Habari rasmi kutoka kwenye kamati ya usajili ya klabu ya Yanga ni kwamba timu hiyo leo imekamilisha usajili wa kinda la timu ya taifa ya Tanzania aliyeng'ara kwenye mchezo wa jumapili iliyopita dhidi ya Gambia Frank Domayo.
Domayo ambaye alikuwa akiichezea JKT Ruvu msimu uliopita, amesaini mkataba wa miaka 3 kuitumikia Yanga, huku akilipwa shilingi millioni 20 kama ada ya usajili na atakuwa akilipwa shilingi millioni moja kama msharaha kwa miaka 3 ijayo.
Naona sasa mambo yamebadilika, badala ya timu ya Taifa kuchukua wachezaji toka kwenye vilabu, Vilabu sasa vinasubiri kambi ya Timu ya Taifa kusajili wachezaji.
ReplyDeleteYeah na huo ndio utaratibu mzuri wa kusajili wachezaji wanaochezea timu za taifa. Wangejitahidi kusajili na wachezaji wa kigeni kutoka kwenye kambi zao timu za taifa tungekuwa na vilabu vyenye timu nzuri.
ReplyDeleteMm nafurahishwa na jinsi mnyama anavyosajili kimya kimya, hana kelele wala kokoro.
ReplyDeletehawa jamaa zetu wa mtaa wa pili zile goli 5 zimewatia kiwewe wanaweweseka tu.
Yanga kwa Promo kama Tusker beer vile....
ReplyDeleteKipindi cha neema hiki kwa wachezaji wacha wavune japo nilitamani sana vijana hawa wadogo wenye vipaji wangesajiliwa Azam wangejengeka sana ila mwisho wa siku mwenye kisu kikali ndio anakula nyama, ila hawa yanga mwisho wa siku watajikuta wana kikundi cha wachezaji wazuri ila hawana timu, usajili wao unazingatia mapungufu waliyonayo kwenye timu ama unaangalia ustaa wa mchezaji.Na utata utakuja pale anayewasili atakapo kosa kura watu watajuta.
ReplyDeleteMdau
Mike
Sasa unasajili mchezaji kwa mali kauli utataka promo?walitudanganya nizar atatambulishwa mechi ya mwisho na kukabidhiwa jezi 8 tena mwenyekiti huyo anasema uongo kumbe mali kauli nizar kachomoa kukopwa
ReplyDeleteNyie mcojua mpira kumtangaza mchezaji mliye msajili co promo acheni kudumaza upeo wenu wa kufikiri!!! Kumbukeni huu ni msimu wa usajili thus kila timu ikikamilisha usajili wa mchezaji fulani lazima imtangaze!!! hivi timu zingekuwa hazitangazi usajili wake leo mngejua kuwa CHELSEA wamemsajili EDEN HAZARD? au MAN UTD imemsajili kinda NICK POWELL? Jamani kumbukeni kuwa mmiriki wa hii BLOG ni mtu wa mpira na ipo kwaajili ya watu wa mpira co CRICKET.. so kama hujui soka linaendeshwaje co lazima ukacomment unazi wako wa USIMBA na UYANGA wa kijinga humu... Big up kaka Shafii kwa kutupa hizi news!!!
ReplyDeleteunajua watu wasimba sasa wamechotwa na huyu mwanasiasa RAGE. lakwanza la pili 5 zimewachanganya. walipotolewa na sandi kule sudani, yule mbunge wao wa tabora akakumba goli 5 walizomfunga yanga. sasa wameshashindwa na manji kwa njuluku za kusajiliwameanza tena hooooo 5 zimewachanganya. jamani simba tuwe makini yanga anatuwinda kagame, na hata ligi kuu . tusahau zile 5. tuanze maandalizi ya 5 nyingine. mbona hata madridi ilifungwa tano na baca, lakini dunia ilikuwa shwari, man u ilifungwa 6 na man city lakini dunia ilikuwa shwari. asernal ilifungwa 8 na man u na dunia ikawa shwari. tena kitendo kile kilimfanya WENGA akasajili upesi na kufunzo club bingwa mwakani.kama wanavyo fanya yanga baada ya kufungwa 5.sasa tuache unazi wa kijinga, yanga wanajiuliza juu zile goli 5 na wanataka kuzirejesha ndio maana wanahaha kusajili timu bora. mkimsikiliza rage na majigambo ya goli tano mtajikuta mnapoteza mechi zote mbili ligi kuu msimu ujao. TUBADILIKE.
ReplyDeletekaka kama hujui soka nyamaza usidanganye watu asubuhi hii. mawakala wengi sasa wapo EURO wanasaka vipaji toka kwenye timu za taifa zinazoshiriki mashindano hayo. sasa unashangaa nini yanga kutafuta vipaji timu ya taifa? acha unazi muuza karanga wewe usiejua soka. kaka shafii nakuomba ubadilishe hizi PASSWORD. ILI MTU ATOE COMMENT LAZIMA UMUULIZE ANGALAU SWALI MOJA LA KIMICHEZO KWA MFANO. muulize hivi simba na yanga nani kamfunga mwezake mara nyingi? au ni timu ip tanzania ianhistoria nzuri kimataifa? au ni timu ipi iliyochuku kombe la ligikuu au kagame au tusker mara nyigi. au ataje majina ya washambuliaji wawili wa timu ya taifa waliong'ara timu ya taifa waliposhiriki kwa mara ya kwanza mataifa afrika miaka ya themanini? au ni timu ipi inayoongozwa kwa viwango vya FIFA barani amerca ya kusini kwa sasa? au nimchezaji gani wa AFRICA analipwa pesa nyingi ligi kuu ya ENGLAND? KWA KUFANYA HIVYO SHAFII UTAWAJUA WANASOKA NA WAUZA SURA. ANAEKOSA SWALI NO COMMENT ILI UTUPUNGUZIE VIBUKUZI WASIOJUA SOKA HUMU NDANI. WANAOCOMMENT KWA UNAZI NA SI KWA UHALISIA WA MABO.
ReplyDeleteYanga nao sasa wamezidi,kila mchzaji wao tu...wachezaji wote hawa watachezaje pale,tukichukulia hiyo nafasi ya kiungo Kijiko,Nurdin,Godfrey Bony,Omega Seme,Chuji,Niyonzima,Nizar na huyu Domayo,sasa sijui nani atacheza nani atasubiri benchi.
ReplyDeletehawa kina domayoni vijana ambaye anaweza kucheza namba yoyote ilwe uwanjani si unaona shomari kapombe ni kiraka hii kutokana na umri alikuwanao
ReplyDelete