba kutokana na kiwango kikubwa anachokionyesha.

Katika michuano ya Super8 alifanikiwa kulinda vizuri lango lake na kupelekea timu yake kuibuka na ubingwa huu yeye mwenye akiibuka na tuzo ya mchezaji bora na kujipatia shilingi millioni 2.5 kama zawadi.

HUYU NDIO ALEXANDER BUTTNER - BEKI MPYA WA KUSHOTO MRITHI WA EVRA

Klabu ya Manchester United leo imetangaza rasmi usajili wa mchezaji Alexander Buttner, kijana wa kidachi mwenye miaka 23 aliyekuwa akiichezea klabu ya Vitesse. Manchester United wameilipa Vitesse kiasi kichopungua £4million kwa ajili kupata saini ya kijana huyo ambaye amesaini mkataba wa miaka 5 kuwepo Theatre of Dreams.

Personal information
Full name Alexander Büttner
Date of birth 11 February 1989 (age 23)
Place of birth Doetinchem, Netherlands
Height 1.74 m (5 ft 9 in)
Playing position Left Back
Club information
Current club Manchester United
Youth career

VV Doetinchem
–2005 Ajax
2005–2008 Vitesse
Senior career*
Years Team Apps (Gls)
2008–2012 Vitesse 107 (10)
2012– Manchester United 0 (0)
National team
2008 Netherlands U-19 1 (0)
2008-2009 Netherlands U-20 8 (0)


RATIBA YA LIGI KUU YA MSIMU UJAO KUTANGAZWA WIKI IJAYO

Kumekuwepo na taarifa tofauti kuhusu kuanza kwa Ligi Kuu ya Bara ambayo kwa mujibu wa kalenda ya Shughuli za Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), inatakiwa kuanza Septemba 01, 2012. Baada ya kikao cha pamoja baina ya TFF na viongozi wa klabu za Ligi Kuu kilichofanyika Jumatatu ya Agosti 20, 2012 kwenye ofisi za TFF, TFF inapenda kutoa ufafanuzi ufuatao:
 
1.   Baada ya kikao cha pamoja baina ya TFF, Kamati ya Ligi na viongozi wa klabu zote za Ligi Kuu, ilionekana kuwa kutokana na kutokamilika kwa mazungumzo baina ya TFF/Kamati ya Ligi na mdhamini wa sasa, yaani Vodacom, mwanzo wa Ligi Kuu unatarajiwa kuwa Septemba 15, 2012. Hii inatokana na ukweli kwamba kukamilika kwa mazungumzo baina ya pande husika, ndio kutatoa picha halisi ya Ligi Kuu ya msimu ujao.
 
2.   Mazungumzo baina ya TFF/Kamati ya Ligi na Vodacom yanatarajiwa kukamilika mwishoni mwa wiki hii kwa kuwa yameshafikia hatua nzuri na hivyo mkataba unaweza kusainiwa wakati wowote baada ya kukamilika kwa mazungumzo hayo.
 
3.   Kukamilika kwa mazungumzo hayo ni muhimu kwa kuwa kutasaidia Ligi Kuu kuanza bila ya matatizo yoyote kwa klabu zinazoshiriki, TFF na Kamati ya Ligi hasa kutokana na ukweli kuwa baadhi ya mambo yatakayokubaliwa yatalazimika kuingizwa kwenye Kanuni za Ligi; yatasaidia upatikanaji wa fedha kwa muda muafaka; upatikanaji wa vifaa kwa muda muafaka na masuala mengine muhimu.
 
4.   Ratiba ya Ligi Kuu sasa inatarajiwa kutangazwa mapema wiki ijayo pamoja na tarehe rasmi ya kuanza kwa Ligi Kuu
 
5.   Kutokana na kusogwezwa mbele kwa tarehe ya kuanza kwa Ligi Kuu, mchezo wa Ngao ya Jamii baina ya mabingwa wa Tanzania Bara na washindi wa pili, nao sasa utapangiwa tarehe nyingine ambayo ni wiki moja kabla ya kuanza kwa Ligi Kuu. Kwa maana hiyo mchezo huo utachezwa katika siku itakayotangazwa baadaye.
 
6.   Kuhusu chombo kitakachoongoza Ligi Kuu, TFF ilitoa mapendekezo ya Kamati ya Utendaji kwa Kamati ya Ligi na baadaye kwa viongozi wa klabu za Ligi Kuu kuhusu muundo wa chombo hicho kulingana na mwongozo wa Katiba ya Shirikisho la Kimataifa la Vyama vya Mpira wa Miguu (FIFA) na Katiba ya TFF na suala hilo kwa sasa linajadiliwa na klabu za Ligi Kuu kwa ajili ya hatua za mwisho.

TENGA AMKATALIA ADEN RAGE KUJIUZULU UJUMBE WA KAMATI YA SHERIA NA MAADILI

Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) Leodegar Tenga amekataa barua ya kuomba kujiuzulu ya mjumbe wa Kamati ya Sheria, Maadili na Hadhi za Wachezaji ya TFF, Ismail Aden Rage.
 
Rage ambaye pia ni Mwenyekiti wa klabu ya Simba alimuandikia Rais Tenga barua ya kujiuzulu wadhifa huo kwa kile alichosema ‘kamati hiyo kushindwa kwa makusudi kusimamia sheria na kanuni za uendeshaji wa mpira Tanzania zinavyoeleza.’
 
Amekataa ombi hilo kwa maelezo kuwa kama Rage amehisi kuwepo udhaifu wa kutosimamia sheria na kanuni kama inavyotakiwa, ni vyema akaendelea kuwemo kwenye kamati hiyo ili kuisaidia kusimamia sheria na kanuni hizo kama inavyotakiwa badala ya kujiuzulu.
 
“Kutokana na uzoefu na uwezo ambao Rage anao katika uongozi wa mpira wa miguu, ni vyema akautumia kuisaidia kamati kutekeleza wajibu wake kama inavyotakiwa kwa mujibu wa sheria ili kusaidia kusukuma mbele gurudumu za maendeleo ya mpira wa miguu,” amesema Rais Tenga.
 
Pia Rais Tenga amesisitiza kuwa ni muhimu kwa mpira wa miguu kuongozwa kwa kufuata sheria na kanuni zilizopo, rai ambayo imetoa kwa kamati zote za TFF ili kuhakikisha kuwa mpira wa miguu unaongozwa bila kuonea wala kupendelea upande wowote.
 
Rais Tenga amesisitiza kuwa kamati hazina budi kuchukua hatua zinazostahili bila woga pale kanuni zinapotaka hatua kuchukuliwa. Amezitaka kamati zisisite kwa namna yoyote ile kuchukua hatua kwa vile kwa kufanya hivyo, uwezekano wa kutokea upendeleo au uonevu utapungua, hivyo mpira wa miguu kuongozwa kwa sheria na haki.
 

AMRI SAID: MAMILIONI YA KUSAJILI WACHEZAJI WA KIGENI YANAWEZA KUTENGENEZA SIMBA B ZA UBORA ZAIDI

Kocha msaidizi wa klabu ya Simba B, na mchezaji wa zamani wa timu ya wakubwa ya Simba, Amri Said aka Jaap Stam amefanya mazungumzo exclusive na www.shaffihdauda.com kuhusiana na mambo mbali kuhusu ushindi wa timu yake ya Simba B anayoiongoza kwa pamoja na mchezaji mwenzie wa zamani wa Simba Suleiman Matola ambaye ndio kocha mkuu. 

 Katika mahojiano hayo Amri Said kwanza aliwapongeza vijana wake kwa kufanya vizuri pia kwa uongozi wa Simba kwa kuwa na imani kiasi cha kuwaruhusu vijana hao kushiriki michuano ya BancABC Super8, ambapo Simba B ilitoa vichapo vikali kwa vilabu vya timu za wakubwa zenye uwezo kama Azam FC na Mtibwa Sugar. Lakini katika hatua nyingine Amri Said anasema imefikia wakati uongozi wa klabu yake ya Simba kuiamini kabisa na kuitunza kwa asilimia 100 timu hiyo ya kikosi cha pili. "Nadhani sasa tumeonyesha kwamba tunaweza basi ni vizuri viongozi wakatuamini moja kwa moja na kutupa sapoti kama wanayopewa kikosi cha kwanza. Mamilioni yanayotumika kusajili wachezaji wa kigeni yanaweza kutengeneza wachezaji wengine kama hawa na kuendelea kuinufaisha klabu. "Nawaamini sana wachezaji wangu na hapa kwa mfano tukipewa experienced players kama wanne tu tunaweza kushindana kwenye ligi kuu. Tuna wachezaji wazuri sana na uzuri wao umeonekana, hivyo wito wangu kwa viongozi millioni 40 ambazo zingeweza kutumika kukuza vipaji vingine vya timu kama Simba B."

KALI YA LEO: MARIO BALOTELLI AMPORA MWANDISHI LENZI YA CAMERA

REKODI ZA MBWANA SAMATTA ZAMPANDISHA THAMANI MARA 3 ZAIDIYA SIMBA WALIYOPEWA NA TP: KTK MECHI 7 AFUNGA MABAO 5, MANNE YA KICHWA.



Mbwana Ally Samatta anazidi kung'ara kwenye soka la anga ya kimataifa akiwa na klabu yake ya TP Mazembe.

Mbwana Samatta ambaye tayari anatimiza mwaka mmoja tangu ajiunge na timu yake hiyo ya Kinshasa Congo akitokea klabu bingwa ya Tanzania bara Simba Sports Club, amekuwa mmoja ya wafungaji bora na tegemeo kabisa kwenye timu hiyo inayomilikiwa na tajiri Moise Katumbi.

Kwa takwimu zilizo sahihi kabisa za Mbwana Samatta katika msimu huu 2011/12 upande wa Ligi ya mabingwa wa Afrika amecheza mechi 7 tu.

Katika mechi hizo saba Samatta "Golden Boy" amefunga mabao 5. Katika magoli hayo matano, kichwa chake kimeweka kambani mabao 4 na moja amefunga kwa guu lake la kulia.

Mabao hayo matano ya Samatta kwenye Africa Champions league amezifunga timu za Power Dynamo akiwa Ugenini, Akafunga bao lingine dhidi ya Al Merreikh aTP wakiwa nyumbani kabla ya kuja kuwafunga tena Wasudan hao nyumbani kwao Khartoum. Alhly wakawa majeruhi wengine wa Mbwana Samatta baada ya kuwaumiza wakiwa kwao Misri. TP Mazembe wakiwa uwanja wao nyumbani Tanzania Golden Boy akatupia bao moja kwenye mechi dhidi ya Berekum Chelsea. Ikafika zamu ya waarabu Zamalek ambaye akawafunga bao moja moja nyumbani na Ugenini na kutimiza mabao matano.

Dakika ambazo Mbwana Samatta anafunga sana magoli ni kuanzia kati ya dakika ya 16-30 ambapo hapo amefunga mabao mawili. kuanzia dk ya 31 mpaka 42 amafunga goli moja tu, huku akionekana kuwa hatari zaidi kwenye dakika ya 75 ya mchezo kwani tayari ameshafunga mabao mawili kwenye dakika hiyo.

Mafanikio hayo ya Samatta kwenye michuano mbalimbali TP Mazembe inayoshiriki yamezidi kumuongezea thamani kwenye soko la usajili duniani, kutoka kuuzwa kwa dola 100,000 na Simba kwenda TP Mazembe mpaka sasa anakadiriwa kuwa na thamani ya £175,000 ambayo ni mara 3 ya zaidi TP waliilipa Simba kumsaini Samatta.


Monday, August 20, 2012

MIAKA 10 YA WAYNE ROONEY KWENYE LIGI KUU YA ENGLAND



Miaka 10 iliyopita mshambuliaji wa Manchester United Wayne Rooney akiwa na miaka 16 alicheza yake ya kwanza ya ligi kuu ya Uingereza akiwa na Everton dhidi Tottenham Hotspur katika mechi iliyoisha 2-2. Kwa kipindi hicho akawa mchezaji mdogo zaidi kiumri kuichezea Everton kwenye EPL, nyuma ya Joe Royle.

Miezi sita baadae akaweka rekodi ambayo mpaka leo haijawahi kuvunjwa katika klabu ya Everton, siku tano kabla ya kuitimiza miaka 17, Wayne Rooney akafunga goli la ushindi dhidi ya Arsenal katika dakika za majeruhi. Goli hilo la ushindi dhidi ya Arsenal - lilimaliza rekodi ya Arsenal kucheza mechi 30 bila kufungwa.


Usiku wa leo katika uwanja ule ule alioweka rekodi ya ajabu, Wayen Rooney atashuka dimbani hapo lakini safari hii akiwa kwenye jezi za rangi nyekundu na sio blue kama ilivyokuwa muongo mmoja uliopita. Atakuwa mchezaji wa Manchester United akipambana na klabu yake ya zamani ya Everton.


MVIVU, MCHELEWAJI MAZOEZINI NA UTOVU WA NIDHAMU VYAMUONDOA ALEX SONG ARSENAL - ATAMBULISHWA RASMI BARCA

Wakati baadhi ya mashabiki wa Arsenal wakiwa wana maumivu ya kuondokewa na mchezaji wao muhimu wa pili ndani ya wiki moja, Alex Song, taarifa zainasema kwamba kocha wa klabu hiyo Arsene Wenger amemuachia kiurahisi mcameroon huyo baada ya kuchoswa na utovu wa nidhamu wa mchezaji huyo, uchelewaji wa kwenye mazoezi na uvivu alionao. Kutokana na tabia zake hizo Wenger hakusita hata mara moja ilipokuja ofa ya Barcelona ya kumsajili Song kwani ilikuwa ni kumuondolea mzigo alioubeba bila kupenda katika kipindi kirefu kilichopita, kuondoka kwa Song kumefungua njia kwa Arsenal kuweza kushinda mbio za usajili wa mkopo wa Nuri Sahin kutoka Real Madrid.

Wakati Wenger akisema cha nini - Barcelona walikuwa wanasema watakipata lini. Pichani Alexander Song akiwa anatambulishwa rasmi baada ya kujiunga na klabu yake mpya ya Barcelona.

MBWANA SAMATA NI NOOMA, AWATANDIKA TENA WAARABU - TP MAZEMBE WAKIITOA ZAMALEK KWENYE CHAMPIONS LEAGUE