Wesley Sneijder amesema angaweza kujiunga na Manchester United kama Sir Alex Ferguson angetuma ofa katika dirisha la usajili la January.
Kiungo mchezeshaji huyo wa Inter Milan alikuwa moja ya top targets wa United katika harakati za kumrithi Paul Scholes kipindi cha kiangazi kilichopita, lakini hitaji lake la mshahara wa £250,000 lilikuwa kikwazo kwa mabingwa hao wa English premier league.
Sneijder, 27, yupo katika mkataba na Inter unaoishia June 2015 lakini anakiri ana wakati mgumu juu ya future yake nchini Italy baada ya kuwa wakati mgumu katika nusu ya kwanza ya msimu.
Sneijder amekiri hakujawahi kuwa na mazungumzi kati yake na Manchester United, lakini akatoa ishara kama kulikuwa na interest kutoka Old Trafford kuhitaji huduma zake.
“Hakujawahi kuwa na mazungumzo ya serious na United. Naangalia kila kitu, mimi sio kipofu, lakini hata sasa bado hakuna mawasiliano rasmi kati yangu na United.
“Nina furaha hapa Inter, lakini tutajua baadae kitakachotokea. Kwa sasa sina mazungumzo wala mawasiliano na klabu yoyote. Kama United au timu yoyote ambayo ingenivutia wangeleta ofa katika siku ya mwisho ya usajili, labda ningeweza kuondoka Inter.
“Ukweli ni kwamba najisikia kama nipo nyumbani hapa Inter, lakini sifahamu wapi nitacheza msimu ujao.”
No comments:
Post a Comment