Search This Blog
Thursday, February 9, 2012
MAONI YANGU:HARAKATI ZA KLABU YA YANGA KATIKA KUTAFUTA “WIMBO WA YANGA
Siku niliyosikia Yanga wanaanza mchakato wa kutafuta WIMBO YA YANGA nilifurahi sana nikajua kwa sasa mabadiliko ya kimawazo ya viongozi wetu wa klabu yanaanza kuonekana,kwa hilo naomba niwapongeze kwa hatua hiyo ambayo klabu yetu kongwe kwa miaka mingi ilishindwa kuwa na WIMBO YA YANGA.Pia niwapongeze Clouds Media kwa kujitahidi kutangaza na kutoa msukumo kwa wadau wote katika kuitikia mwito huo wa Klabu katika harakati za kutafuta WIMBO WA YANGA.Hadi sasa nimeweza kusikiliza Nyimbo zisizo pungua 4 kupitia Radio ya Clouds FM,kwa uwezo wangu “Mdogo” wa uchambuzi nimegundua kuwa nyimbo hizo zote zimetengenezwa si kwa madhumuni yaKuwa WIMBO WA YANGA bali wamefanikiwa kutengeneza NYIMBO ZA KUISHANGILIA YANGA.Tuangalie mfano wa WIMBO wa MANCHESTER UNITED,wimbo umepangwa ukapangika,unatoa ujumbe uliokusudiwa,mawazo yalioko ndani yanaeleweka,lugha iliyotumika pia ni lugha rasmi.Kati ya Nyimbo hizo nne(Nilizo sikiliza hadi sasa),huwezi kuyaona mambo tajwa hapo juu,WIMBO WA YANGA,huwezi kutumia lugha ambayo hata mpenzi wa Yanga haielewi,huwezi taja majina ya watu ovyo ovyo(kwa hakika hayahitajiki,wimbo ya Yanga inabidi uwe umepangika kimawazo na kimantiki,mtiririko wake ni lazima uwe unaotoa mawazo/ujumbe makini,wimbo inabidi uwe na mtundo unaoleweka na sio wa kuiga toka nyimbo fulani fulani maarufu za ulaya au Marekani.Wito wangu kwa uongozi wa YANGA,ni kuwa makini sana katika mchakato huu ili kupata nyimbo bora.Kwa watunzi wa Nyimbo,naomba mtambue YANGA inatafuta WIMBO YA YANGA(YANGA ANTHEM) na sio WIMBO YA KUISHANGILIA YANGA.Asante
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
nimekukubali..mfano wimbo hauwezi kutaja majina ya viongozi wala wachezaji kwani hao ni watu wa kupita.. Yanga ni taasisi inabaki daima
ReplyDeleteby JJ
mashabiki wa yanga hua mnanivunja mbavu sana,yaani hamuelewi priority ni zipi katika muda muafaka,mi nilidhani ingekua vema mngekua na hot debate na brainstorming za hatari kuhusu kuinua mapato yenu na kujiendesha kibiashara,lakini saizi mmekomaa na nyimbo utadhani ni kitu cha maana sana,hata shule za awali binafsi zina nyimbo na its not such a bg deal kiivyo.mnaona mambo yametulia kwakua manji kichaa chake hakijampanda,akikasirika tu mnatuma wazee kumbembeleza maisha hayo ya kufedheheshwa mpaka lini wanayanga?
ReplyDeletechela wa dom
sasa chela! Unataka kusema kuwa wanaupeo mdogo wa kufikiri sio? Maana wanakomaa na kutafuta zuku badala ya kukomaa na michakato ya kuwafunga waarabu na mipango mingine endelevu! Kwanza si wanae mzee yusuf kwann asi2nge taarab moja kwa ajili ya yanga na ndo uwe wimbo wa timu! teh teh teh teh teh teh!
ReplyDeletewe chelA sijui kipele mambo ya young africa yana wahusu nini?mnashindwa kuwashauri viongozi wenu waendele kununua mechi mnakali kuijadili yanga haya sasa villa squad wamewatoa nishai subirini kiyovu wanakuja mnafikiri mtaachiwa kama huko zenji mlivyopita kwa miembeni? viva yanga viva tanzania
ReplyDeleteAnonymous 01:25 PM hakuna asiejua kua yanga na simba wananunua mechi isipokua mmoja kakamatwa na mwingine bado 40 zake hazijafika,mi nakwambia wimbo sio ishu hata kidogo cha msingi ni kujipanga kwa mazoezi na maandalizi mengine halafu muwe na sound financial position sio mpo mpo tu
ReplyDeletechela wa dom