Search This Blog

Wednesday, February 8, 2012

YANGA YAITANDIKA 3-1 MTIBWA SUGAR - YAISHUSHA SIMBA KILELENI


Kiungo wa Yanga Niyonzima akichuana na mabeki wa Mtibwa.
Mabingwa wa Tanzania bara na Afrika mashariki na kati Dar Young African leo wameitiwa shubiri miwa ya Mtibwa Sugar katika muendelezo wa ligi kuu ya Vodacom premier league.

Katika mchezo huo uliofanyika katika uwanja wa Taifa jijini DSM, Yanga ndio walikuwa wa kwanza kuziona nyavu za Mtibwa katika dakika ya 75 kupitia kwa Kenneth Asamoah, kabla ya Said Sued wa Mtibwa kujifunga goli na kuwafanya Yanga kuwa mbele kwa goli 2-0. Zikiwa zimebakia dakika 2 kabla ya mchezo kumalizika Shamte Ally aliongeza goli la 3 kabla ya Mtibwa kupata bao la kufutia machozi hivyo kupelekea matokeo ya mwisho kusomeka Yanga 3-1 Mtibwa.



Kwa matokeo hayo Yanga sasa imepanda hadi kileleni mwa msimamo na kuwapita mahasimu wao Simba kutokana na idadi kubwa ya mabao ya kufunga.

MSIMAMO WA VPL.
Kwenye Mabano Idadi ya Mechi Zilizochezwa.
1. Yanga (16) 34
2. Simba SC (16) 34
3. Azam FC (16) 32
4. JKT Oljoro (16) 26
5. Mtibwa Sugar (16) 22
6. Kagera Sugar (16) 20
7. JKT Ruvu (16) 20
8. Ruvu Shooting (16) 18
9. African Lyon (15) 17
10. Coastal Union (16) 17
11. Moro United (16) 15
12. Villa Squad (16) 13
13. Toto Africa (15) 13
14. Polisi Dodoma (16) 13



Mashabiki wa Yanga wakishangilia ushindi dhidi ya Mtibwa.

1 comment:

  1. tuliwatanguliza simba wa maigizo kwa baiskeli ya miti sasa wenyewe tumefika, ngoma ya watoto haikeshi na siku zote ukitaka kuijua Yanga angalia inavoenda kumaliza ligi, simba hesabuni mmeumia

    by JJ

    ReplyDelete