Luis Suarez bado ameendelea kukataa kuomba samahani kwa Patrice Evra kwa kutoa maneno ya ubaguzi dhidi ya mfaransa huyo.
Straika huyo wa Liverpool alifungiwa mechi 8 baada ya FA kumkuta na hatia ya kumtolea maneno ya ubaguzi Evra, lakini Suarez, ambaye jumamosi hii atakutana na uso kwa uso na Evra katika mfululizo wa EPL, amesema yaliyotokea kiwanjani yalibidi yabaki dimbani.
Alisema: “Sikuwa nimeghafirika hata kidog. Nilijua nilichofanya na natambua kuna sheria inayosema ‘kinachotokea uwanjani kinabidi kibaki uwanjani na huo ndio mwisho wa stori.”
Suarez akiongea na na Radio Sport 890 ya Uruguay, alisema: “Najua dhidi ya Manchester United kutakuwa na wakati mgumu kwa sababu nitakutana na Evra, lakini sasa hivi nimekuwa mzoefu na kelele na matusi ya mashabiki dhidi yangu. Natumai hakuna kitu cha ajabu kitakachotokea.
“Nafahamu fika kwamba mashabiki wa United watajaribu kunifanya nipoteze umakini kwenye mchezo kwa kunizomea, lakini nawaambia hakuna kitakachonizuia kucheza vizuri na kelele zao zinaweza kunipa mwamko zaidi wa kucheza vizuri.”
No comments:
Post a Comment