Search This Blog

Thursday, June 14, 2012

MIAKA 10 ILIYOPITA YA USHUJAA WA IKER CASILLAS ULIANZIA KWENYE MECHI DHID YA IRELAND - HISTORIA KUJIRUDIA USIKU HUU?


Iker Casillas, Spain
Iker Casillas sasa hivi anacheza kwenye michuano ya sita mikubwa ya kimataifa akiwa na Spain. Golikipa wa Real Madrid amekuwa akitajwa ni mmoja ya magolikipa bora duniani tangu alipocheza mechi yake ya kwanza ya kimataifa chini ya Jose Antonio Camacho mwaka 2002, na tangu wakati huo amekuwa hana mpizani kwenye milingoti mitatu ya Spain.

Na ilikuwa miaka 10 iliyopita, dhidi ya wapinzani wao watakaocheza nao leo usiku Ireland, siku ambayo Casillas aliweka jiwe la msingi la kujenga historia yake ndani Spain na kwenye soka kwa ujumla, aliokoa penati tatu kwenye raundi ya pili ya michuano ya kombe la dunia na kuipeleka Spain kwenye robo fainali.

Hivyo katika kuelekea mchezo wa leo usiku dhidi ya Ireland, ebu tuangalie historia ya kishujaa ya Iker Casillas ilivyojengwa kwa matukio makubwa.

2002 WORLD CUP: SPAIN 1-1 IRELAND: THE PENALTY LEGEND BEGINS

Michuano ya World Cup ya Japan na Korea ndio yalikuwa jiwe la kwanza la msingi wa ushujaa wa Casillas kwenye timu ya taifa. Kipa wa Madrid, alikuwa chaguo la pili nyuma ya Santiago Canizares, Iker alipata nafasi ya kucheza baada ya golikipa Santiago kuumia. Casillas, ambaye mwezi mmoja kabla alicheza kwa mafanikio na kuisadia Madrid kushinda kombe la ulaya dhidi ya Bayern Leverkusen baada ya kumbadili majeruhi na Cesar Sanchez katika hatua za mwisho, ambaye pia Casillas alimbadili kwenye kikosi cha Spain baada ya kuumia.

Kwenye hatua ya 16, Spain wakakutana na Ireland na pamoja na kuongoza kwa goli la mapema la Fernando Morientes, lakini mechi hiyo ilikuwa ngumu sana. Casillas aliiokoa Spain kwenye kipindi cha pili baada ya kuokoa penati ya Ian Harte, lakini hakuweza kumzuia Robbie Keane kusawazisha na kupelekea mechi kwenda mpaka kwenye mikwaju ya penati.

Na Casillas alikuwa shujaa tena, akiokoa penati za David Connolly na Kevin Kilbane na kuipeleka Spain hatua ya mbele.

EURO 2008: SPAIN 0-0 ITALY: REWRITING HISTORY

Miaka 6 baadae, Casillas akaisadia Le Roja kuandika historia nyingine kwenye Euro 2008, akiwa nahodha kwa upande Spain kwenye michuano hiyo, wakafanikiwa kupata mafanikio kwa mara ya kwanza tangu mwaka 1964. Na golikipa wa Real Madrid alicheza vizuri sana, akiokoa penati ya Di Natale na Daniele De Rossi kwenye mikwaju ya penati kufuatia dakika 120 kushindwa kutoa mshindi kwenye mchezo wa robo fainali dhidi ya Italia.

2010 WORLD CUP: SPAIN 1-0 PARAGUAY: TAKING REINA'S ADVICE

Wakiwa njiani kwenda kubeba kombe la dunia mwaka 2010 nchini South Africa, Spain wakakutana na Paraguay kwenye robo fainali. Kikosi cha Paraguay kikiongozwa na Gerardo Martino walijipanga vizuri hasa kwenye nafasi ya kiungo na kuwafanya wachezaji wa Vicente Del Bosque kushindwa kucheza vizuri. Gerard Pique akacheza rafu kwenye box na kusababisha penati kwenye kipindi cha pili na kusababisha safari ya La Roja kwenda nusu fainali kutia mashaka.

Pepe Reina alijua kabisa wapi Oscar Cordozo angepiga mpira wa penati kick, baada ya kuwa tayari alikuwa ameshakutana na mparaguay huyo kwenye mechi kati ya Liverpool na Benfica na Cordozo kumfunga kwa penati, Reina akampa ushauri Casillas jinsi amjuavyo Cordozo na penati zake, kwa bahati nzuri Iker akafuata ushauri wa kipa mwenzake na kufanikiwa kuudaka mpira wa Cordozo na kuisadia timu ya kufika hatua iliyofuatia.

2010 WORLD CUP: SPAIN 1-0 NETHERLANDS: CASILLAS TWO; ROBBEN NIL

Katika dakika ya 61 ya mchezo wa fainali ya kombe la dunia, Arjen Robben aliiichambua kama karanga safu ya ulinzi ya Spain na kisha akaingia mpaka kwenye eneo la penati na kukutana uso kwa uso na Casillas, ambaye alizuia mpira uliokuwa ukitinga nyavuni kwa mguu.

Na kwenye dakika ya 90 ya mchezo, wawili hao wakajikuta wakikutana tena ana kwa ana. Matokeo yake yalikuwa yale yale: Robben akanyimwa bao tena na Casillas na mpira ukaenda kwenye muda wa  nyongeza kwa dakika 30, ambapo Andres Iniesta aliibuka shujaa kwa kufunga bao pekee na la ushindi kwa Spain.

Lakini tungekuwa tunaongea mengine bila kuwepo kwa shujaa Casillas.

No comments:

Post a Comment