Search This Blog

Wednesday, June 20, 2012

DAWA YA NYWELE YA CARROLL NDIO SIRI YA USHANGILIAJI WA GOLI LA ROONEY


 Muda mfupi baada ya Wayne Rooney kuwafunga Ukriane kweye Euro 2012 na goli la kichwa, mshambuliaji huyo wa England alishangilia goli kwa mtindo wa kujipulizia dawa ya nywele kichwani.

Haikuwa ishara ya kuonyesha mafanikio ya ya upasuaji alioufanya wa kuotesha nywele, bali ilikuwa ni ishara kwa mchezaji mwenzie Andy Carroll, ambaye alimuazima Rooney dawa hiyo ya nywele na kupulizia kabla ya mechi na Carroll alimwambia Rooney afunge bao la kichwa.

Wazza anaelezea

PAMOJA NA KUONEKANA NA MAJIVUNO: CRISTIANO RONALDO AAMUA KUOKOA MAISHA YA MTOTO WA MIAKA 9 KUMLIPIA MATIBABU YA KANSA

Nuhazet, mtoto wa miaka 9 kutoka Las Palmas, Spain, amekuwa akipambana na kansa tangu alipokuwa na mwaka mmoja. Alipokutana na Cristiano Ronaldo kabla ya mechi ya mwisho ya Real Madrid msimu uliopita mwezi May 2012,  ndoto yake ya kuonana na mchezaji huyo ilitimia na kwa mujibu wake baada ya kumuona Ronaldo alikuwa yupo radhi ya kufa baada ya kuvumilia mateso ya ugonjwa huo tangu udogo wake, lakini mungu si Athumani kukutana kwake na Cristiano kumeanzisha upya mapambano ya kutibiwa kwa ugonjwa wake kwa usaidizi wa Ronaldo pamoja na wakala wake Jorge Mendes.

Stori iliyoandikwa na Canaris Investiga reports kwamba mwezi Machi, MRI ilitoa taarifa kwamba kansa ya Nuhazet imeshambaa kwenye sehemu tatu kutoka kwenye sehemu ya fuvu mpaka kwenye uti wa mgongo. Madakatari waliwaambia wazazi wake kwamba hakuna kinachoweza kufanyika na wakawashauri waache kupoteza fedha kwenye matibabu kwa maana matibabu hayo yanamuumiza mtoto kuliko inavyobidi. Wazazi waliuliza kama kuna kitu chochote wanachoweza kufanya popte pale duniani ambacho kingeweza kumsaidia Nuhazet, lakini waliambiwa matibabu pekee yaliyobakia yatakuwa ni majaribio.

Hivyo kutimiza moja ya ndoto ya Nuhazet, binamu akaanza kuwatafuta moja ya marafiki wazito na mmoja wao alikuwa ni Jorge Mendes, moja ya mawakala wenye nguvu kwenye soka. Wakandaa trip ya familia kutoka katika visiwa vya Canary mpaka Madrid kwa ajili ya kuangalia mechi ya mwisho ya Real Madrid kwa msimu uliopita dhidi ya Mallorca.

Siku ya mchezo, Mendes na familia wakamfanyia suprise Nuhazet kwa kumkutanisha  na Ronaldo, ambaye walitaniana na wakapiga picha za pamoja kabla ya kumuhaidi mtoto huyo kwamba ikiwa atafunga goli siku hiyo basi litakuwa ni kwa ajili ya Nuhazet . Baada ya kukutana, Nuhazet alienda kuangalia mechi akiwa kwenye sehemu maalum ya kukaa wageni wa Ronaldo  akiwemo mchumba wa Ronaldo, Irina Shayk.

Real Madrid walifunga Mallorca 4-1 na kubeba kombe la La Liga kwa mara ya kwanza ndani ya miaka minne. Ronaldo alifunga goli la kwanza la mchezo huo ambalo alilitoa kwa ajili ya mtoto huyo kama alivyomuahidi. Siku iliyofuatia Mendes akiwa na Raisi wa Real Madrid Florentino Perez, ambaye wiki kadhaa baadae alimpoteza mkewe aliyekuwa akiumwa kansa ya mapafu, waliwaita madaktari wa Sanchinarro Hospital. Kwa haraka wakamchukua Nuhazet na kuanza matibabu mapya ambayo yalijumuisha madawa maalum kutoka Marekani huku Ronaldo na Mendes wakilipa kitu.

Stori hii imekuja siku chache baada Lionel Messi kuripotiwa kuamua kulipiwa huduma za matibabu ya mtoto wa miaka 12 Walees Kashash, ambaye anaugua ugonjwa wa upungufu wa homoni za ukuaji (ugonjwa ambao Messi aliugua alipokuwa mdogo),  mpaka atakapofikisha miaka 18. Taarifa hizo baadae zimekuja kugundulika kuwa sio za ukweli, lakini Messi tayari alishaonekana kwa mapana kama binadamu mwenye huruma na roho nzuri sana. Kwa kijana  anayeonekana  mwenye majivuno na mbinafsi kama Cristiano Ronaldo  ambaye tayari ni baba wa mtoto wa miaka miwili - jambp hili alilofanya ni jema sana na linaondoa taswira mbaya iliyojengeka miongoni mwa watu.

Wengine wanaweza kusema ni katika kutaka kujitafutia sifa na kumfanya Ronaldo apendwe, lakini jambo muhimu ni kwamba Nuhazet bado anaendelea na matibabu na anaweza kurudi nyumbani wiki kadhaa zijazo ataanza stage nyingine ya matibabu. Na yote yamefanyika kwa sababu ya soka.

Football is powerful

CHELSEA Tanzania leo imewatangaza wasanii watakaotumbuiza.

CHELSEA Tanzania leo imewatangaza wasanii watakaopamba sherehe za ubingwa zitakazofanyika kwenye ukumbi wa Msasani Beach Club Jumapili hii. Mbali na michezo itakayozikutanisha Chelsea Tz,Arsenal Tz na Manchester Tz pia kutakuwa na burudani mbalimbali wakiwemo Mr.Nice,Sweet Sunday,Muumin Mwinyjuma,Charlesa Baba,Shilole atakayesindikizwa na Irene Uwoya na Akudo Impact. Kiingilio kitakuwa shilingi elfu 10 kwa wakubwa na watoto shilingi elfu 1. Sherehe hizo zitaanza tokea saa 4 asubuhi kwa soka la ufukweni.

Sherehe hizo ni mwanzo tu wa mambo mengi makubwa yatakayofuata baada ya usajili wa Taasisi itakayotambulika pia makao makuu huko London.

Cliford Mario Ndimbo Katibu wa Chelsea Tz akielezea utaratibu mzima utakavyokuwa.

HUYU MTOTO WA MCHEZAJI GANI ALIYEPO KWENYE EURO 2012

MJADALA ! NINI JUKUMU LA MWAMUZI WA NYUMA YA GOLI ?

DROGBA AKUBALI KUJIUNGA NA CHINESE SHANGHAI SHENHUA KWA DEAL LA £25M



Mshambuliaji wa zamani wa Chelsea Didier Drogba juma hili anatarajia kuidhinishwa kujiunga na klabu ya Shanghai Shenhua ya nchini China.
Mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 34 raia wa Ivory Coast inasemekana amekubali kusaini mkataba wa miaka miwili na nusu wenye thamani ya paundi milioni 25.

KIKWETE AKABIDHIWA JEZI YA NEW YORK KNICKS




  Rais Jakaya Kikwete akipokea jezi ya timu ya Mpira wa Kikapu inayocheza ligi ya NBA ya Marekani New York Knicks toka kwa Rais wa Shirikisho la  Basketball (TBF) Bw Mussa Mziya na Makamu wake Bw Phares Magessa walipomtembelea leo  Ikulu Jijini Dar es salaam  na kumueleza mipango ya chama hicho katika kuinua vipaji na viwango vya mchezo.
 
 Rais Jakaya Kikwete akipokea mpira toka kwa Rais wa Shirikisho la  Basketball (TBF) Bw na Makamu wake Bw Phares Magessa walipomtembelea leo  Ikulu Jijini Dar es salaam  na kumueleza mipango ya chama hicho katika kuinua vipaji na viwango vya mchezo
Rais Jakaya Kikwete akiongea na Rais wa Shirikisho la Basketball  (TBF) Bw Mussa Mziya na Makamu wake Bw Phares Magessa walipomtembelea leo  Ikulu Jijini Dar es salaam  na kumueleza mipango ya chama hicho katika kuinua vipaji na viwango vya mchezo

Taifa Stars yarejea nyumbanji salama


 Wachezaji wa Timu ya Taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’ wakiwasili katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Mwalimu JK Nyerere jijini Dar es Salaam jana usiku wakitokea nchini Msumbuji waliposhiriki katika Mchezo wa  mtoano wa kuwania kufuzu Fainali za Mataifa ya Afrika CAF. Taifa Stars ilitolewa katika michuano hiyo kw kufungwa kwa mikwaju ya penati na Msumbiji 8-7.
Wachezaji wa Timu ya Taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’ wakiwa ndani ya basi mara baada ya Kuwasili katika Uwanja  wa Kimataifa wa Mwalimu JK Nyerere jijini Dar es Salaam jana usiku wakitokea nchini Msumbuji waliposhiriki katika Mchezo wa  mtoano wa kuwania kufuzu Fainali za Mataifa ya Afrika CAF. Taifa Stars ilitolewa katika michuano hiyo kw kufungwa kwa mikwaju ya penati na Msumbiji 8-7.
  
 Kocha Mkuu wa Timu ya Taifa, Kim Polsen akizungumza na Sunday Kayuni mara baada ya kuiwasili uwanjani hapo
 

WADAU MNASEMAJE JE HILI LILIKUWA GOLI

BANG!!!!!! WAYNE ROONEY ARUDI NA GOLI NA KUIPELEKA ENGLAND ROBO FAINALI KUCHEZA NA ITALIA


England 1-0 Ukraine (Euro 2012 - Group D) by fasthighlights-2012

IBRAHIMOVIC AAGA NA EURO NA GOLI LA MASHINDANO: SWEDEN WAKIITANDIKA UFARANSA 2-0


Sweden 1-0 France (Euro 2012 - Group D) by fasthighlights-2012

Tuesday, June 19, 2012

HILI NDILO TAMKO LANGU RASMI JUU YA TUHUMA ZILIZOELEKEZWA KWANGU NA MZEE IBRAHIM AKILIMALI!

Siku ya Jumatatu, tarehe 18, June, 2012, majira ya mchana, Katibu wa Baraza la Wazee wa klabu ya Yanga aliitisha mkutano wa waandishi wa habari kwenye makao makuu ya klabu bingwa ya Afrika Mashariki na Kati yaliyopo eneo la Jangwani jijini Dar es Salaam.

 Katika mkutano wake huo na waandishi wa habari jana Mzee Ibrahim Akilimali aliongelea mambo mengi yanayoihusu Yanga lakini pia aliniongelea mimi Shaffih Dauda. Akiwa na akili timamu na nina uhakika bila kulazimishwa na mtu, Mzee Akilimali alinitupia shutuma nzito ambazo nadiriki kuziita za uongo ambazo kwa kweli zinaweza au zimeshafanikiwa kuharibu jina langu kama mwandishi wa habari pia kama binadamu wa kawaida tu.

Hivyo kuniharibia sifa yangu nzuri ambayo nimejijengea kwa kutumia nguvu kuifanya vizuri kazi yangu. Mzee Akilimali alinukuliwa akisema kwamba mimi (Shaffih Dauda) nimekuwa ndio kikwazo cha ujio wa kocha wa kimataifa wa Brazil, Marcio Maximo kuja kuifundisha klabu ya Yanga. Aliendelea kusema kwamba mimi nimekuwa na mawasiliano na Maximo nikimwambia mambo mengi ya uongo kuhusu Yanga ili niweze kutimiza lengo langu la kumuona kocha huyo asije kuifundisha Yanga.

Allinukuliwa akisema kwamba nimekuwa nikimtumia ujumbe mfupi wa simu, barua pepe na kumpigia simu Marcio Maximo nikimwambia asije Yanga kwa kuwa timu hiyo ni maskini na wana madeni hivyo asijaribu kuja Yanga. Katibu huyo wa Baraza la Wazee la Yanga aliendelea kusema kwamba Maximo amewatumia ujumbe akiwaambia mimi namsumbua sana juu ya suala hilo hivyo sasa anaogopa mpaka kupokea simu za Tanzania kwa ajili ya usumbufu wangu Shaffih Dauda. Kiukweli hizi ni tuhuma nzito na chafu dhidi yangu, kamwe siwezi kukaa kimya na kuliacha hili lipite hivi hivi, hivyo nimeona bora nilitolee majibu.

Tuhuma za Mzee Akilimali sio tu zinaweza kunichafua bali pia zinanigombanisha na mamilioni ya wapenzi na wanachama ya klabu Yanga pamoja na wapenzi wote wenye kupenda maendeleo ya mchezo wa soka hapa nchini. Binafsi pamoja na wana sports xtra wenzangu tumekuwa mstari wa mbele kupigania maendeleo ya michezo hapa nchini hususani mchezo wa soka, ujio wa Marcio Maximo hapa nchini kuja kuifundisha Yanga naamini ungeweza kuisaidia klabu iyo pamoja na nchi kwa ujumla,sasa iweje nimzuie kuja nchini kufanya jambo la maendeleo kama hilo ?

Pia tuhuma hizi zinaweza kuniharibia kazi yangu kupitia vipindi vya michezo vya Sports Extra na Sports Bar ambavyo siku zote kwa pamoja na wenzangu tumekuwa tukifanya kazi ya kuhabarisha pamoja na kutoa mawazo yetu kuhakikisha soka na michezo kwa ujumla inapiga hatua kuelekea mbele. Mwisho baada ya kusema yote hayo nimefikia uamuzi wa kumpa siku saba (7) Mzee Akilimali kutoa ushahidi au vielelezo vya shutuma alizonitupia alivyodai anavyo ili kuweza kuthibitisha madai yake dhidi yangu,na kama akishindwa basi itabidi aitishe tena mkutano wa waandishi wa habari kama alivyofanya wakati akitoa tuhuma zake dhidi yangu na akanushe aliyoyasema na kuniomba radhi la sivyo sheria itachukua mkondo wake. Huu ndo ushahidi wa alichokizungumza mzee wangu Akilimali.

GOLI LA SIKU: MWANGALIE SUPER MARIO 'KICHAA' BALOTELLI ALIVYOWAONDOA KINA OSHEA KWENYE EURO

SHERIA YA OFFSIDE INASEMAJE KTK TUKIO HILI ?

CHEMSHA BONGO:UNAHISI BALOTELLI ALIKUA ANATAKA KUZUNGUMZA MANENO GANI?

Beki Leonardo Bonucci akimziba mdomo mshambuliaji Mario Balotelli asizungumze chochote mara tu baada ya kufunga bao la pili na ushindi kwa Italia hapo jana kwenye mchezo dhidi ya Jamhuri ya Ireland.

KAZI NA DAWA: Thanx God my New Ride its finaly here

 


 Hakikisha nawewe kwa macho yako kisha kawasimulie na wenzio...
Nimekula pozi nn,ngozi nyeupe pale nyuma Dooooh ni wasafiiiii!



Ndani sasa hiyo Music System sasa,kama nipo Club vle...

WAREMBO MISS DAR INTERCOLLE​GE KUSUGUA KISIGINO CHA TWANGA, CLUB BILICANAS KESHO

Na Mwandishi Wetu
WAREMBO wanaotarajiwa kushiriki shindano la Miss dar Intercollege 2012 jumatano ya keshjo wanatarajiwa kujivinjari katika ukumbi wa kimataifa wa Club Bilicanas iliopo katikati ya jiji la Dar es Salaam.
Shindano hilo limepangwa kufanyika Ijumaa ya Juni 22 katika ukumbi wa Makumbusho ya Taifa uliopo mkabala na Chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM) ambapo msanii wa bongo Fleva Nasib Abdul ‘Diamond’ anatarajiwa kutumbuiza.
Mratibu wa shindano hilo Dina Ismail amesema leo kwamba, warembo hao watapata kuhudhuria onyesho maalum la bendi ya African Stars "twanga Pepeta' kupitia usiku wa Mwafrika unaorindima kila jumatano katika klabu hiyo.
Dina alisema uongozi wa Bilicanas Group umewaalika warembo hao ili kuweza kuburudika pamoja na mashabiki wa muziki wa dansi nchini kwa lengo la kujipoza baada ya mazoezi yao.
"Warembo wetu wamealikwa kesho pale Bilicanas ambapo bendi ya Twanga Pepeta hutumbhuiza kila Jumatano kupitia usiku wa Mwafrika, hivyo tunaoomba mashabiki wajitokeze kwa wingi kuwashuhudia kabla ya kuja tena Ijumaa katika ukumbi wa Makumbusho ya Taifa,"Alisema
Alisema maandalizi ya shindano hilo yanakwenda vema ambapo warembo 14 watakaoshiriki  wanaendelea na mazoezi katika hoteli ya  The Grand Villa iliyopo Kijitonyama jijini Dar es Salaam

 “Mwaka huu tumejipanga vema kuhakikisha mmoja ya warembo kutoka Miss Dar Intercollege anafanya vema katika fainali za Miss Tanzania ,”alisema Dina.

Warembo watakaoshiriki shindano hilo  wanatoka vyuo vya  Biashara (CBE), Uandishi wa Habari (DSJ) na Time,  Ustawi wa Jamii,  Usimamizi wa Fedha (IFM)  na Chuo Kikuu huria (OUT ambapo taji linashikiliwa na Rose Msuya kutoka IFM, huku mshindi wa pili wa mwaka jana, Blessing Ngowi alitinga fainali za Miss Tanzania.

Dina aliwataja warembo hao kuwa ni pamoja na Veronica Ngota, Rose Muchunguzi, Nancy Maganga, Hilda  Edward, Diana Nyakisinda, Neema Michael, Veronica Yollla, Jacquiline Cliff, Sharifa Ibrahim, Natasha Deo, Saada Suleiman, Rose Masanja na Jamila Hassan.

Shindano hilo limedhaminiwa na kampuni ya Bia Tanzania (TBL) kupitia bia ya Redd’s,Dodoma Wine, Ndege Insurance, Skylight Band,Lamada Hotel, Screen Masters,Makumbusho ya Taifa, Mustafa Hassanali, Shear Illusions, Lamada Hotel,Grand Villa Hotel, Sporti Kizaa zaa, Clouds Fm na blog za Michuzi, Dinaismail(zamani Mamapipiro), Bin Zubeiry,Mtaa kwa Mtaa na Fullshangwe

KENYA YAMTIMUA KOCHA WA TIMU YA TAIFA FRANCIS KIMANZI

Makocha wanaajiriwa ili kufukuzwa (Coaches are hired to be fired)


Wiki kadhaa baada ya Tanzania kumfukuza kazi aliyekuwa kocha wa timu wa timu ya taifa Jan Poulsen na kumpa kazi aliyekuwa kocha wa timu ya vijana Kim Poulsen, leo majirani zetu Kenya nao wamefuata mfano wa Tanzania baada ya kumfukuza kazi Francis Kimazi na benchi lote la ufundi la timu ya taifa ya nchi hiyo Harembee Stars.

Katika jitihada za kujiokoa, shirikisho la nchi hiyo ambalo limekuwa kwenye presha kubwa kutoka wapenzi wa soka wa nchi hiyo waliotaka mabadiliko kwenye timu kufuatiwa kuwa na mfululizo wa matokeo mabaya kwenye michuano ya kufuzu African Cup of Nations na Kombe la Dunia.

Kimanzi alikuta barua ya kufukuzwa kazi inamsubiri muda mchache baada ya kutua kwenye uwanja wa ndege wa Jomo Kenyatta akitokea Togo, alipoenda kuiongoza Harembee Stars kucheza dhidi ya Togo na kufungwa kwa bao 1-0, hivyo kupelekea timu hiyo kupoteza matumaini ya kucheza michuano ya African Cup of Nations in 2013.

Mbadiliko hayo yamehitimisha utawala wa Kimanzi ambaye aliingia Harembee tangu November 1, 2011, akichukua nafasi ya Zedekiah Otieno Zico.


Lakini katika makubaliano ya kusitisha kibarua chake, Kimanzi amakubaliana na KFF kwamba atashushwa cheo na kuwa mkurugenzi wa ufundi huku nafasi ya ukocha kwa sasa ikiwa ipo wazi.

Temeke, Mbeya mabingwa michuano ya ARS

 Mchezaji bora wa michuano ya Airtel Rising Stars,  Abdul Seleman wa timu ya mkoa wa Temeke, akipokea kombe kutoka kwa Mkurugenzi wa Ufundi wa TFF, Sunday Kayuni. Michuano hiyo ilimalizika  juzi kwenye Uwanja wa Karume kwa Temeke kuibuka bingwa wa michuano hiyo baada ya kuifunga Mbeya magoli  3-1.
 Nahodha wa timu ya wasichana ya mkoa wa  Mbeya Mariam Ndauka, akinyanyua juu kombe baada ya kuibuka bingwa wa michuano ya Airtel Rising Stars kwa wanawake baada ya kuifunga Arusha 1-0 kwenye fainali za Airtel Rising Stars zilizofanyika Jumapili kwenye Uwanja wa Karume jijini Dar es Salaam.
 Nahodha wa timu ya wavulana ya Temeke Khalid Salum, akipokea kikombe kutoka kwa Naibu Mkurugenzi wa Michezo kutoka wizara ya Habari, Vijana, Utamanduni na Michez,o Juliana Matagi Yasoda. Temeke iliibuka mshindi wa michuano hiyo kwa wanaume baada ya kuifunga Mbeya 3-1 kwenye fainali iliyochezwa kwenye uwanja wa Karume Jumapili 17 jijini Dar es Salaam.
 Time ya Temeke ikifurahia ushindi mara baada ya kuibuka kuwa washindi wa michuano ya Airtel Rising Stars kwa kutwaa ushindi wa mabao 3-1 thidi ya timu ya Mbeya

Fainali za taifa michuano ya Airtel Rising Stars iliyokuwa ikihusisha timu za mpira wa miguu kwa timu za wavulana na wasichana, zilifikia tamati Jumapili 17 kwenye Uwanja wa Karume huku timu za wavulana Temeke na Mbeya wasichana zikiibuka mabingwa wa michuano hiyo.
Michuano hiyo ya vijana wenye umri chini ya miaka 17 pia imetoa wachezaji sita bora ambao watahudhuria kliniki ya soka ya Kimataifa itakayokuwa chini ya walimu kutoka Klabu ya Manchester United ambayo itafanyika Nairobi. Wachezaji hao ni – Jackline Gibson na Irene Bahisi kutoka Arusha, Madeline Sylvester (Ilala), Abdul Seleman, Denis Richard na Paul Balama (Temeke).
Jumla ya timu za shule za sekondari 24 kutoka mikoa sita zilishiriki michuano ya Airtel Rising Stars kwa mwaka huu huku wachezaji bora wakichanguliwa kuunda timu kombaini za mikoa kwa ajili ya fainali za taifa. Mikoa iliyoshiriki ni Lindi, Mbeya, Arusha, Ilala, Kinondoni na Temeke.
Shule hizo zilichanguliwa kutokana na kufanya vizuri kwenye michuano ya taifa ya shule za sekondari (UMISSETA) mwaka jana. Uzinduzi rasmi wa ARS 2012 ulifanyika Mei, kwenye Hoteli ya Sea Cliff jijini Dar es Salaam na mchezaji wa zamani wa Klabu ya Manchester United ya Uingereza, Quinton Fortune.
Fainali za ARS za wiki moja pia zimetumika kuchangua timu ambayo itawakilisha Tanzania kwenye michuano ya ‘inter-continental’ ambayo itashirikisha nchi 17 ambao Airtel inafanya biashara. Michuano hii itafanyika Nairobi mwezi wa Agosti.
Timu ya wavulana ya Temeke imepata nafasi ya kuwa bingwa wa Airtel Rising Stars 2012 baada ya kuifunga Mbeya 3-1 kwenye fainali kali y a kusisimua huku wasichana wa Mbeya wakiibuka bingwa baada ya kuwafunga wenzao Arusha 3-1. Timu hizo mbili bingwa zilijinyakulia vitabu vya thamani ya Tshs1m, medali ya dhahabu na vyeti vya kushiriki.
Michuano wa Airtel Rising Stars ni mpango kambambe kwa Afrika nzima ambao ni wa kutafuta na kukuza vipaji vya soka vinavyochipukia kwa wavulana na wasichana wenye miaka chini ya kumi na saba ambao watapata muda wa kuonyesha vipaji vyao na kukutana na wataalamu wa mpira wa miguu ambao watawapa mafunzo zaidi na kupata nafasi ya kukuza vipaji vyao.
Airtel Rising Stars ni ushirikiano kati ya Airtel na klabu ya Uingereza ya Manchester United ya kukuza vipaji vya soka barani Afrika. Huu ni mwaka wa pili kwa Airtel kudhamini michuano hii. Mwaka jana, Klabu ya Manchester United ilitoa walimu wake wa soka ya vijana kuendesha kliniki ya soka ya Kimataifa ambazo kliniki hizo zilifanyika Tanzania, Afrika Kusini na Gabon

ENGLAND VS UKRAINE: MECHI YA KWANZA YA ROONEY - NA INAWEZA IKAWA YA MWISHO KWA SHEVCHENKO



Wayne Rooney atarudi kwenye kikosi cha England leo usiku baada ya kumaliza adhabu yake ya kusimamishwa mechi mbili . Anategemewa kucheza sambamba na mchezaji mwenzake wa Man United Danny Welbeck, ingawa Andy Carroll pia anaweza akaanza baada ya kucheza vizuri dhidi ya Sweden.

Theo Walcott, pamoja na kuondoka mazoezini Jumapili akiwa na majeruhi kidogo ya misuli ya nyuma ya paja, lakini anaweza kaanza leo baada kuanya vizuri baada ya kuingia kwenye mchezo dhidi ya Sweden. Winga huyo wa Arsenal, ikiwa atachaguliwa anategemewa kumbadili James Milner, huku England wakitumia mfumo wa 4-2-3-1, lakini pia Milner anaweza kurudi kwenye upande wa kushoto kumbadili Ashley Young ambaye bado hajaonyesha kiwango kikubwa mpaka sasa  kwenye michuano hii.

Andry Shevchenko ni mtu ambaye ana mashaka makubwa kucheza kutokana na majeruhi ya goti lakini bado anapewa ya kucheza ikiwa atapasi vipimo vya afya katika mechi ambayo Ukraine inabidi washinde ili kusonga mbele. Ikiwa hatoweza kucheza, Oleg Blokhin anategemewa kumbadili na Artem Milevskiy au Marko Devic kucheza pamoja na Andriy Veronin.

Blokhin amechezesha safu ya ulinzi na kiungo ile ile katika michezo miwili ya kwanza, huku Antoliy Tymoshchuk akiulinda ukuta wa nyuma huku Serhiy Nazarenko, Yevhen Konoplyanka na Andriy Yarmolenko wakisaidia mashambulizi na washambuliaji.

JE WAJUA

England na Ukraine wamekutana mara mbili katika mechi za mashindano, huku kila timu ikishinda mechi moja walipokutana kwenye michuano ya kufuzu kombe la dunia 2006.

Pia timu hizi zimeshakutana mara mbili kwenye mechi za kirafiki, huku England wakishinda mechi zote mbili, wakifunga mabao 5 na kuruhusu moja.

Andy Carroll alifunga dhidi Sweden lakini pia alikuwa na asilimia chache ya pasi zilizokamilika kuliko mchezaji yoyote wa England. Carroll alimaliza mchezo wote akiwa kapiga pasi 19 tu katik ya 41 alizojaribu.

England wanahitaji japo sare tu kuweza kufuzu kwa robo fainali, lakini wanahitaji kuyazidi matokeo ya France dhidi ya Sweden ili kuweza kuwa viongozi wa group. Timu zote mbili zina pointi sawa lakini England wamezidiwa kwa goli moja na France.

Ukraine watakuwa timu mwenyeji ya tano kutoka kwenye hatua ya makundi tangu  michuano hiyo ilipoanza kushirikisha timu 16 mwaka 1996, ikiwa watashindwa kuwafunga England.

Mchezo wa Jumanne unaweza ukawa wa mwisho wa Andriy Shevchenko kuichezea nchi yake. Mpaka sasa yeye ndiye mfungaji bora wa muda wote wa nchi hiyo akiwa tayari ameshafunga mabao 48 katika mechi 110.

Ukraine watacheza mara mbili na England kwenye michuano ya kufuzu kombe la dunia nchini Brazil 2014.

MISS DAR INDIAN OCEAN 2012,For booking tickets CALL 0779888818

KINA NANI WANAOMTUMIA MZEE AKILIMALI NDANI YA YANGA ?

Hi Mr. Shaffih, Jana usiku nilikuwa nasikiliza kipindi chenu cha Michezo Sports Extra na Sports Bar, vilivyorushwa kwa wakati mmoja kupitia Clouds Fm na Clouds Tv. Nilisikiliza kipande ambacho kuna Mzee Anayeitwa Akilimali, ambaye hujiita katibu wa Baraza la Wazee Wa Yanga. Sina uhakika na hiyo nafasi kwenye Katiba ya Yanga kama ipo.
Amekuwa akitumika sana, nashukuiru kwa kulitambuahilo jana. Waandishi mmempa sana airtime ya kutosha huyu Mzee mpaka imekuwa kero. Amekuwa Msemaji Mkuu wa Yanga kinyume na utaratibu. Wakati wachezaji wetu wamempiga refa Mechi ya Yanga na Azam alilumbana na TFF na kuongea mambo ya ajabu. Kwenye birthday ya Yanga aliwasifia akina Nchunga na akawageuka baadaye. Jana tu Anasema uchaguzi wa Yanga ukiisha atamfukuza Mwanachama Abedi Falcon uanachama kisa ameweka pingamizi kwa wagombea kuhusu uchaguzi.
Kwani hajui ni haki ya mwanachama kuweka pingamizi? alisema ana milioni 750 za usajili, azitoe wapi? Mzee yule na wenzake wasioitakia Yanga Mema ndio hao wamewaponza wachezaji wetu wa Yanga leo hii wamekosa fursa muhimu ya kutumikia timu ya Taifa kutokana na kuwatumia mechi zetu za mwisho wacheze maigizo ili kumkomoa Nchunga. Kiko Wapi leo? Menyekiti hayupo Yanga na Yanga  itaendelea kuwepo. Timu yetu ilipoteza muelekeo mwishoni mwa ligi kwa hujuma za hao wazee dhidi ya Uongozi halali.
Leo wachezaji wanasajiliwa na watu binafsi kwa gharama kubwa, kwa akili ya kawaida wanayanga wanachekelea tu bila kutafakari. Mchezaji anasajiliwa kwa Milioni 30 na Mshahara M 1 kwa chanzo gani cha mapato klabuni? hao wanaowatumia akina Akilimali wakigombana na viongozi halali si ndio wanagoma kutoa mishahara, na kupigwa zile tano? tuna safari ndefu Kaka. Nahitimisha na kusema yule Mzeee alikuwa anatumika tangu mwanzo wa mgogoro wa Yanga, na ameendelea kuwa Msemaji Mkuu, Sekretarieti ya Yanga inamuchia, Nyie waandishi wa Michezo mnampa nafasi bila sababu. Ni bora mmemgundua. Mimi ni Mshabiki wa Yanga wa Kawaida, huyo Mzee hana Mamlaka ya kunivua ushabiki ndio maana nimefunguka.

 Mr. Faraja Emmanuel Mkazi wa Kurasini.

 0717 079727

BREAKING NEWS: BONIFACE MKWASA AJIUZULU UKOCHA TWIGA STARS

Mkwasa

KOCHA wa timu ya soka ya taifa ya wanawake Tanzania, Twiga Stars, Charles Boniface Mkwasa amejiuzulu leo.
Nahodha huyo wa zamani wa timu ya soka ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars ameiambia BIN ZUBEIRY usiku huu kwamba ameamua kujiuzulu kutokana na matokeo mabaya na pia timu hiyo kutothaminiwa na Shirikisho la Soka Tanzania (TFF).
Mkwasa anachukua hatua hiyo, siku mbili tu tangu timu hiyo itolewe katika kinyang’anyiro cha kuwania tiketi ya kucheza Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika na Ethiopia kwa jumla ya mabao 3-1, ikifungwa 2-1 Addis Ababa na baadaye 1-0 Jumamosi mjini Dar es Salaam.
Mapema baada ya kufungwa juzi, Mkwasa alisema kwamba timu hiyo haikuwa na maandalizi mazuri na TFF haikuonekana kuijali kabisa. Lakini Mkwasa atakumbukwa mno kwa kuifikisha juu timu hiyo, akiiwezesha kushiriki fainali za Afrika miaka miwili iliyopita nchini Afrika Kusini, hiyo ikiwa ni mara ya kwanza kihistoria.

JESUS AIPELEKA SPAIN ROBO FAINALI YA EURO 2012


Croatia 0-1 Spain (Euro 2012 - Group C) by fasthighlights-2012

FOWADI YA VICHAA: BALOTELLI NA CASSANO WAIPELEKA ITALY ROBO FAINALI


Italy 2-0 Rep. of Ireland (Euro 2012 - Group C)... by fasthighlights-2012

HII NDIO HATMA YA LIGI KUU YA TANZANIA BARA JUU YA SUALA LA KUENDESHWA NA KAMPUNI

Siku kadhaa baada ya afisa habari wa klabu Villa Squad, bwana Idd Godi Godi kuhoji juu ya harakati za viongozi wa vilabu vinavyoshiriki ligi  kuu ya Tanzania bara kuleta mchakato wa kuunda kampuni itakayoendesha ligi kuu ya msimu ujao. Huku akiwa anahoji ipo wapi ile kasi ya viongozi hao wa vilabu vya ligi kuu waliokuwa wakiongozwa na makamu mwenyekiti wa Simba Geodfrey Nyange Kaburu katika kuhakikisha TFF wanaiachia ligi iendeshwe na kampuni itakayoundwa na vilabu. 


 Baada ya kuripotiwa kwa hoja zile za bwana Godi godi ambaye nae alikuwa mmoja ya viongozi waliokuwa wakishiriki vikao vya kuhakikisha ligi kuu ya msimu ujao inachezwa ikiwa chini ya uendeshwaji wa kampuni kabla ya Raisi wa shirikisho la soka nchini Leodgar Tenga kuunda kamati ya ligi iliyoundwa na baadhi ya viongozi wa vilabu waliokuwa wakipigania kampuni.


Kuchaguliwa kwa viongozi wale kuingia kwenye kamati ya ligi iliyoundwa na Tenga kulionekana kupunguza kelele na kasi ya harakati za viongozi wale akiwemo Kaburu, Celestine Mwesiga, Meja Charles Mbuge, Said Mohamedi, Seif Ahmed 'Magari', na Henry Kabera, na kwa mujibu wa Idd Godi Godi anasema Leogdar Tenga aliwachagua viongozi hawa ili kuweza kutuliza zile harakati zao wote kwa pamoja na alifanikiwa kwani toka wakati huo ule mchakato umepotea au unafanywa kwa siri bila kutangazwa kwa hatua zilizofikiwa kama ilivyokuwa mwanzo.


Kufuatiwa hoja iliyotolewa na Bwana Idd, nikaona ni vizuri kuweza kuwasiliana na mmoja ya viongozi wakuu wa vilabu, Geodfrey Nyange Kaburu, ambaye alikuwa mstari mbele kutaka mabadiliko kabla ya kuingizwa kwenye kamati ya ligi na Tenga.


Baada ya kumuuliza ni wapi wamefikia kwenye mchakato wa kuunda kampuni itakayoendesha ligi kuu msimu ujao na kwanini wamekuwa kimya muda mrefu bila kutoa taarifa kwa vyombo vya habari kama ilivyokuwa zamani, hivi ndivyo bwana Kabaru alivyojibu: "Kwanza kabisa nataka niweke vizuri jambo hili kwamba tumekuwa tumeacha kushughulikia mchakato wa kuunda kampuni ya kusimamia ligi kuu msimu ujao, la hasha viongozi wa vilabu vyote vinavyoshiriki ligi kuu tumekuwa tukikutana mara kwa mara, na mara ya mwisho tumekutana ni Ijumaa ya wiki iliyopita, kwa bahati mbaya Iddi Godi Godi hana taarifa hizo kwa kuwa klabu yake imeshuka daraja hivyo wamepoteza sifa ya kushiriki kwenye vikao. Lakini so far mipango ipo vizuri sana, tumefika hatua za mwisho mwisho kabla ya kupeleka mpango au mfumo mzima jinsi na namna ligi itakavyoendeshwa na kampuni yetu. Kwa bahati nzuri mkutano mkuu wa TFF chini ya Raisi Tenga ulishatoa maamuzi ya kubariki suala la kampuni huku wakitoa mamalka kwa kamati ya utendaji kutusimamia mpaka tukamilishe mchakato huu wa mabadiliko. Tunategemea wiki ijayo kupitia mwanasheria wetu tutapeleka mfumo rasmi na mpango wote wa jinsi ya kuanzisha kampuni hii na mfumo wa kuendeshwa kwa kamati ya utendaji ya TFF ili kupata baraka zao.
"Pia lingine kubwa ambalo tumelipanga kwa sasa tupo kwenye mazungumzo ja kampuni moja ya kimarekani ambayo kama mambo yakienda sawa ndio itakuwa inayosimamia shughuli zote za kampuni yetu na kuziacha klabu zibaki zikicheza mpira tu. Tumefanya hivi ili vilabu visijihusishe na uendeshwaji wa kampuni moja kwa moja ili kutoa ile hali ya klabu fulani kufanya vitu fulani kwa jili ya kujipendelea(conflict of interest) jambo ambao tumelishuhudia kwenye hii kamati ya ligi ambayo tumeiendesha kwenye nusu ya pili ya msimu."

Alipoulizwa kuhusu mipango ya kutafuta mdhamini mpya baada ya mkataba wa mdhamini wa zamani kuisha, huku ikizingatiwa kwamba ligi ipo karibuni kuanza Nyange alijibu: "Hilo nalo ni moja ya majukumu ya mwanzo tuliyonayo viongozi wa viabu na tunalifanyia kazi, mpaka sasa tupo kwenye mazungumzo na kampuni ya Vodacom ambao wameonyesha nia ya kutaka kutoa mkataba mpya na mungu akijaalia tunaweza tukatoa taarifa rasmi wiki jayo wapi tulipofikia," alimalizia Kaburu.





Monday, June 18, 2012

ALI AFIF ON SPORTS BAR YA CLOUDS TV.

MAONI YA MDAU : MPIRA WETU UMEJAA SIASA NYINGI

Mimi kama mpenzi wa mpira na mtanzania nimeudhunishwa sana, kusikitishwa na kufadhaishwa kwa kitendo cha taifa starz kutolewa na msumbiji ktk michuano ya kombe la dunia.
Nna huzuni ingawa matokeo hayo niliyategemea kwa asilimia kubwa,
Mpira wetu umekuwa na siasa nyingi na falsafa yetu ya kujenga timu, kila mwaka na kila kocha anayekuja huwa ana kazi ya kujenga timu tu,.
Kuna maswali yaniniumiza kichwa sana, maswali hayo ni:-
1. Jan paulsen alikuja na kupewa mkataba wa miaka miwili, je ushawahi kuona wapi timu ikajengwa kwa miaka 2?
2. Kim paulsen ana mkataba wa mwaka mmoja, je atajengaje timu kwa mwaka mmoja? Au atafanya kila namna tu ili atufurahishe kwa huu mwaka mmoja aliopewa.
(ntaomba majibu kwa maswali hayo)
kama tungelikuwa na mipango ya muda mrefu toka alipokuja maximo mwaka 2006 ina mana huu ungekuwa ni mwaka wa 6 hvyo tungekuwa tumeshajenga timu nzuri na hapana shaka na sie tungekuwa ni washiriki wa AFCON mwakani, pamoja na WORLD CUP 2014.
MAPENDEKEZO YANGU NI:-
1.Kocha apewe mkataba wa miaka minne na awe na jukumu la kujenga timu haswa kwa kuwatumia U-20 na U-23.
2.Timu isishiriki kwa kipindi fulani mashindano yoyote kama ya AFCON au wORLD CUP na badala yake tujikite katika kuijenga timu na kuipa mechi nyingi za kirafiki zitakazochezwa ndani na nje ya nchi.
3.tutumie mashindano ya CECAFA kama njia mojawapo ya kuijenga timu yetu, haswa kwa kuwatumia hao vijana.
4.katika hiyo timu kuwe na wakongwe wasiozidi wanne ambao watakuwa na jukumu la kuwapa uzoefu vijana hao.

tukifanya hvyo tutakuwa tumejenga timu yetu badala ya kutumia vibaya rasilimali zetu huku tukijua fika kuwa hatufiki kokote zaidi ya kuwa wasindikizaji tu.
Ahsante kwa kunipa nafasi.
Huu ndio mtazamo wangu.
Naomba kutoa hoja.
IBRAHIM SHAWEJI
0717183929

ETI SHAFFIH DAUDA AMEMZUIA MARCIO MAXIMO KUJA YANGA! MSIKILIZE MZEE AKILIMALI HAPA.

DITTO, LINEX NA MWASITI WAPAWISHA EBSS WAKAWAKA PARTY

Linex Sunday Mjeda akifanya vitu vyake kwenye ukumbi wa Royal Village katika EBBS Wakawaka Party

Ikafika zamu ya soldier Mwasiti kusababisha kwenye jukwaa la Epiq BSS Wakawaka Party, alifunika hatari.

Ditto aliwakilisha vizuri nae kwa kupiga show kali iliyoleta hisia kubwa miongoni mwa waudhuruiaji wa Wakawaka Party.

WAZIRI AKITOA BURUDANI KWENYE WAKAWAKA PARTY

WILLIAM PINGO WA ZANTEL, DITTO, MHE. JANUARY MAKAMBA, AWAICHI MAWALLA WA ZANTEL NA IBRAHIM ATTAS WA ZANTEL WAKIPATA GROUP PICTURE NA MHE. JANUARY MAKAMBA

MWASITI, DITTO AND LINEX AT CLUB 84

KAZI NA DAWA: VIDEO MPYA YA MSANII AY YATOKA.

VIDEO YA WIMBO PARTY ZONE WA MSANII AY AKIMSHIRIKISHA MARCO CHALI.

ITALY VS IRELAND: KUMTEGEMEA SANA ANDREA PIRLO NI HATARI KWA ITALIA

Kuna suala la kubishana kidogo kwamba Andrea Pirlo alikuwa ndio kiungo bora wa ulaya msimu uliopita. Alisajiliwa na Juventus na kuisadia kushinda taji la kwanza la serie A tangu ilipotokea skendo ya Calciopoli ya mwaka 2006; chini ya Pirlo Juventus walimaliza msimu bila kufungwa kwenye ligi, na Andrea Pirlo aliifanya bibi kizee wa Turin kutisha tena.

Utulivu na uvumilivu wa Pirlo akiwa na mpira ulikuwa hauna mfano mwingine kwenye bara la ulaya, na akiwa anaelekea kwenye Euro 2012, alikuwa kwenye kiwango cha maisha yake.



MIDFIELD MAESTRO
PIRLO'S STATS VS SPAIN
PASSES MADE
LONG PASSES
SHORT PASSES
PASSING ACCURACY
GOALS
ASSISTS

39
9
30
82.1%
0
1
PIRLO'S STATS VS CROATIA
PASSES MADE
LONG PASSES
SHORT PASSES
PASSING ACCURACY
GOALS
ASSISTS

67
11
56
82.1%
1
0


Akiwa na miaka 33, kiungo mchezeshaji huyo hakutegemewa kucheza kwa kiwango kizuri kwenye msimu wa 201-12. Aliachwa na AC Milan kwa kuwa na umri mkubwa, lakini chini ya uongozi wa Antonio Conte, akaweza kuwa mhimili mkuu wa timu hasa kwenye eno la kiiungo.

Kiwango chake kikubwa kiliwafanya Italia waende kwenye michuano ya Euro nchini Poland na Ukraine wakiwa kwenye hali ya matumaini. Kama ilivyo Juve, kocha Cesare Prandelli amemfanya Pirlo ndio nguzo ya timu yake; huku akicheza pembeni ya Claudio Marchisio na Thiago Motta kwenye kiungo, ilionekana kwamba Azzuri wangepita kwenye hatua ya makundi bila wasiwasi wowote.

Baada ya mechi ya kwanza dhidi ya Spain, ambayo Italy walionekana kucheza vizuri. Walipata suluhu ya kuipigani sana ya 1-1 dhidi ya mabingwa watetezi. Azzuiri walionekana kuwa vizuri kwenye ulinzi, mawinga na ushambuliaji wa mtu kama Di Natale mwenye uwezo wa kufunga mabao muhimu, lakini kubwa kuliko ilikuwa na kiwango cha Pirlo aliyecheza dhidi ya midfield maestros Xavi na Iniesta.

"Mchezaji aliyeleta tofauti kubwa ni Pirlo," Fabio Capello aliiambia UEFA.com. "Kila mara alipoanzisha shambulizi, lilikuwa ni shambulizi la hatari kwa wapinzani Spain."

Corriere dello Sport lilisema kwenye gazeti la asubuhi ya siku iliyofuatia "Beautiful Italy". Lakini gazeti hilo halikuendeleza sifa hizo siku nne baadae, likaandika, "Sare & Shida" kama kichwa cha habari baada ya vijana wa Prandelli kutoka suluhu na Croatia katika mechi ya pili ya kundi C.

Italy walihangaika na kucheza hovyo, hasa kwenye kipindi cha pili, wakipewa presha kubwa na kikosi cha Bilic, na hatimaye wakaruhusu goli la kusawazisha kwa Croatia likifungwa na Mandzukic. Pirlo alitulizwa hasa kwenye dakika 45 za kipindi cha pili, na matokeo yake timu ya Italia ikaonekana imevunjika vipande vipande.

Imekuwa hali kma inayoitokea Portugal kumtgemea sana Ronaldo, Pirlo asipokuwa kwenye kiwango kizuri basi na Italia inapotea kabisa.

Akiwa ndio tishio pekee kwenye creative department, Pirlo alikuwa ndio target kwa vijana wa Slaven Bilic. Alikabwa vilivyo na viungo wa Croatia chini Ognjen Vukojevic,  na hivyo kupelekea kushindwa kucheza vizuri.

Suluhisho pekee kwa Prandelli, ni kuongeza kiungo mwingine mbunifu kwenye safu ya kiungo, Thiago Motta, akiwa mzuri jinsi alivyo lakini sio mchezeshaji mzuri sana kwa mchezo wa kushambulia, hivyo kwenye mechi dhidi ya Ireland, haihatajiki sana. Kwa maana hiyo itabidi Antonio Nocerino aanze kwenye kikosi cha kwanza badala ya Motta. Nocerino ni ni kiungo wa aina ya Box to Box, kiungo ambaye Italy wanahitaji dhidi ya wachezaji aiana ya Keith Andrews na Paul Green, kwa hakika atakuwa mbadla sahihi.

Ikiwa Italy wataendelea mbele kwenye michuano hii itabidi wachezaji wengine waongeze kasi kwenye viwango vyao na kujituma zaidi, na sio kumuachia kiungo mwenye umri wa miaka 33, Pirlo, kubeba mzigo wa taifa kwenye mabega yake.