Search This Blog

Monday, June 11, 2012

EURO 2012 UKRAINE VS SWEDEN: VITA YA ZLATAN IBRAHIMOVIC NA SHEVCHENKO: NANI KUIBUKA MSHINDI?


VIKOSI VINAVOTARAJIWA KUANZA
Ukraine: Pyatov, Selin, Rakitskly, Kucher, Gusev, Tymoschchu, Konoplyanka, Voronin, Yarmolenko, Milevskly, Shevchenko.

Sweden: Isaksson, Olsson, Mellberg, Granqvist, Lustig, Kallstrom, Elm, Larsson, , Rosenborg, Ibrahimovic


MAMBO MUHIMU KUHUSU TIMU ZOTE MBILI
  • Ukraine inabidi wachague kati ya  Artem Milvskiy, Andrey Voronin, Marko Devic na veteran Andrey Shevchenko kuanza kwenye safu ya ushambuliaji, huku tishio lao kubwa likiwa linatokea kwenye winga.
  • Makinda Konoplyanka na Yarmolenko watakuwa na mzigo mkubwa wa kuleta ubunifu kwenye kiungo cha timu hiyo mbele ya mashabiki wao wa nyumbani, kwa hakika watakuwa kwenye presha kubwa ya kufanya vizuri huku wakiwa na umri wa miaka 22 tu.
  • Anatoliy Tymoshchuk ndio atakuwa kiungo mkabaji wa kuulinda ukuta wa timu yake, huku beki wa kulia akiongoza mashambulizi kutokea pembeni.


  • Ishara za mapema zinaonyesha kwamba Markus Rosenborg ataanza mbele ya dhidi ya Johan Elmander, huku tegemeo lao Zlatan Ibrahimovic akiongoza safu hiyo ya ushambuliaji.
  • Toivonen atarudi kwenye nafasi yake aliyoizoea ya bekiwa kushoto, huku Rasmus Elm akitegemewa kushirikiana na Kallstrom mbele ya veteran Anders Svensson.
  • Sweden wanaweza kukichezesha kikosi kile kile kilichoshinda kwenye mechi ya karibuni dhidi ya Serbia, huku Jonas Olsson akiwa nje na Granqvist akianza. 

TAKWIMU
Kumekuwepo na wastani wa zaidi 2.5 wa magoli kwenye mechi 9 za Sweden kwenye Euro.


Sweden wameshinda mechi zao 6 kati ya 7 za mwisho za Euro.


Sweden wamefunga angalau mabao 2 katika kila mechi zao 6 kati ya 7za Euro.




No comments:

Post a Comment