Search This Blog

Thursday, June 14, 2012

EXCLUSIVE: ORLANDO PIRATES WATUMA RASMI BARUA YA KUMTAKA EMMANUEL OKWI

Hatimaye klabu ya Orlando Pirates imetuma rasmi barua ya mualiko kwa mchezaji wa Simba Emmanuel Okwi kwenda nchini South Africa kwa ajili ya kufanya majaribio ya kuweza kujiunga na timu hiyo.
Hii ni sehemu ya barua ya Orlando kumualika Okwi.
Nimefanikiwa kuiona barua hiyo ikiwa inatoa maelekezo kwamba Okwi atapewa majaribio ya wiki mbili na Orlando Pirates, huku akihudumiwa kuanzia usafiri, malazi, matibabu pamoja na gharama nyingine zitakazojitokeza kwa wakati atakaokuwa na klabu hiyo.

Kwa kipindi cha misimu miwili sasa Orlando wamekuwa wakimfuatilia Okwi ambaye klabu yake ya Simba imemuwekea price tag ya Billioni 2 kwa timu inayomtaka, huku pia wapinzani wao wa jadi klabu ya Yanga ikiwa inamfukuzia mshambuliaji huyo wa Uganda ambaye siku za hivi karibuni amekuwa ndio tegemeo la safu ya ushambuliaji ya mabingwa wa Tanzania.

17 comments:

  1. HAYA NDO MAMBO AMABYO TUNATAA SI KUONA WACHEZAJI WANAFUKAZANA KWENDA SIMBA AU YANGA,LAZIMA WAWE NA FOCUS YA KUFIKA NJE ILI KUWEZA KUPATA EXPOSURE YA KIMATAIFA.

    ReplyDelete
  2. Nakuombea Okwi ufanikiwe na hiyo timu ili utoe nafasi kwa kijana mwingine kung'ara ndani ya Simba maana najua Simba ndo timu pekee yenye kung'arisha vijana na hatimaye kupata timu nje. Mkienda huko nje mfanikiwe zaidi kuchezea timu kubwa ili baadaye tuwaone kwenye ligi kubwa kubwa za huko Ulaya.

    ReplyDelete
    Replies
    1. Hivi, Nonda Shabani alitoka Simba? Ni mchezaji gani wa Simba aliyewahi kuenda kuchezea klabu ambayo ipo kwenye ligi ya maana kama ya Ufaransa, Uholanzi?

      Delete
    2. Na ukiacha Nonda kuna mwingine aliyetoka Yanga na kuwika?
      Lakini Simba imewatoa Matola,Mrwanda,Samatta,Njohole,Henry,ezechekwu n.k ~ am just remindind the above

      Delete
    3. apart frm nonda who else?

      Delete
    4. Hao wote uliowataja hakuna aliyewahi kechezea timu ya maana na kuonekana kwenye luninga hapa TZ. Alafu wakichezea timu ya taifa wanachemsha, isipokuwa Samatta tu!

      Delete
    5. Nonda alipokwenda ulaya kucheza soka hakutokea yanga.kama alitokea Yanga tuambie we hapo juu baada ya thread ya Edo,kama aliuzwa na yanga aliuzwa shi ngapi.Simba ndiyo inauza wachezaji bana acha unafiki

      Delete
  3. all the best jembe na hicho ndo kinanifanya nizidi kuipenda na kuishabikia simba sports club kwasababu ya kuibua vipaji na kuwapa fursa ya kwenda kutafuta maisha mazuri zaid ggssc

    ReplyDelete
  4. nonda shaaban yanga hawakumuuza ila alikimbia ubabaishaji, kaw hiyo pale south alienda kama mchezaji huru na mafanikio yake yanaanza kuhesabiwa kuanzia club yake ya south ndio maana yanga hawana fungu lolote wanalopata kutokana na mafanikio ya nonda lakini leo kama sammata atauzwa popote pale simba wana fungu lao sababu kipo kipengele kinachosema hivyo. so migongo wazi acheni kupiga kelele na mafanikio ya nonda ambae hata pa kulala alikua anasaidiwa na kina malima.

    ReplyDelete
    Replies
    1. Umemjibu vizuri sana anayeulizia habari za Nonda, Toka lini Yanga wakauza mchezaji sana sana atakuwa ni Ngasa tu naye Madega alilaumiwa utadhani ameua.

      Delete
  5. Hayo ndomambo yanayotakiwa,sio kusajili wachezaji usiku wa manane

    ReplyDelete
  6. Tuache mambo ya kutorosha wachezaji usiku

    ReplyDelete
  7. Mungu awe nawe okwi kama mwana msimbazi nakuombea ufanikiwe na uitangaze msimbazi na nchi yako mungu nawe

    ReplyDelete
  8. Hongera okwi, hongera simba. Tunapaswa kuwa na mtazamo huo katika soka. Wachezaji wenye malengo ya mbali katika soka waenda simba watafanikiwa. Tazama samata, henry joseph, ochan, mrwanda na sasa ni okwi. Aibu yenu yeboyebo.

    ReplyDelete
  9. Kazi kwako Okwi umeshakubalika kama mwana msimbazi damu sina kinyongo maana zingekuwa ni club za Bongo ningekuwa na kinyongo maana hamna ambacho kingeongeza mafanikio yako hongeraaaa sana kaka.

    ReplyDelete
  10. Wana Msimbazi tunatakiwa tujipongeze maana sisi ndio tunaouza wachezaji nje kama kuna anaebisha alete ushahidi mbele ya umma sasa kazi kwenu timu ya chama mifano mmeiona bado tu hamjajifunza mtajifunza lini?

    ReplyDelete
  11. biashara ni kununua na kuuza acha mshikaji asogee mbele hiyo ndio simba

    ReplyDelete