Search This Blog

Sunday, June 10, 2012

TAIFA STARS YANG'ARA TAIFA - WATANDIKA GAMBIA 2-1

Kikosi cha Taifa Stars kilichoanza leo.
TIMU ya soka ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars imeibuka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Gambia jioni hii kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam, katika mechi ya pili ya Kundi C, kuwania tiketi ya kucheza Fainali za Kombe la Dunia mwaka 2014 nchini Brazil.

Stars ilitoka nyuma kwa 1-0 kipindi cha kwanza na kuibuka na ushindi huo- kwa mabao ya kipindi cha pili ya Shomari Kapombe dakika ya 60 na Erasto Nyoni dakika ya 87 kwa penalti, baada ya beki mmoja wa Gambia kuunawa mpira kwenye eneo la hatari.

Stars ambayo mechi ya kwanza ilifungwa 2-0 na wenyeji Ivory Coast mjini Abidjan Jumamosi iliyopita, kipindi cha kwanza ilicheza ovyo kidogo, lakini kuingia kwa Haruna Moshi ‘Boban’ aliyechukua nafasi John Bocco ‘Adebayor’ kipindi cha pili, kuliifanya Tanzania icheze kwa uhai na kulitia misukosuko lango la Gambia hatimaye kupata mabao hayo mawili.
Gambia walitangulia kupata bao lililofungwa na Mamadou Ceesay dakika ya nne.

Stars sasa imejinasua mkiani mwa kundi C na kupanda nafasi ya pili badaaye Morocco kutoa sare ya 2-2 jana na Ivory Coast inayoongoza kwa pointi zake nne.

Kwa Stars huu ni ushindi wa kwanza nyumbani tangu waifunge Jamhuri ya Afrika ya Kati Machi 26, mwaka jana.
Haruna Moshi Boban na Nurdin Bakary wakiwa kwenye benchi wakiwaangalia wadogo zao wakasakata soka safi dhidi ya Gambia.

Nahodha wa Stars Juma Kaseja na mshambuliaji Mrisho Ngassa wakipozi baada ya kuwatungua Gambia.


2 comments:

  1. Hongera stars kwa ushindi na kwa kocha pia kwa kuwapa nafasi vijana kuonyesha uwezo wao. Tumekuwa na tatizo la kushindwa kutumia vema uwanja wa nyumbani ila kwa mwanzo huu si mbaya wakaye buti tukipata pointi zote 9 za nyumbani inakuwa safi sana na hasa katika kipanda viwango vya FIFA.
    madau
    Mike

    ReplyDelete
  2. Inafurahisha sana! Japo ukiangalia hizo ishara za Mrisho Ngasa na Juma K Juma utagundua Kaseja anaonyesha alama ya FreeMasons!

    ReplyDelete