Search This Blog
Friday, June 15, 2012
Thursday, June 14, 2012
DIDIER DROGBA AMFUNIKA YAYA TOURE: ASHINDA TUZO YA UCHEZAJI BORA WA MWAKA WA IVORY COAST
Didier Drogba ametajwa kuwa mchezaji bora wa mwaka wa Ivory Coast, akimfunika mchezaji wa Manchester City Yaya Toure na mshambulaiji wa Aroune Kone kwenye kura zilizopigwa na waandishi wa nchi hiyo pamoja na watumiaji wa internet.
Mshambuliaji huyo aliye njiani kuondoka Chelsea alipata kura 110 kutoka kwa waandishi wa habari na kura 17, 863 kwa internet, na kwa ujumla akapata asilimia 37.69 za kura zote, huku mchezaji bora wa Africa Yaya Toure akimaliza kwa kupata asilimia 30.16%, huku mchezaji wa Sevilla akimalizia kwa kupata asilimia 12.29%.
Drogba anapata tuzo hii kwa mara ya pili, baada ya kushinda kwa mara ya kwanza mwaka 2007.
Nahodha huyo wa The Elephants aliisadia kucheza mpaka kwenye fainali ya AFCON 2012 nchini Gabon na Equatorial Guinea.
Ingawa alikosa peanti muhimu kwenye mechi ya fainali dhidi ya Zambia.
Drogab, 34, alitangaza uamuzi wa kutaka kuondoka Chelsea siku 3 baada ya kushinda kombe la mabingwa wa ulaya mwezi uliopita, baada ya kuisadia The Blues kwa kufunga bao la kusawazisha dhidi ya Bayern Munich kabla ya kufunga penati ya ushindi iliyoipa Chelsea ubingwa wa kwanza wa ulaya.
Mshambuliaji huyo aliye njiani kuondoka Chelsea alipata kura 110 kutoka kwa waandishi wa habari na kura 17, 863 kwa internet, na kwa ujumla akapata asilimia 37.69 za kura zote, huku mchezaji bora wa Africa Yaya Toure akimaliza kwa kupata asilimia 30.16%, huku mchezaji wa Sevilla akimalizia kwa kupata asilimia 12.29%.
Drogba anapata tuzo hii kwa mara ya pili, baada ya kushinda kwa mara ya kwanza mwaka 2007.
Nahodha huyo wa The Elephants aliisadia kucheza mpaka kwenye fainali ya AFCON 2012 nchini Gabon na Equatorial Guinea.
Ingawa alikosa peanti muhimu kwenye mechi ya fainali dhidi ya Zambia.
Drogab, 34, alitangaza uamuzi wa kutaka kuondoka Chelsea siku 3 baada ya kushinda kombe la mabingwa wa ulaya mwezi uliopita, baada ya kuisadia The Blues kwa kufunga bao la kusawazisha dhidi ya Bayern Munich kabla ya kufunga penati ya ushindi iliyoipa Chelsea ubingwa wa kwanza wa ulaya.
MIAKA 10 ILIYOPITA YA USHUJAA WA IKER CASILLAS ULIANZIA KWENYE MECHI DHID YA IRELAND - HISTORIA KUJIRUDIA USIKU HUU?
Iker Casillas sasa hivi anacheza kwenye michuano ya sita mikubwa ya kimataifa akiwa na Spain. Golikipa wa Real Madrid amekuwa akitajwa ni mmoja ya magolikipa bora duniani tangu alipocheza mechi yake ya kwanza ya kimataifa chini ya Jose Antonio Camacho mwaka 2002, na tangu wakati huo amekuwa hana mpizani kwenye milingoti mitatu ya Spain.
Na ilikuwa miaka 10 iliyopita, dhidi ya wapinzani wao watakaocheza nao leo usiku Ireland, siku ambayo Casillas aliweka jiwe la msingi la kujenga historia yake ndani Spain na kwenye soka kwa ujumla, aliokoa penati tatu kwenye raundi ya pili ya michuano ya kombe la dunia na kuipeleka Spain kwenye robo fainali.
Hivyo katika kuelekea mchezo wa leo usiku dhidi ya Ireland, ebu tuangalie historia ya kishujaa ya Iker Casillas ilivyojengwa kwa matukio makubwa.
Na ilikuwa miaka 10 iliyopita, dhidi ya wapinzani wao watakaocheza nao leo usiku Ireland, siku ambayo Casillas aliweka jiwe la msingi la kujenga historia yake ndani Spain na kwenye soka kwa ujumla, aliokoa penati tatu kwenye raundi ya pili ya michuano ya kombe la dunia na kuipeleka Spain kwenye robo fainali.
Hivyo katika kuelekea mchezo wa leo usiku dhidi ya Ireland, ebu tuangalie historia ya kishujaa ya Iker Casillas ilivyojengwa kwa matukio makubwa.
| 2002 WORLD CUP: SPAIN 1-1 IRELAND: THE PENALTY LEGEND BEGINS |
Michuano ya World Cup ya Japan na Korea ndio yalikuwa jiwe la kwanza la msingi wa ushujaa wa Casillas kwenye timu ya taifa. Kipa wa Madrid, alikuwa chaguo la pili nyuma ya Santiago Canizares, Iker alipata nafasi ya kucheza baada ya golikipa Santiago kuumia. Casillas, ambaye mwezi mmoja kabla alicheza kwa mafanikio na kuisadia Madrid kushinda kombe la ulaya dhidi ya Bayern Leverkusen baada ya kumbadili majeruhi na Cesar Sanchez katika hatua za mwisho, ambaye pia Casillas alimbadili kwenye kikosi cha Spain baada ya kuumia.
Kwenye hatua ya 16, Spain wakakutana na Ireland na pamoja na kuongoza kwa goli la mapema la Fernando Morientes, lakini mechi hiyo ilikuwa ngumu sana. Casillas aliiokoa Spain kwenye kipindi cha pili baada ya kuokoa penati ya Ian Harte, lakini hakuweza kumzuia Robbie Keane kusawazisha na kupelekea mechi kwenda mpaka kwenye mikwaju ya penati.
Na Casillas alikuwa shujaa tena, akiokoa penati za David Connolly na Kevin Kilbane na kuipeleka Spain hatua ya mbele.
| EURO 2008: SPAIN 0-0 ITALY: REWRITING HISTORY |
Miaka 6 baadae, Casillas akaisadia Le Roja kuandika historia nyingine kwenye Euro 2008, akiwa nahodha kwa upande Spain kwenye michuano hiyo, wakafanikiwa kupata mafanikio kwa mara ya kwanza tangu mwaka 1964. Na golikipa wa Real Madrid alicheza vizuri sana, akiokoa penati ya Di Natale na Daniele De Rossi kwenye mikwaju ya penati kufuatia dakika 120 kushindwa kutoa mshindi kwenye mchezo wa robo fainali dhidi ya Italia.
| 2010 WORLD CUP: SPAIN 1-0 PARAGUAY: TAKING REINA'S ADVICE |
Wakiwa njiani kwenda kubeba kombe la dunia mwaka 2010 nchini South Africa, Spain wakakutana na Paraguay kwenye robo fainali. Kikosi cha Paraguay kikiongozwa na Gerardo Martino walijipanga vizuri hasa kwenye nafasi ya kiungo na kuwafanya wachezaji wa Vicente Del Bosque kushindwa kucheza vizuri. Gerard Pique akacheza rafu kwenye box na kusababisha penati kwenye kipindi cha pili na kusababisha safari ya La Roja kwenda nusu fainali kutia mashaka.
Pepe Reina alijua kabisa wapi Oscar Cordozo angepiga mpira wa penati kick, baada ya kuwa tayari alikuwa ameshakutana na mparaguay huyo kwenye mechi kati ya Liverpool na Benfica na Cordozo kumfunga kwa penati, Reina akampa ushauri Casillas jinsi amjuavyo Cordozo na penati zake, kwa bahati nzuri Iker akafuata ushauri wa kipa mwenzake na kufanikiwa kuudaka mpira wa Cordozo na kuisadia timu ya kufika hatua iliyofuatia.
| 2010 WORLD CUP: SPAIN 1-0 NETHERLANDS: CASILLAS TWO; ROBBEN NIL |
Katika dakika ya 61 ya mchezo wa fainali ya kombe la dunia, Arjen Robben aliiichambua kama karanga safu ya ulinzi ya Spain na kisha akaingia mpaka kwenye eneo la penati na kukutana uso kwa uso na Casillas, ambaye alizuia mpira uliokuwa ukitinga nyavuni kwa mguu.
Na kwenye dakika ya 90 ya mchezo, wawili hao wakajikuta wakikutana tena ana kwa ana. Matokeo yake yalikuwa yale yale: Robben akanyimwa bao tena na Casillas na mpira ukaenda kwenye muda wa nyongeza kwa dakika 30, ambapo Andres Iniesta aliibuka shujaa kwa kufunga bao pekee na la ushindi kwa Spain.
Lakini tungekuwa tunaongea mengine bila kuwepo kwa shujaa Casillas.
Bakari Malima ‘Jembe Ulaya’-Episode 7
*Apata balaa jingine, Wasauz wamkatia rufaa
*Yanga yapita, azuiwa kucheza nane bora Afrika
Na Saleh Ally
WIKI ILIYOPITA, tuliishia wachezaji wa Yanga akiwamo Bakari Malima wakiwa wameomba mechi yao ya marudiano dhidi ya Rayon Sports ya Rwanda ichezwe mjini MWanza kwa lengo la kukimbia presha kubwa ya mashabiki jijini Dar es Salaam. Uongozi ukakubali na maandalizi yakaanza. Endelea.
TULIENDELEA na maandalizi siku kadhaa tukiwa jijini Dar es Salaam, baada ya hapo tukafunga safari kwenda Mwanza kwa ajili ya kuweka kambi huku tukiisubiri mechi dhidi ya Rayon Sports.
Wachezaji tulijua ugumu wa Wanyarwanda lakini tulipania kushinda na kuweka rekodi ya kuifikisha Yanga kwenye hatua ya Nane Bora ya Ligi ya Mabingwa Afrika. Mashabiki wengi wa soka walifunga safari kutoka Dar es Salaam kuja Mwanza kutuunga mkono.
Siku ya mechi, kama ambavyo tulitarajia, ilikuwa ni ngumu na wapinzani wetu walionekana walikuwa wamejiandaa vilivyo kushinda ugenini na kusonga mbele. Walijitahidi wakapata bao lakini nasi tulifunga bao zuri lililopachikwa kimiani na mshambuliaji wetu, Mohammed Hussein ‘Mmachinga’.
Mechi iliisha kwa sare ya bao 1-1, maana yake Yanga tulikuwa tumefanikiwa kuvuka hadi hatua ya Nane Bora ya Ligi ya Mabingwa Afrika, wakati huo tulikuwa tunasema Klabu Bingwa Afrika. Sherehe zilianzia pale CCM Kirumba hadi sehemu mbalimbali za mji wa Mwanza.
Sherehe hizo zilikuwa ni za aina yake, kwani ziliendelea jijini Dar es Salaam na sehemu nyingine nchini. Tulikuwa tumeweka rekodi mpya kwa Yanga. Binafsi nilijisikia vizuri kwa kuwa nilikuwa nimetimiza malengo ya kuilipa Yanga mazuri kwa kuwa viongozi walionyesha mapenzi kwangu.
Hakukuwa na muda wa kupoteza, tulianza mara moja maandalizi kwa ajili ya michuano hiyo pamoja na mingine iliyokuwa inakabiri Yanga. Kwangu, angalau niliona kama maisha yalianza kwenda vizuri tena, nilianza kuishi kawaida.
Ingawa suala la mahakamani hukumu ilishatolewa na nikaonekana sina hatia, bado wako ambao waliamini kama haikuwa sawa. Hali hiyo iliniumiza sana, kwani kila aliyejaribu kukumbushia alitonesha jeraha nililopata kwa kupata matatizo kwa kitu nisichokijua hata kidogo. Bado niliendelea kumuachia Mungu.
Niliendelea na maisha yangu ya kawaida, mara kadhaa nilikuwa nikiwasiliana na uongozi wa Vaal Professional kuhusiana na suala la kurejea Afrika Kusini. Niliona ningeweza kufanya hivyo kwa kuwa pamoja na kupata matatizo walionyesha ustaarabu kwangu.
Lakini niliona ni vizuri kama ningemaliza jukumu la kupambana kwa ajili ya Yanga kwenye michuano hiyo mikubwa ya Afrika. Maana tayari ratiba ilishatoka na tulipangiwa kuanza mechi dhidi ya Maning Rangars ya Afrika Kusini.
Nilijua ingekuwa ni mechi ngumu kwa kuwa Wasauz wana kila kitu, hivyo lazima wangejiandaa vya kutosha kwa ajili ya mechi hiyo. Lakini binafsi nilikuwa nikifanya mazoezi kuhakikisha nakuwa fiti sawasawa.
Balaa likaibuka tena, Maning Rangers kwa kuwa walikuwa wananijua wakanikatia rufaa kwamba sitakiwi kucheza michuano hiyo kwa kuwa mkataba wangu wa miaka mitatu na Vaal ulikuwa haujamalizika. Nilichanganyikiwa, lakini nikawa na matumaini huenda Shirikisho la Soka Afrika (Caf), litapuuzia.
Ingawa niliingia hofu ya kutoichezea Yanga, lakini niliamua kuweka pamba masikioni na kuendelea na mazoezi kwa nguvu kama vile nilikuwa na uhakika ningeichezea Yanga kwenye michuano hiyo hatua ya nane bora.
Siku chache kabla ya kuivaa Maning Rangers, Yanga ilipokea barua kutoka Chama cha Soka Tanzania (Fat), ilikuwa inatokea Caf. Barua hiyo ilitoa maelekezo kwamba nisingeruhusiwa kucheza, si mechi dhidi ya Wasauz pekee, badala yake zote.
Kwangu ilikuwa ni kama kisu moyoni, niliona maisha yangu yalikuwa yamejaa misukosuko. Ilikuwa kama wamenikumbusha upya matatizo yaliyonipata wakati ninatokea Sauz. Niliamua kwa mara nyingine kumuachia Mwenyezi Mungu.
Nikakaa kando na kuwa mtazamaji, bahati mbaya Yanga haikufanya vizuri katika michuano hiyo, ilitolewa mapema sana. Nilisikia uchungu kwa kuwa niliona huenda kuwepo kwangu kungekuwa msaada kwa kushirikiana na wenzangu na tungeweza kuikoa Yanga. Kukosekana kwangu ni kama kulipunguza nguvu, sikuwa na namna.
Baada ya hapo, niliichezea Yanga kwenye ligi na tulifanikiwa kuwa wawakilishi wa Tanzania katika michuano ya Afrika Mashariki na Kati iliyofanyika nchini Uganda. Nakumbuka sana, hiyo ni mwaka 1999, safari yetu ilikuwa ni ya kubangaiza.
Tulisafiri kwenda Uganda kwa usafiri wa kuungaunga. Nakukumbusha sisi ndiyo tulitwaa ubingwa kwenye michuano hiyo, lakini safari yetu kwenda ilikuwa ni ngumu kupindukia na hakukuwa na posho, lakini wachezaji tukawa tayari kupambana.
Tulisafikirishwa kwa mafungu mawili kwa basi. Awali uongozi ulitaka kuitoa timu lakini sisi tukasema tutacheza. Tuliondoka tukiwa na pea moja tu ya jezi, maandalizi yetu yalikuwa mabovu kuliko timu yoyote iliyoshiriki michuano hiyo.
MALIMA anaongozana na Yanga kwenda Uganda, maandalizi ni mabovu, timu haina fedha lakini mwaka huo wa 1999, Yanga walikuwa mabingwa. Je, ilikuwaje hadi wakafanikiwa huku maisha yao yalikuwa ya kuungaunga? USIKOSE EPISODE-8
VITA NYINGINE YA MAFUNDI WA SOKA: MODRIC NA PIRLO NA KUIONGOZA VIZURI TIMU YAKE LEO?
VIKOSI VINAVYOTARAJIWA KUANZA
Italy: Buffon, Chiellini, Rossi, Bonucci, Maggio, Motta, Pirlo, Marchisio, Giaccherini, Balotelli, Cassano.- Antonio Di Natale anategemewa kuanza usiku wa leo lakini anaonekana kuwa na hatari zaidi kama akiingia kutokea benchi, hivyo Mario Balotelli anaweza kupata nafasi ya kuanza tena akiwa na Cassano.
- Pengine, Nocerino na Balzaretti wanaweza kuanza kwenye safu ya kiungo ya watu wa tano, huku Giaccherini na Motta wanategemewa kuendelea na nafasi zao walizocheza dhidi ya Spain.
- Prandelli itabidi aanzishe ukuta ule ule ulioanza dhidi ya Italia, huku De Rossi akiwa katikati ya Chiellini na Bonucci kwa mara nyingine tena.
- Slaven Bilic hana wasiwasi wa majeruhi kuelekea kwenye dhidi ya Italia na itabidi aanze na kikosi kile kile kilichocheza vizuri dhidi ya Ireland.
- Perisic alichaguliwa kuanza dhidi ya Kranjcar na kucheza vizuri sana kwenye upande wa kushoto, huku Rakitic akicheza upande wa pili.
- Kwenye ulinzi, beki mwenye asili ya Ujerumani Gordon Schildenfeld alichaguliwa kuanza mbele ya veteran Josip Simunic kusaidiana na Corluka, huku nahodha Srna akiecheza kwa kuelekea mbele kutokea shavu la kulia.
BREAKING NEWS: MWENYEKITI WA VILLA SQUAD AJIUZULU UONGOZI WA KLABU HIYO
| Uongozi wa klabu ya Villa na wachezaji. |
Uledi ambaye aliingia madarakani mwaka jana baada ya kufanyika uchaguzi wa viongozi wa klabu hiyo amejiuzulu kwa kwasababu za kuwajibika. Akiongea na www.shaffihdauda.com Uledi alisema: "Wakati naingia madarakani dhamira yangu kubwa ilikuwa ni kuiwezesha Villa kubaki ligi kuu, lakini nimeshindwa kufanya hivyo, kwa maana hiyo kazi imenishinda. Kwa hiyo ni vizuri kujiuzulu ili kuwajibika, nafikiri sasa kazi hii nimuachie mtu mwingine ili aweze kuliongoza jahazi la Villa na kulirudisha kwenye sehemu nzuri."
Klabu hiyo ya Villa sasa imebakia ikiwa haina uongozi zaidi ya kamati ya utendaji chini Binslum, Ally Kindoile, Mohamed Kimbegele, Hassan Sharif na Moris Simon.
EXCLUSIVE: ORLANDO PIRATES WATUMA RASMI BARUA YA KUMTAKA EMMANUEL OKWI
Hatimaye klabu ya Orlando Pirates imetuma rasmi barua ya mualiko kwa mchezaji wa Simba Emmanuel Okwi kwenda nchini South Africa kwa ajili ya kufanya majaribio ya kuweza kujiunga na timu hiyo.
![]() |
| Hii ni sehemu ya barua ya Orlando kumualika Okwi. |
Nimefanikiwa kuiona barua hiyo ikiwa inatoa maelekezo kwamba Okwi atapewa majaribio ya wiki mbili na Orlando Pirates, huku akihudumiwa kuanzia usafiri, malazi, matibabu pamoja na gharama nyingine zitakazojitokeza kwa wakati atakaokuwa na klabu hiyo.
Kwa kipindi cha misimu miwili sasa Orlando wamekuwa wakimfuatilia Okwi ambaye klabu yake ya Simba imemuwekea price tag ya Billioni 2 kwa timu inayomtaka, huku pia wapinzani wao wa jadi klabu ya Yanga ikiwa inamfukuzia mshambuliaji huyo wa Uganda ambaye siku za hivi karibuni amekuwa ndio tegemeo la safu ya ushambuliaji ya mabingwa wa Tanzania.
KIMENUKA TOTTENHAM: HARRY REDKNAPP ATIMULIWA KAZI - DAVID MOYES NJIANI KUMRITHI
Usiku wa leo umekuwa mmbaya kwa kocha Harry Redknapp baada ya kutimuliwa kazi na Tottenhma Hostpur.
Harry mwenye miaka 65 jana alisisitiza kwamba ataendelea kuwepo White Hart Lane, lakini jioni hii alifanya mazungumzo na mwenyekiti wa Spurs Daniel Levy na hatimaye akatimuliwa.
Kocha huyo wa zamani wa West Ham alifanya mazungumzo na bosi wake Levy ili kuweza kujua hatma yake baada ya mkataba wake kuwa umebakiza miezi 12 uishe, huku akiwa na akiwa anajiamini amefanya kazi nzuri ambayo ingempa nafasi ya kuongezewa mkataba.
Lakini Levy inasemekana hakuwa na furaha na suala la Redknapp kushindwa kuiwezesha timu kupata nafasi ya champions league pamoja na kukaa kwenye nafasi ya tatu kwa muda mrefu kwenye msimamo wa ligi ya msimu uliopita.
Spurs walimaliza nafasi ya nne katika EPL, kwa maana waliweza kupata nafasi nafasi lakini wakaikosa nafasi hiyo baada ya Chelsea waliokuwa nyuma yao kubeba ubingwa wa ulaya jijini Munich dhidi Bayern.
Mpaka sasa Redknapp bado anafanya mazungumzo ya juu ya mapato yake atakayoyapata baada ya Spurs kumtimua akiwa bado na mkataba wa mwaka 1, na anatagemewa kutangazwa rasmi kutimuliwa hapo kesho.
David Moyes wa Everton anatajwa kuwa ndio kocha anayeweza kumrithi Harry Redkanpp pale White Hart Lane.
Harry mwenye miaka 65 jana alisisitiza kwamba ataendelea kuwepo White Hart Lane, lakini jioni hii alifanya mazungumzo na mwenyekiti wa Spurs Daniel Levy na hatimaye akatimuliwa.
Kocha huyo wa zamani wa West Ham alifanya mazungumzo na bosi wake Levy ili kuweza kujua hatma yake baada ya mkataba wake kuwa umebakiza miezi 12 uishe, huku akiwa na akiwa anajiamini amefanya kazi nzuri ambayo ingempa nafasi ya kuongezewa mkataba.
Lakini Levy inasemekana hakuwa na furaha na suala la Redknapp kushindwa kuiwezesha timu kupata nafasi ya champions league pamoja na kukaa kwenye nafasi ya tatu kwa muda mrefu kwenye msimamo wa ligi ya msimu uliopita.
Spurs walimaliza nafasi ya nne katika EPL, kwa maana waliweza kupata nafasi nafasi lakini wakaikosa nafasi hiyo baada ya Chelsea waliokuwa nyuma yao kubeba ubingwa wa ulaya jijini Munich dhidi Bayern.
Mpaka sasa Redknapp bado anafanya mazungumzo ya juu ya mapato yake atakayoyapata baada ya Spurs kumtimua akiwa bado na mkataba wa mwaka 1, na anatagemewa kutangazwa rasmi kutimuliwa hapo kesho.
David Moyes wa Everton anatajwa kuwa ndio kocha anayeweza kumrithi Harry Redkanpp pale White Hart Lane.
OFFICIAL: DI MATTEO APEWA MIAKA MIWILI KUIONGOZA CHELSEA
Roberto Di Matteo leo amethibitishwa kuwa kocha mpya wa kudumu wa Chelsea kwa mkataba wa miaka miwili.
Muitaliano huyo alirudi Stamford Bridge leo akitokea kwenye mapumziko na kukamilisha dili hilo na mabingwa wa ulaya.
Di Matteo alisema: "Nina furaha kuweza kuchaguliwa kuwa manager mpya. Tulipata mafanikio makubwa msimu uliopita ambayo yalijenga historia kwenye klabu.
"Lengo letu ni kuendelea kutokea hapo tulipofika na tayari nimeanza kupanga maandalizi ya msimu ujao."
Di Matteo, 42, alitajwa kama kocha wa muda wa Chelsea baada ya Andre Villas Boas kufukuzwa kazi mwezi wa 3.
Akafanikiwa kuiongoza The Blues kushinda kombe la FA na champions league ndani ya kipindi cha wiki 11.
Muitaliano huyo alirudi Stamford Bridge leo akitokea kwenye mapumziko na kukamilisha dili hilo na mabingwa wa ulaya.
Di Matteo alisema: "Nina furaha kuweza kuchaguliwa kuwa manager mpya. Tulipata mafanikio makubwa msimu uliopita ambayo yalijenga historia kwenye klabu.
"Lengo letu ni kuendelea kutokea hapo tulipofika na tayari nimeanza kupanga maandalizi ya msimu ujao."
Di Matteo, 42, alitajwa kama kocha wa muda wa Chelsea baada ya Andre Villas Boas kufukuzwa kazi mwezi wa 3.
Akafanikiwa kuiongoza The Blues kushinda kombe la FA na champions league ndani ya kipindi cha wiki 11.
Wednesday, June 13, 2012
wadhamini wazidi kujitokeza shindano la Miss Dar Inter College 2012
baadhi ya warembo watakaoshiriki shindano la Miss Dar Inter College 2012 wakimsikiliza mwalimu wao Marlydia Boniface wakati wa mazoezi yao juzi kwenye hoteli ya Grand Villa.
Na Mwandishi Wetu
WAKATI shindano la kumsaka Miss Dar Inter College 2012 likitarajiwa kufanyika Juni 22 kwenye ukumbi wa Makumbusho ya Taifa , uliopo mkabala na chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM) duka la vipodozi la Shear Illusions,pamoja na mbunifu maarufu wa mavazi,Mustafa Hassanali wamejitosa kudhamini shindano hilo .Awali shindano hilo lilipangwa kufanyika juni 8 kabla ya kusogezwa mbele kutokana na sababu mbalimbali ikiwemo baadhi ya warembo kuwa katika mitihani pamoja na mafunzo yao kwa vitendo ‘Field’.Akizungumza jijini Dar es Salaam jana, mratibu wa Shindano hilo Dina Ismail alisema jana kwamba Shear lenye matawi yake jengo la Millennium Tower na Mlimani City linajihusha na uuzaji wa vipodozi halisi ‘original’ kutoka nje ya nchi litatoa vipodozi kwa warembo watakaoshiriki,huku Hassanali atatoa zawadi ya magauni ya warembo.
Alisema maandalizi kwa ajili ya shindano hilo yanaendelea ambapo juzi warembo hao ambao awali walikuwa wakifanya mazoezi kwenye hoteli ya Lamada, walihamishia kambi yao kwenye hoteli ya Grand Villa iliyopo Kijitonyama jijini Dar es Salaam.Dina aliongeza kuwa mpaka sasa wameshapatikana warembo 13 ambao wapo chini ya ukufunzi wa Marlidya Boniface, huku kwa upande wa shoo wakinolewa na dansa aliyepata kufanya vema miaka ya nyuma, Bob Rich.“Mwaka huu tumejipanga vema kuhakikisha mmoja ya warembo kutoka Miss Dar Intercollege anafanya vema katika fainali za Miss Tanzania ,”alisema Dina.Warembo watakaoshiriki shindano hilo wanatoka vyuo vya Biashara (CBE), Uandishi wa Habari (DSJ) na Time, Ustawi wa Jamii, Usimamizi wa Fedha (IFM) na Chuo Kikuu huria (OUT ambapo taji linashikiliwa na Rose Msuya kutoka IFM, huku mshindi wa pili wa mwaka jana, Blessing Ngowi alitinga fainali za Miss Tanzania.Dina aliwataja warembo hao kuwa ni pamoja na Veronica Ngota, Rose Muchunguzi, Nancy Maganga, Hilda Edward, Diana Nyakisinda, Neema Michael, Veronica Yollla, Jacquiline Cliff, Sharifa Ibrahim, Natasha Deo, Saada Suleiman, Rose Masanja na Jamila Hassan.Shindano hilo limedhaminiwa na kampuni ya Bia Tanzania (TBL) kupitia bia ya Redd’s,Dodoma Wine, Ndege Insurance, Skylight Band,Lamada Hotel, Screen Masters,Makumbusho ya Taifa, Mustafa Hassanali, Lamada Hotel,Grand Villa Hotel, Clouds Fm na blog za Michuzi, Mamapipiro, Bin Zubeiry,Mtaa kwa Mtaa na Fullshangwe
Na Mwandishi Wetu
WAKATI shindano la kumsaka Miss Dar Inter College 2012 likitarajiwa kufanyika Juni 22 kwenye ukumbi wa Makumbusho ya Taifa , uliopo mkabala na chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM) duka la vipodozi la Shear Illusions,pamoja na mbunifu maarufu wa mavazi,Mustafa Hassanali wamejitosa kudhamini shindano hilo .Awali shindano hilo lilipangwa kufanyika juni 8 kabla ya kusogezwa mbele kutokana na sababu mbalimbali ikiwemo baadhi ya warembo kuwa katika mitihani pamoja na mafunzo yao kwa vitendo ‘Field’.Akizungumza jijini Dar es Salaam jana, mratibu wa Shindano hilo Dina Ismail alisema jana kwamba Shear lenye matawi yake jengo la Millennium Tower na Mlimani City linajihusha na uuzaji wa vipodozi halisi ‘original’ kutoka nje ya nchi litatoa vipodozi kwa warembo watakaoshiriki,huku Hassanali atatoa zawadi ya magauni ya warembo.
Alisema maandalizi kwa ajili ya shindano hilo yanaendelea ambapo juzi warembo hao ambao awali walikuwa wakifanya mazoezi kwenye hoteli ya Lamada, walihamishia kambi yao kwenye hoteli ya Grand Villa iliyopo Kijitonyama jijini Dar es Salaam.Dina aliongeza kuwa mpaka sasa wameshapatikana warembo 13 ambao wapo chini ya ukufunzi wa Marlidya Boniface, huku kwa upande wa shoo wakinolewa na dansa aliyepata kufanya vema miaka ya nyuma, Bob Rich.“Mwaka huu tumejipanga vema kuhakikisha mmoja ya warembo kutoka Miss Dar Intercollege anafanya vema katika fainali za Miss Tanzania ,”alisema Dina.Warembo watakaoshiriki shindano hilo wanatoka vyuo vya Biashara (CBE), Uandishi wa Habari (DSJ) na Time, Ustawi wa Jamii, Usimamizi wa Fedha (IFM) na Chuo Kikuu huria (OUT ambapo taji linashikiliwa na Rose Msuya kutoka IFM, huku mshindi wa pili wa mwaka jana, Blessing Ngowi alitinga fainali za Miss Tanzania.Dina aliwataja warembo hao kuwa ni pamoja na Veronica Ngota, Rose Muchunguzi, Nancy Maganga, Hilda Edward, Diana Nyakisinda, Neema Michael, Veronica Yollla, Jacquiline Cliff, Sharifa Ibrahim, Natasha Deo, Saada Suleiman, Rose Masanja na Jamila Hassan.Shindano hilo limedhaminiwa na kampuni ya Bia Tanzania (TBL) kupitia bia ya Redd’s,Dodoma Wine, Ndege Insurance, Skylight Band,Lamada Hotel, Screen Masters,Makumbusho ya Taifa, Mustafa Hassanali, Lamada Hotel,Grand Villa Hotel, Clouds Fm na blog za Michuzi, Mamapipiro, Bin Zubeiry,Mtaa kwa Mtaa na Fullshangwe
EXCLUSIVE: MATOLA NJIANI KUWA KOCHA MPYA WA AFRICAN LYON
![]() |
| Rahim Zamunda akiwa na mmiliki wa klabu ya Portsmouth Suleiman Al-Fahim |
Kwa mujibu wa mmiliki wa klabu hiyo Rahim Zamunda amesema kwamba wamefikia uamuzi huo ili kuweza kuisuka upya vizuri timu yao itakayoweza kupambana vizuri na mashindano yajayo.
"Huu ni uamuzi tuliofikia ili kuweza kuleta mabadiliko chanya kwenye timu yetu, na kwa sasa tupo kwenye mazungumzo ya mchezaji wa zamani wa Simba, Selemen Matola ili aweze kuwa bosi wa benchi letu la ufundi. Mpaka sasa tumefikia pazuri na lolote linaweza kutokea,"
EURO 2012: UJERUMANI VS UHOLANZI - WAPINZANI WA JADI WA KIHISTORIA NANI KUCHEKA LEO.
Wakati
timu ya taifa ya Ujerumani au the Die Menschaff ikiwa imetulia kambini
ikisubiri jukumu lililoko mbele ambalo kuwakabili wapinzani wao wa miaka
mingi Uholanza, wapinzani wao hao wamekuwa wakipambana wenyewe kwa
wenyewe kama walivyozoea .
Vichwa
vya habari vya magazeti ya michezo nchini Uholanzi kuelekea kwenye
mchezo huu vimepambwa na kauli mbaya za Rafael Van Der Vart ambaye
amekuwa mwepesi kusema yaliyo moyoni mwake dhidi ya kocha Bert Van
Marwick, Klaas Jan Huntelaar naye hajabaki nyuma huku wengine kina Nigel
De Jong na Wesley Sneijder wakihusika kwenye utata uliokizunguka kikosi
cha Oranje .
Upande
wa pili wajerumani wameshikama wote wakitambua mtihani ulioko mbele na
wamekuwa wakiifikiria timu kwanza kabla ya kufikiria jinsi ambavyo
baadhi wamekuwa wakiwekwa benchi na wengine wakicheza.
Hii ndio tofauti ya kwanza ambayo inaweza kuamua mchezo huu wa watani hawa wa jadi kwa miaka mingi.
Kila
mmoja akiingia uwanjani na ajenda yake tofauti lakini wote wawili wana
agenda ya kufanya vizuri na kuchukua pointi zote tatu huku Uholanzi
wakionekana kuzihitaji pointi hizo pengine kuliko Ujerumani .
Ukiingia
kwenye idara ya ufundi kujaribu kupata ufumbuzi wa kipigo walichopata
Uholanzi toka kwa Denmark utagundua yafautayo, kimsingi kabisa Uholanzi
hawakupaswa kupanga mfumo ambao uliwajumuisha viungo wakabaji wawili
ambao ni De Jong na Van Bommel. Mfumo huu uliwafanya Uholanzi kukosa
ubunifu wa ziada kwenye idara ya ushambuliaji. Tatizo lingine ambalo
limeonekana ni kutomjumuisha Klaas Jan Huntelaar . Robin Van Persie
alipangwa kwenye sehemu ya ushambuliaji wa kati, hakuna anayeweza
kusema kuwa Van Persie si mchezaji mzuri, la hasha lakini kwenye mfumo
wa uholanzi sio mara nyingi amekuwa akipangwa kama mtu ambaye anaongoza
mstari kwenye ushambuliaji na hapa ndio unagundua tatizo. Ibrahim
Affelay hajacheza sehemu kubwa ya msimu huu na kwenye nafasi yake
angeweza kupangwa Van Persie halafu Affelay akasubiri
kuleta impact kama Supersub huku Huntelaar akicheza kama mshambuliaji
wa kati .
Mchezo
dhidi ya Ujerumani hauna budi kushudia mabadiliko haya endapo Uholanzi
watataka kuweka hai matumaini yake ya kusonga mbele.
Ujerumani
kwa upande wao sio kwamba walicheza vizuri kwa kustahili alama za
asilimia mia moja kwenye mchezo wao wa kwanza dhidi ya Ureno, kulikuwa
na matatizo sehemu kadhaa, Lukas Podolski alikuwa na matatizo hasa
kwenye jinsi ya kuipenya ngome ya Ureno na kwenye umaliziaji pia kama
ilivyokuwa kwa Thomas Mueller. Kilichowapa ufanisi mkubwa wajerumani ni
juhudi za wachezaji hawa hasa pale ambapo mambo yalionekana kuwaelekea
kombo , walifanya kazi kwa juhudi kubwa na matokeo yake yalikuwa ushindi
wa bao moja dhdi ya timu nzuri na ngumu ya Ureno.
Ujerumani
wanaweza kufanya mabadiliko endapo watataka kumaliza mchezo mapema,
kuna wachezaji kama Andre Schurrie na Marco Reus ambao wanaweza kuingia
kwenye nafasi za kina Podolski na Mueller japo hakuna ulazima wa haraka
wa kushuhudia mabadiliko haya .
Tatizo
kubwa la Uholanzi siku ya jumamosi lilikuwa umaliziaji . Takwimu
zinaonyesha kuwa Uholanzi kwenye mechi dhidi ya Denmark walipiga mashuti
22 ambayo hayakulenga lango. Hii ndio idadi kubwa ya mashuti
yaliyopotea mwelekeo kuliko timu yoyote ya taifa au klabu yoyote ile
kwenye ligi zote kubwa barani ulaya. Na hapa ndio
panaweza kuhitaji mabadiliko. Pamoja na kwenye ushambuliaji mabadiliko
mengine yanaweza kuonekana kwenye safu ya Ulinzi ambako Joris Mathijsen
amepona na huenda akaingia kwenye nafasi ya Ron Vlaar, hata hivyo
mabadiliko ambayo Kocha Van Marwick anapaswa kufikiria kuyafanya ni yale
ya kupunguza kiungo mkabaji mmoja na kuongeza kiungo mbunifu kama
Rafael Van Der Vart hasa ukizingatia mchezo wa kwanza wa Ujerumani
ambapo wajerumani walikuwa
wanapitika kiwepesi jambo ambalo linaweza kumpa Bert mawazo kwamba
staili ya mchezo ya wajerumani ya kutegemea sana mashambulizi ya counter
itakuwa nzuri akiwa na kiungo wa ziada kama Van Der Vart.
Mchezo
kati ya Uholanzi na Ujerumani kihistoria ni mchezo ambao utazifanya
timu zote ziwe na morali ya ziada kumkabili mpinzani wake. Mara nyingi
Ujerumani wamekuwa wakiwanyanyasa wadachi , mazingira ya michezo ya
kwanza ya timu hizi yanawafanya wadachi kuwa na sababu ya ziada ya
kushinda kwani kitu chochote pungufu ya pointi tatu kitamaanisha kuwa
Uholanzi itakuwa ianchungulia kaburi.
EURO 2012: URENO KUACHA UTEJA KWA DENMARK LEO?
VIKOSI VITAKAVYOANZA LEO
Denmark: Lindergaard, Poulsen, Agger, Kjaer, Jacobsen, Zimling, Kvist, Kron-Dehli, Eriksen, Rommedahl, BendtnerUreno: Patricio, Pereira, Pepe, Alves, Coentrao, Moutinho, Veloso, Meireles, Nani, Postiga, Ronaldo
MAMBO MUHIMU KUHUSU TIMU
- Wakiwa hawana majeruhi mapya, Denmark wanategemewa kutaja kikosi kile kile kilichoshtua watu kwa kuifunga Uholanzi bao 1-0.
- Kwa maana hiyo kipa Stephen Andersen anaweza akaanza mbele ya Lindergaard huku pia Jacobsen na Zimling wakitarajiwa kuanza mbele ya Wass na Poulsen.
- Lasse Schone atakuwa na matumaini ya kuanza mbele ya Rommedahl katika winga sambamba na Kronh-Dehli.
- Ureno nayo haitegemewi kubadili kikosi kilichofungwa na Ujerumani, Paulo Bento hana option kubwa zaidi ya kukianzisha kile kile.
- Nani alicheza dakika zote 90 japokuwa alionekana kuchoka mwishoni mwa mechi, anategemewa atakuwa fiti na kuanza leo dhidi ya Wadenmark na kucheza kwa dakika zote 90 kutegemeana na kiwango chake.
- Nelson Oliveira atakuwa akitaka kuanza mbele ya Postiga ambaye ameonekana butu kwa safu ya ushambuliaji, huku Almeida akisubiri kwenye benchi.
TENGA: WACHEZAJI WOTE WA STARS KUKATIWA BIMA
Bosi wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Leodegar Tenga, amewapongeza wachezaji wa Taifa Stars kwa kiwango walichoonyesha kwenye mchezo dhidi ya Gambia, lakini akasema wachezaji wote wa timu hiyo watakatiwa bima ya afya.
Tenga, akizungumza na waandishi wa habari jana jijini Dar es Salaam, alisema wachezaji hao walionyesha kiwango cha kuridhisha kwenye mchezo huo, lakini akatupa sifa zake zote kwa kocha Kim Poulsen.
“Nimefurahishwa sana na kiwango kilichoonyeshwa na wachezaji wa Stars kwenye mchezo dhidi ya Gambia, hakika kocha amefanya kazi nzuri sana kwa kipindi kifupi alichokaa na timu.
“Wachezaji kama John Bocco na Abubakar Salum walionyesha kiwango kizuri sana, nafikiri timu hii inahitaji sapoti yetu, lakini tumekaa na kukubaliana kuwa wachezaji wote wa timu ya taifa watakatiwa bima ya matibabu.
“Naamini hii itakuwa faraja kubwa kwao, nitafanya kosa kama nitashukuru bila kuishukuru timu ya Azam kwa kutupa mtaalam wao wa mazoezi ya viungo (Paul Gomes), alifanya kazi kubwa sana kwenye timu yetu,” alisema Tenga.
RAMANI NA VIPIMO VYA UWANJA WA SOKA!
Wengi tunaupenda mchezo wa soka lakini je sheria zenyewe zinazoongoza mchezo huu tunazifahamu? blog yako inakuletea sheria za mchezo huu, hii ni kwa ajili ya kuwafanya wasomaji wetu nanyi mfahamu sheria 17 za mchezo huu.
SHERIA YA 1:UWANJA WA MICHEZO
1: vipimo
Kiwanja cha michezo kina umbo la mstatili. Urefu wake
hautazidi yadi 130 na hautapungua yadi 110. Upana wake
hautazidi yadi 100 wala hautapungua yadi 50. Kiwanja cha michezo ya kitaifa urefu hautazidi yadi 80 wala kupungua yadi 110, na upana hautazidi yadi 80 wala kupungua yadi 110, na upana hautazidi yadi 80 wala kupungua yadi 70. Kwa vyovyote vile, marefu yatazidi mapana.
2: Alama
Mistari inayoonekana wazi, yenye unene usiozidi inchi 5
itachorwa kuonyesha mipaka ya kiwanja. Mistari ya urefu
itaitwa mistari ya pembeni na ile ya mapana, itaitwa mistari ya goli.
Bendera iliyootundikwa kwenye mti usiopungua futi 5 kwa urefu itasimikwa katika kila kona ya kiwanja. Bendera ya aina hii yaweza kusimikwa sawa na mstari wa kati umbali usiopungua yadi moja kutoka mstari wa pembeni. Mstari wa katikati utapita katikati ya kiwanja na alama itawekwa
kuonyesha katikati ya kiwanja na alama itawekwa kuonyesha katikati kabisa. Kutoka kwenye alama hiyo,mnviringo wenye nusu kipenyo cha
yadi 10 utachorwa. Alama hiyo ya kati ndipo mahali pa kuanzia michezo.
3: Eneo la goli
Katika kila upannde wa goli mistari miwili itachorwa pembe mraba na mstari wa goli. Eneo lililomo ndani ya mistari hii litajulikana kama eneo la goli.
4: Eneo la Adhabu
Katika kila upande wa goli mistari miwili itachorwa pembe
mraba na mstatiri wa goli umbali wa yadi 18 toka kila nguzo ya goli. Mistari hii itaingia uwanjani umbali wa yadi 18 na itaungwa kwa mstari wa usawa na ule wa goli. Eneo hili litajulikana kama eneo la adhabu. Alama itawekwa umbali wa yadi 12 kutoka katikati ya mstari wa goli, na hapo ndipo pa kupiga penalti. Kutoka alama hiyo
mkato wenye nusu kipenyo cha yadi 10 utachorwa nje ya eneo la adhabu.
5: Eneo la kona
Robo ya mviringo yenye nusu kipenyo cha yadi itachorwa ndani ya kiwanja kutoka mahali ilipo bendera ya kona. Eneo hili ndio eneo la kona.
6: Magoli
Nguzo za goli zitasimikwa katikati ya mistari ya goli, zikiacha urefu sawa toka kila kona. Umbali kati ya nguzo na nguzo utakua yadi 8. Juu ya nguzo kutawekwa mwamba na urefu wa ndani ya gali toka chini hadi hadi juu, mwamba huo hautazidi inchi 5.
Baraza la michezo la mataifa FIFA limeamua katika sheria katika sheri hii ya kwanza ya mchezo wa soka
kwamba;
1: Vipimo vya kiwanja cha mchezo wa kimataifa vitakuwa; si zaidi ya yadi 120 + 80 wala si chini ya yadi 100 + 70. (Wastani
m105 + m70)
Tuesday, June 12, 2012
KALI YA LEO: WACHEZAJI 12 WAPEWA KADI NYEKUNDU KWENYE MCHEZO MMOJA.
Wachezaji 12 walilimwa kadi nyekundu kwenye mchezo wa ligi ya madaraja ya chini nchini Brazil kati ya Votuporanguense na Fernandopolis.
PODOLSKI NA MULLER WALIFELI DHIDI YA URENO: JE REUS NA SCHURRLE WATAANZA DHIDI YA UHOLANZI
Mchezo wao kwanza wa Euro 2012 ulienda kwa mujibu wa Ujerumani walivyotaka - kwa upande wa matokeo, lakini vijana wa Joachim Low hawakuonyesha uwezo mkubwa ambao wengi walikuwa wakiutegemea dhidi ya Ureno. Ushindi wa 1-0 ulikuwa ni bahati kwa timu hiyo kwa kuwa hata Ureno walipoteza sana nafasi kwa kutokuwa na bahati waliyoipata Ujerumani.
Ndio maana haishangazi kuona umma wa Ujerumani ukitegemea kuona mabadiliko kwenye mechi zijazo, kwa kuwa hawakuona timu yao ikicheza kwa kutengeneza nafasi nyingi za magoli dhidi ya kikosi cha Paulo Bento. Low alifanya uamzui mkubwa kwa kumchezesha Mats Hummels na Mario Gomez, lakini mashabiki wanataka kocha wao aongezee ujasiri wakati wa mechi zijazo.
Kuna maswali juu ya nafasi mbili: Thomas Muller na Lukas Podolski wote wanaweza wakaanzia benchi kwenye mechi zijazo. Wote walionyesha kwamba wapo tayari kucheza kwa kujituma bila kuchoka lakini kiukweli hawakucheza vizuri, na sasa Marco Reus na Andre Schurrle wanaweza kuwa wabadili wao dhidi Uholanzi?
Akiwa mmoja ya chipukizi bora wa ligi ya Ujerumani msimu uliopita, kiwango cha Marco Reus akiwa Borussia Monchengladbach kimeonyesha ubora anaoweza kuuleta ndani ya kikosi: akiwa na na rekodi nzuri za ufungaji na ubunifu mzuri kiwanjani. Kwa upande wa Schurrle amekuwa katika form nzuri kwa siku za hivi karibuni katika mechi za kirafiki kuelekea kwenye Euro, pia alikuwa na msimu mzuri na Bayern Leverkusen, na hakuna ubishi kwamba amaelata maswali mengi juu ya nani aanze kati yake na Podolski.
Alifunga magoli kwenye mechi mbili za mwisho za msimu na Leverkusen, na akiwa anatokea benchi dhidi ya Israel aliubadilisha mchezo na kuifanya Ujerumani kuwa tishio tofauti ana alivyokuwepo Podolski kwenye pitch.
"Kiukweli nataka kucheza mara nyingi iwezekanvyo, lakini kuna nafasi moja na watu wengi tunaitaka hivyo mwisho wa siku ni uamuzi wa kocha, japokuwa haijalishi nimecheza au hapana nitaisapoti yangu mwanzo mwisho kiwanjani mpaka nikiwa kwenye benchi." alisema Schurrle muda mfupi kabla ya kuelekea Ukraine.
Wengi wanatabiri kwa tabia ya kocha Low ya kufanya mabadiliko yasiyotegemewa kwenye kikosi, basi ni dhahiri Reus na Schurrle wanwwza wakaanza mbele ya Muller na Podolski
Ndio maana haishangazi kuona umma wa Ujerumani ukitegemea kuona mabadiliko kwenye mechi zijazo, kwa kuwa hawakuona timu yao ikicheza kwa kutengeneza nafasi nyingi za magoli dhidi ya kikosi cha Paulo Bento. Low alifanya uamzui mkubwa kwa kumchezesha Mats Hummels na Mario Gomez, lakini mashabiki wanataka kocha wao aongezee ujasiri wakati wa mechi zijazo.
Kuna maswali juu ya nafasi mbili: Thomas Muller na Lukas Podolski wote wanaweza wakaanzia benchi kwenye mechi zijazo. Wote walionyesha kwamba wapo tayari kucheza kwa kujituma bila kuchoka lakini kiukweli hawakucheza vizuri, na sasa Marco Reus na Andre Schurrle wanaweza kuwa wabadili wao dhidi Uholanzi?
Akiwa mmoja ya chipukizi bora wa ligi ya Ujerumani msimu uliopita, kiwango cha Marco Reus akiwa Borussia Monchengladbach kimeonyesha ubora anaoweza kuuleta ndani ya kikosi: akiwa na na rekodi nzuri za ufungaji na ubunifu mzuri kiwanjani. Kwa upande wa Schurrle amekuwa katika form nzuri kwa siku za hivi karibuni katika mechi za kirafiki kuelekea kwenye Euro, pia alikuwa na msimu mzuri na Bayern Leverkusen, na hakuna ubishi kwamba amaelata maswali mengi juu ya nani aanze kati yake na Podolski.
Alifunga magoli kwenye mechi mbili za mwisho za msimu na Leverkusen, na akiwa anatokea benchi dhidi ya Israel aliubadilisha mchezo na kuifanya Ujerumani kuwa tishio tofauti ana alivyokuwepo Podolski kwenye pitch.
"Kiukweli nataka kucheza mara nyingi iwezekanvyo, lakini kuna nafasi moja na watu wengi tunaitaka hivyo mwisho wa siku ni uamuzi wa kocha, japokuwa haijalishi nimecheza au hapana nitaisapoti yangu mwanzo mwisho kiwanjani mpaka nikiwa kwenye benchi." alisema Schurrle muda mfupi kabla ya kuelekea Ukraine.
Wengi wanatabiri kwa tabia ya kocha Low ya kufanya mabadiliko yasiyotegemewa kwenye kikosi, basi ni dhahiri Reus na Schurrle wanwwza wakaanza mbele ya Muller na Podolski
HATIMAYE YANGA YATHIBITISHA MARCIO MAXIMO KUTUA BONGO JUMAPILI HII
Baada ya siku chache zilizopita website hii ilikuwa ya kwanza kuripoti kwamba klabu ya Yanga ipo katika hatua za mwisho za kumsaini Marcio Maximo, leo hii imefahamika kwamba kocha huyo wa zamani wa timu ya taifa 'Taifa Stars' Mbrazil, Marcio Maximo anatarajia kutua nchini kwa mara nyingine tena toka aondoke nchini mwezi juni mwaka 2010 siku ya jumapili juni 17 saa 9 alasiri.
Maximo anakuja nchini kuchukua mikoba ya Mserbia wa Yanga Kostadin Papic aliyenyimwa mkataba mpya, baada ya ule wa awali wa miezi 6 kuisha wakati ligi kuu ya Vodacom msimu wa 2011/12 ukielekea mwishoni.
Maximo awali alitarajiwa awasili nchini hapo kesho, na kwa mujibu wa taarifa rasmi na zinasema kocha huyo mwenye msimamo mkali atawasili jumapili na shirika la ndege ya Emirates.
Maximo anakuja nchini kuchukua mikoba ya Mserbia wa Yanga Kostadin Papic aliyenyimwa mkataba mpya, baada ya ule wa awali wa miezi 6 kuisha wakati ligi kuu ya Vodacom msimu wa 2011/12 ukielekea mwishoni.
Maximo awali alitarajiwa awasili nchini hapo kesho, na kwa mujibu wa taarifa rasmi na zinasema kocha huyo mwenye msimamo mkali atawasili jumapili na shirika la ndege ya Emirates.
Hii ndiyo ndivyo sivyo ya ubingwa nchi za ulaya
Na Arone Mpanduka(Radio Tumaini)
NDANI ya msimu wa mwaka 2011/2012 tumekuwa tukishuhudia matukio mbalimbali ya kimichezo hasa katika medani ya soka ambayo yamekuwa yakivutia na kusisimua.
Kutokana na kufuatilia kwa karibu zaidi matukio ya soka Barani Ulaya kupitia ligi mbalimbali nimeweza kubaini mambo kadhaa ambayo yamekuwa kinyume na matarajio ya wapenzi wengi wa mchezo wa soka duniani.
Kupitia matukio hayo wengi waliokuwa wanajaribu kutabiri ndivyo, matokeo yake yamekuwa sivyo.Fuatana nami ili tuweze kwenda pamoja hasa kwa kupitia tukio moja hadi lingine kwa kifupi.
BINGWA WA KOMBE LA FA
Hapa wengi walidondosha karata yao ya utabiri kwa timu ya Liverpool hasa kutokana na wachezaji wake kuwa na tabia ya kutokata tamaa katika dakika zote 90 hata kama wakiwa nyuma kwa goli moja ama mawili kitu ambacho wachezaji wa Chelsea wamekikosa.
Licha ya kwamba timu zote zilikuwa na mwenendo mbovu katika msimu wa 2011/2012 lakini Liverpool ilipewa nafasi kubwa zaidi ya kutwaa kombe hili lakini hatimaye mambo yalikuwa kinyume hasa pale ambapo Chelsea ilipofanya maajabu kwa kuinyuka Liver mabao 2-1.
Ramires na Didier Drogba ndiyo waliofanikisha kombe la FA kwenda darajani ambapo kwa mara ya mwisho Chelsea ilitwaa kombe hilo mwaka 2010.
BINGWA WA LIGI KUU YA HISPANIA
Katika ligi hii wengi walikuwa wakiiangalia zaidi Barcelona ambayo ilikuwa ikishiriki ligi kama bingwa mtetezi lakini pia bingwa wa dunia ngazi ya vilabu.
Watu walikuwa na imani na Barcelona hasa kwa uimara iliyonao wa kuweza kumiliki mpira na kupenyezeana pasi za uhakika na hata pia umakini wa washambuliaji wake kama Lionel Messi ambaye ni mgumu kumzuia pindi anaposogelea ‘sebule’ ya timu pinzani.
Hadi ngwe ya mechi za marudiano za ligi kuu ya Hispania inaanza Barcelona ilikuwa kileleni mwa msimamo wa ligi ikifuatiwa na Real Madrid lakini mambo yalibadilika kuelekea mwishoni mwa ligi ambapo Madrid chini ya Jose Mourinho ikafanikiwa kuitangulia Barcelona kwa tofauti ya pointi 4.
Mambo yalizidi kwenda hivyo hasa kwa timu zote kuhakikisha kwamba hazifanyi makosa kwenye mechi zao na kufanya mashabiki wa soka ulimwenguni kusema kwamba bado Barcelona ana nafasi ya ubingwa hasa katika mechi ambayo wanacheza mwenyewe kwa wenyewe hasa ikizingatiwa kwamba mara zote Madrid ni kibonde wa Barcelona.
Lakini mambo hayakuwa mambo kwani hata walipokutana wenyewe kwa wenyewe Barcelona alikubali kichapo kutoka kwa Real Madrid mara baada ya kupigwa 2-1 na kutengeneza tofauti ya pointi 7 kutoka 4, tofauti ambayoi ilikwenda hadi siku ambayo Real Madrid inatangaza ubingwa.
Hapa ndugu msomaji hadi mwisho wa ligi ubingwa wa Real Madrid ulikuwa kinyume na matarajio ya wengi.
BINGWA WA LIGI KUU YA UINGEREZA
Katika ligi hii inayodhaminiwa na benki kubwa duniani ya Backlays tangu inaanza mwezi Agosti mwaka 2011 mashabiki wengi walikwishaipatia ubingwa timu ya Manchester United hasa baada ya kuanza vizuri msimu kwa kuinyuka Manchester City 3-2 katika mechi ya ngao ya jamii.
Kama hiyo haitoshi Manchester United ilionyesha kwamba ipo vizuri baada ya kutoa vipigo kwa timu kadhaa ikiwemo kipigo cha kihistoria ya mabao 8-1 ilichomnyuka Arsenal na kuweka rekodi ya ushindi wa mabao mengi zaidi katika msimu huo wa ligi kuu.
Kumbe wakati huohuo timu iitwayo Manchester City ilikuwa inakimbiza mwizi kimya kimya hasa baada ya kuonyesha ushindani wa hali ya juu kwa kutoa dozi kwa timu ilizokuwa inakutana nazo.
Hadi kufikia mwezi Januari mwaka 2012 Manchester City walikuwa wanaongoza ligi wakifuatiwa na Manchester United kitu ambacho kilihamisha mawazo ya wadau wa soka kutoka kwa United hadi City na kusema kwamba City ndiyo bingwa mtarajiwa.
Lakini mwishoni mwa ligi hiyo mambo yalibadilika ambapo wadau wakarejesha utabiri wao kwa Manchester United kuwa ndiye bingwa wa ligi hiyo hasa baada ya timu hizo kuwa na pointi sawa huku City ikiwa kileleni kwa tofauti ya mabao ya kufunga na kufungwa tu.
Utamu ulikuja katika siku ya mwisho ya kumaliza ligi ambapo bingwa alikuwa bado hafahamiki na watu wengi walitabiri kwamba Manchester United atamfunga Sunderland lakini wakiibeza City kwamba isingeweza kuifunga QPR ambayo nayo ilihitaji ushindi ili isishuke daraja.
Hali hiyo ilifanya siku hiyo hata helikopta iliyobeba kombe kuhangaishwa angani ambapo kila dakika ilikuwa inabadili njia zake, mara iende Sunderland mara ibadilike na kwenda Etihad.
Lakini mwisho wa yote Manchester City nayo iliibuka na ushindi wa mshangao wa mabao 3-2 ikitoka nyuma ya mabao 2-1 dhidi ya QPR huku Manchester United ambayo iliiombea City ifungwe ili yenyewe ichukue ubingwa ikajikuta ikipoteza ndoto hiyo licha ya yenyewe kushinda bao 1-0.
Mwisho wa yote Manchester City aliibuka bingwa kiyume na matarajio ya wengi ulimwenguni.
BINGWA WA KLABU BINGWA BARANI ULAYA
Hapa timu za Bayern Munich na Chelsea hazikupewa nafasi kabisa ya kufika hata nusu fainali lakini matokeo yake miamba hiyo ilitinga fainali na kuchuana pale Allianz Arena nchini Ujerumani.
Utabiri ulianza kushika kasi katika hatua ya 16 bora ambao kwa mtazamo wa haraka haraka mashabiki wengi duniani walihisi kwamba fainali itazikutanisha timu za Real Madrid na Barcelona na hapo yoyote kati ya hizo ndiye atakayekuwa bingwa.
Kinyume chake ni kwamba Real Madrid alibwagwa na Bayern Munich katika hatua ya nusu fainali huku Barcelona akibwagwa na kibonde Chelsea katika hatua ya nusu fainali, kitu ambacho kiliwashangaza wengi hasa kwa hali iliyonayo Chelsea kuweza kuiondosha miamba ya dunia Barcelona ambayo ilikuwa na kila sababu ya kufika fainali na kutwaa taji hilo.
Mechi ya fainali kati ya Bayern Munich na Chelsea nayo iliibua watabiri wengi walioegemea upande wa Bayern kwamba ndiyo wangekuwa mabingwa hasa kutokana na sababu nyingi ikiwemo tofauti ya uwezo wa kuuchezea mpira na kasi ya ushambulizi kwa timu hizo ambapo wajerumani waliizidi Chelsea.
Suala lingine ni kitendo cha Bayern kucheza nyumbani , mahali ambapo pana watu wengi wa kuiunga mkono pindi iwapo dimbani.
Matokeo ya mwisho yalikuwa ndivyo sivyo kwani Chelsea iliibuka na ushindi wa penati 4-3 hasa baada ya kutoka sare ya 1-1 ndani ya dakika 120 za mchezo.
Barua Pepe:mpanduka@yahoo.com
BONDIA JAPHET KASEBA AZUNGUMZA NA MO BLOG KUHUSU ‘FREEMASON’.
MO BLOG: Japhet Kaseba hakuna asiye kufahamu katika ulimwengu wa Tanzania wa mchezo wa Kick Boxing, hebu tutofautishie kati ya mchezo wa kick boxing unaocheza na Muay Thai ambayo pia unacheza.
KASEBA: Unajua kick boxing ni staili ambayo ipo Marekani ambayo inahusisha ngumi na mateke lakini mateke yake yanaanzia kiononi kuelekea juu, na Muay Thai ni staili kutoka Thailand ambayo mateke yake yanaanzia kwenye mapaja kwenda juu.
Pia wanatumia Elbow na kushikana na kudondoshana kitu ambacho kwenye kick boxing hakuna.
MO BLOG: Watanzania wategemee nini maana wewe ndie mwakilishi wetu nje ya nchi.
KASEBA: Kubwa ni kwamba baada ya kukosa wapinzani kwa muda mrefu katika suala zima la Kick Boxing nikaamua mimi nijiweke pembeni kidogo na kuamua kuanzisha ligi ya ‘Bingwa wa Mabingwa’ kwa Tanzania na baadae Afrika nzima kwa sababu nilikuwa nakusudia kuwaleta washiriki kutoka Japan na Wanathailend.
MO BLOG: Sasa nini kilitokea na mipango hiyo kukwama..?
KASEBA: Nilikosa udhamini wa kulipia vitu kama sehemu za kulala kwa sababu gharama nyingine walikuwa tayari kujilipia wenyewe.
MO BLOG: Mara ya mwisho tumekujua kama Bingwa wa mchezo wa kick-boxing, lakini ghafla unacheza mchezo wa masumbwi..?
KASEBA: Kama nilivyosema mwanzo baada ya kukosa mpinzani kwa muda mrefu katika mchezo wa kick-boxing, niliona ni vyema nikaonyesha kipaji changu katika mchezo masumbwi. Ndipo nilipopambana na Francis Cheka na mchezo wetu kuharibika baada ya shabiki kupanda ulingoni.
MO BLOG: Tufafanulie utata uliopo baina yako Francis Cheka katika mchezo wa masumbwi .?.
KASEBA: Kwa mimi binafsi sidhani kama kuna utata, na kwa sasa najiandaa kwa pambano la marudiano ambalo nitalitumia kuweka heshima, ambalo litafanyika tarehe 7 mwezi wa 7 ili kujua nani mshindi wa ukweli.
MO BLOG: Kaseba kuna ukweli wowote kwamba kabla ya kucheza pambano ni vyema siku moja kabla mtu unapaswa kufanya mapenzi.?.
KASEBA: Kwa kweli kwa kuwa mimi nilianzia kwenye mchezo wa ‘Martial Arts’ , hicho kitu kilikuwa kinapingwa sana na sidhani hata katika michezo mingine kinakubalika. Sana sana ningewaasa watanzania kujituma katika mazoezi na kuacha kudanganyana.
MO BLOG: Hebu izungumzie familia yako kwa sababu mengi yamesemwa na hatupendi kuyarudia.
KASEBA: Nampenda sana mke wangu, nawapenda ndugu zangu, pia nawapenda sana wazazi wangu na siku zote namshukuru mwenyezi mungu na naamini hiyo ni moja wapo ya mafanikio yangu, kwa kuwa kila ninachohangaikia nahaingikia kwa sababu ya familia yangu.
MO BLOG: Kumekuwa na taarifa kwamba wewe ni Freemason hebu jitetee.!
KASEBA: Ee bwana ehh, ha…ha..ha Mo Blog mnanizingua lakini nachoweza kusema ni kuwa mimi siwezi kukataa wala kukubali na waacheni wanadamu waseme wanavyotaka, kwa sababu hata Kanumba wamesema ni ‘Freemason ‘ lakini najua ni ile ‘movie’ aliyocheza ndio imemponza.
Upeo wa watu wengi ni mdogo sana, kwa sababu chochote mtu anachokifanya kwa maana ya kuigiza, watu wengi wanaamini ni kweli.
Ndio maana kuna wanawake wameigiza filamu za uchawi na mpaka leo wanaogopwa mitaani wakionekana kweli ni wachawi.
Kwa nchi iliyopo chini kama Tanzania ambayo inaibukia kila utakachokifanya itaonekana ni hivyo hivyo, hata ukiigiza ukasema mimi ni rais ndivyo baadhi ya watu watakavyoamini.
Mimi ni mkristo ninayependa kumtumikia Mungu.
MO BLOG: Japhet Kaseba MO BLOG inakutakia mafanikio katika jitihada zako za kukuza mchezo wa ‘Kick-Boxing’ hapa nchini na katika kufanikisha ligi ya Masumbwi, na bila kusahau mchezo ujao wa ngumi kati yako na Francis Cheka; tuko pamoja nawe.
KASEBA: Akhsante sana nami nawatakia kila la heri katika utendaji wenu wa kazi, na msitusahau wanamichezo kama sisi.
SOURCE: dewjiblog.com
BREAKING NEWS: YANGA YAMSAJILI FRANK DOMAYO KWA MIL.20
Habari rasmi kutoka kwenye kamati ya usajili ya klabu ya Yanga ni kwamba timu hiyo leo imekamilisha usajili wa kinda la timu ya taifa ya Tanzania aliyeng'ara kwenye mchezo wa jumapili iliyopita dhidi ya Gambia Frank Domayo.
Domayo ambaye alikuwa akiichezea JKT Ruvu msimu uliopita, amesaini mkataba wa miaka 3 kuitumikia Yanga, huku akilipwa shilingi millioni 20 kama ada ya usajili na atakuwa akilipwa shilingi millioni moja kama msharaha kwa miaka 3 ijayo.
UFARANSA VS ENGLAND: ROY HODGSON NA FALSAFA YA KUPAKI BASI - KAPATA ALICHOTAKA
Hii ilikuwa mechi ambayo ilikuwa na ubunifu mdogo sana huku ikichezwa kwa kasi ya chini sana .
Laureant Blanc aliteua kikosi ambacho kilicheza mfumo ambao kila mmoja alitarajia mfumo wa 4-3-3, huku Florent Malouda akihangaika mbele akitokea katikati ya uwanja.
Roy Hodgson aliwashangaza watu wengi kwa kumpanga Alex Oxlade Chamberlain ambaye alicheza upande wa kushoto huku James Milner akicheza upande wa kulia na Danny Welbeck akiongoza mashambulizi .
Kama ilivyotarajiwa, Ufaransa ilitawala sana mpira kwa maana ya umiliki huku ikimaliza kwa wastani wa asilimia 65 ya umiliki wa mpira huku wakipiga mashuti 21 tofauti na England ambao walipiga mashuti matano pekee. Hata hivyo mashuti mengi ya Ufaransa yalikuwa ya mbali yasiyokuwa na madhara ukiachilia mbali shuti la Nasri ambalo lilizaa bao la kusawazisha, yote kwa yote Ufaransa walihangaika kutengeneza nafasi za wazi.
Vita ya Mfumo
Ilikuwa vita nyepesi. England walikuwa na makundi ya wachezaji wanne wanne kwenye ulinzi na kiungo huku Ashley Young na Welbeck wakicheza mbele - Laureant Blanc alimpa Alou Diarra maelekezo ya kumkaba Ashley Young na kumnyima nafasi ya kufanya kazi kwa uhuru hasa pale ambapo Young alikuwa anarudi chini kusaka mpira. Yohan Cabaye alikuwa akicheza juu karibu na sehemu aliyokuwa Gerard na Malouda alikuwa akijaribu kumvuta Scott Parker kutoka kwenye nafasi yake aliyokuwa. Kiujumla kulikuwa na nafasi finyu sana kwa Ufaransa kufanya mambo yake kwa uhuru kwani England walijaza upande wao na kuwanyima Ufaransa uhuru wa kupiga pasi walizohitaji kupanga mashambulizi. Ufaransa walijaribu mbinu ya kupitisha mipira jambo ambalo liliwafanya England kutoa mipira mingi iliyoza kona ambazo hazikuzaa matunda .
Mashambulizi ya Ufaransa.
Wachezaji wanne wa Ufaransa waliokuwa wanacheza kwenye eneo la mbele akiwemo Malouda walikuwa wakipeana pasi kwa ufanisi. Wakati Riberry akiwa anacheza sana pembeni upande wa kushoto, Samir Nasri yeye alikuwa akisafa uwanja mzima na kucheza kila mahali jambo ambalo lilifungua nafasi kwa Mathieu Debuchy. Kiujumla mbinu na mipango yote ya Ufaransa ilimzunguka Samir Nasri na hata takwimu zilionyesha kuwa alicheza pasi nyingi kuliko wachezaji wote waliokuwa uwanjani jana. Kiujumla Nasri alitengeneza nafasi nane kwenye mchezo wote.
Nasri alikuwa mtu pekee ambaye alikuwa akitumia nafasi akijaribu kujenga mashambulizi, alikuwa akiingia kwenye eneo ambalo lilikuwa wazi na kuwachanganya wachezaji wa England wasijue la kufanya ili kumkabili. Wakati mwingine Lescott alikuwa akitoka nyuma na kujaribu kumfuata kumbugudhi asilete madhara, wakati mwingine Ashley Cole angetoka kwenye eneo lake na kujaribu kumkaba, kiujumla ile hali ya kuwavuruga wachezaji wa England kwenye jinsi ya kumkabili Nasri ndio ilikuwa msingi wa mashambulizi ya Ufaransa. Hata bao alilofunga Nasri lilikuja wakati ambao mabeki wa England walikuwa wamesogea ndani sana na kumuachia Nasri nafasi ambayo ilimfanya achague sehemu ya kupiga mpira na kusawazisha .
Ukiachilia mbali Movement za Nasri, England waliyamudu mashambulizi ya Ufaransa. Kikosi cha Laureant Blanc kilicheza kwa uvumilivu huku wakingoja nafasi ya wazi ambayo ingewapa mwanya wa kuidhuru England na hawakuwa wakiwaachia wachezaji wengi mbele katika hali ambayo pengine ingeweza kuwa na madhara hasa ukizingatia England walivyo wepesi kwenye mashambulizi ya Counter.
Mashambulizi ya England.
Mchezo wa England kwa ujumla ulijengwa kwenye kukubali presha ya Ufaransa na kujaribu kuvunja mashambulizi kwa hataka na kushambulia kwa kushtukiza –walifanikiwa katika hili kwenye michezo miwili ya kirafiki kabla ya michuano hii kuanza lakini kwa mchezo dhidi ya Ufaransa walikosa ufanisi kwenye jinsi ya kumalizia nafasi chache zilizotokea ndani ya mchezo. Sababu kubwa ya hili ilikuwa jinsi Ashley Young alivyoshindwa kutumika kwenye mchezo kama ilivyozoeleka. Alimaliza pasi 12 pekee kati ya 20 alizotengeneza .
Hata hivyo sifa kubwa ilimuendea Alou Diarra ambaye alikuwa mjanja sana kwa jinsi alivyojipanga na kumzuia Young wakati England walipokuwa na mpira . Kitakwimu Diarra Diarra alimaliza au alifikisha pasi zote alizopiga na tackles zake zote 5 alizopiga zilikuwa za mafanikio .
Nafasi pekee ya wazi ambayo England walitengeneza wakati mchezo ukiendelea ilikuja wakati James Milner alipomzunguka kipa Hugo Lloris lakini alipiga nje . Alex Oxlade Chamberlain aliingia katikati ya uwanja na Alou Diarra alimfuata jambo ambalo lilimfanya Ashley Young kuwa huru na kumpa Milner pasi, nafasi kama hii haikujitokeza tena. Danny Welbeck alicheza vizuri akikaa na mipira, lakini hakuwa na wakati mzuri kwa kuwa msaada wake mkubwa unatoka kwa Ashley Young ambaye alibanwa kwa kiasi kikubwa .
Young na Welbeck walicheza vizuri sana hasa walipokuwa bila mpira. Hawakukimbiza na kukaba mabeki wa pembeni wa Ufaransa, badala yake walisimama njiani na kuzuia pasi za wafaransa kupita njiani. Philipe Mexes na Adil Rami walikuwa wakipiga mipira ya moja kwa moja na walishindwa kupeleka mipira mbele toka nyuma, matokeo yake mchezo ulikuwa wa taratibu jambo ambalo kwa England lilikuwa zuri.
Kipindi cha Pili.
Mchezo ulikosa mwendelezo kwenye kipindi cha pili . England waliendelea kukaa mbele ya lango na Ufaransa walishindwa kuongeza idadi ya wachezaji waliokuwa wakishambulia nao. Bado mchezo uliendelea kuwa wa taratibu na timu zote zilionekana kuchoka mapema na kutambua kuwa sare yalikuwa matokeo mazuri.
Labda maendeleo pekee yalikuwa kwenye movement za Karim Benzema ambaye alionekana kukerwa na kukosekana kwa ubunifu na huduma ya pasi zilizoelekea kwake jambo lilomfanya ajaribu kufanya kila kitu mwenyewe . Mwishoni alijaribu kuiga alichokuwa anafanya Samir Nasri na kusogea kwenye maeneo ambayo yalikuwa na nafasi na alifanya hivi na kupiga mashuti ya mbali ambayo Jo Hart aliokoa. Timu zote zilichelewa kufanya mabadiliko, England walimuingiza Jermaine Defoe ambaye aliingia kwenye nafasi ya Alex Oxlade Chamberlain ambapo Ashley Young alienda kushoto na Jordan Henderson aliingia kwneye nafasi ya Scott Parker aliyeonekana kuchoka . Haya yalikuwa mabadiliko ambayo yalilenga kujenga mashambulizi zaidi hasa ukizingatia mabeki wa Ufaransa walionekana wamechoka .
Laureant Blanc alimuingiza Hatem Ben Arfa na Marvin Martin waliochukua nafasi za Malouda na Cabaye lakini mabadiliko haya yalifanywa muda ukiwa umepita na walikosa muda wa kufanya kazi ya kuokoa mchezo.
Mwisho.
Kwenye michezo yote ya raundi ya kwanza kumekuwa na soka la wazi sana ambalo kiujumla limetoa burudani kubwa lakini mchezo wa ufaransa na England ulikuwa wa kasi ya chini kupita yote . Ni kama timu zote zilikuwa zimepanga kutopoteza mchezo huukuliko zilivyopanga kutafuta ushindi na sare ilikuwa kama imepangwa huku Ufaransa wakionekana kupiga zaidi mashuti ya mbali baada ya kuona wameshindwa kuivunja defense ya England .
Shape ya England haikuwa mbaya , hata hivyo mabadiliko ya movement toka wakati ambapo timu haina mpira na pale ilipokuwa na mpira hazikuwa nzuri na hii ilitokana na Ashley Young kufichwa sana . Kwa mfumo wa England Young ni mtu muhimu lakini Ufaransa walifanya kazi kubwa ya kumtia mfukoni . Hodgson anapaswa kufanya kazi kubwa ya kuifanya England kuwa na madhara zaidi inapokuwa na mpira
Subscribe to:
Posts (Atom)














