A TO Z KUHUSU MARIO BALOTELLI
B - Bib. Ni kipande cha nguo anachovaa Balotelli juu ya fulana yake ya kufanyia mazoezi.
C - Ni kwa ajili ya Camorra. Balotelli anatuhumiwa na wengi kwamba ana mahusiano na kundi la The Camorra - kundi ambalo linafanan kabisa na Mafia - na hii ilitokana na yeye kuonekana akipewa muongozo wa jiji la Napoli hasa kwenye viunga vya maeneo yenye sifa ya uhalifu sana na wahuni wa eneo hilo ambao ni wafanyakazi wa Camorra. Balotelli mwenyewe anadai hakuwa akiwafahamu watu hao kama wahalifu.
D - Ni kwa ajili ya Derby. Manchester United 1-6 Manchester City. Mario Balotelli alifunga mabao mawili na kuisadia City kuipa UTD kipigo kizito katika historia yao katika premier league - kitu ambacho sio rahisi kwa washabiki wa United kusahau.
E - Ni kwa jili ya Ego - Kujiona au Majivuno: "Kuna mchezaji mmoja ambaye ana uwezo mkubwa kuliko mie lakini sio sana Lionel Messi. Wngine wote wananifuatia mimi."
F - Kwa ajili ya Fireworks - Aina ya vifaa vya ulipuaji moto: Msimu uliopita aliripotiwa kurusha fireworks bafuni kwake na kusababisha moto mkubwa kwenye nyumba anayoishi.
G - Kwa ajili ya Generosity - Ukarimu: Mario Balotelli amekuwa na kawaida ya kutoa noti za £20 kwa wapita njia barabarani.
H - Homeless - Kutokuwa na makazi - Baada ya kushinda £25,000 kwenye Casino, Balotelli akampa mwanaume mmoja ambaye hakuwa na makazi £1,000 cash. Alipoulizwa kwanini amefanya vile, alijibu ni kwa sababu alipenda nywele za yule aliyempa msaada.
I - Impound - kuwa chini miliki ya kisheria: Balotelli ameripotiwa kuwa gari lake aina Maserati sports limekuwa likikimatwa na kuwekwa kwenye kizuizi cha kisheria kwa mara 27 na kumfanya Balotelli alipe kiais cha £10,000 kama faini za kupaki ovyo gari lake hilo.
J - Jenny Thompson. Changudoa ambaye alishawahi kuhusishwa kutembea na Wayne Rooney, alikuwepo kwenye mgahawa mmoja jijini Manchester na ndani ya mgahawa huo alikuwepo Balotelli, muitaliano huyo alipomuona msichana yule akaanza kuimba "Rooney Rooney Rooney" tena kwa sauti kubwa.
K - Karma - Jaribio la Balotelli kufunga bao kwa kisigino dhidi ya LA Galaxy lilimpa wakati mgumu mbele ya kocha wake Roberto Mancini. Alitolewa haraka baada ya kufanya jaribio hilo. Balotelli akadai alijaribu kufunga kwa kisigino kwa sababu alidhani alikuwa ameotea tayari.
L - Lothario. Balotelli aliripotiwa kumuita kwa nguvu mwanadada Lothario katika Mgahawa mmoja huko Manchester. Huku chakula kikimtoka mdomoni alimwambia Lothario amfuate. Kwa bahati nzuri msichana yule akaja. Akampa simu yake na kumwambia Lothario aandike namba yake ya simu na aifadhi. Binti yule akafuata maelekezo ya Balo na akaondoka bila kuongea kingine chochote na Mchizi Balotelli, na baadae ikaripotiwa kuwa wamekuwa wapenzi.
M - Kwa ajili ya Mario
N - Ni kwa ajili ya Nicklas Bendtner Syndrome. Balotelli anagua kwa kile kitu ambacho wanasaikolojia wanakiita "Nicklas Bendtner Syndrome" - Mario Balotelli anaamini yeye ndio mchezaji bora kabisa ambaye duniani imewahi kumshuhudia.
O - Open top bus. Wakati City waliposhinda kombe la FA, Balotelli alitoa sharti kwamba angeenda kupanda basi la kulitembeza kombe barabarani ikiwa tu kama angepanda na mbwa wake. Kwa bahati mbaya sharti lake hilo lilikataliwa.
P - Passenger seat - Siti ya abiria. - Mario Balotelli alisimamishwa na polisi muda mfupi baada ya kuhamia Manchester kwa sababu alikuwa akiendesha gari hilo huku akiwa ameweka £25,000 cash kwenye siti ya abiria. Alipoulizwa kwanini anafanya vile akajibu kwa sababu anazo fedha za kufanya vile.
Q - Question. Ni nani anayefaa zaidi kusimama mbele kwa ajili ya kampeni ya usalama wa fireworks? - Jibu ni Mario Balotelli, kiumbe kilichochoma jumba lake la £3million kwa fireworks, siku mbili kabla ya kampeni ya usalama dhidi ya fireworks.
R - Role Model - Mario Balotelli amekuwa ni kioo kwa watoto wadogo kwa michezo yake ya kijinga na ya maana. Aidha anachezea fireworks au anacheza mchezo wa darts.
S - Show off - Kujionyesha. - Wakati Balotelli aliposhinda tuzo ya mchezaji bora chipukizi wa Ulaya alijitamba sana na kusema hakuwahi kumuona wala kumsikia mpinzani wake wa karibu, Jack Wilshare, lakini angejaribu kujua ni nani huyo mtuthen amkumbushe kwamba amekuwa namba 2 nyuma yake.
U - Undoubted Talent - Kipaji kisichotia shaka. - Akiwa na miaka 22 Balotelli tayari ameshafunga mabao 50 kwenye level ya juu soka, kashinda makombe 7 makubwa likiwemo ya Champions league.
V - Visitor - Mtembeleaji - Balotelli siku moja alimchukua mdogo wake wa kiume na kwenda nae kuwatembelea akina mama walio jela. Alipoulizwa na walinzi wa jela Mario alisema yeye na mdogo wake walikuwa wanataka tu kujua ukweli tu kama ilikuwa jela ya wanawake.
W - Why always me?
X- Xray. Balotelli amekuwa akisumbuliwa sana matatizo ya goti jambo ambalo limemfanya awe karibu sana na mashine za Xray.
Y - Youth team. Uchizi wa Balotelli siku ulimtuma awafanyie uchizi wachezaji wa timu ya vijana ya Man City. Akawarushia vimishale vinavyotumika kuchezea mchezo wa Darts. Alipoulizwa kisingizio chake akajibu kwamba alikuwa bored ikabidi acheze mchezo ule kupitisha muda.
Z - Zoom, kufuatiwa ushindi wa 6-1 dhidi ya mahasimu wao Man United. Mario Balotelli aliripotiwa kuendesha gari lake mji mzima na kutoa tano kwa washabiki wote wa City akiwa ndani ya gari lake.
No comments:
Post a Comment