Search This Blog

Thursday, February 9, 2012

MANCHESTER UNITED WAZIDI KUNYANYASWA NA BARCELONA - RIPOTI YA DELOITTE YAONYESHWA IMEPITWA KIMAPATO MSIMU WA 2010/11


Ripoti mpya ya timu tajiri duniani imetoka na inavyoonekana Manchester United wanazidi kupotezwa na wapinzani wake wa muda mrefu klabu mbili za Spain Real Madrid na Barcelona.

Ripoti hiyo inayotolewa na kampuni ya Deloitte inasema ingawa mapato ya United yanazidi kukua lakini bado wmeshindwa kufikia mapato ya Real wala Barca, ambao wana faida ya kufanya mazungumzo ya haki zao za matangazo ya TV.


Kushindwa kwa United kupita katika hatua ya makundi ya Champions league msimu huu kutasababisha kuongezeka kwa gap kubwa kati yao na watoto wa kispain mwaka ujao, Deloitte wamesema.

Real Madrid wamebaki kuwa namba 1 katika ligi ya timu zenye mapato makubwa katika msimu wa 2010/2011 wakiwa wameingiza £438million, huku Barcelona wakiwa wapili wakiweka kibindoni £398million na Manchester United wakishika nafasi ya 3 wakiingiza £349million 

Bayern Munich wemakata nafasi ya nne, Arsenal wa 5, Chelsea wamebaki nafasi ya 6, AC Milan wapo nafasi ya 8,  Liverpool wameshuka hadi nafasi 9 mbele ya Inter Milan, na taarifa zinasema Majogoo wa jiji wataondoka kabisa Top 10 ikiwa watashindwa kurudi katika michuano ya ulaya.

Tottenham wapo nafasi ya 11, mbele ya Manchester City washukuru mapato ya champions league msimu uliopita, City wanategemewa kuingia katika top 10 msimu ujao kutokana na tu na udhamini wa Etihad stadium wenye thamani ya £400million.

No comments:

Post a Comment