Search This Blog

Friday, February 10, 2012

ADRIANO AFUNGIWA HOTELINI NA KLABU YAKE KWA AJILI YA DIET YA KUPUNGUZA UNENE.


BONGE ADRIANO AKISHANGILIA BAADA YA KUFUNGA GOLI KATIKA MECHI MOJAWAPO ALIZOCHEZA.
Alikuwa mshambuliaji wa kutisha enzi zake, na mshindi wa mara nne wa Scudetto akiwa na Inter Milan, Adriano Leite Ribeiro alikuwa moja ya washambuliaji walionekana kuwa wamekuja kumrithi El Phenomena Ronaldo De Lima.

Kama isingekuwa kwa kupenda kwake maisha ya starehe na kujirusha, angeweza leo hii kuwa amekaribia au kupita mafanikio ya wachezaji wenzie kama Ronaldo au Ronaldinho, lakini mambo yamezidi kumuendea kombo Adriano na akaamua kurudi kucheza nyumbani kwao Brazil.

Kibonge Ronaldo amkaribisha Adriano baada ya kusajiliwa na timu hiyo last season.
Sasa akiwa nyumbani @Corinthians, uzito wa mwili wa Adriano umekuwa kikwazo na tatizo kubwa kwa klabu yake, sasa wameamua kumfungia mchezaji huyo katika chumba cha hotel na kumpa chakula ambacho kitakuwa kimepitishwa na daktari wa timu hiyo.

Msemaji wa Corinthians Fabio Mahseredjian alisema: “Akiwa hotelini tumeweza zaidi katika kum-control. Anajua tunafanya haya yote kwa ajili yake ili aweze kufanya vizuri. Sisi sote tumejitolea kufanya haya, lakini yote inategemea nay eye. Kupunguza uzito kunawezekana kwa kufanya diet nzuri tu, huwezi kupunguza uzito kwa kufanya mazoezi pekee.

 

KALI YA LEO: ETI JAMANI HUYU ALIDHAMIRIA KUFUNGA HIVI?

HUYU NDIYE MSHABIKI WA KWELI WA MANCHESTER CITY - KAANZA KUISHABIKIA MWAKA 1933




ANAITWA CECILIA HODKIN.

Thursday, February 9, 2012

WATAKAOTHIRIKA NA WATAKAOFAIDIKA NA KUONDOKA KWA FABIO CAPELLO KATIKA KIKOSI CHA ENGLAND






Fabio Capello alijiuzulu ukocha wa England jana, baada ya kufanya mazungumzo makali dhidi ya FA juu ya chama hicho cha soka kumvua unahodha John Terry.
FA walimnyang’anya kitambaa cha unahodha mlinzi wa Chelsea kutokana na kesi ya ubaguzi wa maneno ya ubaguzi dhidi ya Anton Ferdinand.

Capello aliamua kwenda hadharani na kuuponda uamuzi wa FA, na kwa haraka aliitwa na mwenyekiti wa FA David Bernstein @Wembley Stadium.
Baada ya mkutano huo ilitangazwa kwamba FA imekubali uamuzi wa Capello kujiuzulu.
Maamuzi ya kujiuzulu kwa Fabio Capello yameacha majeruhi kwa baadhi ya watu huku wengine wakiwa  na furaha tupu.
Sasa tuangalia watu waliothirika na waliofaidika na uamuzi wa Fabio Capello.

ALIYEATHIRIKA: JOHN TERRY
Fabio Capello alikuwa anamuona John Terry kama kiongozi asilia katika timu yake, na maoni yake kupitia television ya Italia yalionyesha dhahiri kuwa kesi ya ubaguzi inayomkabili Terry haikubadili chochote kuhusu anavyomchukulia Nahodha huyo wa Chelsea.
Sasa Capello akiwa hayupo kwenye picha, kuna wasiwasi mkubwa kwamba kocha ajaye anaweza asiwe na mtazamo kama wa Capello kuhusu Terry.
Pia anaweza asimuite kabisa Terry katika kikosi cha England, akizingatia hali inavyoweza kuwa mbaya katika dressing room ya Three Lions. Uwepo wa John Terry unaweza kuleta hali ya kutokuwepo kwa umoja na mshikamano.
Hivyo John Terry anakosa mtu wa kumtetea kutokana na kuondoka kwa Capello – Ameathirika.


ALIYEFAIDIKA: HARRY REDKNAPP
Bila shaka Harry Redknapp ndio chaguo la watu wengi katika mchakato wa kumpata mrithi wa Capello na kuna asilimia kubwa anawza akawa ndiye kocha ajaye wa England.
Hali imekuwepo siku zote, lakini sasa hata baadhi ya wachezaji wa sasa na zamani na makocha kama Wayne Rooney,  Martin Oneill, Gazza, Rio Ferdinand, Gary Lineker wamekuwa wamkitaja Redknapp kama chaguo sahihi la nafasi ya ukocha wa England.
Harry Redknapp amefaidika na kuondoka kwa Capello.


WALIOTHIRIKA: CHAMA CHA SOKA ENGLAND – FA
FA walikuwa wakimlipa Fabio Capello £6million kwa mwaka kwa kuiongoza England, na kiukweli Capello hakufanya jambo lolote la kukumbukwa katika timu hiyo.
Walipata nafasi ya kucheza kombe la dunia 2010, lakini England walienda South Africa na kufanya madudu.

Capello pia aliiongoza England kupata nafasi ya EURO 2012, lakini matumaini ya kufanya vizuri katika michuano hiyo madogo mno.

Japokuwa hakufanya vibaya sana, lakini matokeo ya World Cup 2010 yanaficha mazuri yote ya wakati wa utawala wake.
Kwa fedha aliyokuwa akilipwa iliyomfanya kuwa kocha anayelipwa zaidi ulimwenguni na mambo aliyoifanyia England – FA wamepata hasara kubwa.


WALIOFAIDIKA: MEDIA
Ni fair kusema kwamba vyombo vya habari vya Uingereza havikuwa na mapenzi na Capello.
Pia ni sawa kusema vita yao au mapmbano yao ya kuona muingereza Harry Redknapp anakuwa manager mpya wa England karibia inaanza kufanikiwa kwa kuwa watapata kazi rahisi zaidi kufanya coverage ya matukio ya timu ya taifa.

Pia waandishi wa habari wa England wanakaribia kufanikisha adhma yao ya kumuweka kocha raia wa Uingereza kuwa kiongozi wa benchi la ufundi la England.

Pia kikubwa zaidi kwa media, kuondoka kwa Capello kutauuza sana habari zao, kwa kuwa watu wengi watakuwa wakisubiri kupitia vyombo vya habari tangazo la nani atakuwa kocha mpya.
Kuondoka kwa Fabio Capello ni ushindi kwa vyombo vya habari vya England.


WALIOTHIRIKA: TOTTENHAM HOTSPUR?
Mashabikiw wa Spurs siku zote walikuwa wanajua huu wakati unakuja. Harry Redknapp amekuwa mwokozi wao katika misimu ya hivi karibuni, ikiirudisha Spurs katika kushindana na vilabu vikubwa na kuleta matumaini mapya ya makombe @White Hart Lane.

Kama atapewa ukocha wa England, kiukweli Spurs wataathirika. Kocha mpya kwao anaweza asiwe na ushawishi wa kuwazuia Gareth Bale, Van Der Vaart na Luka Modric kubaki London ya kaskazini.
Kama ikiwa Redknapp atapewa jukumu la ukocha wa England, at least mashabiki wa Spurs wataomba apewe option la kumalizia kwanza msimu huu huku akiwa kocha England mpaka utakapoisha msimu wa EPL 2011-12.

SNEIJDER: INGEKUJA OFA JANUARY NINGEWEZA KUJIUNGA NA UNITED


Wesley Sneijder amesema angaweza kujiunga na Manchester United kama Sir Alex Ferguson angetuma ofa katika dirisha la usajili la January.

Kiungo mchezeshaji huyo wa Inter Milan alikuwa moja ya top targets wa United katika harakati za kumrithi Paul Scholes  kipindi cha kiangazi kilichopita, lakini hitaji lake la mshahara wa £250,000 lilikuwa kikwazo kwa mabingwa hao wa English premier league.

Sneijder, 27, yupo katika mkataba na Inter unaoishia June 2015 lakini anakiri ana wakati mgumu juu ya future yake nchini Italy baada ya kuwa wakati mgumu katika nusu ya kwanza ya msimu.

Sneijder amekiri hakujawahi kuwa na mazungumzi kati yake na Manchester United, lakini akatoa ishara kama kulikuwa na interest kutoka Old Trafford kuhitaji huduma zake.

“Hakujawahi kuwa na mazungumzo ya serious na United. Naangalia kila kitu, mimi sio kipofu, lakini hata sasa bado hakuna mawasiliano rasmi kati yangu na United.

“Nina furaha hapa Inter, lakini tutajua baadae kitakachotokea. Kwa sasa sina mazungumzo wala mawasiliano na klabu yoyote. Kama United au timu yoyote ambayo ingenivutia wangeleta ofa katika siku ya mwisho ya usajili, labda ningeweza kuondoka Inter.
“Ukweli ni kwamba najisikia kama nipo nyumbani hapa Inter, lakini sifahamu wapi nitacheza msimu ujao.”

MMEMUONA BABA FERGIE?

KIPRE BOLOU APATA ITC

Mchezaji wetu Kipre Bolou Michael Wilfried (pichani) ambaye ITC yake ilichelewa kutua nchini imewasili leo. Hivyo basi Kipre Bolou atashuka dimbani kwa mara ya kwanza kwenye mechi za ligi kuu dhidi ya Simba SC jumamosi hii. Shukrani kwa wote waliofanikisha mchakato huu hasa watu wa FIFA, TFF na Chama cha soka cha Ivory Coast

KUNA TOFAUTI GANI KWENYE HIZI PICHA!

                                                          GIGGS
                                                                   SIR ALEX FERGUSON


                                                                         SHAFFIH
                                                                        BECKHAM
                                                                  ROONEY

BREAKING NEWS! KIKOSI CHA MORO UTD KIMENUSURIKA KWENYE AJALI.


kikosi cha Moro Utd kimepata ajali katika eneo la salanda mkoani Singida wakati kikielekea mkoani mwanza kucheza mchezo wa ligi kuu dhidi ya Toto Africans hapo siku ya Jumamosi.
taarifa zilizotufikia hivi punde hakuna aliyeumia kwenye ajali hiyo.

MAONI YANGU:HARAKATI ZA KLABU YA YANGA KATIKA KUTAFUTA “WIMBO WA YANGA

Siku niliyosikia Yanga wanaanza mchakato wa kutafuta WIMBO YA YANGA nilifurahi sana nikajua kwa sasa mabadiliko ya kimawazo ya viongozi wetu wa klabu yanaanza kuonekana,kwa hilo naomba niwapongeze kwa hatua hiyo ambayo klabu yetu kongwe kwa miaka mingi ilishindwa kuwa na WIMBO YA YANGA.Pia niwapongeze Clouds Media kwa kujitahidi kutangaza na kutoa msukumo kwa wadau wote katika kuitikia mwito huo wa Klabu katika harakati za kutafuta WIMBO WA YANGA.Hadi sasa nimeweza kusikiliza Nyimbo zisizo pungua 4 kupitia Radio ya Clouds FM,kwa uwezo wangu “Mdogo” wa uchambuzi nimegundua kuwa nyimbo hizo zote zimetengenezwa si kwa madhumuni yaKuwa WIMBO WA YANGA bali wamefanikiwa kutengeneza NYIMBO ZA KUISHANGILIA YANGA.Tuangalie mfano wa WIMBO wa MANCHESTER UNITED,wimbo umepangwa ukapangika,unatoa ujumbe uliokusudiwa,mawazo yalioko ndani yanaeleweka,lugha iliyotumika pia ni lugha rasmi.Kati ya Nyimbo hizo nne(Nilizo sikiliza hadi sasa),huwezi kuyaona mambo tajwa hapo juu,WIMBO WA YANGA,huwezi kutumia lugha ambayo hata mpenzi wa Yanga haielewi,huwezi taja majina ya watu ovyo ovyo(kwa hakika hayahitajiki,wimbo ya Yanga inabidi uwe umepangika kimawazo na kimantiki,mtiririko wake ni lazima uwe unaotoa mawazo/ujumbe makini,wimbo inabidi uwe na mtundo unaoleweka na sio wa kuiga toka nyimbo fulani fulani maarufu za ulaya au Marekani.Wito wangu kwa uongozi wa YANGA,ni kuwa makini sana katika mchakato huu ili kupata nyimbo bora.Kwa watunzi wa Nyimbo,naomba mtambue YANGA inatafuta WIMBO YA YANGA(YANGA ANTHEM) na sio WIMBO YA KUISHANGILIA YANGA.Asante

GERVINHO AIPELEKA IVORY COAST FAINALI YA MATAIFA HURU YA AFRIKA

ASAMOAH GYAN AKOSA TENA PENATI - ZAMBIA WAKIITOA GHANA MATAIFA YA AFRIKA

FABREGAS AIPELEKA BARCELONA FAINALI

MAKOCHA WENGINE WATANO WANAOPEWA NAFASI YA KUMRITHI CAPELLO NYUMA YA HARRY REDKNAPP




JOSE MOURINHO
Amekuwa na mafanikio kila anapoenda. Sasa yupo karibuni kuweka rekodi ya kuwa kocha wa kwanza kushinda mataji katika nchi za Ureno, England, Italy na Spain. Anaweza kufanya vizuri katika level ya kimataifa.




MARTIN O’NEILL
Wengi wanaamini staili yake inafaa zaidi kwa level ya kimataifa. Wachezaji wanapenda kumtumikia. Pia utaifa wake (Englishman) unampa sifa nyingine dhidi ya wengine.





STUART PEARCE
Icon wa soka la Uingereza ambaye ana sifa zote za kocha kiingereza. Ni boss wa kikosi cha England chini miaka 21 na pia atakuwa manager wa kikosi cha Great Britain kitachoshiriki katika michuano ya Olympics. Kuwa mkuu wa Three lions itakuwa step nyingine kwake.



ROY HODGSON

Huyu ndio ana CV kubwa kuliko amkocha wote wa kiingereza wanaopewa nafasi ya kuchukua nafasi ya Capello. Ameshafundisha katika klabu kubwa kama Liverpool, na Inter Milan. Pia katika ngazi za kimataifa ameshafundisha Switzerland, UAE na Finland, hivyo ana experience kubwa ya timu za taifa.





GUUS HIDDINK
Ana CV nzuri sana: Holland, South Korea, Australia, Russia na Uturuki – timu hizi zote alipata mafanikio na anaonekana kuwa sifa kuliko wengine wote wanaopewa nafasi.

STUART PEARCE NA SIR TREVOR BROOKING KUIONGOZA ENGLAND KWA MUDA



                         

Stuart Pearce of England
Stuart Pearce the England coach




































Mara ya mwisho wakati Uholanzi wamecheza @Wembley, Staurt Pearce alikuwa moja ya wachezaji waliocheza vizuri sana katika mechi ya kukumbukwa sana.

Miaka 16 kutoka siku ya ushindi wa 4-1 katika Euro 96, sasa Pearce anajiandaa kwenda Udachi pamoja na Sir Trevor Brooking kwa jaili ya kuoingoza England amabayo haina kocha kwa sasa katika mechi ya kirafiki dhidi ya Uholanzi on February 29.

Kutoka timu iliyokuwa na wachezaji akama Alan Shearer, Tony Adams, Paul Ince, Gareth Southgate na Gary Neville, nani ambaye angeweza kutabiri leo hii beki huyu wa kushoto angekuwa anachagua kikosi cha wakubwa England.?

Pearce anategemewa kupewa jukumu la muda kuweza kuziba nafasi ya Capello aliyejiuzulu, huku akisaidiwa na Trevor Brooking.

MANCHESTER UNITED WAZIDI KUNYANYASWA NA BARCELONA - RIPOTI YA DELOITTE YAONYESHWA IMEPITWA KIMAPATO MSIMU WA 2010/11


Ripoti mpya ya timu tajiri duniani imetoka na inavyoonekana Manchester United wanazidi kupotezwa na wapinzani wake wa muda mrefu klabu mbili za Spain Real Madrid na Barcelona.

Ripoti hiyo inayotolewa na kampuni ya Deloitte inasema ingawa mapato ya United yanazidi kukua lakini bado wmeshindwa kufikia mapato ya Real wala Barca, ambao wana faida ya kufanya mazungumzo ya haki zao za matangazo ya TV.


Kushindwa kwa United kupita katika hatua ya makundi ya Champions league msimu huu kutasababisha kuongezeka kwa gap kubwa kati yao na watoto wa kispain mwaka ujao, Deloitte wamesema.

Real Madrid wamebaki kuwa namba 1 katika ligi ya timu zenye mapato makubwa katika msimu wa 2010/2011 wakiwa wameingiza £438million, huku Barcelona wakiwa wapili wakiweka kibindoni £398million na Manchester United wakishika nafasi ya 3 wakiingiza £349million 

Bayern Munich wemakata nafasi ya nne, Arsenal wa 5, Chelsea wamebaki nafasi ya 6, AC Milan wapo nafasi ya 8,  Liverpool wameshuka hadi nafasi 9 mbele ya Inter Milan, na taarifa zinasema Majogoo wa jiji wataondoka kabisa Top 10 ikiwa watashindwa kurudi katika michuano ya ulaya.

Tottenham wapo nafasi ya 11, mbele ya Manchester City washukuru mapato ya champions league msimu uliopita, City wanategemewa kuingia katika top 10 msimu ujao kutokana na tu na udhamini wa Etihad stadium wenye thamani ya £400million.

ROONEY, GAZZA, WILSHARE, SMITH, NA WACHEZAJI WENGINE WATOA MAONI YAO NANI ANAFAA KUWA MRITHI WA CAPELLO





Masaa machache baada ya Fabio Capello kujiuzulu ukocha wa Engkand, mshambuliaji tegemeo wa timu hiyo Wayne Rooney amesema mtu sahihi kupewa kazi hiyo na kuziba nafasi ya Capello ni kocha wa Tottenham Hotspur Harry Redknapp.

Capello alijiuzulu jana usiku baada ya kukutana na FA at Wembley.
Na Rooney aliutumia ukurasa wake wa mtandao wa kijamii wa Twitter kuongeza mwangi wa watu wanaomtaja Redknapp kama mtu sahihi wa kuchukua jukumu la ukocha wa England.

Harry Redknapp mtu anayepigiwa chapuo na wachezaji wengi kuchukua jukumu la ukocha wa England
Rooney aliandika: “Capello amejiuzulu. Mtu mzuri na kocha wa kiwango cha juu. Anayepaswa kumbadili inabidi awe muingereza. Kwangu mimi ningependa Harry Redknapp.”

Lakini mchezaji wa zamani wa United Roy Keane amesema haikuwa sahihi kwa Rooney kusema yeye anamtaka nani. “Wayne inabidi ajiondoe katika hili. Hakufanya la maana wakati Capello akiwa kocha. Pia nimeshangazwa sana na uamuzi wa Capello sikuwa nikitegemea hili kutokea haraka hivi. Harry Redknapp atakuwa akipewa nafasi kubwa sana ya kuchukua jukumu hili, na nina uhakika yeye ndio chaguo la washabiki.

Jack Wilshare nae hakukosa la kusema juu ya uamuzi wa Capello: “Nimeshutushwana habari za Fabio Capello …….. ana ujasiri sana niwe mkweli, alinipa nafasi ya kucheza na akaniamini. Asante Mr. Capello! #Kocha Mkubwa.”

Legend wa England pia nae alitoa maoni yake juu ya nani anafaa kuchukua jukumu la ukocha wa timu ya taifa. “Harry Redknapp anafaa kuwa kocha wa England, ni kocha wa aina ya a day-to-day manager, anapenda kufanya kazi kila siku. Nimeshaongea nae kwa mara kadhaa na nimegundua ni mtu mzuri sana, kocha mzuri na kila anachofanya ni kizuri.
“Nafikiri mtu ambaye anastahili zaidi kwa sasa ni Harry, ni chaguo la kila mtu, lakini sidhani kama Spurs watakubali kumuachia. Huyu ni kiunganishi cha wachezaji. Anapendwa sana na wachezaji, na hilo linaleta umoja katika timu na amethibitisha yote haya katika klabu aliyokuwa. Yupo kama Terry Venables na anasema kama FA watamkosa Harry, Venables anastahili nafasi nyingine.”

Rio Ferdinand yeye amesema: “ So Capello amejiuzulu………..nini sasa…..”

Alan Smith alisema: “Tulifahamu hakuwa na furaha juu ya suala la John Terry na alitoa sababu zake, lakini sikutegemea angejiuzulu.

Wednesday, February 8, 2012

BREAKING NEWS! FABIO CAPELLO AMEJIUZULU UKOCHA WA ENGLAND

Aliyekua kocha wa England amejiuzulu wadhifa huo kutokana na kitendo cha chama cha soka cha nchi hiyo kumvua unaodha beki John Terry!

Taarifa zaidi zitafuata!!!

YANGA YAITANDIKA 3-1 MTIBWA SUGAR - YAISHUSHA SIMBA KILELENI


Kiungo wa Yanga Niyonzima akichuana na mabeki wa Mtibwa.
Mabingwa wa Tanzania bara na Afrika mashariki na kati Dar Young African leo wameitiwa shubiri miwa ya Mtibwa Sugar katika muendelezo wa ligi kuu ya Vodacom premier league.

Katika mchezo huo uliofanyika katika uwanja wa Taifa jijini DSM, Yanga ndio walikuwa wa kwanza kuziona nyavu za Mtibwa katika dakika ya 75 kupitia kwa Kenneth Asamoah, kabla ya Said Sued wa Mtibwa kujifunga goli na kuwafanya Yanga kuwa mbele kwa goli 2-0. Zikiwa zimebakia dakika 2 kabla ya mchezo kumalizika Shamte Ally aliongeza goli la 3 kabla ya Mtibwa kupata bao la kufutia machozi hivyo kupelekea matokeo ya mwisho kusomeka Yanga 3-1 Mtibwa.



Kwa matokeo hayo Yanga sasa imepanda hadi kileleni mwa msimamo na kuwapita mahasimu wao Simba kutokana na idadi kubwa ya mabao ya kufunga.

MSIMAMO WA VPL.
Kwenye Mabano Idadi ya Mechi Zilizochezwa.
1. Yanga (16) 34
2. Simba SC (16) 34
3. Azam FC (16) 32
4. JKT Oljoro (16) 26
5. Mtibwa Sugar (16) 22
6. Kagera Sugar (16) 20
7. JKT Ruvu (16) 20
8. Ruvu Shooting (16) 18
9. African Lyon (15) 17
10. Coastal Union (16) 17
11. Moro United (16) 15
12. Villa Squad (16) 13
13. Toto Africa (15) 13
14. Polisi Dodoma (16) 13



Mashabiki wa Yanga wakishangilia ushindi dhidi ya Mtibwa.

SUAREZ AKATAA KUMUOMBA EVRA MSAMAHA ASEMA KELELE ZA MASHABIKI WA MAN U J,MOSI ZITAMPA KASI YA KUCHEZA ZAIDI


Luis Suarez bado ameendelea kukataa kuomba samahani kwa Patrice Evra kwa kutoa maneno ya ubaguzi dhidi ya mfaransa huyo.

Straika huyo wa Liverpool alifungiwa mechi 8 baada ya FA kumkuta na hatia ya kumtolea maneno ya ubaguzi Evra, lakini Suarez, ambaye jumamosi hii atakutana na uso kwa uso na Evra katika mfululizo wa EPL, amesema yaliyotokea kiwanjani yalibidi yabaki dimbani.

Alisema: “Sikuwa nimeghafirika hata kidog. Nilijua nilichofanya na natambua kuna sheria inayosema ‘kinachotokea uwanjani kinabidi kibaki uwanjani na huo ndio mwisho wa stori.”

Suarez akiongea na na Radio Sport 890 ya Uruguay, alisema: “Najua dhidi ya Manchester United kutakuwa na wakati mgumu kwa sababu nitakutana na Evra, lakini sasa hivi nimekuwa mzoefu na kelele na matusi ya mashabiki dhidi yangu. Natumai hakuna kitu cha ajabu kitakachotokea.

“Nafahamu fika kwamba mashabiki wa United watajaribu kunifanya nipoteze umakini kwenye mchezo kwa kunizomea, lakini nawaambia hakuna kitakachonizuia kucheza vizuri na kelele zao zinaweza kunipa mwamko zaidi wa kucheza vizuri.”

MTAMBUE MTOTO WA BEBETO ALIYEMSHANGILIA WAKATI WA WORLD CUP 1994





Ni moja kati ya tukio la kukumbukwa sana katika michuano ya kombe la dunia katika miaka ya karibuni. Ni moja ya aina za ushangiliaji unaotumika sana na wachezaji wanaokaribia kupata watoto katika kipindi husika.



Kumbuka hii, Bebeto alikuwa amefunga goli ambalo liliwaeka Brazil mguu moja ndani ya hatua ya robo fainali dhidi ya Uholanzi, Bebeto akifuata na wenzake Romario na Mazinho walienda mpaka kwenye chaki na wakaanza kuanza kushangilia kwa mtindo wa kumbembeleza mtoto. Bebeto alikuwa anashangilia namna kwa ajili ya kufurahia kumpata mtoto wake wa kiume Matheus.


Hii ilikuwa miaka 18 iliyopita, katika 1994 World Cup finals, lakini mpaka leo tukio hili lipo katika kumbukumbu za Bebeto.


Mtoto wake Matheus juzi alimkumbusha baba yake tukio la mwaka 1994 baada ya kuingia akitokea benchi katika mechi kati ya Flamengo.


Bebeto ambaye kwa sasa ni mwanasiasa wa chama cha Democratic Labour aliungana na mashabiki wapatao 40,000 katika uwanja Engenhao pamoja na mashabiki wa Flamengo.

Mtheus Bebeto kushoto akiwa na mchezaji mwenzie wa Flamengo.




“Kipindi nilipomuona Matheus akiingia uwanjani, kumbukumbu za tukio langu la 1994 zilirudi tena kichwani mwangu. Ilikuwa kama movie inachezwa kichwani mwangu, nikawa nakumbuka namna nilivyofunga goli lile dhidi ya Holland na mwanangu Matheus akiwa na siku mbili tu tangu azaliwe. Nilikuwa natokwa na machozi ya furaha kumuona mwanangu akicheza soka tena katika klabu ambayo mimi mwenyewe nilianzia kucheza.”

BREAKING NEWS: HARRY REDKNAPP ASHINDA KESI DHIDI YA UKWEPAJI KODI

Manager wa Tottenham Hotspur Harry Redknapp ameshinda kesi iliyokuwa ikamkabili ya kukwepa kodi nchini Uingereza.

Kocha huyo wa Spurs ambaye anapigiwa chapuo la kuwa mrithi wa Fabio Capello katika kikosi cha ‘Three Lions’ amefutiwa mashtaka yote yaliyokuwa yakimkabili.

Redknapp alikuwa anatuhumiwa kukwepa kodi ya kiasi cha fedha cha £189,000 kilichokutwa katika akaunti moja iliyopo Monaco-Ufaransa.

BAADA YA KUVULIWA UNAHODHA, TERRY SASA KUTEMWA NA WADHAMINI WAKE.


John Terry ameendelea kupata mikosi kutokana na kesi yake ya maneno ya ubaguzi dhidi ya Anton Ferdinand.

Nahodha huyo wa Chelsea alivuliwa unahodha wa England pamoja na suala hilo kupingwa na Fabio Capello baada ya kufunguliwa mashtaka ya kumtolea maneno ya kibaguzi mlinzi wa QPR Anton Ferdinand wakati wa mechi kati ya Chelsea na QPR @Loftus Road.

Sasa mlinzi huyo mwenye miaka 31 baada ya kuvuliwa unahodha wa England, balaa jingine limemuangukia baada ya wadhamini wa viatu anavyovaa Umbro kuamua kujitoa kumdhamni. Umbro wamekuwa na Terry tangu akiwa na miaka 18.

Tangu Desemba mwaka jana zilitoka taarifa kuwa UMBRO walikuwa wamemuondoa Terry katika matangazo yao na kwamba Terry alikuwa tayari ameanza kutafuta sponsor mpya kwa kuwa mkataba wake na kampuni ya Umbro ulikuwa ukielekea mwishoni na hakukuwa na dalili za kupata dili mpya.

WAMBURA AUSIMAMISHA UCHAGUZI WA DRFA.



KUTOKA-
MICHAEL RICHARD WAMBURA
P.O. BOX 22557,
TEL. 0713/0754/O787 326 485
DAR ES SALAAM.
February 7, 2012


KWENDA-
MWENYEKITI,
KAMATI YA UCHAGUZI ,
SHIRIKISHO LA MPIRA WA MIGUU TANZANIA (TFF)


YAH: KUSIMAMISHA UCHAGUZI WA CHAMA CHA MPIRA WA MIGUU CHA DAR-ES-SALAAM(DRFA) ULIOPANGWA KUFANYIKA 18/3/2012


MR MICHAEL RICHARD WAMBURA (Mlalamikaji), nimelazimika kuleta maombi na malalamiko yangu mbele yako na kamati yako kuhusiana na uchaguzi tajwa hapo juu wa DRFA kutokana na uvunjifu wa kanuni, maagizo na Katiba ya TFF sambamba na katiba ya DRFA na sheria za nchi katika mchakato mzima wa kuelekea katika uchaguzi huo kama ifuatavyo.
1. Uundwaji wa kamati ya chaguzi ya DRFA umevunja kanuni ya uchaguzi wa wanachama wa TFF (TFF MEMEBERS STANDARD ELECTROL CODE) Ibara ya 3(2) inakataza mtu mmoja kuwa mjumbe wa kamati mbili za uchaguzi za wanachama wa TFF au wanachama washiriki wa TFF “The members of the Committee shall under no circumstances be member of the executive body of TFF or Executive body of the Association or Executive of other TFF member Association or the Elections Committee of the other member association of TFF or Executive body /Elections Committee of a subordinate” kwa kuwa Mwenyekiti wa kamati ya uchaguzi ya DRFA Muidin Ndolanga Pia Mwenyekiti wa kamati ya Uchaguzi ya FRAT(taifa ambao wote ni wanachama wa TFF basi uhalali wake wa kuwa m/kiti wa kamati ya Uchaguzi wa DRFA unakuwa haupo kwa kuwa unavunja kanuni za uchaguzi , aidha Nd Damas Ndumbaro ambae pia ni Mwenyekiti wa kamati ya uchaguzi wa Simba, Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Uchaguzi ya DRFA na katibu wa Kamati ya uchaguzi wa FRAT, anapoteza sifa za kuwa Mjumbe wa kamati ya uchaguzi ya DRFA, kwa maana hiyo naomba tamko la kuwa mchakato mzima wa uchaguzi ufutwe na kuanza upya kwa kuwa haukufuata taratibu na kanuni husika .
2. Katiba ya DRFA toleo la 2008 ibara ya 1(6) inatamka kuwa “DRFA itaheshimu Katiba, Kanuni Maagizo na Maamuzi ya TFF na kuhakikisha kuwa zinaheshimiwa na wanachama wake” TFF kupitia barua yake kumbukumbu TFF/ADM/EC/36 ya tarehe 22/7/2011 yenye kichwa cha habari “ Katiba za Wanachama na Wanachama wao” kwenda kwa makatibu ambapo iliagiza kufanyika mabadiliko katiba zao ili ziendane kikamilifu na katiba ya mfano ya TFF aidha TFF kupitia barua yake ya tarehe 12/12/2012 yenye kumbukumbu TFF/TECH?GC11/115 kwenda kwa makatibu wa wilaya ikikumbushia kurekebisha katiba zao ili ziendane na Katiba ya mfano ya TFF, Kwa kuwa Katiba za wanachama wa DRFA na DRFA hazijafanyiwa marekebisho na wahusika ni wazi hawajatekeleza maagizo ya TFF hivyo kwenda kinyume na Katiba ya TFF 12(d)(e) & (n) na Ibara ya 9 ya kanuni za uchaguzi za TFF na Wanachama wake.
3. Kwa kuwa wilaya wanachama wa DRFA hawakufuata kanani za Uchaguzi za TFF na Wanachama wake, kumepelekea baadhi ya viongozi waliochaguliwa kutokuwa na sifa ikiwemo ya Elimu isiyopungua kidato cha Nne ikiambatana na Cheti cha Matokeo kama ilivyoagizwa na TFF katika barua yake kwa wanachama wake na wilaya, kwa kuwa viongozi hao wa wilaya wanakosa sifa ya kuwa viongozi ni wazi pia wanakosa sifa ya kupiga kura katika Uchaguzi wa DRFA, itakumbukwa katika Uchaguzi wa Chama cha mpira Mkoa Mara(FAM) ambapo Mwenyekiti wa Kamati ya Uchaguzi ya TFF alikuwepo ambapo Nd MAGOTI ambaye alikuwa Katibu wa Chama cha mpira Wilaya ya Bunda aliondolewa katika kugombea na hakurusiwa kupiga kura baada ya kuonekana hakuwa na sifa ya kuwa Katibu wa wilaya kutokana na tatizo la Elimu halikadhalika Katibu wa Wilay ya Serengeti Ombeni Magati nae aliondolewa katika kugombea ujumbe wa kamati ya Utendaji na pia hakuruhusiwa kupiga kura na nafasi walizokuwa wanazishikilia kutangazwa kuwa ziko wazi, hivyo ni matumaini yangu hata katika DRFA na wanachama wake mkondo utafuata huo huo.
4. Katiba ya DRFA ibara ya 30(2) inayozungumzia sifa za wagombea “Awe na kiwango cha Elimu cha kidato cha nne au inayoyolingana nayo” hivyo inakinzana na katiba ya mfano na kanuni za uchaguzi za TFF ibara ya 9(2) amboyo ina tamka wazi any person contesting any position “ Must have minimum academic qualification of form Four and holder of a certificate of ordinary Secondary Education” kwa mantiki hiyo katiba hii inazua mgongano sio tu na katiba kanuni na maagizo ya TFF bali hata sheria za nch kwa katika Tanzania hakuna elimu nyingine yoyote inayofanana na ya Kidato cha Nne.
5. Katiba ya DRFA Ibara ya 30(6) “ kiongozi anaemaliza muda wake atakuwa na haki ya kutetea nafasi yake ili mradi awe na afya njema na akili timamu” ibara hii inaukinzani mkubwa na kanuni katiba na maelekezo ya TFF, aidha kanuni hii inatoa taswira ya kuwa kiongozi anaye maliza muda wake hapaswi kuwa na sifa za Msingi kama zilivyo ainaishwa kwenye kanuni za uchaguzi za TFF na wanachama wake Ibara ya 9, aidha , ibara hii inalenga kumruhusu hata mtu aliyeingia madarakani kimakosa kuendelea kugombea nafasi aliyoipata kimakosa hata baada ya kugundua makosa kwa kuwa tu ndie anayemaliza muda wake hivyo ana haki ya kugombea, kipengele hicho kingekuwa na maana kama kingemruhusu mgombea ili mradi awe na sifa za msingi za kugombea.itakumbukwa kwenye uchaguzi wa Klabu ya Simba Mwenyekiti aliyekuwa anamaliza muda wake Mzee Hasan Dalali aliondolewa kugombea kwa sababu ya kukosa sifa ya Elimu ya kidato cha nne huku Mwenykiti wa sasa wa DRFA ndugu Amin (AKA Bakhresa) na Nd Damas Ndumbaru wakiwa wajumbe wa Kamati ya Uchaguzi ya Simba iliyotekeleza na kuzingatia Kanuni za uchaguzi za TFF, aidha Nd A. Bulembo nae aliondolewa kwa vigezo hivyo hivyo katika uchaguzi wa timu Villa Squad ya DSM, kanuni haikuishia hapo iliendelea mpaka kwa timu ya Coastal Union ya Tanga, kwa misingi hiyo ni wazi kamati hii haitafumbia macho kwenye hili la DRFA.
Kwa kuzingatia Maelozo hayo hapo, Ninawasilisha katika maombi ya dharura kama ifuatavyo:


(a) Tamko kuwa Kamati ya Uchaguzi ya DRFA imeundwa bila kufuata kanuni za Uchaguzi za Wanachama wa TFF, hivyo ivunjwe na kuundwa upya.
(b) Tamko kuwa Mchakato mzima wa uchaguzi uanze upya mara baada ya Kamati mpya kuundwa.
(c) Tamko katiba ya DRFA ina kinzana na katiba Kanuni na Maelekezo ya TFF hivyo ifanyiwe marekebisho. yanayostahili kabla ya kuitisha uchaguzi mwingine.
(d) Tamko la kufanyika kwa Uhakiki wa sifa za viongozi wa wanachama na wanachama washiriki wa DRFA ili kuridhia matakwa ya kanuni za uchaguzi na katiba za Mfano za wiliya zilizotolewa na TFF.