Kocha msaidizi wa klabu ya Simba B, na mchezaji wa zamani wa timu ya wakubwa ya Simba, Amri Said aka Jaap Stam amefanya mazungumzo exclusive na www.shaffihdauda.com kuhusiana na mambo mbali kuhusu ushindi wa timu yake ya Simba B anayoiongoza kwa pamoja na mchezaji mwenzie wa zamani wa Simba Suleiman Matola ambaye ndio kocha mkuu.
Katika mahojiano hayo Amri Said kwanza aliwapongeza vijana wake kwa kufanya vizuri pia kwa uongozi wa Simba kwa kuwa na imani kiasi cha kuwaruhusu vijana hao kushiriki michuano ya BancABC Super8, ambapo Simba B ilitoa vichapo vikali kwa vilabu vya timu za wakubwa zenye uwezo kama Azam FC na Mtibwa Sugar.
Lakini katika hatua nyingine Amri Said anasema imefikia wakati uongozi wa klabu yake ya Simba kuiamini kabisa na kuitunza kwa asilimia 100 timu hiyo ya kikosi cha pili. "Nadhani sasa tumeonyesha kwamba tunaweza basi ni vizuri viongozi wakatuamini moja kwa moja na kutupa sapoti kama wanayopewa kikosi cha kwanza. Mamilioni yanayotumika kusajili wachezaji wa kigeni yanaweza kutengeneza wachezaji wengine kama hawa na kuendelea kuinufaisha klabu.
"Nawaamini sana wachezaji wangu na hapa kwa mfano tukipewa experienced players kama wanne tu tunaweza kushindana kwenye ligi kuu. Tuna wachezaji wazuri sana na uzuri wao umeonekana, hivyo wito wangu kwa viongozi millioni 40 ambazo zingeweza kutumika kukuza vipaji vingine vya timu kama Simba B."
No comments:
Post a Comment