Search This Blog

Sunday, June 10, 2012

EURO 2012: JAMHURI YA IRELAND DHIDI MAFUNDI WACROATIA NANI KUIBUKA MBABE.

VIKOSI VITAKAVYOANZA LEO

Ireland: Shay Given, John O'Shea, Ledger, Richard Dunne, Ward, Damian Duff, Whelan, Andrews, McGeady, Keane, Doyle.


Croatia: Pletikosa, Srna, Corluka, Simunic, Strinic, Kranjcar, Luka Modric, Dujmovic, Rakitic, Eduardo, Mandzukic


  • Giovanni Trapattoni ametoa ishara kwamba anaweza kuuacha mfumo wake wa 4-4-2 uliokuwa ukimpa nafasi ya kuwa na viungo wengi, lakini pia akasema anahisi Robbie Keane anaweza kucheza kama mshambuliaji pekee hivyo mabadiliko kwenye kikosi yanaweza kujitokeza.
  • Kevin Doyle anapewa nafasi kubwa ya kuanza mbelel ya Long na Walters pamoja na kutokuwa na msimu mzuri na Wolves.
  • Mashabiki wengi wa Ireland wamekuwa wakitaka kumuona James McClean ajaribiwe kwenye mechi kubwa lakini wanaweza kumuona kinda hili likipata nafasi ya kucheza kama sub, huku Andrews na Whelan wanaweza kumtoa Gibson.
  • Utawala wa Slaven Bilic kama kocha wa Croatia utaisha baada ya michuano hii na kwa hakika ana maamuzi ya kugumu kwenye kikosi chake hasa katika safu ya ulinzi, huku bekiwa kati Dejan Lovren na Ivica Olic wakiondolewa kwenye mashindano kwa majeruhi.
  • Kwenye safu ya ushambuliaji kichwa kinampasuka juu ya uteuzi wa kuanza na Jelavic au Eduardo, huku Mario Mandzukic akicheza kama mshambuliaji wa pili.
  • Dujmovic na Vukojevic wanapigania nafasi ya kuanza kwenye kiungo mkabaji, wakati Kranjcar na Rakitic wakipewa nafasi kubwa ya kucheza kwenye wings. 
TAKWIMU

Croatia hawajafungwa katika mechi 25 kati ya 28 za mwisho za EURO Cup.

Croatia wamekuwa na ukuta mgumu usioruhusu bao kwenye mechi 3 za mwisho za EURO.

Ireland hawajafungwa katika mechi zao 9 za mwisho za EURO.

No comments:

Post a Comment