Siku chache baada ya mchezaji Shedrack Nsajigwa kumaliza mkataba wa kuichezea klabu ya Yanga huku akiripotiwa kuwepo nchini Kenya akifanya mazungumzo na klabu ya Gor Mahia, leo taarifa za uhakika kutoka kwenye kamati ya usajili ya Simba, zinasema viongozi wa mabingwa wa Tanzania wapo tayari kumsaini nahodha huyo wa zamani wa Yanga na Taifa Stars.
Simba ambao leo hii wamepata pigo baada ya beki wao wa upande wa kulia Said Nassoro Chollo kuripotiwa kupata majeraha makubwa kama yale yaliyompata Uhuru Seleman, wanamuona Nsajigwa kama mbadala halisi atakayefaa kuziba mapengo kwenye safu ya ulinzi ya timu hiyo.
Mtoa taarifa anasema, "Nsajigwa bado ni mchezaji mzuri sana, na uwezo mkubwa na kikubwa zaidi ni uzoefu alionao ambao ni hazina kubwa kwa klabu kama yetu ambayo sasa tunajaribu kuingiza vijana wadogo kama akina Singano, na ndio maana tumeamua kuanza harakati za kumsajili na kwa hakika tutafanikiwa."
Hizi habari kama ni za kweli itakuwa safi sana, mimi mwenyewe nilikuwa najiuliza sana hili jembe kwa nini Yanga wameliacha, Nsajigwa usikatae ofa hiyo karibu Msimbazi upige soka la uhakika.
ReplyDeleteI don't think if this guy is good enough to play for SIMBA, ameshachoka tunaitaji vijana wadogo kama Kapombe huyu Nsajigwa lazima anamiaka Zaidi ya Arobaini mwacheni akachezee Tanzania Stars hata kama hiyo timu siku hizi haipo.
ReplyDeleteSijui Kama kweli Simba watapata output wanayotegemea-----hii dhana ya kuchukua wachezaji waliochoka Yanga siyo sahihi hata kidogo na haitatusaidia---sisi tunajua Kamati ya usajiri Simba umefulia ndiyo maana unaona tunachukua makapi ya Yanga.
ReplyDeleteSimba wana mashindano mengi mwakani kwa hiyo mimi sioni kosa akisajiliwa na simba.uzoefu wake unahitajika kwa watu kama kina kapombe,singano na chipukizi wengine kujifunza kupitia yeye.
ReplyDeleteBinafsi nina muda mrefu sijamuona Nsajigwa akicheza kwa dk 90 ila nilimuona kwenye highlights alizoweka shaffih za mechi ya simba na yanga kidogo naamini si nsajigwa yule tuliyekuwa tunamjuwa na hilo linatokana na suala la umri ila Nsajigwa ni lulu katika timu ana mengi ya ku offer, mchezaji kama huyu unampa mkataba wa mwaka 1 anawapa uzoefu vijana wadogo. nshajigwa kwangu mimi ni moja ya mabeki bora kabisa kuwahi kutokea tanzania, hastahili kuachwa kama alivyoachwa ila vilabu vyetu hivi uhuni mwingi.
ReplyDeleteKwa hiyo hao simba kama wanataka kumsajili wamsajili wakijua kwamba wanamtumia kuwapa ujuzi vijana wao.
Nakumbuka kuna kipindi Fergie aliwahi kumsajili mchezaji mmoja hivi wa sweden aliyekuwa anacheza barca ila akawa amemaliza mkataba alikuwa na miaka 34 ama 35 hivi kila mtu akapinga lile wazo ila fundi ni fundi alipiga kamba za hatari na mwisho Fergie akataka kumpa offer ya kuendelea jamaa akagoma, jina limenitoka kwa hiyo aina hii ya wachezaji mimi nawafaninisha na nshajigwa.
Mdau
Mike
Simba itakuwa imefanya jambo la maana sana maana kwa mashindano makubwa wanaweza kumtumia Nsajigwa na kwenye ligi vijana wakacheza sababu Nsajigwa atacheza kwa mwaka mmoja tu baada ya hapo vijana watakuwa wamekomaa'
ReplyDelete