France: Lloris, Debuchy, Rami, Mexes, Evra, Diarra, Cabaye, Ribery, Malouda, Nasri, Benzema
England: Joe Hart, Johnson, Terry, Lescot, Ashley Cole, Milner, Parker, Steven Gerrard, Oxlade-Chamberlain, Ashley Young, Welbeck
MAMBO MUHIMU KUHUSU TIMI ZOTE MBILI
- France wanaingia kwenye mchezo wao huku wakiwa na crisis kwenye safu ya kiungo huku Yohan Cabaye ndio pekee aliye fiti kwa asilimia mia, huku M'Vila, Matuidi na Diarra wakiwa na shaka juu ya ufiti wao.
- Patrice Evra amekuwa akishutumiwa kwa kucheza chini ya kiwango lakini anaonekana ataanza mbele ya Gael Clichy, huku vita kubwa ya namba ya kiungo mshambuliaji ikiwa kati ya Menez, Malouda na Valbuena.
- Karim Benzema atapata nafasi ya kuanza, huku Olivier Giroud akiwa anasubiri kwenye benchi.
- Akifunga goli lake la kwanza la mechi ya kimataifa katika mchezo wa hivi karibuni dhidi ya Ubelgiji, kumemfanya Welbeck apate nafasi kubwa ya kuanza leo mbele ya Andy Carroll, ambaye nae kama Giroud, ni hatari sana kwa mipira ya juu.
- Ashley Young anategemewa kupewa free role nyuma ya mshambuliaji, huku James Milner na Alex Oxlade Chamberlain wakipewa nafasi ya kuanza mbelel ya Downing na Theo Walcott kwenye winga.
- Safu nyingine yenye upinzani mkubwa ni ulinzi wa kati, mtu wa kucheza sambamba na Terry, Hodgson kichwa kinamuuma ampe nafasi nani kati ya Lescott au Phil Jagielka.
- Wayne Rooney ndio anaanza adhabu yake ya kusimamishwa michezo miwili baada ya kutolewa nje kwa kadi nyekundu kwenye mchezo wa kufuzu dhidi Montenegro.
TAKWIMU
England wamefunga atleast magoli 2 katika mechi zao 12 kati ya 15 za Euro Cup.Kumekuwepo na wastani wa 2.5 wa mabao yaliyofungwa kwenye mechi 9 za mwisho za Euro za Ufaransa.
Ufaransa hawajafungwa kwenye mechi zao 9 za Euro Cup.
Ufaransa wameifunga England katika mechi zao 3 za mwisho kwenye mashindano yote.
England hawajafungwa kwenye mechi zao 8 za mwisho za Euro Cup.
Kiwango cha Molouda hakistahili timu ya taifa kwa sasa
ReplyDeleteKiwango cha Molouda hakistahili timu ya taifa kwa sasa
ReplyDeleteWaingereza na team yao mbovu na kocha mbovu mwisho wao ni makundi hawafiki popote
ReplyDelete