Search This Blog
Wednesday, June 13, 2012
TENGA: WACHEZAJI WOTE WA STARS KUKATIWA BIMA
Bosi wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Leodegar Tenga, amewapongeza wachezaji wa Taifa Stars kwa kiwango walichoonyesha kwenye mchezo dhidi ya Gambia, lakini akasema wachezaji wote wa timu hiyo watakatiwa bima ya afya.
Tenga, akizungumza na waandishi wa habari jana jijini Dar es Salaam, alisema wachezaji hao walionyesha kiwango cha kuridhisha kwenye mchezo huo, lakini akatupa sifa zake zote kwa kocha Kim Poulsen.
“Nimefurahishwa sana na kiwango kilichoonyeshwa na wachezaji wa Stars kwenye mchezo dhidi ya Gambia, hakika kocha amefanya kazi nzuri sana kwa kipindi kifupi alichokaa na timu.
“Wachezaji kama John Bocco na Abubakar Salum walionyesha kiwango kizuri sana, nafikiri timu hii inahitaji sapoti yetu, lakini tumekaa na kukubaliana kuwa wachezaji wote wa timu ya taifa watakatiwa bima ya matibabu.
“Naamini hii itakuwa faraja kubwa kwao, nitafanya kosa kama nitashukuru bila kuishukuru timu ya Azam kwa kutupa mtaalam wao wa mazoezi ya viungo (Paul Gomes), alifanya kazi kubwa sana kwenye timu yetu,” alisema Tenga.
RAMANI NA VIPIMO VYA UWANJA WA SOKA!
Wengi tunaupenda mchezo wa soka lakini je sheria zenyewe zinazoongoza mchezo huu tunazifahamu? blog yako inakuletea sheria za mchezo huu, hii ni kwa ajili ya kuwafanya wasomaji wetu nanyi mfahamu sheria 17 za mchezo huu.
SHERIA YA 1:UWANJA WA MICHEZO
1: vipimo
Kiwanja cha michezo kina umbo la mstatili. Urefu wake
hautazidi yadi 130 na hautapungua yadi 110. Upana wake
hautazidi yadi 100 wala hautapungua yadi 50. Kiwanja cha michezo ya kitaifa urefu hautazidi yadi 80 wala kupungua yadi 110, na upana hautazidi yadi 80 wala kupungua yadi 110, na upana hautazidi yadi 80 wala kupungua yadi 70. Kwa vyovyote vile, marefu yatazidi mapana.
2: Alama
Mistari inayoonekana wazi, yenye unene usiozidi inchi 5
itachorwa kuonyesha mipaka ya kiwanja. Mistari ya urefu
itaitwa mistari ya pembeni na ile ya mapana, itaitwa mistari ya goli.
Bendera iliyootundikwa kwenye mti usiopungua futi 5 kwa urefu itasimikwa katika kila kona ya kiwanja. Bendera ya aina hii yaweza kusimikwa sawa na mstari wa kati umbali usiopungua yadi moja kutoka mstari wa pembeni. Mstari wa katikati utapita katikati ya kiwanja na alama itawekwa
kuonyesha katikati ya kiwanja na alama itawekwa kuonyesha katikati kabisa. Kutoka kwenye alama hiyo,mnviringo wenye nusu kipenyo cha
yadi 10 utachorwa. Alama hiyo ya kati ndipo mahali pa kuanzia michezo.
3: Eneo la goli
Katika kila upannde wa goli mistari miwili itachorwa pembe mraba na mstari wa goli. Eneo lililomo ndani ya mistari hii litajulikana kama eneo la goli.
4: Eneo la Adhabu
Katika kila upande wa goli mistari miwili itachorwa pembe
mraba na mstatiri wa goli umbali wa yadi 18 toka kila nguzo ya goli. Mistari hii itaingia uwanjani umbali wa yadi 18 na itaungwa kwa mstari wa usawa na ule wa goli. Eneo hili litajulikana kama eneo la adhabu. Alama itawekwa umbali wa yadi 12 kutoka katikati ya mstari wa goli, na hapo ndipo pa kupiga penalti. Kutoka alama hiyo
mkato wenye nusu kipenyo cha yadi 10 utachorwa nje ya eneo la adhabu.
5: Eneo la kona
Robo ya mviringo yenye nusu kipenyo cha yadi itachorwa ndani ya kiwanja kutoka mahali ilipo bendera ya kona. Eneo hili ndio eneo la kona.
6: Magoli
Nguzo za goli zitasimikwa katikati ya mistari ya goli, zikiacha urefu sawa toka kila kona. Umbali kati ya nguzo na nguzo utakua yadi 8. Juu ya nguzo kutawekwa mwamba na urefu wa ndani ya gali toka chini hadi hadi juu, mwamba huo hautazidi inchi 5.
Baraza la michezo la mataifa FIFA limeamua katika sheria katika sheri hii ya kwanza ya mchezo wa soka
kwamba;
1: Vipimo vya kiwanja cha mchezo wa kimataifa vitakuwa; si zaidi ya yadi 120 + 80 wala si chini ya yadi 100 + 70. (Wastani
m105 + m70)
Tuesday, June 12, 2012
KALI YA LEO: WACHEZAJI 12 WAPEWA KADI NYEKUNDU KWENYE MCHEZO MMOJA.
Wachezaji 12 walilimwa kadi nyekundu kwenye mchezo wa ligi ya madaraja ya chini nchini Brazil kati ya Votuporanguense na Fernandopolis.
PODOLSKI NA MULLER WALIFELI DHIDI YA URENO: JE REUS NA SCHURRLE WATAANZA DHIDI YA UHOLANZI
Mchezo wao kwanza wa Euro 2012 ulienda kwa mujibu wa Ujerumani walivyotaka - kwa upande wa matokeo, lakini vijana wa Joachim Low hawakuonyesha uwezo mkubwa ambao wengi walikuwa wakiutegemea dhidi ya Ureno. Ushindi wa 1-0 ulikuwa ni bahati kwa timu hiyo kwa kuwa hata Ureno walipoteza sana nafasi kwa kutokuwa na bahati waliyoipata Ujerumani.
Ndio maana haishangazi kuona umma wa Ujerumani ukitegemea kuona mabadiliko kwenye mechi zijazo, kwa kuwa hawakuona timu yao ikicheza kwa kutengeneza nafasi nyingi za magoli dhidi ya kikosi cha Paulo Bento. Low alifanya uamzui mkubwa kwa kumchezesha Mats Hummels na Mario Gomez, lakini mashabiki wanataka kocha wao aongezee ujasiri wakati wa mechi zijazo.
Kuna maswali juu ya nafasi mbili: Thomas Muller na Lukas Podolski wote wanaweza wakaanzia benchi kwenye mechi zijazo. Wote walionyesha kwamba wapo tayari kucheza kwa kujituma bila kuchoka lakini kiukweli hawakucheza vizuri, na sasa Marco Reus na Andre Schurrle wanaweza kuwa wabadili wao dhidi Uholanzi?
Akiwa mmoja ya chipukizi bora wa ligi ya Ujerumani msimu uliopita, kiwango cha Marco Reus akiwa Borussia Monchengladbach kimeonyesha ubora anaoweza kuuleta ndani ya kikosi: akiwa na na rekodi nzuri za ufungaji na ubunifu mzuri kiwanjani. Kwa upande wa Schurrle amekuwa katika form nzuri kwa siku za hivi karibuni katika mechi za kirafiki kuelekea kwenye Euro, pia alikuwa na msimu mzuri na Bayern Leverkusen, na hakuna ubishi kwamba amaelata maswali mengi juu ya nani aanze kati yake na Podolski.
Alifunga magoli kwenye mechi mbili za mwisho za msimu na Leverkusen, na akiwa anatokea benchi dhidi ya Israel aliubadilisha mchezo na kuifanya Ujerumani kuwa tishio tofauti ana alivyokuwepo Podolski kwenye pitch.
"Kiukweli nataka kucheza mara nyingi iwezekanvyo, lakini kuna nafasi moja na watu wengi tunaitaka hivyo mwisho wa siku ni uamuzi wa kocha, japokuwa haijalishi nimecheza au hapana nitaisapoti yangu mwanzo mwisho kiwanjani mpaka nikiwa kwenye benchi." alisema Schurrle muda mfupi kabla ya kuelekea Ukraine.
Wengi wanatabiri kwa tabia ya kocha Low ya kufanya mabadiliko yasiyotegemewa kwenye kikosi, basi ni dhahiri Reus na Schurrle wanwwza wakaanza mbele ya Muller na Podolski
Ndio maana haishangazi kuona umma wa Ujerumani ukitegemea kuona mabadiliko kwenye mechi zijazo, kwa kuwa hawakuona timu yao ikicheza kwa kutengeneza nafasi nyingi za magoli dhidi ya kikosi cha Paulo Bento. Low alifanya uamzui mkubwa kwa kumchezesha Mats Hummels na Mario Gomez, lakini mashabiki wanataka kocha wao aongezee ujasiri wakati wa mechi zijazo.
Kuna maswali juu ya nafasi mbili: Thomas Muller na Lukas Podolski wote wanaweza wakaanzia benchi kwenye mechi zijazo. Wote walionyesha kwamba wapo tayari kucheza kwa kujituma bila kuchoka lakini kiukweli hawakucheza vizuri, na sasa Marco Reus na Andre Schurrle wanaweza kuwa wabadili wao dhidi Uholanzi?
Akiwa mmoja ya chipukizi bora wa ligi ya Ujerumani msimu uliopita, kiwango cha Marco Reus akiwa Borussia Monchengladbach kimeonyesha ubora anaoweza kuuleta ndani ya kikosi: akiwa na na rekodi nzuri za ufungaji na ubunifu mzuri kiwanjani. Kwa upande wa Schurrle amekuwa katika form nzuri kwa siku za hivi karibuni katika mechi za kirafiki kuelekea kwenye Euro, pia alikuwa na msimu mzuri na Bayern Leverkusen, na hakuna ubishi kwamba amaelata maswali mengi juu ya nani aanze kati yake na Podolski.
Alifunga magoli kwenye mechi mbili za mwisho za msimu na Leverkusen, na akiwa anatokea benchi dhidi ya Israel aliubadilisha mchezo na kuifanya Ujerumani kuwa tishio tofauti ana alivyokuwepo Podolski kwenye pitch.
"Kiukweli nataka kucheza mara nyingi iwezekanvyo, lakini kuna nafasi moja na watu wengi tunaitaka hivyo mwisho wa siku ni uamuzi wa kocha, japokuwa haijalishi nimecheza au hapana nitaisapoti yangu mwanzo mwisho kiwanjani mpaka nikiwa kwenye benchi." alisema Schurrle muda mfupi kabla ya kuelekea Ukraine.
Wengi wanatabiri kwa tabia ya kocha Low ya kufanya mabadiliko yasiyotegemewa kwenye kikosi, basi ni dhahiri Reus na Schurrle wanwwza wakaanza mbele ya Muller na Podolski
HATIMAYE YANGA YATHIBITISHA MARCIO MAXIMO KUTUA BONGO JUMAPILI HII
Baada ya siku chache zilizopita website hii ilikuwa ya kwanza kuripoti kwamba klabu ya Yanga ipo katika hatua za mwisho za kumsaini Marcio Maximo, leo hii imefahamika kwamba kocha huyo wa zamani wa timu ya taifa 'Taifa Stars' Mbrazil, Marcio Maximo anatarajia kutua nchini kwa mara nyingine tena toka aondoke nchini mwezi juni mwaka 2010 siku ya jumapili juni 17 saa 9 alasiri.
Maximo anakuja nchini kuchukua mikoba ya Mserbia wa Yanga Kostadin Papic aliyenyimwa mkataba mpya, baada ya ule wa awali wa miezi 6 kuisha wakati ligi kuu ya Vodacom msimu wa 2011/12 ukielekea mwishoni.
Maximo awali alitarajiwa awasili nchini hapo kesho, na kwa mujibu wa taarifa rasmi na zinasema kocha huyo mwenye msimamo mkali atawasili jumapili na shirika la ndege ya Emirates.
Maximo anakuja nchini kuchukua mikoba ya Mserbia wa Yanga Kostadin Papic aliyenyimwa mkataba mpya, baada ya ule wa awali wa miezi 6 kuisha wakati ligi kuu ya Vodacom msimu wa 2011/12 ukielekea mwishoni.
Maximo awali alitarajiwa awasili nchini hapo kesho, na kwa mujibu wa taarifa rasmi na zinasema kocha huyo mwenye msimamo mkali atawasili jumapili na shirika la ndege ya Emirates.
Hii ndiyo ndivyo sivyo ya ubingwa nchi za ulaya
Na Arone Mpanduka(Radio Tumaini)
NDANI ya msimu wa mwaka 2011/2012 tumekuwa tukishuhudia matukio mbalimbali ya kimichezo hasa katika medani ya soka ambayo yamekuwa yakivutia na kusisimua.
Kutokana na kufuatilia kwa karibu zaidi matukio ya soka Barani Ulaya kupitia ligi mbalimbali nimeweza kubaini mambo kadhaa ambayo yamekuwa kinyume na matarajio ya wapenzi wengi wa mchezo wa soka duniani.
Kupitia matukio hayo wengi waliokuwa wanajaribu kutabiri ndivyo, matokeo yake yamekuwa sivyo.Fuatana nami ili tuweze kwenda pamoja hasa kwa kupitia tukio moja hadi lingine kwa kifupi.
BINGWA WA KOMBE LA FA
Hapa wengi walidondosha karata yao ya utabiri kwa timu ya Liverpool hasa kutokana na wachezaji wake kuwa na tabia ya kutokata tamaa katika dakika zote 90 hata kama wakiwa nyuma kwa goli moja ama mawili kitu ambacho wachezaji wa Chelsea wamekikosa.
Licha ya kwamba timu zote zilikuwa na mwenendo mbovu katika msimu wa 2011/2012 lakini Liverpool ilipewa nafasi kubwa zaidi ya kutwaa kombe hili lakini hatimaye mambo yalikuwa kinyume hasa pale ambapo Chelsea ilipofanya maajabu kwa kuinyuka Liver mabao 2-1.
Ramires na Didier Drogba ndiyo waliofanikisha kombe la FA kwenda darajani ambapo kwa mara ya mwisho Chelsea ilitwaa kombe hilo mwaka 2010.
BINGWA WA LIGI KUU YA HISPANIA
Katika ligi hii wengi walikuwa wakiiangalia zaidi Barcelona ambayo ilikuwa ikishiriki ligi kama bingwa mtetezi lakini pia bingwa wa dunia ngazi ya vilabu.
Watu walikuwa na imani na Barcelona hasa kwa uimara iliyonao wa kuweza kumiliki mpira na kupenyezeana pasi za uhakika na hata pia umakini wa washambuliaji wake kama Lionel Messi ambaye ni mgumu kumzuia pindi anaposogelea ‘sebule’ ya timu pinzani.
Hadi ngwe ya mechi za marudiano za ligi kuu ya Hispania inaanza Barcelona ilikuwa kileleni mwa msimamo wa ligi ikifuatiwa na Real Madrid lakini mambo yalibadilika kuelekea mwishoni mwa ligi ambapo Madrid chini ya Jose Mourinho ikafanikiwa kuitangulia Barcelona kwa tofauti ya pointi 4.
Mambo yalizidi kwenda hivyo hasa kwa timu zote kuhakikisha kwamba hazifanyi makosa kwenye mechi zao na kufanya mashabiki wa soka ulimwenguni kusema kwamba bado Barcelona ana nafasi ya ubingwa hasa katika mechi ambayo wanacheza mwenyewe kwa wenyewe hasa ikizingatiwa kwamba mara zote Madrid ni kibonde wa Barcelona.
Lakini mambo hayakuwa mambo kwani hata walipokutana wenyewe kwa wenyewe Barcelona alikubali kichapo kutoka kwa Real Madrid mara baada ya kupigwa 2-1 na kutengeneza tofauti ya pointi 7 kutoka 4, tofauti ambayoi ilikwenda hadi siku ambayo Real Madrid inatangaza ubingwa.
Hapa ndugu msomaji hadi mwisho wa ligi ubingwa wa Real Madrid ulikuwa kinyume na matarajio ya wengi.
BINGWA WA LIGI KUU YA UINGEREZA
Katika ligi hii inayodhaminiwa na benki kubwa duniani ya Backlays tangu inaanza mwezi Agosti mwaka 2011 mashabiki wengi walikwishaipatia ubingwa timu ya Manchester United hasa baada ya kuanza vizuri msimu kwa kuinyuka Manchester City 3-2 katika mechi ya ngao ya jamii.
Kama hiyo haitoshi Manchester United ilionyesha kwamba ipo vizuri baada ya kutoa vipigo kwa timu kadhaa ikiwemo kipigo cha kihistoria ya mabao 8-1 ilichomnyuka Arsenal na kuweka rekodi ya ushindi wa mabao mengi zaidi katika msimu huo wa ligi kuu.
Kumbe wakati huohuo timu iitwayo Manchester City ilikuwa inakimbiza mwizi kimya kimya hasa baada ya kuonyesha ushindani wa hali ya juu kwa kutoa dozi kwa timu ilizokuwa inakutana nazo.
Hadi kufikia mwezi Januari mwaka 2012 Manchester City walikuwa wanaongoza ligi wakifuatiwa na Manchester United kitu ambacho kilihamisha mawazo ya wadau wa soka kutoka kwa United hadi City na kusema kwamba City ndiyo bingwa mtarajiwa.
Lakini mwishoni mwa ligi hiyo mambo yalibadilika ambapo wadau wakarejesha utabiri wao kwa Manchester United kuwa ndiye bingwa wa ligi hiyo hasa baada ya timu hizo kuwa na pointi sawa huku City ikiwa kileleni kwa tofauti ya mabao ya kufunga na kufungwa tu.
Utamu ulikuja katika siku ya mwisho ya kumaliza ligi ambapo bingwa alikuwa bado hafahamiki na watu wengi walitabiri kwamba Manchester United atamfunga Sunderland lakini wakiibeza City kwamba isingeweza kuifunga QPR ambayo nayo ilihitaji ushindi ili isishuke daraja.
Hali hiyo ilifanya siku hiyo hata helikopta iliyobeba kombe kuhangaishwa angani ambapo kila dakika ilikuwa inabadili njia zake, mara iende Sunderland mara ibadilike na kwenda Etihad.
Lakini mwisho wa yote Manchester City nayo iliibuka na ushindi wa mshangao wa mabao 3-2 ikitoka nyuma ya mabao 2-1 dhidi ya QPR huku Manchester United ambayo iliiombea City ifungwe ili yenyewe ichukue ubingwa ikajikuta ikipoteza ndoto hiyo licha ya yenyewe kushinda bao 1-0.
Mwisho wa yote Manchester City aliibuka bingwa kiyume na matarajio ya wengi ulimwenguni.
BINGWA WA KLABU BINGWA BARANI ULAYA
Hapa timu za Bayern Munich na Chelsea hazikupewa nafasi kabisa ya kufika hata nusu fainali lakini matokeo yake miamba hiyo ilitinga fainali na kuchuana pale Allianz Arena nchini Ujerumani.
Utabiri ulianza kushika kasi katika hatua ya 16 bora ambao kwa mtazamo wa haraka haraka mashabiki wengi duniani walihisi kwamba fainali itazikutanisha timu za Real Madrid na Barcelona na hapo yoyote kati ya hizo ndiye atakayekuwa bingwa.
Kinyume chake ni kwamba Real Madrid alibwagwa na Bayern Munich katika hatua ya nusu fainali huku Barcelona akibwagwa na kibonde Chelsea katika hatua ya nusu fainali, kitu ambacho kiliwashangaza wengi hasa kwa hali iliyonayo Chelsea kuweza kuiondosha miamba ya dunia Barcelona ambayo ilikuwa na kila sababu ya kufika fainali na kutwaa taji hilo.
Mechi ya fainali kati ya Bayern Munich na Chelsea nayo iliibua watabiri wengi walioegemea upande wa Bayern kwamba ndiyo wangekuwa mabingwa hasa kutokana na sababu nyingi ikiwemo tofauti ya uwezo wa kuuchezea mpira na kasi ya ushambulizi kwa timu hizo ambapo wajerumani waliizidi Chelsea.
Suala lingine ni kitendo cha Bayern kucheza nyumbani , mahali ambapo pana watu wengi wa kuiunga mkono pindi iwapo dimbani.
Matokeo ya mwisho yalikuwa ndivyo sivyo kwani Chelsea iliibuka na ushindi wa penati 4-3 hasa baada ya kutoka sare ya 1-1 ndani ya dakika 120 za mchezo.
Barua Pepe:mpanduka@yahoo.com
BONDIA JAPHET KASEBA AZUNGUMZA NA MO BLOG KUHUSU ‘FREEMASON’.
MO BLOG: Japhet Kaseba hakuna asiye kufahamu katika ulimwengu wa Tanzania wa mchezo wa Kick Boxing, hebu tutofautishie kati ya mchezo wa kick boxing unaocheza na Muay Thai ambayo pia unacheza.
KASEBA: Unajua kick boxing ni staili ambayo ipo Marekani ambayo inahusisha ngumi na mateke lakini mateke yake yanaanzia kiononi kuelekea juu, na Muay Thai ni staili kutoka Thailand ambayo mateke yake yanaanzia kwenye mapaja kwenda juu.
Pia wanatumia Elbow na kushikana na kudondoshana kitu ambacho kwenye kick boxing hakuna.
MO BLOG: Watanzania wategemee nini maana wewe ndie mwakilishi wetu nje ya nchi.
KASEBA: Kubwa ni kwamba baada ya kukosa wapinzani kwa muda mrefu katika suala zima la Kick Boxing nikaamua mimi nijiweke pembeni kidogo na kuamua kuanzisha ligi ya ‘Bingwa wa Mabingwa’ kwa Tanzania na baadae Afrika nzima kwa sababu nilikuwa nakusudia kuwaleta washiriki kutoka Japan na Wanathailend.
MO BLOG: Sasa nini kilitokea na mipango hiyo kukwama..?
KASEBA: Nilikosa udhamini wa kulipia vitu kama sehemu za kulala kwa sababu gharama nyingine walikuwa tayari kujilipia wenyewe.
MO BLOG: Mara ya mwisho tumekujua kama Bingwa wa mchezo wa kick-boxing, lakini ghafla unacheza mchezo wa masumbwi..?
KASEBA: Kama nilivyosema mwanzo baada ya kukosa mpinzani kwa muda mrefu katika mchezo wa kick-boxing, niliona ni vyema nikaonyesha kipaji changu katika mchezo masumbwi. Ndipo nilipopambana na Francis Cheka na mchezo wetu kuharibika baada ya shabiki kupanda ulingoni.
MO BLOG: Tufafanulie utata uliopo baina yako Francis Cheka katika mchezo wa masumbwi .?.
KASEBA: Kwa mimi binafsi sidhani kama kuna utata, na kwa sasa najiandaa kwa pambano la marudiano ambalo nitalitumia kuweka heshima, ambalo litafanyika tarehe 7 mwezi wa 7 ili kujua nani mshindi wa ukweli.
MO BLOG: Kaseba kuna ukweli wowote kwamba kabla ya kucheza pambano ni vyema siku moja kabla mtu unapaswa kufanya mapenzi.?.
KASEBA: Kwa kweli kwa kuwa mimi nilianzia kwenye mchezo wa ‘Martial Arts’ , hicho kitu kilikuwa kinapingwa sana na sidhani hata katika michezo mingine kinakubalika. Sana sana ningewaasa watanzania kujituma katika mazoezi na kuacha kudanganyana.
MO BLOG: Hebu izungumzie familia yako kwa sababu mengi yamesemwa na hatupendi kuyarudia.
KASEBA: Nampenda sana mke wangu, nawapenda ndugu zangu, pia nawapenda sana wazazi wangu na siku zote namshukuru mwenyezi mungu na naamini hiyo ni moja wapo ya mafanikio yangu, kwa kuwa kila ninachohangaikia nahaingikia kwa sababu ya familia yangu.
MO BLOG: Kumekuwa na taarifa kwamba wewe ni Freemason hebu jitetee.!
KASEBA: Ee bwana ehh, ha…ha..ha Mo Blog mnanizingua lakini nachoweza kusema ni kuwa mimi siwezi kukataa wala kukubali na waacheni wanadamu waseme wanavyotaka, kwa sababu hata Kanumba wamesema ni ‘Freemason ‘ lakini najua ni ile ‘movie’ aliyocheza ndio imemponza.
Upeo wa watu wengi ni mdogo sana, kwa sababu chochote mtu anachokifanya kwa maana ya kuigiza, watu wengi wanaamini ni kweli.
Ndio maana kuna wanawake wameigiza filamu za uchawi na mpaka leo wanaogopwa mitaani wakionekana kweli ni wachawi.
Kwa nchi iliyopo chini kama Tanzania ambayo inaibukia kila utakachokifanya itaonekana ni hivyo hivyo, hata ukiigiza ukasema mimi ni rais ndivyo baadhi ya watu watakavyoamini.
Mimi ni mkristo ninayependa kumtumikia Mungu.
MO BLOG: Japhet Kaseba MO BLOG inakutakia mafanikio katika jitihada zako za kukuza mchezo wa ‘Kick-Boxing’ hapa nchini na katika kufanikisha ligi ya Masumbwi, na bila kusahau mchezo ujao wa ngumi kati yako na Francis Cheka; tuko pamoja nawe.
KASEBA: Akhsante sana nami nawatakia kila la heri katika utendaji wenu wa kazi, na msitusahau wanamichezo kama sisi.
SOURCE: dewjiblog.com
BREAKING NEWS: YANGA YAMSAJILI FRANK DOMAYO KWA MIL.20
Habari rasmi kutoka kwenye kamati ya usajili ya klabu ya Yanga ni kwamba timu hiyo leo imekamilisha usajili wa kinda la timu ya taifa ya Tanzania aliyeng'ara kwenye mchezo wa jumapili iliyopita dhidi ya Gambia Frank Domayo.
Domayo ambaye alikuwa akiichezea JKT Ruvu msimu uliopita, amesaini mkataba wa miaka 3 kuitumikia Yanga, huku akilipwa shilingi millioni 20 kama ada ya usajili na atakuwa akilipwa shilingi millioni moja kama msharaha kwa miaka 3 ijayo.
UFARANSA VS ENGLAND: ROY HODGSON NA FALSAFA YA KUPAKI BASI - KAPATA ALICHOTAKA
Hii ilikuwa mechi ambayo ilikuwa na ubunifu mdogo sana huku ikichezwa kwa kasi ya chini sana .
Laureant Blanc aliteua kikosi ambacho kilicheza mfumo ambao kila mmoja alitarajia mfumo wa 4-3-3, huku Florent Malouda akihangaika mbele akitokea katikati ya uwanja.
Roy Hodgson aliwashangaza watu wengi kwa kumpanga Alex Oxlade Chamberlain ambaye alicheza upande wa kushoto huku James Milner akicheza upande wa kulia na Danny Welbeck akiongoza mashambulizi .
Kama ilivyotarajiwa, Ufaransa ilitawala sana mpira kwa maana ya umiliki huku ikimaliza kwa wastani wa asilimia 65 ya umiliki wa mpira huku wakipiga mashuti 21 tofauti na England ambao walipiga mashuti matano pekee. Hata hivyo mashuti mengi ya Ufaransa yalikuwa ya mbali yasiyokuwa na madhara ukiachilia mbali shuti la Nasri ambalo lilizaa bao la kusawazisha, yote kwa yote Ufaransa walihangaika kutengeneza nafasi za wazi.
Vita ya Mfumo
Ilikuwa vita nyepesi. England walikuwa na makundi ya wachezaji wanne wanne kwenye ulinzi na kiungo huku Ashley Young na Welbeck wakicheza mbele - Laureant Blanc alimpa Alou Diarra maelekezo ya kumkaba Ashley Young na kumnyima nafasi ya kufanya kazi kwa uhuru hasa pale ambapo Young alikuwa anarudi chini kusaka mpira. Yohan Cabaye alikuwa akicheza juu karibu na sehemu aliyokuwa Gerard na Malouda alikuwa akijaribu kumvuta Scott Parker kutoka kwenye nafasi yake aliyokuwa. Kiujumla kulikuwa na nafasi finyu sana kwa Ufaransa kufanya mambo yake kwa uhuru kwani England walijaza upande wao na kuwanyima Ufaransa uhuru wa kupiga pasi walizohitaji kupanga mashambulizi. Ufaransa walijaribu mbinu ya kupitisha mipira jambo ambalo liliwafanya England kutoa mipira mingi iliyoza kona ambazo hazikuzaa matunda .
Mashambulizi ya Ufaransa.
Wachezaji wanne wa Ufaransa waliokuwa wanacheza kwenye eneo la mbele akiwemo Malouda walikuwa wakipeana pasi kwa ufanisi. Wakati Riberry akiwa anacheza sana pembeni upande wa kushoto, Samir Nasri yeye alikuwa akisafa uwanja mzima na kucheza kila mahali jambo ambalo lilifungua nafasi kwa Mathieu Debuchy. Kiujumla mbinu na mipango yote ya Ufaransa ilimzunguka Samir Nasri na hata takwimu zilionyesha kuwa alicheza pasi nyingi kuliko wachezaji wote waliokuwa uwanjani jana. Kiujumla Nasri alitengeneza nafasi nane kwenye mchezo wote.
Nasri alikuwa mtu pekee ambaye alikuwa akitumia nafasi akijaribu kujenga mashambulizi, alikuwa akiingia kwenye eneo ambalo lilikuwa wazi na kuwachanganya wachezaji wa England wasijue la kufanya ili kumkabili. Wakati mwingine Lescott alikuwa akitoka nyuma na kujaribu kumfuata kumbugudhi asilete madhara, wakati mwingine Ashley Cole angetoka kwenye eneo lake na kujaribu kumkaba, kiujumla ile hali ya kuwavuruga wachezaji wa England kwenye jinsi ya kumkabili Nasri ndio ilikuwa msingi wa mashambulizi ya Ufaransa. Hata bao alilofunga Nasri lilikuja wakati ambao mabeki wa England walikuwa wamesogea ndani sana na kumuachia Nasri nafasi ambayo ilimfanya achague sehemu ya kupiga mpira na kusawazisha .
Ukiachilia mbali Movement za Nasri, England waliyamudu mashambulizi ya Ufaransa. Kikosi cha Laureant Blanc kilicheza kwa uvumilivu huku wakingoja nafasi ya wazi ambayo ingewapa mwanya wa kuidhuru England na hawakuwa wakiwaachia wachezaji wengi mbele katika hali ambayo pengine ingeweza kuwa na madhara hasa ukizingatia England walivyo wepesi kwenye mashambulizi ya Counter.
Mashambulizi ya England.
Mchezo wa England kwa ujumla ulijengwa kwenye kukubali presha ya Ufaransa na kujaribu kuvunja mashambulizi kwa hataka na kushambulia kwa kushtukiza –walifanikiwa katika hili kwenye michezo miwili ya kirafiki kabla ya michuano hii kuanza lakini kwa mchezo dhidi ya Ufaransa walikosa ufanisi kwenye jinsi ya kumalizia nafasi chache zilizotokea ndani ya mchezo. Sababu kubwa ya hili ilikuwa jinsi Ashley Young alivyoshindwa kutumika kwenye mchezo kama ilivyozoeleka. Alimaliza pasi 12 pekee kati ya 20 alizotengeneza .
Hata hivyo sifa kubwa ilimuendea Alou Diarra ambaye alikuwa mjanja sana kwa jinsi alivyojipanga na kumzuia Young wakati England walipokuwa na mpira . Kitakwimu Diarra Diarra alimaliza au alifikisha pasi zote alizopiga na tackles zake zote 5 alizopiga zilikuwa za mafanikio .
Nafasi pekee ya wazi ambayo England walitengeneza wakati mchezo ukiendelea ilikuja wakati James Milner alipomzunguka kipa Hugo Lloris lakini alipiga nje . Alex Oxlade Chamberlain aliingia katikati ya uwanja na Alou Diarra alimfuata jambo ambalo lilimfanya Ashley Young kuwa huru na kumpa Milner pasi, nafasi kama hii haikujitokeza tena. Danny Welbeck alicheza vizuri akikaa na mipira, lakini hakuwa na wakati mzuri kwa kuwa msaada wake mkubwa unatoka kwa Ashley Young ambaye alibanwa kwa kiasi kikubwa .
Young na Welbeck walicheza vizuri sana hasa walipokuwa bila mpira. Hawakukimbiza na kukaba mabeki wa pembeni wa Ufaransa, badala yake walisimama njiani na kuzuia pasi za wafaransa kupita njiani. Philipe Mexes na Adil Rami walikuwa wakipiga mipira ya moja kwa moja na walishindwa kupeleka mipira mbele toka nyuma, matokeo yake mchezo ulikuwa wa taratibu jambo ambalo kwa England lilikuwa zuri.
Kipindi cha Pili.
Mchezo ulikosa mwendelezo kwenye kipindi cha pili . England waliendelea kukaa mbele ya lango na Ufaransa walishindwa kuongeza idadi ya wachezaji waliokuwa wakishambulia nao. Bado mchezo uliendelea kuwa wa taratibu na timu zote zilionekana kuchoka mapema na kutambua kuwa sare yalikuwa matokeo mazuri.
Labda maendeleo pekee yalikuwa kwenye movement za Karim Benzema ambaye alionekana kukerwa na kukosekana kwa ubunifu na huduma ya pasi zilizoelekea kwake jambo lilomfanya ajaribu kufanya kila kitu mwenyewe . Mwishoni alijaribu kuiga alichokuwa anafanya Samir Nasri na kusogea kwenye maeneo ambayo yalikuwa na nafasi na alifanya hivi na kupiga mashuti ya mbali ambayo Jo Hart aliokoa. Timu zote zilichelewa kufanya mabadiliko, England walimuingiza Jermaine Defoe ambaye aliingia kwenye nafasi ya Alex Oxlade Chamberlain ambapo Ashley Young alienda kushoto na Jordan Henderson aliingia kwneye nafasi ya Scott Parker aliyeonekana kuchoka . Haya yalikuwa mabadiliko ambayo yalilenga kujenga mashambulizi zaidi hasa ukizingatia mabeki wa Ufaransa walionekana wamechoka .
Laureant Blanc alimuingiza Hatem Ben Arfa na Marvin Martin waliochukua nafasi za Malouda na Cabaye lakini mabadiliko haya yalifanywa muda ukiwa umepita na walikosa muda wa kufanya kazi ya kuokoa mchezo.
Mwisho.
Kwenye michezo yote ya raundi ya kwanza kumekuwa na soka la wazi sana ambalo kiujumla limetoa burudani kubwa lakini mchezo wa ufaransa na England ulikuwa wa kasi ya chini kupita yote . Ni kama timu zote zilikuwa zimepanga kutopoteza mchezo huukuliko zilivyopanga kutafuta ushindi na sare ilikuwa kama imepangwa huku Ufaransa wakionekana kupiga zaidi mashuti ya mbali baada ya kuona wameshindwa kuivunja defense ya England .
Shape ya England haikuwa mbaya , hata hivyo mabadiliko ya movement toka wakati ambapo timu haina mpira na pale ilipokuwa na mpira hazikuwa nzuri na hii ilitokana na Ashley Young kufichwa sana . Kwa mfumo wa England Young ni mtu muhimu lakini Ufaransa walifanya kazi kubwa ya kumtia mfukoni . Hodgson anapaswa kufanya kazi kubwa ya kuifanya England kuwa na madhara zaidi inapokuwa na mpira
Bakari Malima ‘Jembe Ulaya’-EPISODE 6
BAKARI MALIMA MWENYE JEZI YA NJANO.
*Azuiawa kwenda Rwanda, aitwa mahakamani
*Aifungia Yanga bao ugenini, alitoa zawadi
Na Saleh Ally
WIKI ILIYOPITA tuliishia Malima akiwa ameanza mazoezi na Yanga kujiandaa dhidi ya Rayon. Lakini hofu yake kubwa ilikuwa ni namna ya kuieleza timu yake ya Vaal Professional ya Afrika Kusini kwamba amejiunga Yanga na hatarudi kuichezea. Je atafanyaje? Endelea.
NILIWAZA namna ya kuwaeleza jamaa, mmiliki wa timu alikuwa ni rafiki yangu na tulikuwa tukiwasiliana mara kadhaa kabla sijaenda kule. Hata kile kipindi nilichonyimwa kibali kutoka Fat halafu Nonda akapata kutoka Burundi, bado aliendelea kunikarimu.
Nilijisikia vibaya sana kuona nawaangusha, lakini haikuwa nia yangu kufanya hivyo na sikuwa na ujanja pia. Niliamua kupiga simu na kuwaleza kila kitu, walishangazwa na hali hiyo ingawa walishasikia angalau kidogo kuhusiana na suala hilo.
Walionekana wako upande wangu na kuahidi wangesubiri nimalize suala hilo halafu nirejee kuichezea timu hiyo maana nilikuwa na mkataba wa miaka mitatu na nilikuwa nimecheza nusu msimu tu.
Huku nyumbani, awali sikuelewa vizuri. Yanga ilitakiwa kucheza na Rayon Sports ya Rwanda mechi mbili, nyumbani na ugenini, mshindi anmgevuka na kucheza hatua ya nane bora ya Ligi ya Mabingwa Afrika kwa mara ya kwanza.
Hivyo maandalizi hapa Dar es Salaam yaliendelea chini ya Kocha Mkuu, Tito Mwaluvanda na msaidizi, Fred Felix Minziro. Wakati huo tuliweka kambi Chuo cha Posta, Kijitonyama.
Ila mimi niliendelea na maandalizi kwa ajili ya mechi ya pili ambayo ingechezwa Dar es Salaam, maana mahakama ilizuia paspoti yangu. Sikutakiwa kusafiri nje ya nchi kutokana na kesi yangu ya tuhuma za kuhusishwa na madawa ya kulevya iliyokuwa inaendelea.
Hali hiyo iliniumiza sana, lakini niliamua kukubaliana nayo. Nilichofanya ni kuendelea kujifua kwa nguvu sana, nilijua siku moja suala hilo litaisha tu. Kwa ninavyojijua, nilianza kuwa fiti, niliamini nitacheza vizuri katika mechi yoyote nitakayopangwa.
Siku nne kabla ya Yanga kusafiri kwenda Rwanda, nilitakiwa kwenda mahakamani baada ya uchunguzi kukamilika. Nilikuwa nina hofu sana, nilijua ni wakati mgumu. Lakini nilimuachia Mungu, maana nilijiamini sikuwa nimefanya makosa yoyote.
Tulipofika mahakamani, watu wengi walikuwa pale lakini si sana kwa kuwa kesi haikuripotiwa sana kwenye vyombo vya habari kutokana na kwamba ilikuwa ni ghafla sana baada ya upelelezi kuwa umekamilika.
Niliongozana na wanasheria wangu na mahakama ikafanya kazi yake muda mrefu , nilikuwa pale kimya muda wote. Nilijua kila kitu kitaenda vizuri kwa uwezo wake Mungu. Baada ya muda mrefu wa taratibu za kimahakama, tuliachiwa huru.
Kesi hiyo kwa kumbukumbu zangu ilikwenda kwa mwaka mzima, nakumbuka niliachiwa Mei, 1998. Nilikuwa nina furaha ambayo haina mfano, nilichanganyikiwa. Mashabiki walinifuata na kunikumbatia, baadhi ya ndugu zangu walikuwa pale. Wanayanga na wengi pia wlaikuwa pale na tukafanya sherehe ya muda pale. Baada ya hapo nikaondoka na viongozi kurudi kambini. Sikuamini, niliona kama ninaota.
Pamoja na kufurahi kuachiwa, nilijua ningeweza kusafiri na Yanga kwenda Rwanda, kitu ambacho nilikitaka kwa nguvu sana. Nilitaka kuitumikia Yanga na kuwalipa kutokana na msaada mkubwa walionipa kutoka katika kitu hicho kibaya kabisa maishani mwangu.
Suala hilo la kutuhumiwa kuwa na madawa ya kulevya, lilirudisha nyuma maisha yangu. Niliona ulikuwa ni kama mpango uliosukwa kwa ajili ya kuniharibia maisha yangu. Lakini bado mwisho, niliona acha nimuachie Mungu kwa mara nyingine.
Nilipofika kambini, nilikuwa kama nimepagawa, sikuchelewa. Nilivaa viatu na moja kwa moja nikaenda uwanjani kuanza mazoezi. Baada ya saa moja wenzangu walikuja, tukaungana na kuendelea pamoja tena.
Alhamisi tukaondoka kwenda Kigali, tukiwa tayari kwa vita. Mechi ilichezwa Jumapili na mechi ilipoanza tu, dakika ya tano, mchezaji wetu, Banza Tshikala akalambwa kadi nyekundu. Maana yake tukawa pungufu halafu tuko ugenini.
Lakini mimi nilijituma sana, nilijua kasi haikuwa lahisi. Rayon walipata bao lakini Seki (Chambua) akasawazisha kitaalamu. Baadaye nami nikafunga bao kw akichwa baada ya kuunganisha mpira wa adhabu wa Seki.
Mwishoni kabisa, jamaa wakasawazisha. Matokeo yakawa 2-2, tukarudi nyumbani kusubiri mechi ya marudiano ambayo angalau sare ya bila kufungana au moja moja ingetupeleka mbele. Nilipofika Dar es Salaam, nikalitoa zawadi bao langu kama zawadi kwa Wanayanga.
Kwa pamoja, wachezaji tuliuomba uongozi wa klabu uturuhusu mechi dhidi ya Rayon ichezwe CCM Kirumba, Mwanza. Tulihofia presha ya Dar es Salaam, wangeweza kutuchanganya. Kitu kizuri uongozi ukakubaliana nasi. Maandalizi ya mechi inayofuatia, yakaanza.
MALIMA ameungana na Yanga hadi Rwanda na mchango wake ukawa mkubwa sana. Macho na masikio yameelekezwa katika mechi ya pili iliyopangwa kuchezwa mjini Mwanza. Je, watafanikiwa kuvuka. Kuna kitu kingine Malima atafanya na timu yake ya Afrika Kusini itaendelea kukaa kimya?
WAREMBO 12 wanaotarajia kuwania taji la kitongoji cha Kigamboni mwaka huu
Na Mwandishi Wetu
WAREMBO 12 wanaotarajia kuwania taji la kitongoji cha Kigamboni mwaka huu 'Miss Kigamboni City 2012' leo Jumatano wanatarajiwa kufanyiwa usaili kwa ajili ya kuanza safari ya kumpata mshindi wa shindano hilo litakalofanyika Ijumaa kwenye ukumbi wa Navy Beach jijini Dar es Salaam.
Mratibu wa shindano hilo, kutoka kampuni ya K&L Media Solutions, Somoe Ng'itu, alisema jana kuwa maandalizi ya zoezi hilo yamekamilika na wanachosubiri ni siku ya shindano ifike.
Alisema kuwa kitongoji hicho kina warembo wenye sifa na wanaojiamini ambao wamepania kurudisha taji la Miss Tanzania kwenye Kanda ya Temeke.
Aliongeza kuwa ili kuboresha shindano hilo bendi ya muziki wa dansi ya FM Academia maarufu Wazee wa Ngwasuma na msanii na mchekeshaji mahiri hapa nchini, Mpoki watatumbuiza kwenye kinyang'anyiro hicho.
"Tunawaomba wadau wa sanaa ya urembo kufika kushuhudia mrembo wa Kigamboni atakavyopatikana, ni Kitongoji kilichoko sehemu pekee hapa nchini na kulikosa kushuhudia itakuwa ni kujinyima burudani wewe mwenyewe," alisema mratibu huyo.
Aliwataja warembo watakaochuana kuwa ni pamoja na Susanne Jeremiah, Agness Goodluck, Elizabeth Boniface, Dorothea Kessy, Esther Albert, Edda Silyvester, Sophia Martin, Doreen Kweka, Khadija Kombo, Linnah David, Rosemary Peter na Winnie Karaya.
Aliwashukuru wadhamini ambao wamejitokeza kusaidia shindano hilo ambao ni Redd's, Dodoma Wine, hoteli ya Hope Country, Screen Masters, Global Publishers, Nobro Collections, Times FM na Clouds FM.
Aliongeza kuwa warembo watakaoshika nafasi tatu za juu kutoka katika shindano hilo wataungana na wenzao kutoka vitongoji vya Kurasini na Chang'ombe ili kuwania taji la Kanda ya Temeke baadaye mwaka huu.
EXCLUSIVE: SIMBA KWENYE MIKAKATI MIZITO YA KUMNYAKUA SHEDRACK NSAJIGWA
Siku chache baada ya mchezaji Shedrack Nsajigwa kumaliza mkataba wa kuichezea klabu ya Yanga huku akiripotiwa kuwepo nchini Kenya akifanya mazungumzo na klabu ya Gor Mahia, leo taarifa za uhakika kutoka kwenye kamati ya usajili ya Simba, zinasema viongozi wa mabingwa wa Tanzania wapo tayari kumsaini nahodha huyo wa zamani wa Yanga na Taifa Stars.
Simba ambao leo hii wamepata pigo baada ya beki wao wa upande wa kulia Said Nassoro Chollo kuripotiwa kupata majeraha makubwa kama yale yaliyompata Uhuru Seleman, wanamuona Nsajigwa kama mbadala halisi atakayefaa kuziba mapengo kwenye safu ya ulinzi ya timu hiyo.
Mtoa taarifa anasema, "Nsajigwa bado ni mchezaji mzuri sana, na uwezo mkubwa na kikubwa zaidi ni uzoefu alionao ambao ni hazina kubwa kwa klabu kama yetu ambayo sasa tunajaribu kuingiza vijana wadogo kama akina Singano, na ndio maana tumeamua kuanza harakati za kumsajili na kwa hakika tutafanikiwa."
Monday, June 11, 2012
EURO 2012 UKRAINE VS SWEDEN: VITA YA ZLATAN IBRAHIMOVIC NA SHEVCHENKO: NANI KUIBUKA MSHINDI?
VIKOSI VINAVOTARAJIWA KUANZA
Ukraine: Pyatov, Selin, Rakitskly, Kucher, Gusev, Tymoschchu, Konoplyanka, Voronin, Yarmolenko, Milevskly, Shevchenko.Sweden: Isaksson, Olsson, Mellberg, Granqvist, Lustig, Kallstrom, Elm, Larsson, , Rosenborg, Ibrahimovic
MAMBO MUHIMU KUHUSU TIMU ZOTE MBILI
- Ukraine inabidi wachague kati ya Artem Milvskiy, Andrey Voronin, Marko Devic na veteran Andrey Shevchenko kuanza kwenye safu ya ushambuliaji, huku tishio lao kubwa likiwa linatokea kwenye winga.
- Makinda Konoplyanka na Yarmolenko watakuwa na mzigo mkubwa wa kuleta ubunifu kwenye kiungo cha timu hiyo mbele ya mashabiki wao wa nyumbani, kwa hakika watakuwa kwenye presha kubwa ya kufanya vizuri huku wakiwa na umri wa miaka 22 tu.
- Anatoliy Tymoshchuk ndio atakuwa kiungo mkabaji wa kuulinda ukuta wa timu yake, huku beki wa kulia akiongoza mashambulizi kutokea pembeni.
- Ishara za mapema zinaonyesha kwamba Markus Rosenborg ataanza mbele ya dhidi ya Johan Elmander, huku tegemeo lao Zlatan Ibrahimovic akiongoza safu hiyo ya ushambuliaji.
- Toivonen atarudi kwenye nafasi yake aliyoizoea ya bekiwa kushoto, huku Rasmus Elm akitegemewa kushirikiana na Kallstrom mbele ya veteran Anders Svensson.
- Sweden wanaweza kukichezesha kikosi kile kile kilichoshinda kwenye mechi ya karibuni dhidi ya Serbia, huku Jonas Olsson akiwa nje na Granqvist akianza.
Kumekuwepo na wastani wa zaidi 2.5 wa magoli kwenye mechi 9 za Sweden kwenye Euro.
Sweden wameshinda mechi zao 6 kati ya 7 za mwisho za Euro.
Sweden wamefunga angalau mabao 2 katika kila mechi zao 6 kati ya 7za Euro.
EURO 2012: ENGLAND BILA WAYNE ROONEY KUACHA UTEJA KWA UFARANSA LEO?
VIKOSI VITAKAVYOANZA
France: Lloris, Debuchy, Rami, Mexes, Evra, Diarra, Cabaye, Ribery, Malouda, Nasri, Benzema
England: Joe Hart, Johnson, Terry, Lescot, Ashley Cole, Milner, Parker, Steven Gerrard, Oxlade-Chamberlain, Ashley Young, Welbeck
MAMBO MUHIMU KUHUSU TIMI ZOTE MBILI
Kumekuwepo na wastani wa 2.5 wa mabao yaliyofungwa kwenye mechi 9 za mwisho za Euro za Ufaransa.
Ufaransa hawajafungwa kwenye mechi zao 9 za Euro Cup.
Ufaransa wameifunga England katika mechi zao 3 za mwisho kwenye mashindano yote.
England hawajafungwa kwenye mechi zao 8 za mwisho za Euro Cup.
France: Lloris, Debuchy, Rami, Mexes, Evra, Diarra, Cabaye, Ribery, Malouda, Nasri, Benzema
England: Joe Hart, Johnson, Terry, Lescot, Ashley Cole, Milner, Parker, Steven Gerrard, Oxlade-Chamberlain, Ashley Young, Welbeck
MAMBO MUHIMU KUHUSU TIMI ZOTE MBILI
- France wanaingia kwenye mchezo wao huku wakiwa na crisis kwenye safu ya kiungo huku Yohan Cabaye ndio pekee aliye fiti kwa asilimia mia, huku M'Vila, Matuidi na Diarra wakiwa na shaka juu ya ufiti wao.
- Patrice Evra amekuwa akishutumiwa kwa kucheza chini ya kiwango lakini anaonekana ataanza mbele ya Gael Clichy, huku vita kubwa ya namba ya kiungo mshambuliaji ikiwa kati ya Menez, Malouda na Valbuena.
- Karim Benzema atapata nafasi ya kuanza, huku Olivier Giroud akiwa anasubiri kwenye benchi.
- Akifunga goli lake la kwanza la mechi ya kimataifa katika mchezo wa hivi karibuni dhidi ya Ubelgiji, kumemfanya Welbeck apate nafasi kubwa ya kuanza leo mbele ya Andy Carroll, ambaye nae kama Giroud, ni hatari sana kwa mipira ya juu.
- Ashley Young anategemewa kupewa free role nyuma ya mshambuliaji, huku James Milner na Alex Oxlade Chamberlain wakipewa nafasi ya kuanza mbelel ya Downing na Theo Walcott kwenye winga.
- Safu nyingine yenye upinzani mkubwa ni ulinzi wa kati, mtu wa kucheza sambamba na Terry, Hodgson kichwa kinamuuma ampe nafasi nani kati ya Lescott au Phil Jagielka.
- Wayne Rooney ndio anaanza adhabu yake ya kusimamishwa michezo miwili baada ya kutolewa nje kwa kadi nyekundu kwenye mchezo wa kufuzu dhidi Montenegro.
TAKWIMU
England wamefunga atleast magoli 2 katika mechi zao 12 kati ya 15 za Euro Cup.Kumekuwepo na wastani wa 2.5 wa mabao yaliyofungwa kwenye mechi 9 za mwisho za Euro za Ufaransa.
Ufaransa hawajafungwa kwenye mechi zao 9 za Euro Cup.
Ufaransa wameifunga England katika mechi zao 3 za mwisho kwenye mashindano yote.
England hawajafungwa kwenye mechi zao 8 za mwisho za Euro Cup.
Azam FC yaanza rasmi mazoezi Leo
Stewart alikuwa nchini Uingereza kwa mapumziko baada ya kumaliza msimu uliopita kwa mafanikio ya kutwaa medali ya fedha kwa kuwa washindi wa pili wa VPL.
Katibu Mkuu wa Azam FC, Nassor Idrissa jana ameiambia tovuti ya http://www.azamfc.co.tz/ kuwa wataanza mazoezi jioni kutokana na kocha huyo kurudi asubuhi ya siku hiyo.
Akizungumzia wachezaji wengine alisema, wachezaji wote wa kimataifa wameshawasili tayari kwa kuanza mazoezi hayo wakiwa pamoja na wachezaji wengine. Mazoezi hayo yatafanyika kwenye uwanja wa Azam Chamazi jijini Dar es Salaam.
Idrissa aliongeza kuwa wachezaji waliopo timu ya Taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’ watajiunga mara baada ya kumaliza michezo yao, na wale wa Zanzibar Heroes watarejea nchini baada ya kumaliza michezo ya Kombe la Dunia kwa nchini ambazo sio wanachama wa FIFA.
Aliwataja wachezaji waliowasili kuwa ni George Odhiambo na Ibrahim Shikanda kutoka nchini Kenya ambao wote waliingia Alhamis, Tchetche Kipre na Michael Kipre kutoka nchini Ivory na Joseph Owino wa Uganda.
Idrissa alisema wachezaji wa Tanzania nao wameshaandaa mazingira kwa ajili ya kuanza mazoezi hayo wakiwemo vijana kutoka Azam Academy ambao wamepanda kuicheza timu kubwa, Aishi Salum, Juckson Wandwi, Dizana Issa, Ibrahim Rajab ‘Jeba’ na Joseph Kimwaga.
Aidha Idrissa alisema Azam Academy wameshaanza mazoezi siku ya Ijumaa isipokuwa wacheza watatu ambao bado hawajawasili kujiunga na timu hiyo.
SOURCE: azamfc.co.tz
Sunday, June 10, 2012
TAIFA STARS YANG'ARA TAIFA - WATANDIKA GAMBIA 2-1
![]() |
| Kikosi cha Taifa Stars kilichoanza leo. |
Stars ilitoka nyuma kwa 1-0 kipindi cha kwanza na kuibuka na ushindi huo- kwa mabao ya kipindi cha pili ya Shomari Kapombe dakika ya 60 na Erasto Nyoni dakika ya 87 kwa penalti, baada ya beki mmoja wa Gambia kuunawa mpira kwenye eneo la hatari.
Stars ambayo mechi ya kwanza ilifungwa 2-0 na wenyeji Ivory Coast mjini Abidjan Jumamosi iliyopita, kipindi cha kwanza ilicheza ovyo kidogo, lakini kuingia kwa Haruna Moshi ‘Boban’ aliyechukua nafasi John Bocco ‘Adebayor’ kipindi cha pili, kuliifanya Tanzania icheze kwa uhai na kulitia misukosuko lango la Gambia hatimaye kupata mabao hayo mawili.
Gambia walitangulia kupata bao lililofungwa na Mamadou Ceesay dakika ya nne.
Stars sasa imejinasua mkiani mwa kundi C na kupanda nafasi ya pili badaaye Morocco kutoa sare ya 2-2 jana na Ivory Coast inayoongoza kwa pointi zake nne.
Kwa Stars huu ni ushindi wa kwanza nyumbani tangu waifunge Jamhuri ya Afrika ya Kati Machi 26, mwaka jana.
| Haruna Moshi Boban na Nurdin Bakary wakiwa kwenye benchi wakiwaangalia wadogo zao wakasakata soka safi dhidi ya Gambia. |
![]() |
| Nahodha wa Stars Juma Kaseja na mshambuliaji Mrisho Ngassa wakipozi baada ya kuwatungua Gambia. |
EURO 2012: JAMHURI YA IRELAND DHIDI MAFUNDI WACROATIA NANI KUIBUKA MBABE.
VIKOSI VITAKAVYOANZA LEO
Ireland: Shay Given, John O'Shea, Ledger, Richard Dunne, Ward, Damian Duff, Whelan, Andrews, McGeady, Keane, Doyle.
Croatia: Pletikosa, Srna, Corluka, Simunic, Strinic, Kranjcar, Luka Modric, Dujmovic, Rakitic, Eduardo, Mandzukic
Croatia hawajafungwa katika mechi 25 kati ya 28 za mwisho za EURO Cup.
Croatia wamekuwa na ukuta mgumu usioruhusu bao kwenye mechi 3 za mwisho za EURO.
Ireland hawajafungwa katika mechi zao 9 za mwisho za EURO.
Ireland: Shay Given, John O'Shea, Ledger, Richard Dunne, Ward, Damian Duff, Whelan, Andrews, McGeady, Keane, Doyle.
Croatia: Pletikosa, Srna, Corluka, Simunic, Strinic, Kranjcar, Luka Modric, Dujmovic, Rakitic, Eduardo, Mandzukic
- Giovanni Trapattoni ametoa ishara kwamba anaweza kuuacha mfumo wake wa 4-4-2 uliokuwa ukimpa nafasi ya kuwa na viungo wengi, lakini pia akasema anahisi Robbie Keane anaweza kucheza kama mshambuliaji pekee hivyo mabadiliko kwenye kikosi yanaweza kujitokeza.
- Kevin Doyle anapewa nafasi kubwa ya kuanza mbelel ya Long na Walters pamoja na kutokuwa na msimu mzuri na Wolves.
- Mashabiki wengi wa Ireland wamekuwa wakitaka kumuona James McClean ajaribiwe kwenye mechi kubwa lakini wanaweza kumuona kinda hili likipata nafasi ya kucheza kama sub, huku Andrews na Whelan wanaweza kumtoa Gibson.
- Utawala wa Slaven Bilic kama kocha wa Croatia utaisha baada ya michuano hii na kwa hakika ana maamuzi ya kugumu kwenye kikosi chake hasa katika safu ya ulinzi, huku bekiwa kati Dejan Lovren na Ivica Olic wakiondolewa kwenye mashindano kwa majeruhi.
- Kwenye safu ya ushambuliaji kichwa kinampasuka juu ya uteuzi wa kuanza na Jelavic au Eduardo, huku Mario Mandzukic akicheza kama mshambuliaji wa pili.
- Dujmovic na Vukojevic wanapigania nafasi ya kuanza kwenye kiungo mkabaji, wakati Kranjcar na Rakitic wakipewa nafasi kubwa ya kucheza kwenye wings.
TAKWIMU
Croatia hawajafungwa katika mechi 25 kati ya 28 za mwisho za EURO Cup.
Croatia wamekuwa na ukuta mgumu usioruhusu bao kwenye mechi 3 za mwisho za EURO.
Ireland hawajafungwa katika mechi zao 9 za mwisho za EURO.
EURO 2012: SPAIN DHIDI YA ITALIA - VITA YA WAPIGA PASI BORA XAVI NA ANDREA PIRLO
VIKOSI VINAVYOATARAJIWA KUANZA LEO
Spain: Iker Casillas, Arbeloa, Sergio Ramos, Jordi Alba, Segio Busquets, Xavi, Alonso, Iniesta, Torres, Silva.
Italia: Buffon, Bonucci, Chiellini, Rossi, Baizaretti, Marchisio, Pirlo, Nocerino, Maggio, Balotelli, Cassano.
MAMBO MUHIMU KUHUSU MECHI HII
- Tangu kuumia kwa Carles Puyol na David Villa wote waondolewe kwenye Euro 2012 kwa majeruhi, Spain hawajapata habari nyingine mbaya ya majeruhi.
- Wamecheza mechi kadhaa za kirafiki hivi karibuni huku Del Bosque akikbadilisha kikosi mara kwa mara bila tatizo lolote, na katika michezo yote walipata matokeo.
- Kiuhalisia wachezaji wote wenye majina makubwa wataanza kwenye hii mechi, baada ya mambo kubadilika kwenye mechi za kirafiki. Andres Iniesta alitokea benchi na kucheza vizuri kusababisha ushindi dhidi ya China, leo atarudi kwenye line up katika mchezo ambao unatajwa kama mgumu zaidi kwa Spain kwenye hatua ya makundi.
- Andrea Barzagli ameripotiwa kuwa na mashaka juu ya kucheza kutokana na majeruhi ambayo yatafanya asiweze kucheza mbili za kwanza au zaidi. Cesare Prandelli amemuita Davide Astori kwenye stand by list na atafanya maamuzi Ijumaa kama amrudishe Barzagil nyumbani au kuendelea nae mbele akiwa na matumaini ya atapona.
- Waitaliano leo wanaweza kutumia mfumo wa 3-5-2 huku Daniele de Rossi akicheza nyuma na Marchisio na Balzaretti wakicheza kwenye mashavu ya kushoto na kulia.
TAKWIMU
Spain wameshinda mechi 10 zilizopita kwenye Euro CupItaly hawajaruhusu wavu wao kuguswa katika mechi 8 kati ya 9 kwenye Euro Cup.
Spain wamefunga atleast goli 2 katika mechi zao 8 za Euro Cup
Italy hawajafungwa katika mechi zao 13 kwenye Euro Cup.
Spain hawajaruhusu wavu kuguswa katika mechi zao 3 za mwisho dhidi ya Italia kwenye mashindano yote.
Subscribe to:
Posts (Atom)














